TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,747
Kila wakiona wanaelekea kushindwa wanagoma, imekula kwao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika Ukawa Ni Wasaka Tonge Ndani Ya Ile Katiba Kuna Haki Za Wakulima,wafugaj,walemavu,wavuvi,vijana Na Wanawake Lakini Ukawa Haya Yote Hawayataki Wao Wanataka Mambo Ya Kuwapeleka Ikulu Tu,hakika Ukawa Hawana Uzalendo
Hili jambo niliwahi kuwatahadharisha UKAWATuko,
..uko sahihi by 50%.
..katiba kugomewa huku Tanganyika siyo jambo linaloweza kuitisha CCM.
..lakini Znz wakigoma ni jambo kubwa na la hatari sana ktk muungano wetu.
..kumbuka kwamba katiba inabidi ikubaliwe pande mbili za muungano, Tanganyika na Zanzibar.
.
Katika thead ya jana niliandika kuw ahoja ya mnyika haina maana kwa kuwa inawezekana sana haijashirikisha wenzao wa UKAWA pia madhara ya kusita kisha kuingia kichwa kichwa. Kama ni kususa jambo hili lingalifanyika mapema. Kitendo cha Mnyika kuanza kulialia ni ishara ya viongozi kukosa kujipanga sasa wanahofia defeat.
Nawaambieni hakuna mwaka wapinzani hasa CDM wamekoroga mambo kama mwaka 2015. Pia msije kuwa na mawazo ya kuitisha maandamano kwa kuwa wananchi hawaungi mkono hayo wananchi wanataka kupambana na CCM uwanjani
Hili jambo niliwahi kuwatahadharisha UKAWA
Tuko yupo sahihi kuwa kutojiandikisha inaweza kuwa ni sehemu ya ‘voter suppression'' na kwamba uchaguzi mkuu ni CCM watakaokuwa wamejiandikisha
Hivyo hoja hapa ni kuwa lazima watu wajiandikishe kwa matayarisho ya chaguzi na si kura ya maoni
Kuhusu kura ya maoni, hilo lisusiwe kwasababu haikutokana na wananchi.
Na hadi sasa inaonekana imeshasusiwa.
UKAWA wasizungumzie kabisa kura ya maoni ili kutotoa uhalali wa mzoga
Kura ya maoni ya CCM hakuna namna ya kuizuia isishinde.
Kama Samwel Sitta amefanya madudu ya wizi bungeni kwenye watu 600 na kisha kupewa nishani kwa utendaji hovyo, hakuna namna tume ya uchaguzi (NEC) ya CCM inaweza kutoa matokeo tofauti na maelezo ya mgaogoni. Hatuna tume huru.
UKAWA waendelee kudai katiba, na kama itakuwa ni lazima basi ile rasimu ya Warioba irudi mezani si hii ya Chenge na genge la mafisadi wengine.
UKAWA wanaweza kutumia sheria za uchaguzi kukiukwa kama inavyofafanuliwa. Kwamba, JK anakiuka sheria alizosaini kwa kulazimisha kura ya maoni chini ya ratiba na muda uliopangwa
Mgogoro wa kikatiba hauepukiki, tayari JK ameshatengeneza fertile environment, nadhani si jambo jema lakini kuna busara ndani yake.
Hiyo ndiyo itakuwa lesson na turning point ya wananchi kusikilizwa. Itakuwa painful lakini tukubali kuwa haki haipatikani katika sahani ya dhahabu.
Haki haiombwi inatafutwa na huu ndio wakati wa kuwaambia watawala, tumechoka na tupo tayari kujitetea
Muhimu zaidi, wananchi waache kabisa kuzungumzia katiba ya Chenge.
Si maoni yao.Hata kama itachukua miaka 10 mingine, ni bora kuliko mafisadi walioandika katiba ili kuleta msisimko na kuficha wizi wao wa Escrow
Ukitaka kujua hilo angalia, wote waliokuwa vinara wa katiba ni sehemu ya ufisadi.
Mkuu mimi siangalii matokeo ya kura ya maoni... bali impact yake kwenye uchaguzi mkuu ujao...
Ttatizo la UKAWA, mara zote hucheza mirindimo ya ngoma za CCM..itabidi UKAWA wake creative/crafty kwa kuwashawishi wanachama wao kujiandikisha kwa wingi lakini wasishiriki ktk kura ya maoni.
..pia kwenye uchaguzi mkuu Ukawa wahakikishe kwamba wanashinda in the 1st round by knock out. wakizembea wakapata ushindi kiduchu, wajue imekula kwao. they need to win by such big numbers so that it impossible to rig the elections.
cc Molemo, Tuko, Candid Scope
Hili jambo niliwahi kuwatahadharisha UKAWA
Tuko yupo sahihi kuwa kutojiandikisha inaweza kuwa ni sehemu ya voter suppression na kwamba uchaguzi mkuu ni CCM watakaokuwa wamejiandikisha
Hivyo hoja hapa ni kuwa lazima watu wajiandikishe kwa matayarisho ya chaguzi na si kura ya maoni
Kuhusu kura ya maoni, hilo lisusiwe kwasababu haikutokana na wananchi.
Na hadi sasa inaonekana imeshasusiwa.
UKAWA wasizungumzie kabisa kura ya maoni ili kutotoa uhalali wa mzoga
Kura ya maoni ya CCM hakuna namna ya kuizuia isishinde.
Kama Samwel Sitta amefanya madudu ya wizi bungeni kwenye watu 600 na kisha kupewa nishani kwa utendaji hovyo, hakuna namna tume ya uchaguzi (NEC) ya CCM inaweza kutoa matokeo tofauti na maelezo ya mgaogoni. Hatuna tume huru.
UKAWA waendelee kudai katiba, na kama itakuwa ni lazima basi ile rasimu ya Warioba irudi mezani si hii ya Chenge na genge la mafisadi wengine.
UKAWA wanaweza kutumia sheria za uchaguzi kukiukwa kama inavyofafanuliwa. Kwamba, JK anakiuka sheria alizosaini kwa kulazimisha kura ya maoni chini ya ratiba na muda uliopangwa
Mgogoro wa kikatiba hauepukiki, tayari JK ameshatengeneza fertile environment, nadhani si jambo jema lakini kuna busara ndani yake.
Hiyo ndiyo itakuwa lesson na turning point ya wananchi kusikilizwa. Itakuwa painful lakini tukubali kuwa haki haipatikani katika sahani ya dhahabu.
Haki haiombwi inatafutwa na huu ndio wakati wa kuwaambia watawala, tumechoka na tupo tayari kujitetea
Muhimu zaidi, wananchi waache kabisa kuzungumzia katiba ya Chenge.
Si maoni yao.Hata kama itachukua miaka 10 mingine, ni bora kuliko mafisadi walioandika katiba ili kuleta msisimko na kuficha wizi wao wa Escrow
Ukitaka kujua hilo angalia, wote waliokuwa vinara wa katiba ni sehemu ya ufisadi.
Kuna mambo mawili pengine hujaweza kuyapambanuaKwamba wananchi wasusie kura ya maoni kwa sababu katiba haikutokana na wananchi, NO, haina mantiki kwa sababu hata kwenye uchaguzi mkuu sio wagombea wote watatoka kwa wananchi. Kuukataa uhalali wa mzoga you must say NO!
Kusimamia kura ya maoni ni kama mechi nyingine ya majaribio kuona udhaifu wa usimamizi ukoje. Hii itasaidia kuweka mikakati bora kwa tukio kuu la october.
Nachelea kusema ccm watapenda sana ukawa wasuse kama ilivyo kuwa kwenye bunge la katiba, iliwapa nafasi ya kufanya kila mbwembwe na hakuna aliyewauliza. Walipewa uhuru wa kupika mapishi wayapendayo.
Kuna mambo mawili pengine hujaweza kuyapambanua
UKAWA walipoondoka bunge lengo kubwa ni kutokuwa sehemu ya mchakato uliokuwa unachakachuliwa.
Hivyo walitaka kuji-dissociated na process nzima ambayo kwao ilikuwa null and void ab initio
Kwenda kuongelea kura ya ndiyo au hapana ni kutoa uhalali kwa mchakati ule ule walioukataa.
Endapo ni hivyo, kulikuwa hakuna sababu za wao kutoka kwasababu wangeweza kubaki na kupiga kura ya hapana bungeni ambayo sisingebailfilisha matokeo kutokana na process nzima kuwa ya hovyo kama Samwel Sitta alivyoiendesha
CCM walijua kuwa bunge ndicho kikwazo kwao. Ndio hasa maana ya kuchakachua kura hata pale walipobaki wenyewe.
Walitambua kuwa nje ya bunge uwezekano wa kutumia tume yao ya uchaguzi kufanya uhalaifu upo. Na hicho ndicho wanakifanya sasa.
Kuzungumzia katiba na kura ya maoni ndicho wanakitaka ili kutoa uhalali kuwa mchakato mzima ulikuwa umekubalika na kilichoamua ni kura ya maoni.Yaani wanatupa mzoga wakijua wana mbinu za wewe kuuchukua halafu unashiriki katika kuamua ima uchukue mzoga au la.
Mzoga ni mzoga hauna mjadala, hata wewe nyumbani kwako huwezi kuletewa mzogo wa paka, kisha mtu akwambie mjadiliane ndiyo au hapana. Kwa mtu mwenye akili, hatakubali hata kusikiliza hadithi za mzoga huo na hatafikiria kusema ndio au hapana.
Wananchi wasiingizwe mkenge kujadili katiba ya Chenge/Sitta. Waache CCM wapitishe ili wananchi nao wajenge uhalali wa kupata katiba yao.
Tatizo ulilonalo wanalo Watanzania wengi. Kwamba, basi hata hicho kibaya ni afadhali.
Hakuna haramu nzuri kidogo, haramu ni haramu na katiba hii iliyoandikwa na mafisadi ili kuficha escrow ni haramu
Unposema mechi ya majaribio, nakushangaa sana. Asali haijaribiwi kwa kisu. Katiba ikishaandikwa ndiyo basi tena, kuna majaribio gani unataka kufanya hapo?
Hata kama itachukua miaka 10 kupata nyingine, hoja si bora katiba ni katiba bora.
mcharo kawa mtamuu!ndugu zangu ukawa sijui mshauri wenu ni nani katika masuala ya siasa mnakurupuka sana.
Tuko,
..uko sahihi by 50%.
..katiba kugomewa huku Tanganyika siyo jambo linaloweza kuitisha CCM.
..lakini Znz wakigoma ni jambo kubwa na la hatari sana ktk muungano wetu.
..kumbuka kwamba katiba inabidi ikubaliwe pande mbili za muungano, Tanganyika na Zanzibar.
cc Barubaru, takashi, Kibunango, Nguruvi3, GHIBUU