Ni dhahiri kwamba mchakato wa katiba umekwama. Tutafika uchaguzi mkuu ujao bila ya katiba mpya. Huu ni msiba mkubwa sana kwa CCM, lakini kutokana na UKAWA kukosa umakini, msiba huu unaweza kuwa mkubwa kwa upinzani badala ya ccm.
Nguruvi3 alijadili hili vyema sana. Tunabaki jiuliza - nini kinaendelea ndani ya UKAWA????
Upinzani una karata kubwa sana ya kutumia kisiasa iwapo uchaguzi ujao utakuja bila ya katiba au na katiba ya ki-ccm. Hoja za upinzani ni rahisi na za wazi:
*Wangepita mijini na vijijini kuwaambia wananchi kwamba mmetaka katiba mpya lakini CCM wamewakatalia kwa kutumia wingi wao bungeni.
*CCM na makada wake hawapo tayari kuheshimu maoni ya raia.
Upinzani ulitakiwa watumie ripoti ya tume na kusema yale ndio maoni ya wananchi.
Baada ya hapo, upinzani ungewaomba wananchi kura kwa ahadi kwamba wakipata madaraka, watatekeleza maoni yao bila ya hila wala ghiriba.
Upinzani ukifanya kazi nzuri, sioni jinsi gani ubabe wa ccm utaendelea kwa muda. Wananchi wengi sasa hawapo tayari kuendelea kuwa chini ya katiba isiyowatendea haki na ambayo ina halalisha ukandamizaji wa wananchi kwa wazi kabisa.
Upinzani ulitakiwa uwe busy kuwahakikishia wafanyakazi serikalini kupata mafao ya kwa wakati muafaka;
Ahidi wananchi usimamizi mzuri wa rasilimali zao na kodi zao;
Kuboresha huduma zote za kijamii, hasa kulenga watoto, kina mama, na vijana.
Kutoa ujira wa haki na kwa mujibu wa sheria, sio kwa fadhila, au huruma ya watawala.
Upinzani ungekuwa busy kuelezea ufisadi ulivyo kithiri serikalini na jinsi gani serikali mbili zinavyofanikisha hili - EPA, Radar, mabilioni ya uswisi. Hapa wangetaja jina moja hadi jingine la mamilionea wa uswisi kwa mgongo wa walala hoi. Wangetaja wenye akaunti, wadhamini wanavyoonekana kwenye nyaraka za benki, nafasi yake kwenye uongozi, hata kama ni mstaafu etc etc.
Upinzani ungemwaga hadharani nyaraka za fedha zilizoibiwa na kupelekwa nje ya nchi. Mali za viongozi dubai, london, capetown etc. Wangeonyesha mali na fedha hizi zimetokana na miradi gani ya fedha za umma. Wangeonyesha taifa limepata hasara kiasi gani kwa kurudhia mikataba ya kinyonyaji.
Yote haya yange set tone ya haja ya katiba mpya, lakini pia madudu ambayo upinzani utaenda kuyafanyia kazi "kimfumo", huku upinzani ukiahidi kuandaa tume itakayopita nchi nzima kutafuta maoni ya wananchi juu ya Dira mpya ya taifa iweke vipaumbele gani. Dira ikipatikana, iwe implemented in 3 years. Na kazi za serikali zipimwe kwa utekelezaji wa dira hiyo. Hapo tutakuwa tumepata taifa jipya lenye kufufua matumaini ya wali wengi.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums