Ukatili wa beer ya brutal hauko kwenye kiwango cha kilevi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Inaitwa Brutal beer! Jina moja la kibabe sana! Yaani BIA KATILI
Kama hujawahi kuiona kwa sura unaweza kuogopa sana.. Lakini once unapoiona unaanza kupata mashaka
.Chupa yake ni ndogo halafu kimodo
. Rangi yake ni pink iliyofifia
. Ladha yake ni ya matunda
. Kilevi chake ni asilimia 5%

Kwahiyo sasa ukatili wake unatokana na nini? BEI!
Kimoja kinauzwa Tsh. 5000! Kinanywewa na wadada wa mjini kwa asilimia 99.. Ni kilevi laini sana lakini bei ni katili
Ukatili wake uko kwenye mfuko wa mlipaji.. Michepuko inavipenda sanaπŸ™ŒπŸΏπŸ˜Ž! Akija na mashosti wawili wakanywa tano tano tuu ni laki kasoroπŸ˜‚
Na vilivyo laini wanaweza kila mmoja akamaliza 10 pekeyakeπŸ₯Ί
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…