Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
CCM MAJI YA SHINGO,AIBU YATAWALA, BUNGE LAVUNJIKA KIAINA
WAGAWE UWATAWALE, MBINU INAYOPIKWA DHIDI YA UKAWA
UKAWA KUREJEA MAKOSA YA SIKU ZA NYUMA (JUISI NA CHAI IKULU)
Sehemu ya I
Ndugu wana wanajmvi na wanaduru
Si mara moja au mbili tumeonyesha mwisho wa BMLK(Bunge maalumu la katiba) kutokana na hila zinazoendelea.Wiki iliyopita tulisema ndani ya wiki mbili bunge litavurugika.
Ukweli ni siku 10 tangu tuyaseme.
Kuondoka kwa wajumbe wa UKAWA ndani ya BMLK ni mwiba kwa CCM.
Chama tawala kilikuwa mbioni kuingiza rasimu yao ya mafichoni, soma hapa.... ili ipate ridhaa ya wajumbe kutoka uwakilishi wote hivyo kujenga uhalali.
Rasimu ya CCM iliyoandikwa na kikundi cha watu wachache inaongozwa na Samwel Sitta,soma hapa...... .
Mbinu zilianza ndani ya bunge la JMT kupitisha miswada kibabe kukiwa na mkono mkubwa wa Rais wa JMT. Mbinu zikahamia bungeni, Sitta akapewa jukumu la kusimamia rasimu ya CCM kwa malengo maalumu na dhamira maalumu na wala si wanachama wa CCM.
Ili kuhakikisha rasimu ya CCM inafanikiwa wabunge wa CCM wakakalishwa kitako na kufundishwa nini cha kusema. Hawakupewa nafasi ya kutumia akili zao, wanachotakiwa ni kuimba tu, ndivyo ilivyo sasa bungeni.
Mbinu ya kuhalalisha rasimu ilichomekwa katika kamati za CCM bungeni.
Huko 2/3 ikakosekana. Mh Samwel Sitta akairudisha mbinu hiyo kwa kujadili rasimu kifungu 1 na 6 ndani ya bunge. Mh Sitta alikuwa na sababu, na alifanya hivyo ili kupata 2/3 kwa nguvu.
Katika kamati 2/3 ni ngumu kupatikana, kwa wingi ndani ya bunge na ile 'kamba' ya kura ya wazi 2/3 ingepatikana. Hilo ndilo Sitta, mwakilishi wa kundi la rasimu ya CCM alilolenga.
Sitta akiwa ametumwa na CCM alipanga waongeaji, wengine wakiwakilisha maoni yao na si ya kamati kama alivyofanya Ummy Mwalim.
Kwa kuelewa mpango Mzima Makamu mwenyekiti akaruhusu watu waeleze maoni yao na si ya kamati wakitumia neno 'walio wengi' bunge likachafuka
'Walio wengi' ilikusudia kuubabaisha umma kuwa suala zima linaungwa mkono na wengi.
Hili ni suala la katiba, kinachoangaliwa si wingi bali hoja na mantiki.
Tunakumbuka mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa 'walio wengi' walikataa.
Busara zikaelekeza kuwa hoja na nyakati ni muhimu kuliko walio wengi.
Haiwezekani kuwepo 'walio wengi' tukijua CCM iliwafungia na kuwalazimisha wawe 'wengi'
Mbunge Lembeli alipotoa maoni yake, CCM mkoa ikamshukia kwasababu alikwenda kinyume na 'mafunzo' yaliyoamuliwa na chama. Wapi hoja ya walio wengi inapopatikana?
sehemu ya II bunge linakokotwa kuepeuka aibu
Tutaendelea.........
https://www.jamiiforums.com/great-t...shaji-na-kiwewe-cha-kuzinduka-tanganyika.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...a-katiba-je-katiba-itatokana-na-wananchi.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...-gharama-za-muungano-siri-isiyozungumzwa.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...ba-ya-jk-kuzindua-bunge-maalum-la-katiba.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...asa-vijana-katiba-mpya-na-kiu-ya-uongozi.html