Ukarabati wa Kituo cha Mabasi Bukoba kwa "Bilioni Moja ya Rais Samia" hakuna kinachoendelea, Je, Watumishi wamepiga dili tena?

Ukarabati wa Kituo cha Mabasi Bukoba kwa "Bilioni Moja ya Rais Samia" hakuna kinachoendelea, Je, Watumishi wamepiga dili tena?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
photo_2025-01-10_18-14-40.jpg
Mwaka 2023 kuna fedha Tsh Bilioni 1 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani Kagera iliamuliwa na Serikali ya Mkoa kuwa zinatakiwa kutumika kukarabati Stendi ya Mabasi ya Bukoba, lakini hadi sasa mradi haujakamilika.

Oktoba 2023, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwasa alisema fedha hizo zitatumika kukarabati Stendi ya Bukoba Mjini.

Alisema maamuzi hayo yamefanyika kwa kuwa awali kulikuwa na mpango wa fedha hizo kupigwa na Wajanja wachache waliotaka ‘kuzuga’ kuwa fedha hizo zinatumika katika ujenzi wa Stendi ya Bukoba eneo la Kyakairabwa jambo ambalo halikuwa kwenye bajeti kwa kuwa mradi wa hapo ulipangwa kujengwa chini ya Benki ya Dunia kupitia Mradi wa uboreshaji wa miundombinuya Miji ya Tanzania (TACTIC).

Aidha, Oktoba hiyohiyo 2023, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Steven Byabato akizungumza na Wananchi alisema maborfesho hayo ya Stendi ya Bukoba unatarajiwa kuchukua miezi sita.
photo_2025-01-10_18-13-53.jpg

photo_2025-01-10_18-13-51.jpg

photo_2025-01-10_18-13-55.jpg

photo_2025-01-10_18-13-55 (2).jpg
MABORESHO YAMESIMAMA
Eneo hilo la ujenzi limezungushiwa uzio zaidi ya mwaka sasa, tuliamini tutaona mambo mazuri lakini kilichofanyika ni kusawazisha eneo husika na kuweka zege chini.

Jengo la ghorofa ambalo tuliambiwa linajengwa kwa ajili ya ofisi halijajengwa wala vyoo vya kisasa kama ilivyoonekana kwenye michoro, mpaka sasa hakuna mkandarasi saiti wala vifaa vya ujenzi eneo hilo ni kama limetelekezwa.

Inawezekana tayari fedha za Mradi wa maboresho zimepigwa au kuna wahusika wanajinufaisha kupitia utaratibu usio rasmi.

Wito wangu kwa mamlaka ikiwemo TAKUKURU wachunguze matumizi ya fedha hizo kwa kuwa kazi ambayo imefanyika hadi sasa haiendani na kiwango kilichotajwa kutolewa, lakini kama kuna uzembe wa mkandarasi au baadhi ya viongozi wawajibike ikizingatiwa muda uliobainishwa umepitiliza zaidi ya miezi sita sasa.

NYUMA YA PAZIA, FEDHA ZILIVYOTAKA KUPIGWA
Inadaiwa wakati mzigo ukiwa njiani kwenda Bukoba, kuna watumishi wachache wa Manispaa ya Bukoba walianzisha mchakato wa ujenzi wa Stendi ya Bukoba eneo la Kyakairabwa, ndipo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwasa akashtuka na kusimamisha mchakato, ambapo aliyasema hayo hadharani Oktoba 2023.

Mkandarasi aliyekuwa akianza ujenzi eneo la Kyakairabwa akafichua kuwa hakuwa na ramani, aliambiwa atoe Tsh. Milioni 50 kama kishika uchumba, akatoka.

Baadaye wakati ameanza ujenzi bila ramani akaambiwa atapewa Tsh Milioni 150 lakini kwa sharti kuwa arejeshe Milioni 50 kwa hao wapigaji, akakataa akaona hu oni upuuzi, ndipo wakaamua kumchunia.

Hivyo basi, kama hao watu walishtukiwa mara ya kwanza na ndio haohao wanaosimamia mradi wa maboresho ya Stendi uliosimama kwa zaidi yam waka inawezekana ndio wamehusika kufanya yao pia, Serikali inakubali kupigwa kirahisi hivi?
 
Mbona hapo kwenye financer imeandikwa serikali ya Tanzania, ila ww mtoa mada umesema n pesa za samia?
 
Mbona hapo kwenye financer imeandikwa serikali ya Tanzania, ila ww mtoa mada umesema n pesa za samia?
Siku Mkuu wa Mkoa anafafanua kilichotokea hadi wakataka kupiga deal mara zote alisema :"Fedha za Rais Samia" so nami nimeruka nayo kama walivyozungumza, hayo mambo mengine ni masuala ya karatasi.
 
Billion moja haitoshi hata kurepea nyumba. Waongeze mshiko
 
Back
Top Bottom