Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Wana JF,
Hii habari iko kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA
embu muisome mchangie kidogo sio maswala ya mamluki kama kawaida yetu?
BABA wa Taifa hayati Julius Nyerere, aliwahi kusema kuwa upinzani wa kweli utakaokiondosha madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM), utatoka ndani ya chama hicho.
Wakati akitoa kauli hiyo, alijua fika kuwa baadhi ya makada wa chama hicho walikuwa hawakubaliani na baadhi ya mambo, hivyo wangeweza kuondoka na kujiunga na upinzani.
Miaka hiyo ni tofauti na sasa, wapinzani hivi sasa wana nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa miaka hiyo. CCM wanahangaika kufanya hila kuwafitinisha na kuwafifisha kwa kuwa wanaona dalili ya kuondoka madarakani.
Ujio wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na vinginevyo, unaonekana kutoa taswira mpya ya siasa za kishindani.
UKAWA wameshatangaza nia kuungana na kuweka mgombea mmoja kwenye uchaguzi mkuu ujao mwakani, na taarifa kutoka ndani ya kundi hilo zimedokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mgombea kutoka ndani ya CCM.
Kinachofanywa na UKAWA kwenye mchakato wa katiba mpya kinaipeleka Tanzania kwenye mazingira ya kisiasa kama yale yaliyoikumba Kenya kwenye uchaguzi mkuu uliopita, baada ya kuibuka kwa makundi mawili yenye nguvu kisiasa; Cord (Coalition for Reforms and Democracy) na Jubilee ambayo yalikuwa na ushindani mkubwa.
Kundi maarufu la UKAWA linaongoza mkakati wa kupatikana kwa katiba mpya yenye mtazamo wa hoja za wananchi, hasa zilizotolewa kwenye mapendekezo ya rasimu ya katiba iliyotolewa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba.
Wakati UKAWA wakionekana kupata umaarufu zaidi, limejitokeza kundi jingine linaloitwa Tanzania Kwanza. Hili limebeba wajumbe kutoka CCM, TLP na baadhi ya vyama vya upinzani.
Makundi haya mawili yamechukua sura za makundi ya Cord na Jubilee yaliyokuwapo Kenya. Katika hatua hii, ni lazima wananchi watagawanyika.
Binafsi nimefuraishwa sana niliposikia vyama vikuu vya upinzani vinafikiria kuungana kwenye uchaguzi mkuu ujao na kusimamisha mgombea mmoja. Hatua hii imezua hofu kubwa ndani ya chama tawala – CCM kinachotajwa kuwa na mpasuko mkubwa, lakini kinakwenda kwa woga na kuvumiliana.
Nina imani kuwa hii ni fursa adhimu kwa vigogo wa CCM waliodhibitiwa ndani ya chama hicho kwa kupata sehemu ya kurukia endapo wataamua kuchukua maamuzi magumu kisiasa yasiyokubaliana na chama chao.
Tayari CCM wameshawafungia mwaka mmoja makada wake sita wanaotajwa kuanza kampeni za kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani kabla ya wakati.
Makada hao ni William Ngeleja, Edward Lowassa, Stephen Wassira, Benard Membe, January Makamba na Fredrick Sumaye. Hawa wote wanaweza kuingia UKAWA kwa lengo la kutimiza ndoto zao.
Najua Nyerere alisema upinzani wa kweli utatoka CCM kwa kuwa anajua chama hicho kina mizizi mikubwa sana, kina uwezo wa kucheza na Tume ya Uchaguzi, polisi, wasimamizi wa uchaguzi na watendaji wengine wahusikao na uchaguzi ili mradi ushindi upatikane.
Kwangu itakuwa faraja kama makada nguli wa CCM wakihamia UKAWA, najua wakihamia huko wataungwa mkono, kuna wenzao watawaunga mkono, watadhibiti wizi wa kura kwa kuwa wanajua njia walizokuwa wakizitumia wakiwa CCM.
Ndani ya UKAWA kuna uwezekano wa namna mbili, ambapo wa kwanza ni ule wa mgombea urais kutoka ndani ya kundi hilo na wa pili ambao ni mkubwa zaidi, ni kupata mgombea kutoka ndani ya CCM.
Ndani ya CCM kuna mvutano mkubwa sana wa chini kwa chini katika urais. Makada wake hawaivi chungu kimoja katika hili, wapo wanaoamini kwamba kwa namna yoyote hawawezi kutendewa haki katika uteuzi huo.
Pia wapo wanaotembea na madukuduku yao ya muda mrefu, lakini wameshindwa kuibuka na kujitoa ndani ya CCM kuhofia kushindwa kwani bado inaonekana kama chama chenye nguvu.
Ninaamini kuwa UKAWA watafanya mazungumzo na vigogo wenye majina na nafasi nyeti ndani ya CCM kama njia ya kuhakikisha inatumia vyema muungano huo kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Sina shaka UKAWA wako vitani katika kutafuta uongozi wa nchi, hivyo hawatoacha fursa ya kuwatumia vigogo wa CCM wanaobezwa na kukejeliwa kila siku ndani ya chama chao, hata pale wanapofanya mambo mazuri na yenye maslahi kwa nchi. Hawa watakuwa silaha muhimu ya kuhakikisha chama hicho tawala kinashindwa katika uchaguzi mkuu ujao.
Ni jambo la kheri mageuzi yanaonekana kupata mwelekeo mpya baada ya CCM kutaka kushinikiza matakwa yake ndani ya Bunge la Katiba linaloendelea, jambo ambalo limesaidia kuibua hasira za wapinzani kususia vikao vya Bunge hilo.
Naamini kuwa CCM wamefanya kosa kuonyesha moja kwa moja shinikizo la kutaka kupata katiba yenye maslahi yao. UKAWA wanapaswa kulitumia kosa hilo kujipatia uungwaji mkono wa wananchi.
UKAWA wameamua kwenda kuwaelimisha wananchi sababu za kususia vikao vya Bunge Maalumu, vilivyotawaliwa na kauli za vitisho, ubaguzi, matusi na misimamo ya vyama ambayo kwa kiasi kikubwa haitotoa katiba ya wananchi.
Najua ushirikiano wa umoja huo pia ni faraja kwa makada wa CCM kupata kimbilio pale watakaposhindwa kuafikiana na chama chao katika mambo mbalimbali, hususani hili la urais.
Si lazima kila atakayetoka CCM akagombee urais kupitia UKAWA, lakini ukweli ni kwamba, watu wanaotajwatajwa kuwa wameanza kunyemelewa na UKAWA wana majina makubwa na kuheshimika ndani ya jamii.
Kuondoka kwao na kujiunga UKAWA kutasababisha kundi kubwa kuondoka ndani ya CCM. Inawezekana kuwa UKAWA itatengeneza njia nzuri ya CCM kuondoka madarakani mapema zaidi kuliko ilivyotarajiwa.
Mabadiliko ya uongozi katika nchi hii ni jambo la muhimu sana kwa kuwa kwa muda mrefu imeshindwa kupiga hatua kubwa za maendeleo licha ya kuwa na rasilimali lukuki.
Bado hadi sasa bajeti ya Tanzania inategemea wahisani na wafadhili kwa asilimia 30-40. Madini, mbuga za wanyama, mito, maziwa, bahari vimeshindwa kuwasaidia wananchi. Tatizo kubwa hapa ni uongozi mbovu.
UKAWA wanaweza kuleta mabadiliko kama wataendelea kuunganisha nguvu zao na kuibomoa CCM. Nawasihi wasifunge milango kwa makada wa CCM wanaotaka kujiunga nao
 
Hatutaki mgombea kutoka Chama Cha Mashetani ,kama yupo na najua wapo walioko CCM ambao wana fikra na mawazo yenye kutaka kuliendeleza taifa hili kwa moyo wa dhati kabisa na wakizalendo ,ambao hawana makundi na tabia na vitendo vyao vya kiungwana vinakubalika ndani ya jamii ,wajibu wao ni kutangaza rasmi kuachana na chama hicho ,kwa taarifa tu wasichelewe na isitokee mtu akawa wa mwisho ,wakati ni huu kujua bivu na bichi. Saa ya ukombozi ikifika msibakie nyuma jitoeni huko kwa haraka na kwa umoja wenu fikra na mawazo yenu yatazidi kuwakwamua WaTz kutoka hapa kwenye jangwa la matope ya CCM.
 
Hao wote uliowataja waliofungiwa na CCM ni waroho wa madaraka. Hawa wanatafuta power tu sidhani wanaweza kuchangia lolote katika mabadiliko Tanzania
 
Edward L and Magufuli!! opportunity never come twice. welcome welcome ukawa the doors are open. Tunahitaji majembe yaliyofichwa store yaje kuchapa kazi. el ukija tutakusaidia kukuombea msamaha kwa ajili ya rchmond utakuwa mpya tena na umma wote utakupokea. Magufuli hina doa karibu uende magogoni. Vingnevyo Lissu atapewa ikulu shauri yenu maana naona slaa ameanza kujitoa polepola anasubiri uwazr mkuu.
 
Kiongozi yoyote mzuri au bora ni yule atakayeweza kukemea maovu on spot na siyo mpaka atoke nje ya chama chake.Akisha toka nje ya chama chake hatakuwa na weledi wa kusema chohote na wala uwezo wa kusemea chochote.

Viongozi wengi ndani ya CCM wapo kwa ajili ya mali tu na si wazalendo kwa ajili ya Taifa lao.Waone wanapokuwa nje na ndani ya bunge au ndani ya mikutano yao ya chama,hawawezi hata kusimama na kukemea uovu au ubaya unaotendwa na viongozi wenyewe,marafiki zao au familia zao.
 
Wakati mwingine binadamu mwenye akili timamu na iliyotulia hahitaji kuhangaika katika kutofautisha mbivu na mbichi , Hebu fikiria mtu mzima anaibuka na kushangilia UKAWA , yaani Umoja wa Katiba ya Wachache, maana yake nini? Huu ukawa uliundwa kwa matakwa ya nani? Je wananchi waliwatuma hao viongozi wa vyama na wafuasi kwenda kuunda UKAWA? Nijuavyo mimi Hawa ndugu wanaotumia Kali tatu kila kukicha wakitumwa kwenda juchambua maoendekezo tryin sisi Wananchi na kuyaboresha imo kila nyanja inayomgusa mtanzania iingizwe kwenye Katiba ambayo kimsingi ndiyo kimbilio la kila mtanzania. Kama wazo hili ni sahihi, sasa hana ya kuwa na UKAWA inakujaje? Je wasiokuwa ndani ya UKAWA itakuwaje? Pia hoja ya eti Kenya kulijitokeza makundi hasimu mawili na yakafaulu kukiondoa chama tawala madarakani! Wazo la manna hii ni wazo la kizamani sana, ni wazo lisilokuwa na Ukweli wowote, Demokrasia siyo Kama. soda ya coca cola kwamba kila anayekunywa anapata radha ile ile , Kwani Kama ndani huo ni sahihi hebu fikilia haya yafuayayo; Sudan walipigana kwa miaka takribani 30, Je Tanzania NATO lazima ipigane hadi ijitenge Kaskazini na kusini? Kenya ilipigana vita vya MAU MAU , Tz nayo lazima ipigane vita hivyo? Zimbabwe ilipigana kwenye chaguzi zao hivyo na Tx lazima itokee ? Morgan T' shangarai ametoswa na chama chake kwa kushindwa kukiongoza, haya lazima yatokee Chadema ? Vyama vya Unita, chama Nkomo wa Zimbabwe hadi Leo hazijaingia Ikulu, ndivyo inavyotakiwa itokee kwa cdm? inavyotakiwa kutokea kwa cdm?
Savimbi alikuwa mpinzani hadi kifo chake, ndivyo itakavyokuwa kwa Mbowe na Slaa? Mleta hoja acha kujishebedua kwa mambo yanayokuzidi Elimu. Waachie wayaalamu wenye shule zao. Wewe ni mwananchi lakini wenye nchi wapo.
 
Kwa mtazamo wangu ni ngumu sana kwa ukawa kusimamisha mgombea mmoja wa urais, kwa kuwa ukawa inaundwa na vyama vyenye mrengo tofauti kisiasa na kiitikadi, labda waunde chama kimoja chenye mrengo mmoja!
 
Kikundi haramu kinachojulikana kwa kinyarwanda 'intarahamwe' a.k.a UKAWA kwa kibongo, walitangaza kuwa uchaguzi wa mwaka kesho watasimamisha mgombea uraisi.
Je kati ya wasaka tonge hao ni yupi anaefaa kupewa nafasi ya kupeperusha bendera ya UKAWA kuomba ridhaa kwa wananchi kuliongoza taifa hili kwa miaka kumi ijayo? Hahahahahaha...,hivi hili nalo linahitaji shule kujua ni jinsi gani akil za watu zinachezewa? "wajinga'z ndio waliwao"
 
Bw.Majeshi naona leo umekesha zamu hapo ccm mkoa arusha kulinda gate.

Ccm tulikuajiri kwa kazi hiyo,suala la propaganda waachie akina Vuta Nikuvute.
 
Bw.Majeshi naona leo umekesha zamu hapo ccm mkoa arusha kulinda gate.

Ccm tulikuajiri kwa kazi hiyo,suala la propaganda waachie akina Vuta Nikuvute.

Kati ya hawa wasaka tonge ni yupi atakayegombea Uraisi kupitia UKAWA (hatujui kama ni chama cha Siasa au ni kitu gani)?

Jibu swali hayo mengine ni porojo zako.
 
....katika kuufanyia kazi umoja wao (coalition) nategemea UKAWA watengeneze dira ya pamoja (manifesto/vision) itakayotokana na sera za vyama vyao....alafu wainadi kwa wananchi kwenye chaguzi za mwakani(2015)...tena jambo la kwanza kwenye dira yao ya pamoja liwe kuwapatia wananchi katiba ya matakwa yao....kwa kufanya hivi lazima watawapiga chini ccm....Waacheni ccm waendelee kuichezea rasimu ya katiba....hicho ndo kitakua mwanzo wa kifo chao....UKAWA watumieni wasomi wenu wawatengenezee dira ya pamoja kwa ajili ya chaguzi za 2015.....dira itokane na sera za vyama vyenu....
 
WANA JAMVI MAONI YANGU NINGE PENDA KUONA DR SLAA ANAPITISHWA NA UKAWA KUGOMBEA URAIS 2015 HUKU WAFUATAO WANA KUWA HIVYI;
1;prof lipumba makamo wa rais
2;freeman mbowe- waziri mkuu
3;james mbatia-waziri wa fedha na uchumi
4;tindu lissu- katiba na uchumi
5;habibu mnyaa-muungano
6;jussa-afrika mashariki
7;david kafulila-viwanda na uwezeshaji
8;mkosa mali -maji
9;zitto kabwe-mambo ya nje
10;mothes machali-tamisemi
11;mnyika nishati na madini

ongezeni majina na nafasi zao;angalizo hii ni kama mfumo wa serikali 2 utabakia Kama mfumo wa serikali 3 utakuwepo; urais tanganyika
1;-dr slaa makamo wake james mbatia
2;prof lipumba-muungano makamo wake zitto kabwe
3;maalim seif-zanzibar makamo wake juma duni haji;

naomba kuwasilisha ila kuboreshwa kwa ruhusiwa na si matusi
 
WANA JAMVI MAONI YANGU NINGE PENDA KUONA DR SLAA ANAPITISHWA NA UKAWA KUGOMBEA URAIS 2015 HUKU WAFUATAO WANA KUWA HIVYI; 1;prof lipumba makamo wa rais 2;freeman mbowe- waziri mkuu 3;james mbatia-waziri wa fedha na uchumi 4;tindu lissu- katiba na uchumi 5;habibu mnyaa-muungano 6;jussa-afrika mashariki 7;david kafulila-viwanda na uwezeshaji 8;mkosa mali -maji 9;zitto kabwe-mambo ya nje 10;mothes machali-tamisemi 11;mnyika nishati na madini---;ongezeni majina na nafasi zao;angalizo hii ni kama mfumo wa serikali 2 utabakia; kama mfumo wa serikali 3 utakuwepo; urais tanganyika 1;-dr slaa makamo wake james mbatia 2;prof lipumba-muungano makamo wake zitto kabwe 3;maalim seif-zanzibar makamo wake juma duni haji; naomba kuwasilisha ila kuboreshwa kwa ruhusiwa na si matusi

Prof Lipumba ndio anayefaa kuliko slaa. Ni mchumi huyo mtu hadimu. Tumuunge mkono.
 
Back
Top Bottom