Habari wakuu,
Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA uliundwa na viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF NA NCCR ndani ya Bunge maalum la Katiba ili kukabilina na nguvu ya kambi ya TANZANIA KWANZA inayoongozwa na CCM. Baada ya umoja huo kutozaa matunda ndani ya Bunge uliamua kususia vikao vya bunge na kuamua kufanyia shughuli zake nje ya Bunge, na pengine tunaweza kusema nje umezaa matunda japo siyo rasmi na siyo matunda ya kisheria. Midahalo toka kwa UKAWA wenyewe, wanaharakati, wana taaluma ya sheria, wajumbe wa iliyokuwa tume ya badiliko ya Katiba na makundi mengine mengi yalioombwa au kudhaminiwa na UKAWA ni miongoni mwa hayo matunda yaliooza mitini kabla hayajakomaa.
UKAWA wakiwa nje ya Bunge wametangaza rasmi kuwa mwaka 2015 watakuwa kitu kimoja katika uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais, eti wanasema mgombea wa chama mshirika wa UKAWA anayekubalika eneo fulani atasimama kwa niaba ya UKAWA. Lakini tujiulize swali moja tu kwamba, lini mgombea wa CUF atakubalika Moshi mjini aachiwe? au lini mgombea wa CHADEMA atakubalika PEMBA aachiwe? au lini mgombea wa NCCR atakosa umaarufu KIGOMA na nafasi hiyo asimame wa CHADEMA? Jibu ni hakuna, na kwa maana hiyo mambo yatakuwa ni yale yale ya ZAMANI, yaani CHADEMA, CUF na NCCR kila mmoja atashinda aliko maarufu.
Hoja yangu kubwa katika mada hii, NI NANI ANAPASWA KUJIFICHA KWENYE HIKI KIVULI CHA UKAWA KWENYE UCHAGUZI WA 2015?.
Binafsi naona atakaeathirika endapo UKAWA watashindwa kutimiza azma yao ya kuwa kitu kimoja 2015 ni CHADEMA kwa sababu zifuatazo:
1. Ni ukweli usiopingika kuwa wazo la kuundwa kwa UKAWA ni la CHADEMA na liliwaijia ili kupisha upepo uliokuwa ukivuma ndani ya chama chao, upepo wa vurugu zilizopelekea kuondokewa na watu wao muhimu kama akina SAMSON MWIGAMBA, KITILA MKUMBO, na sasa kuna uwezekano wa ARFI, SHIBUDA, LETICIA na ZITTO KABWE.
2. CUF na NCCR wao wamekuwa wakikua siku hadi siku wakati CHADEMA wanaporomoka na ushahidi ulio wazi ni bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopita, Wabunge wa NCCR mageuzi kama akina MACHALI, KAFURILA na wengine waling'ara huku wale wa CHADEMA wakipiga majungu tu
3. CHADEMA bado wana OMBWE la kitendawili kilichokighubika chama, kitendawili cha Uchaguzi wa chama ngazi ya Taifa, hakuna anayejua kama kitendawili kitatenguliwa au la? Hii ni sababu nyingine ya CHADEMA kuendelea kung'ang'ania UKAWA wasirudi bungeni kwa vile wanajua wakitimba tu kule upepo wa ndani ya Chama chao utaanza kuvuma tena kwa sababu ya UKAWA na bunge maalum la katiba yatakuwa yamekwisha.