UKAWA kugomea kura ya maoni ya katiba ni kujivisha kitanzi uchaguzi mkuu 2015

UKAWA kugomea kura ya maoni ya katiba ni kujivisha kitanzi uchaguzi mkuu 2015

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Sababu kubwa ni moja: Huu mchakato unaambatana pamoja na mambo mengine, kuandikisha wapiga kura katika daftari la kudumu.

Kugomea mchakato katika hatua hii, ina maana supporters wao watakuwa demoralized hata kujiandikisha. Watakaojiandikisha watakuwa wale wanaoiunga mkono katiba ambao majority ni wafuasi wa CCM. As a result, ikifika uchaguzi october mikutano yetu itajaa watu kama kawaida but hawatapiga kura...

Niwahakikishie UKAWA kuwa, under no circumstance katiba inayopendekezwa inaweza ikapita. Tuitumie hii fursa kama sehemu ya kuwaandaa wananchi wetu kisaikolojia kupiga kura kwa wingi uchaguzi mkuu baadae mwaka huu. Tukijenga spirit ya kugoma, tukawapa CCM uwanja wa kuzunguka majukwaa nchi nzima sasa, hakika wafuasi wao watakuwa tayari zaidi kisaikolojia kwa ajili ya uchaguzi mkuu, na watashinda kiulaini sana...

Uchaguzi huu utumike kama sehemu ya kujijengea uwezo wa kuendesha kampeni, kushawishi wapiga kura na kusimamia kura... uwezo ambao utahitajika sana uchaguzi mkuu ujao...

Ni hayo tu...
 
Maamuzi ya UKAWA ya kugomea kura ya maoni ya katiba ya Maintarahamwe ni maamuzi ambayo yanastahili kupongezwa. Itakuwaje wakubali kushiriki katika kura ya maoni ya Maintarahamwe ambayo waliyagomea na kuamua kutoka nje ya majadiliano ya Bunge la katiba na juhudi zao za kutaka maoni ya Watanzania yasichakachuliwe hayakuwa na mafanikio yoyote. Hongera sana UKAWA kwa msimamo thabiti kuhusiana na uhuni na uharamia wa Maintarahamwe.
 
Maamuzi ya UKAWA ya kugomea katiba ya Maintarahamwe ni maamuzi ambayo yanastahili kupongezwa.
Basi:
tuwapongeze kwa makofi matatu ya nguvu, haya 1,2, 3........ pa, pa, papapa! paaaaaa!
 
Sisi ni ACT Mwigamba....wewe ni ACT Limbu au ACT Nyakarungu?
Kwa kweli franco Luambo Makiadi alikuwa ni mwanamuziki mkubwa mno Kongo na enelote la Afrika,Ijapokuwa alifariki muda mrefu, lakini hata leo hii ukiusikia mziki wake utasema naam!
 
Kujiandikisha nitajiandikisha na kupiga kura nitapiga ya 'HAPANA' kwisha, na mwezi wa kumi ni kura ya 'HAPANA' kwisha...
 
Maamuzi ya UKAWA ya kugomea kura ya maoni ya katiba ya Maintarahamwe ni maamuzi ambayo yanastahili kupongezwa. Itakuwaje wakubali kushiriki katika kura ya maoni ya Maintarahamwe ambayo waliyagomea na kuamua kutoka nje ya majadiliano ya Bunge la katiba na juhudi zao za kutaka maoni ya Watanzania yasichakachuliwe hayakuwa na mafanikio yoyote. Hongera sana UKAWA kwa msimamo thabiti kuhusiana na uhuni na uharamia wa Maintarahamwe.

Mkuu nakuelewa...
But impact ya kura ya maoni kwenye suala la kuhamasisha uandikishaji wapiga kura (uandikishaji ambao ndio utakaotumika katika uchaguzi mkuu ujao), pamoja na morale nzima ya ushiriki wa uchaguzi huo ni kubwa na sio ya kubeza...
 
Kujiandikisha tutajiandikisha na tutahamasisha watu wajiandikishe kwa ajili ya october sio katiba,interahamwe ccm waendelee na katiba yao.tukutane field october.
 
Haya ni mawazo ya kisaliti.

Ndani ya UKAWA huwa hatupingi mawazo, maazimio na maagizo ya viongozi.

Kwa mawazo haya ya kisaliti, inawezekana wewe siyo mwanaUKAWA!
 
Ikitokea wakianzisha kampeni yakuwashawishi watu wasishiriki, wewe utagundua nini kwa haraka haraka na utajifunza jambo gani la msingi kwenye siasa za upinzani Tanzania?
 
Haya ni mawazo ya kisaliti.

Ndani ya UKAWA huwa hatupingi mawazo, maazimio na maagizo ya viongozi.

Kwa mawazo haya ya kisaliti, inawezekana wewe siyo mwanaUKAWA!
Mkuu, Tuko ameamua kuwasaliti wenzake na sifikiri UKAWA wanaweza kuwavumilia watu jamii ya akina Tuko na Freeland . wala sioni kama ukawa wanasababu ya kufanya hivyo kwa kuwa kile anachokisimamia mtoa mada kinaenda kinyume na misingi mkuu na strategia za ukawa (Msingi wa kugoma na kususa).
 
Last edited by a moderator:
Maamuzi ya UKAWA ya kugomea kura ya maoni ya katiba ya Maintarahamwe ni maamuzi ambayo yanastahili kupongezwa. Itakuwaje wakubali kushiriki katika kura ya maoni ya Maintarahamwe ambayo waliyagomea na kuamua kutoka nje ya majadiliano ya Bunge la katiba na juhudi zao za kutaka maoni ya Watanzania yasichakachuliwe hayakuwa na mafanikio yoyote. Hongera sana UKAWA kwa msimamo thabiti kuhusiana na uhuni na uharamia wa Maintarahamwe.

Kushiriki zoezi hili Haramu ni kuhalalisha katiba yao Haramu.

Historia itatuhukumu.Kamwe hatuwezi kushiriki ujinga huu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kujiandikisha tutajiandikisha na tutahamasisha watu wajiandikishe kwa ajili ya october sio katiba,interahamwe ccm waendelee na katiba yao.tukutane field october.
haya ila sitegemei kama novemba, baada ya matokeo kutangazwa, kutakuwa na sababu ya kuendelea kuilaumu tume ya uchaguzi. AAny way ila kulaumu ni haki yako, unaweza kuitumia tu upendavyo! khaaa! halafu nakuambia kama ni wewe na wakati sio wewe.
 
Naunga mkuno wasigomee kura ya maoni hapa watu hawatajiandikisha ni bora washiriki katika kampein then wafuasi wao waambiwe wapige kura ya hapana ili kutuanda na uchaguzi mkuu chonde ukawa shiriki.
 
Mkuu nakuelewa...
But impact ya kura ya maoni kwenye suala la kuhamasisha uandikishaji wapiga kura (uandikishaji ambao ndio utakaotumika katika uchaguzi mkuu ujao), pamoja na morale nzima ya ushiriki wa uchaguzi huo ni kubwa na sio ya kubeza...

Tuko

Wala usihofu kabisa.

Ipo mikakati mingi imepangwa.Ukawa ina viongozi wakubwa na wanasiasa waliobobea wanaojua wanafanya nini

Mikakati mingine siwezi kuiweka hapa kwa maslahi ya Ukawa kwa sababu CCM wanakodolea macho hapa.

Kwa kifupi amini viongozi wa Ukawa.Akina Maalim Seif na kina Mbowe wanajua wanasimamia nini.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom