Hapa kuna baadhi wamevuta mafuba ya nguvu kuisaliti CDM na wengne wanafuata tu kama bendera maskini.akina SAMSON MWIGAMBA, KITILA MKUMBO, na sasa kuna uwezekano wa ARFI, SHIBUDA, LETICIA na ZITTO KABWE.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa kuna baadhi wamevuta mafuba ya nguvu kuisaliti CDM na wengne wanafuata tu kama bendera maskini.akina SAMSON MWIGAMBA, KITILA MKUMBO, na sasa kuna uwezekano wa ARFI, SHIBUDA, LETICIA na ZITTO KABWE.
wewe u punguwani.... ukawa wamewashika pabayaumoja upi mkuu, labda wajiite jina lingine, UKAWA ni umoja wa KATIBA na siyo umoja wa UCHAGUZI wa wananchi
leo ODM iko wapi sasa?
Habari wakuu,
Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA uliundwa na viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF NA NCCR ndani ya Bunge maalum la Katiba ili kukabilina na nguvu ya kambi ya TANZANIA KWANZA inayoongozwa na CCM. Baada ya umoja huo kutozaa matunda ndani ya Bunge uliamua kususia vikao vya bunge na kuamua kufanyia shughuli zake nje ya Bunge, na pengine tunaweza kusema nje umezaa matunda japo siyo rasmi na siyo matunda ya kisheria. Midahalo toka kwa UKAWA wenyewe, wanaharakati, wana taaluma ya sheria, wajumbe wa iliyokuwa tume ya badiliko ya Katiba na makundi mengine mengi yalioombwa au kudhaminiwa na UKAWA ni miongoni mwa hayo matunda yaliooza mitini kabla hayajakomaa.
UKAWA wakiwa nje ya Bunge wametangaza rasmi kuwa mwaka 2015 watakuwa kitu kimoja katika uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais, eti wanasema mgombea wa chama mshirika wa UKAWA anayekubalika eneo fulani atasimama kwa niaba ya UKAWA. Lakini tujiulize swali moja tu kwamba, lini mgombea wa CUF atakubalika Moshi mjini aachiwe? au lini mgombea wa CHADEMA atakubalika PEMBA aachiwe? au lini mgombea wa NCCR atakosa umaarufu KIGOMA na nafasi hiyo asimame wa CHADEMA? Jibu ni hakuna, na kwa maana hiyo mambo yatakuwa ni yale yale ya ZAMANI, yaani CHADEMA, CUF na NCCR kila mmoja atashinda aliko maarufu.
Hoja yangu kubwa katika mada hii, NI NANI ANAPASWA KUJIFICHA KWENYE HIKI KIVULI CHA UKAWA KWENYE UCHAGUZI WA 2015?.
Binafsi naona atakaeathirika endapo UKAWA watashindwa kutimiza azma yao ya kuwa kitu kimoja 2015 ni CHADEMA kwa sababu zifuatazo:
1. Ni ukweli usiopingika kuwa wazo la kuundwa kwa UKAWA ni la CHADEMA na liliwaijia ili kupisha upepo uliokuwa ukivuma ndani ya chama chao, upepo wa vurugu zilizopelekea kuondokewa na watu wao muhimu kama akina SAMSON MWIGAMBA, KITILA MKUMBO, na sasa kuna uwezekano wa ARFI, SHIBUDA, LETICIA na ZITTO KABWE.
2. CUF na NCCR wao wamekuwa wakikua siku hadi siku wakati CHADEMA wanaporomoka na ushahidi ulio wazi ni bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopita, Wabunge wa NCCR mageuzi kama akina MACHALI, KAFURILA na wengine waling'ara huku wale wa CHADEMA wakipiga majungu tu
3. CHADEMA bado wana OMBWE la kitendawili kilichokighubika chama, kitendawili cha Uchaguzi wa chama ngazi ya Taifa, hakuna anayejua kama kitendawili kitatenguliwa au la? Hii ni sababu nyingine ya CHADEMA kuendelea kung'ang'ania UKAWA wasirudi bungeni kwa vile wanajua wakitimba tu kule upepo wa ndani ya Chama chao utaanza kuvuma tena kwa sababu ya UKAWA na bunge maalum la katiba yatakuwa yamekwisha.
Na kweli, umoja wa Katiba ya WANANCHI na Uchaguzi wapi na wapi?
Mimi ni CCM damu, ila
linapokuja suala la maslahi kwa Taifa huwa CCM huwa inakuwa nambari
MBILI. Manake tulio wengi huwa tunachezeshwa ngoma tusiyoijua na wapenda
madaraka ili waendelee kututawala. Mzee Sinde Warioba pamoja na makada
wenzetu wa CCM ambao waliteuliwa kukusanya maoni kwenye tume ya
mabadiliko ya katiba walitanguliza Utanzania kwanza na kuacha UCCM kando
na ndio maana wakaja na mapendekezo yaliyotokana na watanzania pamoja
na kuangalia mahitaji ya sasa kwa Watanzania, cha ajabu wapenda Uraisi
wakaona mapendekezo haya ya watanzania yanaweza yakawa kikwazo cha wao
kusaka uraisi.
Ushauri wangu ni kwamba ili kazi iliyofanywa na tume ya Warioba ya
kutuletea katiba mpya ambayo ndio mkataba kati ya watawala na watawaliwa
na hivyo kuwa msingi mkuu wa maendeleo yetu, hivyo ningewashauri UKAWA
waachane na kusaka uraisi na kumshawishi Mzee Warioba Akubali kusimama
kama mgombea kupitia mgombea atakayeteuliwa na ukawa na hapo ndipo
ukombozi wa Mtanzania utapatikana kwa kila mmoja wetu kuwaunga mkono.
Mkisimama peke yenu hamuwezi kuishinda CCM kwani wana fedha za
kumwaga.
Mimi ni CCM damu, ila linapokuja suala la maslahi kwa Taifa huwa CCM huwa inakuwa nambari MBILI.
Mimi ni CCM damu, ila linapokuja suala la maslahi kwa Taifa huwa CCM huwa inakuwa nambari MBILI. Manake tulio wengi huwa tunachezeshwa ngoma tusiyoijua na wapenda madaraka ili waendelee kututawala. Mzee Sinde Warioba pamoja na makada wenzetu wa CCM ambao waliteuliwa kukusanya maoni kwenye tume ya mabadiliko ya katiba walitanguliza Utanzania kwanza na kuacha UCCM kando na ndio maana wakaja na mapendekezo yaliyotokana na watanzania pamoja na kuangalia mahitaji ya sasa kwa Watanzania, cha ajabu wapenda Uraisi wakaona mapendekezo haya ya watanzania yanaweza yakawa kikwazo cha wao kusaka uraisi.
Ushauri wangu ni kwamba ili kazi iliyofanywa na tume ya Warioba ya kutuletea katiba mpya ambayo ndio mkataba kati ya watawala na watawaliwa na hivyo kuwa msingi mkuu wa maendeleo yetu, hivyo ningewashauri UKAWA waachane na kusaka uraisi na kumshawishi Mzee Warioba Akubali kusimama kama mgombea kupitia mgombea atakayeteuliwa na ukawa na hapo ndipo ukombozi wa Mtanzania utapatikana kwa kila mmoja wetu kuwaunga mkono.
Mkisimama peke yenu hamuwezi kuishinda CCM kwani wana fedha za kumwaga.