Mkuu wangu nashindwa kukujibu maana jibu umeliweka wewe mwenyewe. sasa ikiwa ktk muungano huu wa serikali 2 kuna serikali 3 unaitaka serikali ya 3 ili iweje? hapo ndipo mnaponishinda maana sioni kuwepo kwa jina la Tanganyika kutabadilisha mfumo wa uliopo ama kuondoa MAPUNGUFU ila yawezekana ikapoza kero zilizopo. Nimesema sana na nitarudia kusema ya kwamba nyote mnaopendekeza serikali hizi iwe 1, 2 au 3 mnafanya hivyo kwa kutazama njia ya kuondoa kero zilizopo wakati kero ni matokeo ya mahitaji kupitiliza. Kama vile kukosekana kwa barabara nzuri za Usafiri Dar, serikali na Manispaa imeamua kuwafungia Daladala na Boda boda kutofika mjini wakati ukweli ni kwamba foleni za magari bado zitaendela kuwepo na njia pekee ni kuongeza na kupanua mabarabara ya mjini sii kuongeza usafiri wa mabaus wala kuwafutia watu liseni za biashara wasifike mjini.Mkuu Mchambuzi, inaonekana pamoja na usomi wake wote, Mkandara hajui hata mfumo tulio nao hivi sasa unafanyaje kazi. Ngoja nimpe A,B,C ya tunaouita mfumo wa serikali mbili ndani ya nchi mbili...tunazo mamlaka tatu;
Mtizamo wa watu kama Mkandara naufananisha na msimamo wa Wamarekani wasiompenda Obama. Utawakuta wakipinga kinachoitwa Obama care huku wakiisifia ACA, Affordable Care Act bila kujua ni kitu hicho hicho. Saha hapa mtu anakiri kwamba mamlaka ziko tatu lakini hapo hapo anapinga serikali tatu bila kujua kwamba ni kitu kile kile. Inaonekana wasichotaka kukisikia ni maneno serikali ya Tanganyika na wakati huo huo hawaoni tatizo kuitaja na kuitetea serikali ya Zanzibar; eti serikali ya Zanzibar ikae na serikali ya Muungano ili waongee nini? Mambo ya Zanzibar, ya Muungano ama ya Tanganyika? CCM ilijiunga na CUF kuunda serikali lakini leo Chadema ikijiunga na CUF hiyo hiyo kudai katiba ya wananchi, huo umoja unatiliwa shaka na kuhusishwa na ugaidi/usultani! Akili gani hizi?
- Kuna mamlaka inayosimamia mambo ya Muungano.
- Kuna mamlaka inayosimamia mambo yasiyo ya Muungano kwa Zanzibar
- Kuna mamlaka inayosimamia mambo yasiyo ya Muungano kwa (Tanganyika) Tanzania bara.
Mkandara, ukweli ni kwamba hapa hatuna Muungano, tuna shirikisho, period. Hatuwezi kuwa na Muungano tukawa na serikali mbili, tatu, nne, tano na kuendelea! Matapeli wa kisiasa ndio wanataka watuaminishe kuwa tuna Muungano wa serikali mbili wapate pa kuficha uovu wanaoutendea Tanganyika, wapate kichaka cha kufujia rasilimali za Watanganyika na wapate kambi ya kuendeshea ufisadi kwa kung'ang'ania madaraka. Sasa ilichofanya Tume ni kuuambia utawala kuwa mbinu zao chafu wananchi wamezishtukia, Watanganyika kama walivyo Wazanzibar wamechoka kudhulumiwa kwa kivuli cha Muungano. The good news kwao ni kwamba wapo watu kama wewe, tena wasomi, mko tayari kutumiwa/kutumika kutetea hiyo hali; the bad news kwenu ni kwamba wananchi walio wengi wameamka na kwa sauti kubwa wamesema imetosha.
Sipingi kuwa na serikali 1 maana huko ndiko tulikotakiwa kwenda lakini sidhani kama ni suluhisho ikiwa bado KATIBA yetu imebeba kwa sehemu kuwa ITIKADI ya siasa ya Chama cha MAPINDUZI. Hofu ya CCM sio ujio wa serikali 3 kwa maana hii isipokuwa wanahofia kupoteza nguvu yao Zanzibar kwa chama cha CUF ambacho wao wanajua fika kina wafuasi wengi wa HIzbu, hivyo CDM mnapoungana na CUF pasipo kujua wenzenu wanapigania nini ktk mfumo huu ni kujiweka ktk nafasi mbaya sana kisiasa. Na kibaya zaid nasikia UKAWA watakuwa Zanzibar kuwashtakia wananchi badala ya kundi hili kuendelea na mjadala bungeni kutushawishi sisi wananchi ili kesho katiba itakapo letwa mbele yetu tuikatae!
Kinachoendelea Bungeni ni sawa na Bunge la Taifa yaani watu wanabishana pasipo kujua dhumuni la Ubishi wao. Pale wanatakiwa kutushawishi sisi wananchi ambao ndio sauti ya mwisho. Kupiga kwao kura haina maana ndio mwisho wa utunzi wa Katiba kwa sababu ni lazima sisi wananchi tuikubali katiba hiyo. Hivyo kama wananchi wanaitaka serikali 3 mbele ya utunzi wa Katiba wataikataa katiba ilopitishwa na Wajumbe wengi wa CCM.