Ukisema hakuna Ukawa hapa una maana gani? sio wewe ulo quote maandishi yangu na kusema nina wasuppoort CCM kwa S2? sasa iweje unaanza kukataa maneno yako mwenyewe na kuingiza hoja ambayo haihusiani. Matatizo yako na hao kina
Mdondoaji takashi GHIBUU hayahusiani na mjadala wetu. Laukama ungejua mfumo wa S2 tusingekuwa hapa kwani yaonyesha wazi unatoka kapa na kwa bahati mbaya wewe mwenyewe una majibu yako hutaki kufundishwa ama kuambiwa nje ya majibu ulojitungia kichwani. Hivyo sitoweza kuendelea kuzungumzia kitu kile kile day in day out! - nimechoka.
Labda nikuulize wewe na hao UKAWA. Ni nani alowapa dhamana ya kuandika mkataba mpya wa Muungano wa JMT! Hizi serikali 3 zinahusiana vipi na Katiba mpya tuloiomba sisi wananchi hadi wakajikabidhi mamlaka ya kujadili na hata kuitaka hati ya Muungano maana yaonyesha hawaamini kuwepo kwa Muungano halali lakini wapo mbele kupokea posho za kuandika katiba ya JMT, Jamhuri wasioamini kuwa halali! Hii mijitu imesoma na kujifanya mianasiasa iloapa kuulinda Muungano usokuwa halali mioyoni mwao. Ujinga huu hata uwe na degree 10 hautasaidia kitu maana watu kama hawa wamefungwa macho na masikio yao japo wanaona na kusikia!
Ebu tuambie, kati ya hao wajumbe wa baraza maalum la Katiba ni kina nani wanawakilisha Upande wa Tanganyika au Zanzibar ktk swala hili la Muungano. Ni nani kati yao ana utaalam na uzoefu wa kuandika Katiba maana nijuavyo hakuna hata mmoja wao alowwahi kuandika haya sura mojawapo leo wapo mbele kudai muungano wa shirikisho!
Huyo Warioba na kundi lake nani kawapa dhamana ya kuuliza juu ya Muungano wetu! unapotaka kusuluhisha wana ndoa unaweza vipi kuanza na kuuliza cheti cha ndoa? na ili iweje? Ujinga huu mkuu wangu sitoukubali na sitouendekeza maana hao jamaa ulowataja ndio kila siku waliokuwa wakisema Muungano wetu sio halali, na sasa wewe umeungana nao japo zamani ulipingana nao. Huoni kama umevutwa walipotaka kukuweka na ukabakia uchi wa nyama...
Mkuu Mkanadara kama unanisoma vema, mimi sizungumzii Ukawa leo nilishazungumzia kabla ya kuwepo kwakwe.
Nazungumzia UKAWA kama ninavyozungumzia vyama vyote. Hilo naomba ulielewe.
Nimeweka uzi na kusema watarudia juisi ya maembe. Nikaonyesha jinsi walivyobofoa siku za mwanzo na huko wanakotarajia.
Nimesimama kutetea Tanganyika kabla ya Mbatia hajateuliwa. Ndiyo maana nasema mengi unayoyaona mbona tuliyashayazungumza.
Nikutoe wasi wasi, muungano unaousema ni halali si halali. Uhalali ni miaka 50 tu,kisheria kuna matatizo mengi.
Uhalali umeondolewa kabisa na katiba ya SMZ ya 2010 iliyomsimika Amir jeshi na nchi yetu kuwa na Maamir jeshi 2.
Ninaweza kuwa sielewei ,ni mapungufu ya mwanadamu.Tupe mfano, ni taifa gani lina Maamir Jeshi 2?
Huko Ontario, Premier wa Ontario anapigiwa mizinga 21 kama Prime minister wa Canada?
Je, kuna majeshi mangapi nchini Marekani, na nani Amir jeshi wa kila states.
Ukinitaji moja tu basi naunga mkono S2. Ukishindwa kutaja hapo kuna mambo 2.
Kwanza unathibitisha kuwa kilichopo ni kasha tupu, muungano ulishaoza
Pili, katika mfumo wa sasa wa S2, kuwa na maamir jeshi 2 wa majeshi tofauti ni hatari kuliko mfumo mwingine wowote
Mkuu nifahamishe kidogo, ni jinsi gani tunagawa shughuli za Tanzania ili kuwa na za znz na zile za Tanganyika ili kuvua koti.
Ukisema Tanganyika ishughulikiwe na Tanzania hapo si kuwa umevaa koti bali utakuwa na kikoi na mkwiji.
Mkuu, wewe na CCM kwa umoja wenu mnasema gharama za muungano zinaongezeka katika S3.
Kwavile sielewi ningependa kujifunza kutoka kwako, S2 gharama zake zina unafuu maeneno gani na kwa njia zipi.
Mkandara, hadidu za rejea za tume ya Warioba zimeeleza kuzungumzia suala la muungano.
Hazikusema muundo au serikali ngapi. Hazikusema gharama au kitu kingine. Zimesema kwa ujumla wake zungumzieni muungano.
Unamhukumu bure Warioba,kama angekuwa ni yeye wakati anawasiliana na Kikwete, JK angesimamisha mchakato.
Hakuna sehemu yoyote na mwanasheria yoyote aliyesimama kusema Tume imeenda kinyume na hadidu za rejea.
Si JK wala si CCM wenye akili timamu wanaosema .Tume imefanya kazi kisheria na hakuna pingamizi.
Ni tume iliyosheheni wanasheria, maprofesa, wanadiplomasia na watu kutoka katika jamii.
Weledi na uadilifu wa watu wa tume huwezi kuuweka katika mizani na wale wanaoandika rasimu ya CCM ya S2 chini ya Andrew Chenge, au washabiki kama Lusinde, Nape, Mwigulu n.k.
Katika bunge la Katiba, Zanzibar inawakilishwa na makundi matatu
1. Kutoka BLW
2. Kautoka Bunge la JMT
3. Kautoka Makundi ya Rais
Tanganyika haina mwakilishi hata mmoja., ahsante kuliona hilo.
Waliopo ni wajumbe wa Tanzania bara ambao unasema wanaserikali ya bara.
Waliopo ni wajumbe wa nchi ya Tanzania bara iliyopata uhuru mwaka 1977. Hakuna mjumbe wa Tanganyika.
Kwavile unaelewa hilo, basi unatuelewa tunaposema muungano wa sasa hauna haki wala usawa.
Hakuna Tanganyika au Mtanganyika anayewakilisha. Na bunge hilo halina Mtanganyika.
Kwavile umetambua hilo, pakuanzia si hapa tulipo. Ni kuanza kuzindua Tanganyika ili isimame na masilahi ya Tanganyika kama ilivyo znz. Halafu tuangalie mambo 7 kwasababu znz haitaki mambo yote kama kule Canada unakosema.
Kama hayo 7 hawataki, wasipigwe mabomu , njia ni nyeupee kabisa, waondoke zao kwa amani.
Kwa suala la cheti cha ndoa, Tanzania ambako mtu anaweza kuingia na kuishi tu bila nyaraka ni makosa kuulizia vitu kama hivyo. Huko Canada ulipo unaweza kuulizwa cheti cha ndoa hata miaka 90 iliyopita.
Cheti cha ndoa ni kutafuta ukweli hata kama ndoa hiyo ilishakuwepo. Swali la kwanza utakaloulizwa huko Canada ulipo au Marekani, uwe katika ofisi binafsi au ya umma ni ID yako na ikibidi proof of marriage kama una claim za aina hiyo. Haijalishi ni miaka mingapi mumeishi, kinachotakiwa ni proof ya marriage. Tanzania unaweza ku prove kwa maneno, huko kwingine ney!