UKAWA kugomea kura ya maoni ya katiba ni kujivisha kitanzi uchaguzi mkuu 2015

Usijidanganye, kura zitakazo pigwa ndo zitakazo hesabiwa, Kama wazanzibari watagoma, wazanzibara walobaki watapiga kura,hata kama Mia moja Kama katika Mia kuna theluthi mbili imepita.

eeh!!!
 
Ukawa hapo ndo mmejimaliza,ccm watapata kura nyingi za ndiyo kwenye kura za maoni ya katiba pendekezwa. Hongera sana lipumba na mbatia kwa ushauri huo kwa wanaukawa.

Hapana yako itabadilishwa kuwa ndiyo, na hatuna wasimamizi wa hapana wenye bunduki, pingu, risasi za moto kulinda hapana yako. Tumia huo muda kwenda ibadani, au tulia na familia.
Eg kama wah. Wabunge walifufuka kutoka, wafu(RIP) wakapiga kura ya ndiyo bmk leo hii mkulima atapiga HAPANA????
 
Nyie wote hamjawaelewa ukawa. Ukawa walichokataa ni ushiriki katika mchakato wa katiba pendekezwa na sio kupiga kura. Wiki iliyopita nilishuhudia lipumba akihamasisha watu waweke hapana katika katiba pendekekezwa. Hivyo ukawa watashiriki kuweka hapana siku ya kura ila hawatoshiriki katika maandalizi ya aina yeyote pamoja na ccm.
 
Mkuu nakuelewa...
But impact ya kura ya maoni kwenye suala la kuhamasisha uandikishaji wapiga kura (uandikishaji ambao ndio utakaotumika katika uchaguzi mkuu ujao), pamoja na morale nzima ya ushiriki wa uchaguzi huo ni kubwa na sio ya kubeza...

Acha woga mkuu, hilo si la kuogopa, tushaamua hatupigi kura maoni, maana sisi hata tuwe wengi kiasi gani, jamaa wenyewe wameshahamua kuwa nuru iwe giza. Sasa ya nini kujisumbua.
Nachokiona hapo iwapo tungesema tupige hiyo kura ni kwamba mwisho wa siku watatu tumia sisi kama karai la zege, watasema si mnaona wame piga kura ya ndio na ndio maana katiba pendekezwa imepita, maana kwa uchakachuaji huu ambao tumeshuudia hata viongozi serikali za mtaa wanapitishwa kiubabe, je kura ya maoni si ndo kabisaa balaaa.
 
yani huu mchakato wa katiba ni siasa tupu sasa na ambavyo sipendi siasa yani mpaka naona kichefuchefu,,,af nasdindwa kuelewa kwa nini ccm wanahimiza sana watu kuipigia kura katiba inayopendekezwa utadhani ni katiba ya chama !!!
 

Kugoma kupiga kura siyo kuacha kujiandikisha,ukawa watahamasisha watu wajiandikishe kwa ajili ya uchaguzi October na siyo kura ya katiba ya ccm.Kwahiyo hayo mawazo uliyonayo wewe siyo waliyonayo ukawa,usidhani unvyowaza ndivyo na wenzako wanavyowaza.
 
Tuko na Freeland , misimamo yenu hiyo ni ya kisaliti.UKAWA wanataka kugoma ninyi mnapinga au ninyi ni CCM?


Kaka jamaa yuko sawa kwa upande flan kwa sababu UKAWA wanachogomea ni kushiriki kwenye mchakato wa kura ya maoni sio kujiandikisha,wananchi wengi wanauelewa mdogo ni bora wakawaelimisha watu wajiandikishe tu ila swala la kuipigida au kutoipigia kura ya maoni katiba ni lingine.Wanapokuwa wanasisitiza kugomea kura ya maoni kuna watu hawaelewi hivyo wanasema sasa nijiandikishe ili iweje wakati kura ya maoni sipigi.
 
Last edited by a moderator:
Tuko nakuunga mkono maoni yako yako balanced sana nafikiri ukawa wangewahamasisha wanachama wao kuikataa katiba hii ya nyoka wa magekeza na mwenzake six badala ya kugomea kwa hesabu za harakaharaka ni wazi kuwa ukawa wanawafuasi wengi zaidi ya ccm hinyo kama watapiga kura ya hapata kuikataa katiba hii ya kidhalimu italeta impact zaidi ya kugomea na kuwapa mwanya ccm kutamba wanavyotaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…