Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,497
- 4,775
Siku ya Tarehe kumi na tano ya wiki iliyopita, katika eneo la Engaruka wilaya Monduli mkoani Arusha,palitokea tukio la Kinyama la mtoto wa Miaka kumi na Tano ajulikanae kwa JIna la Namasi kufungwa katika Mti na kuadhibiwa kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kupata majeraha makubwa ambayo yalimpelekea kupata Ugonjwa wa Kisaiokolojia ujulikanao kama Post Traumatic Stress Disorder,Ugonjwa ambao unamfanya Muhanga kuchanganyikiwa na kuwa na kuwa kama kichaa kutokana na matukio aliyofanyiwa kujirudia katika akili yake.
Sababu ya mtoto huyo wa darasa la SIta,kupata adhabu hiyo,ni kukataa kuolewa na mtu ajulikanae kwa jina la Munjeree AMbae ndie aliemuoa Mtoto huyo na ambae ndie alietekeleza adhabu hiyo ya kikatili na Mtu huyo hadi sasa yupo uraiani bila ya kukamatwa.
Tukio hili ni muendelezo wa Matukio ya kikatili yanayoendelea katika jamii ya kimasai ambapo mtoto wa chini ya umri wa miaka kumi na nane anaweza kuolewa na kugeuzwa mtu mzima.
Baada ya mtoto huyo kupata adhabu kali na kuchanganyikiwa kiakili,alipelekwa kwa mchungaji mmoja ili aombewe kwani familia iliamini kuwa mtoto huyo ana mapepo kwa sababu alikuwa akivua nguo na kuongea hovyo hovyo.
SIku ya Alhamisi wiki,Shirika la kutetea wanawake na Wasichana lijulikanalo kwa jina la Mimutie Women Organization lilifanya juhudi za kumtafuta mtoto huyo sehemu aliyokuwa amefichwa na kumleta Arusha mjini kwa ajili ya matibabu, na hadi sasa mtoto huyo amelazwa katika Hospitali ya MKoa wa Mount Meru akiwa katika hali mbaya ,huku alietenda kosa hilo akiwa bado anadunda mtaani.
Tunaomba serikali ichukue hatua kali za kisheria kwa kumtia nguvuni watuhumiwa wote waliomuozesha mtoto huyo ndoa ya utotoni pamoja na aliempiga hadi mtoto kurukwa na akili.
Ni wakati wa kutenda Haki.
Update: Tunamshukuru sana Muheshimiwa Waziri,Mama Dorothy Gwajima kwa kuona Uzito wa Binti wa Engaruka na kutoa tamko