Mkuu hata akisimama Warioba bado watamwaga fedha..... dawa ni kula hela za wajinga halafu kura unapiga kwa unayemtaka
Mimi ni CCM damu, ila linapokuja suala la maslahi kwa Taifa huwa CCM huwa inakuwa nambari MBILI. Manake tulio wengi huwa tunachezeshwa ngoma tusiyoijua na wapenda madaraka ili waendelee kututawala. Mzee Sinde Warioba pamoja na makada wenzetu wa CCM ambao waliteuliwa kukusanya maoni kwenye tume ya mabadiliko ya katiba walitanguliza Utanzania kwanza na kuacha UCCM kando na ndio maana wakaja na mapendekezo yaliyotokana na watanzania pamoja na kuangalia mahitaji ya sasa kwa Watanzania, cha ajabu wapenda Uraisi wakaona mapendekezo haya ya watanzania yanaweza yakawa kikwazo cha wao kusaka uraisi.
Ushauri wangu ni kwamba ili kazi iliyofanywa na tume ya Warioba ya kutuletea katiba mpya ambayo ndio mkataba kati ya watawala na watawaliwa na hivyo kuwa msingi mkuu wa maendeleo yetu, hivyo ningewashauri UKAWA waachane na kusaka uraisi na kumshawishi Mzee Warioba Akubali kusimama kama mgombea kupitia mgombea atakayeteuliwa na ukawa na hapo ndipo ukombozi wa Mtanzania utapatikana kwa kila mmoja wetu kuwaunga mkono.
Mkisimama peke yenu hamuwezi kuishinda CCM kwani wana fedha za kumwaga.
Kwa hali ya kisiasa nchini, Chadema imeimarika zaidi ya miaka ilio pita kama 2010, naweza kusema kwamba Chadema jinsi ilivyo imarika ni Mara Mbili au tatu an zaidi ya 2010, hivi tujiulize ccm 2015 itakuwa hai? Kwa vigezo vipi? Hebu tuangalie uchaguzi wa 2010.
MATOKEO RASMI YALIYOTANGAZWA LEO
1. KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO: 96, 933 (1.12%)
2. KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM: 5,276,827 (61.17%)
3. SLAA WILLIBROD PETER/CHADEMA: 2,271,941 (26.34%)
4. LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF: 695,667 (8.067%)
5. RUNGWE HASHIM SPUNDA/NCCR-MAGEUZI: 26,388 (0.31%)
6. MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT/TLP:17,482 (0.20%)-
7. DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA/UPDP: 13,176 (0.15%)
----------------------------------------------
WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA: 20, 137, 303
WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA: 8, 626 (42.64%)
KULA HALALI ZILIZOPIGWA: 8,398,394
KURA ZILIZOHARIBIKA 227,889 (2.64)
Ukiangalia hapo ccm imeanguka asilimia 20 ukilinganisha uchaguzi wa 2000 -2005, hivyo 2015 tunaizika, tuanze kushona sanda, ah haina haja mana hawa wamekula mali za umma sana.
Ukawa oyeee,
Tanganyika kwanza
Zanzibar kwanza,
Shirikisho daima