Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Demokrasia si utitiri wa vyama vya upinzani!

Nchi maskini kama yetu inahitaji chama tawala imara lakini vile vile upinzani ulio imara ili kuiletea nchi na wananchi wote maendeleo!

Najua CCM hawataipenda hatua hii ya upinzani kuunganisha nguvu lakini WANANCHI WAMECHOKA ADITHI ZA CCM!

WANANCHI WANATAKA MABADILIKO! WAMECHOKA KUONGOZWA NA WATU WALE WALE WA FAMILIA ZILE ZILE KWA STAHILI ILE ILE YA MIAKA ILE YA ZAMANI!
 
- Lipumba adai Katiba imewaunganisha wapinzani na kuongeza kuwa huu ni mwanzo mzuri unaoweza kutoa mwanga wa nini kitatokea mbeleni.

- Mbatia asisitiza kuwa suala la wapinzani kuungana si la kujadili maana ndiyo mahitaji ya wananchi kwa sasa!
hili nimelipenda zaidi, kwenye Majonzi au Furaha kama misiba na harusi ndipo mahali pekee ambapo huwakutanisha na kuwapatanisha hata Ndugu wa damu waliokorofishana au kutengana miaka nenda rudi kwa sababu mbalimbali. Yawezekana haya yote ni mipango ya Mola - who knows!!

CUF, CDM and NCCR to sit on the same table is one step forward. Inapendeza sana.
 
Siyo utaratibu ngeni kuona vyama vya siasa vinamuunga mkono mgombea moja. CHADEMA walishawahi kumwunga mkono Mrema mwaka 1995, na mwaka 2000 walimwunga mkono Lipumba.

Kumwondoa adui ccm kunahitaji mshikamano....... Big up!
 
Mungu ibariki Tanganyika Mungu bariki Ukawa.
 
Hahahahaaa MWENYEZI MUNGU naomba unijaalie afya njema niuone mwaka 2015 niwaangalie wale wakaanga sumu watakavyo tapatapa juu ya lindi la ufisadi, uwongo, ushirikina, uzandiki na mengineyo meengi watakavyo shindwa na kulegea nyumba zetu za masaki obay na msasani walizomegeana kiuswahiba zikirudi mikononi mwa wananchi wanyonge MUNGU ibariki Tanzania.
 
Wakiwaingiza Mrema, Mziray na Cheyo wajue wamekwisha!!!!!
 
Maendeleo yapi unayaongelea kufungua viwanda vya gongo.

Yaah! kwa kuwa jina la gongo linakupa shida tulaiita "Tanzano". au vipi? kuwa mzalendo mkuu kunywa vya kwetu product of Tanganyika, achana na kuwa soko la gongo (whisky) kutoka magharibi.
 
Hili jambo ni gumu kwa waafrika. Wengi tunaweka mslahi yetu binafsi mbele.

Mfano, uchaguzi mkuu uliopita Lipumba alikiri kumpigia Jakaya Kikwete kampeni kwa maslahi yake binafsi.
 
Mwisho wa maintarehamwe, majambazi,waizi,wehu,majangiri,wauza.
 
Binafsi nimefurahi kwa taarifa ya Wapinzani kuungana ili wasimamishe mgombea mmoja wa Urais na ubunge katika uchaguzi wa 2015,katika utafiti mdogo niliofanya kupitia tume ya Taifa ya uchaguzi,(The National Electrol Commission of Tanzania - Homepage) ni kuwa upinzani walipoteza majimbo mengi kutokana na kukosa umoja.

Yapo majimbo yasiyipungua hamsini ambayo upinzani uliongoza lkn ccm walishinda kwa ushindi mwembamba kutokana na wapinzani kuzigawa kura.

Mfano ni majimbo matatu ya Dar es Salaam,ya Kinondoni,kigamboni na segerea,

Pia ukienda mikoani ndio utalia kwa jinsi upinzani walivyokosa umoja.


Binafsi nashauri kuwa vyama vya CUF,CHADEMA NA NCCR

Wakae meza moja na kugawana majimbo kwa kuzingatia uwiano na kukubalika kwa vyama.

katika mgao wa majimbo kusiwepo na mmoja anaekiona chama chake ni kikubwa kuliko vyama vingine.

kwa umoja huo kila chama kinaweza pata majimbo yasiyopungua 80,kisha kila kiongozi kushiriki kumnadi mgombea wa upinzani na kumuombea kura kwa wapinzani ili kuongeza nguvu ya kura na mapambano Bungeni.

Kwa maoni yangu,Hata kama ccm watabaki na Urais,kama bunge litakuwa chini ya upinzani ,ccm haitakuwa na nguvu tena ya kukejeli hoja za wananchi kwa kuwa upinzani utakuwa na nguvu ya maamuzi.

pia wingi wa wapinzani bungeni utawasaidia kumpata Spika wa upinzani atakae tenda haki na kuruhusu hoja za kuisomamia serikali kikamilifu kuliko hali ilivyo sasa .

Chande chonde Prof Lipumba,Mh.Mbowe,Mh Mbatia,Zitto Kabwe.

Hakikisheni mnakubaliana ktk hili ili kukomesha utawala wa kuwa na bunge la ccm,

Ccm watatumia kila hila kuwagawa ili kuhalisha kubaki madarakani.

Nawaomba msigawanyike,muendelee kuwa wamoja ili kulikomboa Taifa hili kutoka mikononi mwa wakoloni weusi.

Kubalianeni kugawana madaraka,Kwa mmoja wenu mwenye sifa na ushawishi kwa wananchi qa rika zote kupeperusha bendera ya upinzani,huku wengine wakipewa ahadi za uwaziri mkuu na mgawanyo sawa wa wizara endapo mtashinda kuongoza serikali.


Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko lkn wamekosa mtu wa kuwaunganisha.
 
Hakika hiki wananchi tulikuwa tunakisubiria kwa hamu sana!!!!

Ila ktk suala la ugombea ili kuondoa mkanganyiko, mgombea asiwe kati ya hawa +Dr. Nadhani Lisu ata-fit sana.

Kila la kheri NCCU (NCCR+CHADEMA-CUF=UNION)
 
Dar es Salaam. Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeanza maandalizi ya kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais, gazeti hili limebaini.

Kadhalika, vyama hivyo ambavyo ni Chadema, NCCR Mageuzi na CUF vinakusudia kuwa na mgombea mmoja wa nafasi za wabunge na madiwani, ikiwa ni hatua ya kuzikabili nguvu za chama tawala, CCM.

Habari zilizolifikia gazeti hili zinasema tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo wamekubaliana kuanza mchakato huo na wameandika mapendekezo na kuyapeleka katika sekretarieti za vyama vyao kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi.

Chanzo chetu kilidokeza kuwa kamati ya wataalamu kutoka vyama hivyo tayari imeundwa ili kuandaa taratibu zitakazotumika katika kufanikisha mkakati huo.

Wenyeviti wa vyama hivyo walipoulizwa kwa nyakati tofauti kuhusu mpango huo hawakukubali moja kwa moja, badala yake walisema ni mapema mno kuzungumzia suala hilo katika vyombo vya habari.

Ukawa ni umoja ambao uliviunganisha vyama vyenye malengo yanayofanana katika Bunge Maalumu la Katiba na vimekuwa vikishinikiza kuzingatiwa kwa mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba hususan muundo wa Muungano wenye serikali tatu, tofauti na serikali mbili za sasa.

Umoja huo pia uliwaongoza wajumbe wa Bunge Maalumu ambao ni wanachama wake kutoka nje kususia mchakato wa Katiba Mpya kutokana na kile walichodai kuwa ni kutokuridhishwa na jinsi mambo yanavyokwenda.

Taarifa za kuwapo kwa mpango wa kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao, zimekuja siku chache tangu kufichuliwa kwa mpango mwingine wa kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri kivuli ambalo litawajumuisha wabunge wa vyama hivyo katika Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Baraza la kivuli la sasa linawajumuisha wabunge kutoka Chadema pekee, ambacho kinaunda Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni tangu kuanza kwa Bunge la 10, Novemba 2010.

Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema atapanga upya baraza lake katika siku za mwanzo za Bunge la Bajeti, linalotarajiwa kuanza Mei 6, mwaka huu mpango ambao umeungwa mkono na wenyeviti wa CUF na NCCR Mageuzi.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema uamuzi huo ni hatua kubwa katika ushirikiano na kwamba tayari alikwishawaarifu wabunge wa chama chake wawe tayari kushiriki katika baraza hilo.

Wenyeviti wa vyama

Mbowe alisema: "Hivi sasa suala la sisi kuungana kwa maana ya kuwa na nguvu ya pamoja halikwepeki. Siasa ni dynamic (zinabadilika), fikra za jana ni tofauti na fikra za leo kwa hiyo ni ukweli usiopingika kwamba sisi wapinzani tunahitajiana kwa manufaa ya watu wetu na nchi yetu."

Hata hivyo, alisema ni mapema kuzungumzia uwezekano wa ushirikiano wao katika vyombo vya habari na kwamba wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi.

Kwa upande wake Profesa Lipumba alisema: "Ningefurahi kama tungeweza kufikia kiwango hicho cha ushirikiano maana kama unavyoona hatuwezi kusonga tusiposhikamana na kuwa wamoja, lakini hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa maana muda mwafaka bado."

Aliongeza: "Ni kweli Katiba imetuunganisha na huu ni mwanzo mzuri ambao unaweza kutoa mwanga kwamba huko mbele tutakwenda vipi, tumeona kwamba Serikali haina nia njema kwenye suala hili la Katiba, hivyo tukiendelea kutengana hatutaweza kuukabili udhalimu huu."

Alipoulizwa wataweza kushirikiana vipi na Chadema hali CUF wakiwa washirika wa CCM katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar, Profesa Lipumba alisema mazingira yaliyowafanya kuingia katika ubia huo yanafahamika kwani ulikuwa ni uamuzi wa Wazanzibari kupitia kura ya maoni.

"Kuwamo katika SUK siyo tatizo kwa sasa, siku zilizopita wenzetu walikuwa hawajatuelewa lakini sasa nadhani tunakubaliana kwamba kuwamo kwenye Serikali huko Visiwani siyo kikwazo tena cha kushirikiana na wenzetu," alisema.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alisema muungano wa vyama hivyo kupitia Ukawa limekuwa darasa kwa viongozi wakuu wa vyama husika kutafakari walikotoka, walipo na wanakokwenda. Hata hivyo, alisema ni mapema sana kuzungumzia suala la kuungana kwao hadharani.

"Tunapata nafasi ya kutafakari na kujifunza kwa kurejea tulikotoka kwa mfano hebu tuifikirie NCCR Mageuzi ya 1995 na ya sasa, CUF ya 2000 na 2005 na CUF ya leo na Chadema ya miaka iliyopita na Chadema ya sasa, haya yote yanatupa fursa ya kutafakari kwa kina tunakotaka kuupeleka upinzani katika nchi yetu," alisema Mbatia na kuongeza:

"Kwa hiyo suala la kuungana siyo la kujadili kwa sababu ndiyo mahitaji ya sasa, mjadala pengine ni kwamba tunaungana vipi, katika maeneo gani na kwa madhumuni gani?"

Alisema katika siasa, chochote kinaweza kutokea na kwamba mfano mzuri ni Kenya... "Hakuna aliyekuwa akiwaza kwamba leo Rutto (William) angekuwa Makamu wa Kenyatta (Uhuru) kwenye Serikali ya Kenya," alisema.

Source: Mwananchi
 
Hahahahahaaaaaa, CHADEMA kwishney. Ukiona chama kinakimbilia kuomba msaada wa vyama vingine ujue ndo mwisho wake. Ila watambue kuwa nguvu ya CCM ni mara 100 ya nguvu ya UKAWA
 
T2015CCM sijui wewe ni HE/SHE?? hivi huwa unalipwaaaaaaaaaaaa kiasi gani?? maana inaonekana kazi yako ni kushinda JF.
Ngoja nikuache uendeleee na kibarua chako.
 
upinzani.jpg


Hicho ndicho tunachotaka kuungana kuwa na nguvu za kutosha. Kura za CUF kutoka Zanzibar zitajaza pengo ambalo huwa linaibuka bara, haba na haba hujaza kibaba.

CCM imekuwa ikitumia mbinu za kizamani divide and rule, leo hao UKAWA shughuli za Katiba mpya zimewafungua upeo zaidi na kusoma janja ya CCM ya kizamani ya divide and rule ambayo itabaki kuwakumbatia vyama vidogovidogo visivyo na wafuasi wengi wakati vyama vikuu vitatu vya upinzani vikiungana.
 
Hahahahahaaaaaa, CHADEMA kwishney. Ukiona chama kinakimbilia kuomba msaada wa vyama vingine ujue ndo mwisho wake. Ila watambue kuwa nguvu ya CCM ni mara 100 ya nguvu ya UKAWA
upinzani.jpg


Mnaogopa kuunganisha nguvu, nilipata kuongea huko nyuma kwamba kilichotokea Kenya Mwai Kibaki kuunganisha nguvu za upinzani kuiondoa KANU madaraka kitatokea Tanzania, leo tunasikia tamko lao.
 
Wote ni waroho wa madaraka. Suala la katiba mpya wamelimalizaje?
 
upinzani.jpg


Mnaogopa kuunganisha nguvu, nilipata kuongea huko nyuma kwamba kilichotokea Kenya Mwai Kibaki kuunganisha nguvu za upinzani kuiondoa KANU madaraka kitatokea Tanzania, leo tunasikia tamko lao.
Hahahahahaaaa! Hapo mbunge mmoja ni wa CCM, wengine ni rejected
 
Back
Top Bottom