SoC02 Ukatili kwa watoto wa kike kutoka kwa wazazi wao

SoC02 Ukatili kwa watoto wa kike kutoka kwa wazazi wao

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Sep 9, 2022
Posts
3
Reaction score
3
Mimi ni nibinti wa miaka 25 niliye aliwa mkoani Kilimanjaro wilaya ya Hai, ni wa pili katika familia ya bwana Festo familia ambayo ilikuwa na hali duni kiasi kwamba tulikuwa tukipewa mavazi chakula na watu majirani.

Kutokana na na mfumo dume wanaotumia wanaume wa kichagga kiukweli baba alinipiga sana kipigo ingalikuwa sisi ni mabinti huku akitumia miadarati kama bangi lkn mama yetu mzazi alipambana pamoja na sisi huku baba akiishia jela.

Maisha yetu yalikuwa nikufanya vibarau angali tu watoto ili mradi tumsaidie mama kwa wakati baba yupo jela huku Dada mkubwa aliamua kutoroka kwenda kutafuta maisha kwa vipigo.

Mwishowe baba alitoka jela hapo niko form one, hakubadilika tabia yake ilikuwa ile ile ya upigaji. Nakumbuka alikuwa anashika mashamba ya watu anasema nina watoto watalima na hela alikuwa haleti nyumbani, tunalimishwa. Nakumbuka nilikuwa nalima huku nableed mpk inateremka na miguuni.

Tuliendelea kukua tukipitia ukatili ule, nakumbuka kuna dada alinisaidia msaada wa baiskeli nilikuwa nasoma shule ya mbali lkn baba bila kujali alinipiga. Kupitia ulezi aliyekuwa anatulelea nilishindwa kuendelea kukaa nyumbn nikaamua kutoroka kuja Dar na kuacha shule ingalikuwa nilikuwa nikiongoza shule ya msingi mpaka sekondari na mwishowe niliolewa nikiwa na miaka 14 hatimaye nina watoto 4.

Sasa Niko mbele yenu kupinga vikali malezi mabaya kama baba alivyotulea sisi na wilaya ya Hai mabinti wengi hawasomi, wazazi kutengana, wanaume Wanapiga wake zao wanalewa pombe kiasi cha kushindwa kulea mabinti zao.

Nilikuwa napenda elimu niliishi katika ndoto za kusoma mpaka sasa ninasoma nina ndoto ya kuwa daktari mkubwa sana na kutetea haki za watoto na pia Serikali ninaiomba sana ifungue shule za QT nying ili mabinti wenye ndoto kama zangu wafanikiwe kutokana na ada kuwa kubwa.

Nina mifano mingi ndani ya miaka kumi niliyokuwa kwenye ndoa pia ni story kubwa ya kuuzunisha japo napambana nisome nitimize ndoto zangu na nilivyorudi shule mambo ni mazuri nasoma masomo ya sayansi. Nina picha ninaweza kuwatumia mkihiitaji ufaulu wangu ni kwa ufupi sana.

Na pia niwape moyo mabinti wote kama unaamini ulikwamishwa kielimu na bado una ndoto unaweza kuwa Nina Imani na Mimi ninaweza kuwa.

Serikali ilitoa ruhusa ya kurudishuleni lkn ilikuwa ina ubaguzi wa miaka uliyoacha shule. Ninaiomba serikali tena nina imani wapo wengi kama mimi waliokwamishwa na bado wana ndoto kama mimi itusaidie kwa kufungua shule za QT nyingi mpaka vijijini.

Kuna mabinti wengi naweza kuwatolea mifano wengi wamezaa. Watoto chini ya miaka kumi na nane wengi sana hapo nilipotoka na maisha yao ni magumu. Mwingine ameenda kufanya kazi za ndani akiwa na mtoto wa miezi 2 huku yeye akiwa na miaka 16 na kesi nyingi za wilaya ya Hai zinazimwa na rushwa rushwa ndio mkandamizaji wa haki za watoto hao au mabinti hao.

Nakumbuka nikiwa shule ya msingi nilikuwa nashiriki kwenye mabunge ya watoto kusoma risala kwenye maadhimisho ya mtoto wa Afrika lkn ndoto zangu zilizimwa na mzazi wangu mwenyewe.

Wazazi nawaita tena wazazi tusimtafute mchawi nani, ni malezi yenu wenyewe ndio yanapelekea watoto wenu kuwakimbia sasa.

Niliolewa na mwanaume mwenye watoto wawili huku nikiwa nina miaka 14 na hapa nilipo nina familia ya watu 12.

Ninawasaidia mabinti wanne ambao wazazi wao wamezama kwenye dimbwi la kuwatelekeza kulelewa na watu.

Athari zilizo ikuta failia yangu
Dada mkubwa yule aliye toroka sasa mimarehemu alifariki akiwa na miaka 21. Mtoto yule aliye pigwa nae alisoma akafika secondar akamaliza akajiunga na jeshi la kujenga taifa kipindi akiwa anasubiri ajira akaumwa na madaktari wakasema alipata kreki ya ubongo akafa pia.

Mama nae kutokana na kuachwa marakwamara alee watoto mwenyew nae alipata HIV na haikuishia hapo nae aliondoka nyumbn na ameacha mapacha wawili wakike na wakiume wako darasa la 6.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom