Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

I was praying for this thing to happen and now it looks like God has listened to my deep prayers.Now CCM have to prepare themselves to face a political juggernaut they could never imagine in 2015,It will be like a swift wind sweeping across the country.It's about time now to send these unscrupulous thugs (CCM) parking.
 
imewahi kuvuja sana hii, hivi mnawajua ccm na serikali? inaweza kuwanunua baadhi yao hata kwa bilioni 5, cha msingi tu wavurugane, au wanaweza kutumia propaganda chafu kuwachonganisha hivi kuna umbali hadi uchaguzi mkuu wa mwakani!!!
 
Chadema imeshawahi kudai CUF chama cha kiislamu na lengo ni kuifanya Tanzania nchi ya kiislamu at the sametime CHADEMA kinasemekana ni cha kikristo na malengo yake ni kuimarisha mfumokristo ukioasisiwa na Mwl Nyerere. Wale walioshutumiana leo wanaungana. Vyema na mimi kutoka ndani ya moyo wangu nawaombea Muungano wenu uwe imara na wenye matunda ili CCM isibwete iongeze bidii kuwasaidia wananchi. Twawatakia kila kher
 
Khaa!!! Kwani huu muungano ni dini gani au kabila gani??
 
Kwa kifupi hilo la kuungana wengi wetu ndicho tunatamani kifanyike, ila wasiwasi je hili litawezekana? Kwani CCM wakilisikia hili wako radhi kuhonga ili hawa jamaa huu ushirikiano usiendelee, anyway kwa sasa UKAWA endeleeni kushirikiana katika hili la katiba, mkilifanikisha hili basi 2015 mkishirikiana njia nyeupe kuigaragaza CCM na ikiwa kinyume chake tu basi itakuwa hatari sana kwa upinzani na demokrasia Tanzania
 
Usiongope, ninakumbukumbu, Mbowe mara baada ya kuingia bungeni, kulikuwa na mtafaruku fulani uliosababishwa na Rashid Hamad, alisema kwa sasa tutaunda peke yetu hadi majeraha yaliyotokea kipindi cha uchaguzi yapone kisha tutaangalia uwezekano wa kuunganisha kambi ya upinzani. Umeyasahau haya maneno?

Nikweli Mbowe alisema hivyo na sababu ni Hamadi Rashidi :my take kufuatana na kauli za Hamadi Rashidi juzi kwenye bunge la katiba .kumnanga Maalimu Seifu mpaka kudai ni msaliti .inajionesha wazi Hamadi Rashidi alikuwa toka siku nyingi alikuwa amenunuliwa na ccm .kuua Cuf na upinzani kwa ujumla .kama ilivyokuwa kwa Zito na chadema ,juzi amejiweka wazi kabisa kwenye bunge la katiba mpaka Mwigulu akampongeza kwa kumpa ile scurf yake bendera ya taifa ,Hamadi Rashidi ni msaliti mkubwa kwa wapenda mabadiliko wote Tanzania
 
SIASA

upinzani.jpg


Viongozi wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKawa). Kutoka kushoto, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu. Viongozi hao wapo katika mkakati wa kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Picha ya Maktaba

Na Neville Meena, Mwananchi

Posted Jumatatu,Aprili28 2014 saa 8:55 AM

KWA UFUPI

  • Mbowe, Mbatia na Profesa Lipumba wazungumza
  • Pia kusimamisha mgombea ubunge mmoja katika majimbo


Dar es Salaam. Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeanza maandalizi ya kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais, gazeti hili limebaini.

Kadhalika, vyama hivyo ambavyo ni Chadema, NCCR Mageuzi na CUF vinakusudia kuwa na mgombea mmoja wa nafasi za wabunge na madiwani, ikiwa ni hatua ya kuzikabili nguvu za chama tawala, CCM.

Habari zilizolifikia gazeti hili zinasema tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo wamekubaliana kuanza mchakato huo na wameandika mapendekezo na kuyapeleka katika sekretarieti za vyama vyao kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi.

Chanzo chetu kilidokeza kuwa kamati ya wataalamu kutoka vyama hivyo tayari imeundwa ili kuandaa taratibu zitakazotumika katika kufanikisha mkakati huo.

Wenyeviti wa vyama hivyo walipoulizwa kwa nyakati tofauti kuhusu mpango huo hawakukubali moja kwa moja, badala yake walisema ni mapema mno kuzungumzia suala hilo katika vyombo vya habari.

Ukawa ni umoja ambao uliviunganisha vyama vyenye malengo yanayofanana katika Bunge Maalumu la Katiba na vimekuwa vikishinikiza kuzingatiwa kwa mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba hususan muundo wa Muungano wenye serikali tatu, tofauti na serikali mbili za sasa.

Umoja huo pia uliwaongoza wajumbe wa Bunge Maalumu ambao ni wanachama wake kutoka nje kususia mchakato wa Katiba Mpya kutokana na kile walichodai kuwa ni kutokuridhishwa na jinsi mambo yanavyokwenda.

Taarifa za kuwapo kwa mpango wa kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao, zimekuja siku chache tangu kufichuliwa kwa mpango mwingine wa kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri kivuli ambalo litawajumuisha wabunge wa vyama hivyo katika Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Baraza la kivuli la sasa linawajumuisha wabunge kutoka Chadema pekee, ambacho kinaunda Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni tangu kuanza kwa Bunge la 10, Novemba 2010.

Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema atapanga upya baraza lake katika siku za mwanzo za Bunge la Bajeti, linalotarajiwa kuanza Mei 6, mwaka huu mpango ambao umeungwa mkono na wenyeviti wa CUF na NCCR Mageuzi.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema uamuzi huo ni hatua kubwa katika ushirikiano na kwamba tayari alikwishawaarifu wabunge wa chama chake wawe tayari kushiriki katika baraza hilo.

Wenyeviti wa vyama


Mbowe alisema: “Hivi sasa suala la sisi kuungana kwa maana ya kuwa na nguvu ya pamoja halikwepeki. Siasa ni dynamic (zinabadilika), fikra za jana ni tofauti na fikra za leo kwa hiyo ni ukweli usiopingika kwamba sisi wapinzani tunahitajiana kwa manufaa ya watu wetu na nchi yetu.”

Hata hivyo, alisema ni mapema kuzungumzia uwezekano wa ushirikiano wao katika vyombo vya habari na kwamba wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi.

Kwa upande wake Profesa Lipumba alisema: “Ningefurahi kama tungeweza kufikia kiwango hicho cha ushirikiano maana kama unavyoona hatuwezi kusonga tusiposhikamana na kuwa wamoja, lakini hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa maana muda mwafaka bado.”

Aliongeza: “Ni kweli Katiba imetuunganisha na huu ni mwanzo mzuri ambao unaweza kutoa mwanga kwamba huko mbele tutakwenda vipi, tumeona kwamba Serikali haina nia njema kwenye suala hili la Katiba, hivyo tukiendelea kutengana hatutaweza kuukabili udhalimu huu.”

Alipoulizwa wataweza kushirikiana vipi na Chadema hali CUF wakiwa washirika wa CCM katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar, Profesa Lipumba alisema mazingira yaliyowafanya kuingia katika ubia huo yanafahamika kwani ulikuwa ni uamuzi wa Wazanzibari kupitia kura ya maoni.

“Kuwamo katika SUK siyo tatizo kwa sasa, siku zilizopita wenzetu walikuwa hawajatuelewa lakini sasa nadhani tunakubaliana kwamba kuwamo kwenye Serikali huko Visiwani siyo kikwazo tena cha kushirikiana na wenzetu,” alisema.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alisema muungano wa vyama hivyo kupitia Ukawa limekuwa darasa kwa viongozi wakuu wa vyama husika kutafakari walikotoka, walipo na wanakokwenda. Hata hivyo, alisema ni mapema sana kuzungumzia suala la kuungana kwao hadharani.

“Tunapata nafasi ya kutafakari na kujifunza kwa kurejea tulikotoka kwa mfano hebu tuifikirie NCCR Mageuzi ya 1995 na ya sasa, CUF ya 2000 na 2005 na CUF ya leo na Chadema ya miaka iliyopita na Chadema ya sasa, haya yote yanatupa fursa ya kutafakari kwa kina tunakotaka kuupeleka upinzani katika nchi yetu,” alisema Mbatia na kuongeza:

“Kwa hiyo suala la kuungana siyo la kujadili kwa sababu ndiyo mahitaji ya sasa, mjadala pengine ni kwamba tunaungana vipi, katika maeneo gani na kwa madhumuni gani?”

Alisema katika siasa, chochote kinaweza kutokea na kwamba mfano mzuri ni Kenya... “Hakuna aliyekuwa akiwaza kwamba leo Rutto (William) angekuwa Makamu wa Kenyatta (Uhuru) kwenye Serikali ya Kenya,” alisema.
 
Chadema imeshawahi kudai CUF chama cha kiislamu na lengo ni kuifanya Tanzania nchi ya kiislamu at the sametime CHADEMA kinasemekana ni cha kikristo na malengo yake ni kuimarisha mfumokristo ukioasisiwa na Mwl Nyerere. Wale walioshutumiana leo wanaungana. Vyema na mimi kutoka ndani ya moyo wangu nawaombea Muungano wenu uwe imara na wenye matunda ili CCM isibwete iongeze bidii kuwasaidia wananchi. Twawatakia kila kher

Mkuu umeongea jambo la msingi sana, sio tu ccm isibweteke bali itikiswe kwa kila ngazi.
Naamini ikiwezekana upuuzi unaondelea Bungeni wa kupigia Makofi kila Pumba utaisha

Hofu yangu ni ghiriba na mbinu za ccm kuuwa upinzani kwa nguvu zote kuanzia propaganda mpaka fedha.

Ila najua kwenye propaganda wanaweza kushinda Hofu yangu ni kwenye Pesa tu kununua Viongozi waandamizi.!
 
Why CCM is doing this? Wamewaamsha walio lala... Sasa CCM inaonekana ITALALA...

Imefanikiwa kuwaunganisha WAPINZANI...
 
Mkuu umeongea jambo la msingi sana, sio tu ccm isibweteke bali itikiswe kwa kila ngazi.
Naamini ikiwezekana upuuzi unaondelea Bungeni wa kupigia Makofi kila Pumba utaisha

Hofu yangu ni ghiriba na mbinu za ccm kuuwa upinzani kwa nguvu zote kuanzia propaganda mpaka fedha.

Ila najua kwenye propaganda wanaweza kushinda Hofu yangu ni kwenye Pesa tu kununua Viongozi waandamizi.!
Hakuna kingozi wa kununuliwa hapo bali naona kuna mapandikizi tu. Walisha nunuliwa kabla hata ya kujiunga
 
Ni wazo zuri sana na ndicho watanzania tulikuwa tunahitaji. Ila mnahitaji kuweka mipango mikakati mizuri ili kuepuka migogoro hapo mbeleni. ALL THE BEST!
Wazo zur, ila nan atakae simama kugombea urais? Maana naona kila mtu hapo anautaka,

M cjaona muungano hapo,ila maluelue!
 
Hakuna kingozi wa kununuliwa hapo bali naona kuna mapandikizi tu. Walisha nunuliwa kabla hata ya kujiunga

Tisikatishane tamaa raia wengi tunaimani na huo umoja, Tumechoka na ghiriba za ccm.
 
CUF ilisha shuka daraja siku nyingi mkuu, CDM ndio wanajaribu wabaki hata wa mwisho ili mradi wawepo ligi ya mwaka kesho.
Muungano huu unapaswa kuwepo lakini hautawezekana. wewe mtoa mada tayari umeshaonesha uroho wa madaraka.
unasema cuf imeshuka daraja na chadema ndio mambo yote, mshabiki wa cuf naye atasema chadema wameishiwa sera sisi cuf ndio mpango mzima.
Ukawa mmeshindwa kabla filimbi haijapulizwa.ukiona watoto wanagombania nyama fahamu wametumwa na wazazi wao.
 
Siasa za nchi yetu kuhusu muungano wa vyama kwa katiba iliyopo n wa kinadharia zaidi.
1: Uwepo wa ruzuku utawagombanisha UKAWA. watazigawanaje ruzuku? Tujadili kidogo.
2: sera za vyama UKAWA ni tofauti kati ya chama kimoja na kingine. Hii ni sawa na muungano wa tanganyika na zanzibar.
3:TUWE NA CHAMA KIMOJA CHA UPINZANI tofauti na hapo ni sawa na muungano wa serikali tatu. CCM,UKAWA na akina MREMA.
 
Back
Top Bottom