Binafsi nimefurahi kwa taarifa ya Wapinzani kuungana ili wasimamishe mgombea mmoja wa Urais na ubunge katika uchaguzi wa 2015,katika utafiti mdogo niliofanya kupitia tume ya Taifa ya uchaguzi,(
The National Electrol Commission of Tanzania - Homepage) ni kuwa upinzani walipoteza majimbo mengi kutokana na kukosa umoja.
Yapo majimbo yasiyipungua hamsini ambayo upinzani uliongoza lkn ccm walishinda kwa ushindi mwembamba kutokana na wapinzani kuzigawa kura.
Mfano ni majimbo matatu ya Dar es Salaam,ya Kinondoni,kigamboni na segerea,
Pia ukienda mikoani ndio utalia kwa jinsi upinzani walivyokosa umoja.
Binafsi nashauri kuwa vyama vya CUF,CHADEMA NA NCCR
Wakae meza moja na kugawana majimbo kwa kuzingatia uwiano na kukubalika kwa vyama.
katika mgao wa majimbo kusiwepo na mmoja anaekiona chama chake ni kikubwa kuliko vyama vingine.
kwa umoja huo kila chama kinaweza pata majimbo yasiyopungua 80,kisha kila kiongozi kushiriki kumnadi mgombea wa upinzani na kumuombea kura kwa wapinzani ili kuongeza nguvu ya kura na mapambano Bungeni.
Kwa maoni yangu,Hata kama ccm watabaki na Urais,kama bunge litakuwa chini ya upinzani ,ccm haitakuwa na nguvu tena ya kukejeli hoja za wananchi kwa kuwa upinzani utakuwa na nguvu ya maamuzi.
pia wingi wa wapinzani bungeni utawasaidia kumpata Spika wa upinzani atakae tenda haki na kuruhusu hoja za kuisomamia serikali kikamilifu kuliko hali ilivyo sasa .
Chande chonde Prof Lipumba,Mh.Mbowe,Mh Mbatia,Zitto Kabwe.
Hakikisheni mnakubaliana ktk hili ili kukomesha utawala wa kuwa na bunge la ccm,
Ccm watatumia kila hila kuwagawa ili kuhalisha kubaki madarakani.
Nawaomba msigawanyike,muendelee kuwa wamoja ili kulikomboa Taifa hili kutoka mikononi mwa wakoloni weusi.
Kubalianeni kugawana madaraka,Kwa mmoja wenu mwenye sifa na ushawishi kwa wananchi qa rika zote kupeperusha bendera ya upinzani,huku wengine wakipewa ahadi za uwaziri mkuu na mgawanyo sawa wa wizara endapo mtashinda kuongoza serikali.
Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko lkn wamekosa mtu wa kuwaunganisha.