Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nzi , hayo unayosema ni sehemu ya vitimbwi vya huu muungano. Nadhani umesoma katika mjadala unaohusu nchi kuwa na Amir Jeshi wakuu wawili, Kikwete na Sheni wakipokezana majukumu.Mimi mgeni katika mjadala huu. Lakini nina jambo moja la kuuliza:
Wakati wa Mei Mosi mwaka huu nilisikia Rais wa JMT alitangaza ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi wa Jamhuri. Baadaye tena, nikaja sikia kwamba Waziri wa Fedha, Zanzibar akitangaza kuwa mwaka hakutakuwa na ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi wa Zanzibar.
Sasa,
1. Tangazo la Rais lilikuwa ni kwa ajili ya Jamhuri ambayo Zanzibar haimo?
2. Suala la Fedha siyo la Muungano?
3. Tangazo la Rais lilihusu wafanyakazi wa Tanganyika tu? Kwahiyo aliongea kama Rais wa Tanganyika ama?
Asante.
Katika swala hili, mkuu wangu hata kama tungekuwa na serikali 3 bado mishahara ingekuwa vile vile Zanzibar wakitangaza yao na Bara tukitangaza yetu. Nachoweza kusema mimi ni kwamba Mishahara alotangaza JK ni kwa serikali ya JMT hivyo watumishi wote waloajiliwa kupitia serikali kuu JMT ndio wamelengwa hivyo serikali ya Zanzibar haihusiki na kwa maana ile ile viongozi wa Bara wametumia tena JMT kupandishwa mishahara. Na sidhani kama TUKTA wanahusika Zanzibar ama wanapodai mishahara huzungumzia pia watumishi wa Umma wa Zanzibar.Mimi mgeni katika mjadala huu. Lakini nina jambo moja la kuuliza:
Wakati wa Mei Mosi mwaka huu nilisikia Rais wa JMT alitangaza ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi wa Jamhuri. Baadaye tena, nikaja sikia kwamba Waziri wa Fedha, Zanzibar akitangaza kuwa mwaka hakutakuwa na ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi wa Zanzibar.
Sasa,
1. Tangazo la Rais lilikuwa ni kwa ajili ya Jamhuri ambayo Zanzibar haimo?
2. Suala la Fedha siyo la Muungano?
3. Tangazo la Rais lilihusu wafanyakazi wa Tanganyika tu? Kwahiyo aliongea kama Rais wa Tanganyika ama?
Asante.
Mchambuzi,
Kwa hiyo muda woote tulokuwa tukilumbana hapa ulikuwa hujanipata sio? Mkuu wangu mimi nachoklsema S2 ktk mfano wangu ni ndoa ya Mume na Mke. Hii inasimamia NCHI zetu ambazo ktk kugawana mamlaka ya mambo ktk SERIKALI 2 yaani ile ya mke na mume. Hivyo ktk kukaa na kutazama hali ya maisha na nafasi ya mke, mwanamme anachukua jukumu kubwa zaidi ya kuhudumia Familia nzima kwa kila shida inayohusiana na fedha, mawasilio ya nje, mikopo na kadhalika kwa kuaminiwa na mkewe. Hivyo huwezi kusema ana wake wawili kwa sababu ajnajihudumia pia yeye ktk matakwa yake.
Kwa hiyo auankuwa na bajeti ya nyumbani na pia bajeti yake yeye ktk matumizi yake wakati mkewe fedha yake ya vitumbua sii lazima itumike ndnai ya familia ila anaponunua vitu vyake vya maswala ya kike inahesabika kama ni swala la familia sii lazima mama amuombe mume fedha za kununua Thong, lipstick na wanja. Hivyo basi jukumu la Mume halikomei tu kwake bali kwa familia nzima ila kwake yeye yapo mambo yake kama mume na yapo kama kiongozi mkuu mwenye kusimamia mabo yote ya familia.
Hivyo kwa ke ndnai ya nyumba kuwa na mamlaka zaidi ya Mume haimfanyi naye kuwa Amir jeshi mkuu hapana, Ila naye pia ana mamlaka makubwa ktk ndoa hiyo kama Mke, unless nyie mnataka kunambia mke ofisi yake ni jikoni tu akiinua kichwa kuonyesha usawa wake kwa mume huyo sii mke anataka kuwa baba wa Familia.
Kwetu sisi hatutakliwi kutofautisha baina ya Baba na Mama na tuwaheshimu kwa sabau huyu ni baba na huyu ni mama jhivyo mmoja akiingilia mamlaka ya mwenzake tunaanza kuulizanana. Nachosema mimi hakuna swala lolote linaloihusu familia hii sii la Familia. Hakuna shida wala raha ya mtu mmoja isomhusu mwenzi na hakuna watoto wa Mama ama watoto wa baba. Ila kuna kugawana mamlaka ya shughuli baina yao.
Hivyo basi, kama mke kazi yake iko jikoni haina maana haimhusu Mume na kama mume kazi yake ni shambani haina maana haimuhusu Mke.
Mkuu wangu unajua unanichekesha sana maana ninachopinga mimi na ktk mifano yangu ni jinsi Tanganyika inavyowafanya Zanzibar kama mke wa kukaa ndani (housewife). Ni mfumo uu ninao ukemea kila wakati iwe ndani ya S1,S2 au S3 ila maadam hapa swla ni kuhusu S2 na S3, nyie mnafikiri naipinga S3, hivyo lazima naiunga mkono S2. Mkuu hizi serikali zote sioni tofauti yake , watu wale wale ikiwa mfumo wa Kiutawala utabakia vile vile..Ni hii tabia ya bwana ambayo inamweka chini mwanamke (msome Nguruvi3 vizuri utaona kila kosa ni upande wa pili). Bwana anayetaka ajulikane kuwa ndani ya nyumba bwana ni nani na mke hana mpango.. Hii tabia ndio tunatakiwa kuikemea na sii kuitazama upya ndoa yenyewe.Basi ndio maana huwa unajichanganya kwani ndoa unayozungumzia wewe ni zile za zama za kale sana ambapo mwanamke alikuwa anaolewa kuwa ni mashine ya kumzalia mwanaume, kufanya kazi za ndani na kumpa usingizi. Unaishi zama za ndoa za ubabe ubabe, kutegeana na kunyonyana. Unaishi enzi za ndoa za wake magolikipa, wasio na elimu wala mchango wowote wa maana kiuchumi katika familia. Unaishi enzi zile ambapo prenuptual agreement wasn't an option.
Zama hizi ni za Gender Equity. Zama hizi ni za barrack na michelle, ni za Hillary na Bill, sio za Ali na Siti.
Isitoshe, katika ndoa ya mume na mke, kuna mamlaka tatu - ya kwanza ni ile ya mke na mume na watoto wao, ya pili ni ile ya wazazi na ukoo wa mume na ya tatu ni ile ya wazazi na ukoo wa mke. Siku ya harusi/muungano au siku ya kutafuta suluhu ya kero za muungano ndio utajua mipaka ya mamlaka hizi tatu.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Nzi , hayo unayosema ni sehemu ya vitimbwi vya huu muungano. Nadhani umesoma katika mjadala unaohusu nchi kuwa na Amir Jeshi wakuu wawili, Kikwete na Sheni wakipokezana majukumu.
Tangazo zililihusu Watanganyika kama JMT na siyo znz.
Katika swala hili, mkuu wangu hata kama tungekuwa na serikali 3 bado mishahara ingekuwa vile vile Zanzibar wakitangaza yao na Bara tukitangaza yetu. Nachoweza kusema mimi ni kwamba Mishahara alotangaza JK ni kwa serikali ya JMT hivyo watumishi wote waloajiliwa kupitia serikali kuu JMT ndio wamelengwa hivyo serikali ya Zanzibar haihusiki na kwa maana ile ile viongozi wa Bara wametumia tena JMT kupandishwa mishahara. Na sidhani kama TUKTA wanahusika Zanzibar ama wanapodai mishahara huzungumzia pia watumishi wa Umma wa Zanzibar.
Katika mkanganyiko huu ndio huleta kero za Muungano na sidhani kama kuwepo kwa Tanganyika tunaweza kuondosha hili maana akitangaza JK kupanda kwa mishahara sijui atakuwa na maana gani ambayo leo hii haiwezi kutumika vile vile. Mnachotaka kusiia ni kwamba hata Zanmzibar nao mishahara imepanda sawa na bara. Lakini ukitazama huku majuu mishahara kati ya nchi za muungano huwa hazifanani na hii hutokana na mfumko wa bei (soko huria).
Unaweza kuta Ontario mshahara wa chini ni dollar 11, Quebec dollar 9, Alberta dollar 16 na kadhalika (mifano). Yote hii inatokana na ugumu wa maisha kwa sehemu husika. Hivyo yoote hayayanawachanganya ni kutokana na sisi kutobadilisha mfumo wa Utawala na kiuchumi ambao bado serikali kuu ndio hutangaza mishahara ya taifa wakati JUWATA imeshakufa kifo cha nyani ikilenga Bara kwenyea TUKTA. Badala ya kila nchi, kila jimbo hadi vijijini kuwa na mishahara yake kulingana na hali ya maisha ya sehemu izo.
Mtumishi wa Umma wa Lindi haiwezekani akapokea mshahara sawa na mtumishi wa Dar kwa sababu hali ya maisha baina ya mikoa hiyo hailingani kabisa. Uuwiano tunaozidi kuutumia ni asili ya mfumo wa Utawala wa Kisoshalist.
Hikanganyi kama utajaribu kuelewa kwamba Tanganyika ipo ndani ya JMT na hivyo ka kila jambo lisilokuwa la Muungano ina maana Rais atasimamia maslahi ya Bara. Hivyo badala ya kuwa na marais wawili wa bara na JMT tunae mmoja. Wakati wa Mwalimu Rais alipokea mshahara mdogo sana tofauti na huyu wa soko huria na utandawazi, na hata watumishi wa Umma walipewa mishahara midogo sana ukilinganisha na hawa wa leo hivyo kulikuwa na asilimia ndogo sana ya mapishano baina ya Kiongozi wa serikali na Mtumishi wa Umma.Nyekundu: Chifu, huoni kama ikiwa hivyo ulivyoandika, inakuwa heri na vyema? Hiyo itaondoa mikangayiko kama hiyo ya Rais wa JMT kutoa tangazo ambalo halina mashika katika mshirika wa Jamhuri!! La sivyo, ina maana Rais huyo wa JMT, pia kwa namna moja ama nyingine ni Rais wa mshirika mwanachama mwingine wa Jamhuri, mwanachama 'aliyejificha'.
Bluu:Chifu, unazidi kunichanganya!! Watumishi wote walioajiriwa kupitia serikali kuu ya JMT?!? Sasa, si nasikia suala la fedha ni la 'Muungano'? Kama ndivyo, basi suala la mishahara linapaswa kuwa la 'Muungano' ama sivyo? Vilevile, mtumishi wa wizara ya fedha pale Zanzibar, tamko lile la Rais wa JMT halitamhusu? Maana yeye kaajiriwa na SMZ na vile vile anahusika na suala la 'Muungano'!! Dang it! Viongozi gani tena wa Bara? Hiyo 'Bara' ndiyo mwanachama mwingine wa Jamhuri ama? Mbona nazidi kuchanganyikiwa!!
Nyekundu: Chifu, naamini kama kungekuwepo na Serikali ya Tanganyika na kiongozi wake, basi huu mkanganyiko husingetokea. Kwani, kiongozi huyo angesema wazi kabisa kwamba, wafanyakazi wote wa Tanganyika mishahara yao itapanda. Na ninaanza kuhisi kuwa pengine yule waziri wa fedha wa SMZ aliamua kusema kwamba hakutakuwa na ongezeko la mishahara Zanzibar ili kuweka jambo hilo wazi, pengine wafanyakazi wa SMZ (ambayo ni mwanachama wa JMT) walifurahia kauli ya Rais wao wa JMT!
Bluu:Chifu, huko majuu (Canada? US?), nchi zilizoungana si ziko wazi aisee? Sasa hapa nchi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni SMZ na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!! Sijui nimeandika sawa, maana nahisi nimeshachanganyikiwa tena!
Chifu, hapo juu nadhani umezungumzia suala la kiutendaji ambalo linaweza kumalizika kama wanachama wa Muungano wetu huu wakitambulika na kujulikana bayana na kiuhalisia!! Vilevile, hayo uliyoyasema si ni majimbo yenye mamlaka kamili ama? Ina maana yana mamlaka ya kuamua mishahara kwa watumishi wake.. Kwa hali ya JMT, mwenye kuamua mishahara si Rais wa JMT ama? Sasa kama ndiyo, inakuwaje mwanachama wa JMT apingane na kiongozi wake mkuu?
Chifu, naamini kuwa hata pale Texas (kama nchi mshirika wa USA), mtumishi wa umma aliyepo Houston, San Antonio na Dallas, mishahara yao haiwezi kutofautiana (naweza sahihishwa kama nimekosea). Si nchi moja bwana ama? Sasa ukitaka iwe unavyosema, ni kuamua Lindi, DSM n.k. ziwe na sehemu zenye mamlaka kamili kwa mfumo wa serikali za majimbo. Ziwe na serikali ambazo zinaweza kuamua mishahara ya watumishi wake. Jambo ambalo ndilo hilo nalisema kwamba, wanachama wa JMT watambulike bayana, ili kila mwanachama kupitia serikali yake, aamue mishahara ya watumishi wake.
Ama nimekosema chifu wangu?
Mkuu Mkanadara suala la afya halipo katika yale 11 ya muungano wala yale ya kinymela.Tuna wabunge wa kutoka Zanzibar ktk bunge la JMT wakati huo huo Zanzibar ina wabunge wake ktk baraza lao. Tuna mawaziri na manaibu Wazanzibar ktk serikali kuu mambo ya muunano, tunao watumishi wa Umma Wazanzibar ndani ya wizara mambo ya Muungano, wapo Watanganyika vile vile Zanzibar ktk serikali ya mambo ya Muungano. Na sidhani kama ipo siku mwanancjhi wa Zanzibar kawahi kushika madaraka ya mambo yasokuwa ya Muungano. Cha ajabu kipi hapa kama sii mfumo mbaya sana wa kuwa na haya mambo ya Muungano na yasiyokuwa na Muungano!
Mkuu wangu unajua unanichekesha sana maana ninachopinga mimi na ktk mifano yangu ni jinsi Tanganyika inavyowafanya Zanzibar kama mke wa kukaa ndani (housewife). Ni mfumo uu ninao ukemea kila wakati iwe ndani ya S1,S2 au S3 ila maadam hapa swla ni kuhusu S2 na S3, nyie mnafikiri naipinga S3, hivyo lazima naiunga mkono S2. Mkuu hizi serikali zote sioni tofauti yake , watu wale wale ikiwa mfumo wa Kiutawala utabakia vile vile..Ni hii tabia ya bwana ambayo inamweka chini mwanamke (msome
Hapanaaa! Ninaangalia pande zote.Nguruvi3 vizuri utaona kila kosa ni upande wa pili). Bwana anayetaka ajulikane kuwa ndani ya nyumba bwana ni nani na mke hana mpango.. Hii tabia ndio tunatakiwa kuikemea na sii kuitazama upya ndoa yenyewe.
Ni nyie mnaoitunuku Tanganyika na CCM kwa ubabe wake kwa kutoamini kwamba wanayoyafanya sii kinyume ila ni haki yao kwa sababu Tanganyika ndio bwana anayeilisha Zanzibar, hao Zanzibar hawana kitu kazi yao kulalamika na kadhalika, haya ni sawa na matusi ya wanaume watindiga ambao hawajui umuhimu wa mke ndani ya nyumba na kwamba mke ni Partner ktk Ndoa sii Kijakazi. Malalamishi yenu makubwa ni pale mnapoona mke kachukua jukumu la bwana, hivyomnajiuliza bwana nani ndani ya nyumba? i majukumu yapio hay? oooh mke gani huyu amekaa kiti cha bwana!
Ni katika fikra hizi ndio mimi nasimamia ya kwamba tatizo ni jinsi Mume anavyo m treat mke wake na sii ndoa ya Mkeka ama ndoa ya kanisani hivyo tufuate maadili ya Kiislaam ruksa kuoa wake zaidi ya mmoja itaondoa kero na matatizo ya huyu mke mmoja na sii yake bwana maana hana tatizoAma kufikiri kusaini upya prenuptial Agreement ku define upya ndoa ili kila Mtu awe na mali zake na isomeke wazi kuwa hati ya nyumba ni ya Yussuph na sii Mr and Mrs. Ila wakutane kitandani kama mume na mke kwa mambo ya Kindoa maana mnaamini kuwa ndoa maana yake ni uzazi tu! hakuna jingine laa sivyo msingeoa abadan mkitishia mnaweza kuishi masela vile vile. Haya madini na gas inawazuzua sana Tanganyika.
Sasa hii ndio hofu yangu kubwa sana ya Muungano huu na mtazamo wa Mranganyika kama wewe mwenye kuelewa taffsiri moja tu ya Ukabila. Ebu nifahamishe vizuri, huyu hivi Rashid ni mkazi wa wapi na mbunge wa jimbo gani kwanza! Sasa kweli nyie mnaotaka serikali 3, kesho mkipewa sii mtanfukuza mbunge huyu na kina Baklhresa wataitwa Wazanzibar warudi kwao ama!Mkuu Mkanadara suala la afya halipo katika yale 11 ya muungano wala yale ya kinymela.
Leo waziri wa Afya ni mzanzibar unataka kutuambia nini.
Leo bodi ya NECTA si ya muungano, wajumbe wa bodi ya NECTA nusu ni wznz.
Ndivyo ilivyo katika bodi zote
Hivi hawa wnajadili kitu gani kinachowahusu? Bodi zote na wizara kama afya haina masilahi kwao.
Hapa ndipo tunasema wznz wanataka muungano kwa jina ili wakitafuta ajira na manufaa mengine waingie kirahisi.
Sisi tunasema mambo 7 kama hawataki njia nyeyupee. Hatuwezi kubeba furushi la samadi tena.
Mkuu unazungumzia Canada watu wa TAIFA moja. Sisi si watu wa taifa moja, narudia sisi si taifa moja.Sasa hii ndio hofu yangu kubwa sana ya Muungano huu na mtazamo wa Mranganyika kama wewe mwenye kuelewa taffsiri moja tu ya Ukabila. Ebu nifahamishe vizuri, huyu hivi Rashid ni mkazi wa wapi na mbunge wa jimbo gani kwanza! Sasa kweli nyie mnaotaka serikali 3, kesho mkipewa sii mtanfukuza mbunge huyu na kina Baklhresa wataitwa Wazanzibar warudi kwao ama!
Ebu jifunze kwanza kitu kimoja, tazama huko USA au Canada hakuna watu wenye asili ya jimbo jingine wanaoitumikia serikali kama watumishi wa Umma? Hivi sisi tumeungana kwa sababu zipi haswa maana unatisha kuanza kuitafuta asili badala ya Ukazi wa mtu.
Mkuu napotumia hili neno Mzanzibar ktk mjadala huu ni muhimu uelewe tunazungumzia watu wanaoishi sehemu (nchi) hiyo kama tulivyopendekeza ktk katiba hii mpya kuwa kila Mbunge lazima awe mkazi wa jimbo analogombea, hii haina maana mtu huo lazima awe ni wa makabila ya pale. Mkuu wangu hata hiyo serikali ya Zanzibar, wapo wengi wenye asili ya Bara ila sii wakazi tena wa Bara. Tukianza kutazama mjadala huu kwa fikra za kusema Mzanzibar ni mzawa wa Zanzibar ama mwenye asili ya Zanzibar badala ya Mkazi basi tutakuwa tunapoteza tena maana ya hata kuwepo kwa serikali 2 ama 3.
Labda nikuulize hivi Kwa nini watu kama sisi Diaspora mnatuita sio Raia wa Tanzania japo tuna asili ya hapa? Na inakuwaje sisi mnatuita Wa Canadian..Mimi nilikuwa nikiishi Montreal, Quebec na nikapewa karatasi za kuihsi Quebec nikaitwa Mquebec. Nikafanya kazi nalipa kodi za Quebec, ktk hali hiyo Quebec walifaidika na asilimia 5 ya kodi yangu wakati huo huo Canada wakifaidika na asilimia 7. Nilipohamia Toronto, Ontario kama mkazi na raia nilianza kulipa kodi kwa serikali ya Ontario kama mkazi wa Ontario na hivyo Ontario Kufaidika na kodi yangu sio Quebec tena. record zangu zote zikahamishiwa Ontario. Kwao wao haijalishi wewe una asili ya wapi isipokuwa wewe unatumikia serikali gani? na hivyo unakuta Mchina, Mspanish Mghana na Mimi sote tunaitwa Wana Ontario na tunajivunia kuwa kitu kimoja.
Mkuu unaizidisha hofu yangu ktk swala la serikali 3 na ndio maana naomba saana swala hili liondolewe ktk mjadala wa katiba mpya kwa sababu watu wengi wanafikiria kama wewe. Kesho mimi Mkerewe nitaambiwa nirudi kwetu Dar sii mahala pangu na siruhusiwi kuitumikia manispaa ya Dar.
Huwezi kwenda Quebec kugombea Uongozi wa serikali ya Quebec kama wewe sii Mkazi wa Quebec. Vivyo hivyo ktk majimbo mengine ila unaweza kuwa kiongozi ktk serikali kuu inayounganisha majimbo yote na kwa mambo yote ni ya Muungano, isipokuwa kila mmoja wenu atakuwa ktk nafasi yake ya kazi, mahala pake na kadhalika. Mkuu ndio maana nasema nyie mnataka muundo wa S3 wakati hamjui muundo huo ni utawala wa aina gani na unaendeshaje shughuli zake ili wapate kufanikiwa.Mkuu unazungumzia Canada watu wa TAIFA moja. Sisi si watu wa taifa moja, narudia sisi si taifa moja.
Pili, ukienda Quebec unagombea uongozi, ukienda znz huna nafasi wewe ni Mtanganyika.
Tatu, mznz akija Tanzania kama waziri wa afya ni Mtazanzani, yupi waziri mtanganyika znz. Kama hata kuishi unahitaji kibali kuna muungano hapo.
Wewe unaleta hoja halfu unapiga kona. Hoja kubwa ilikuwa kama yupo mznz mwenye madaraka Tanganyika. Tukakwambia waziri afya isiyo mhusu mznz sasa unaleta habari za kuhama n.k.
Katiba ya znz 2010 inambagua Mtanganyika, imeshavunja muungano hili lazima ukubali hata kama unagoma.
Hakuna muungano kwa kuanzia kuna kitu kama muungano.
Ndiyo maan tunasema we don't need usumbufu wa znz, kama hawataki kuishi kwa amani na adabu njia nyeupe.
Mezani tutajadiliana mambo 7, mtaaniitakuwa hadithi nyingine kabisa.
Hakuna muungano na wala znz haina manufaa yoyote kwa Mtanganyika.Period.
S2 zimeshindwa kulinda muungano JK akivunja katiba halafu leo unalinganisha na Canada.
Mkuu ukileta hoja uwe na mahali pa kuismamia, sio ulete hoja halafu ukate kona bila indicator.
Nkaubaliana na Mag3 hapo juu kuwa Mkandara haeleweki ingawa anashangaa kwanini hatumwelewi.Huwezi kwenda Quebec kugombea Uongozi wa serikali ya Quebec kama wewe sii Mkazi wa Quebec. Vivyo hivyo ktk majimbo mengine ila unaweza kuwa kiongozi ktk serikali kuu inayounganisha majimbo yote na kwa mambo yote ni ya Muungano, isipokuwa kila mmoja wenu atakuwa ktk nafasi yake ya kazi, mahala pake na kadhalika. Mkuu ndio maana nasema nyie mnataka muundo wa S3 wakati hamjui muundo huo ni utawala wa aina gani na unaendeshaje shughuli zake ili wapate kufanikiwa.
Ndani ya serikali ya Zanzibar kuna viongozi kibao wenye asili ya Bara yaani Watanganyika lakini maadam ni wakati wa Zanzibar wanahesabuiwa kama Wazanzibar. Na huku bara wapo Wazanzibar wanaoishi Bara na wanahesabiwa kama Watanganyika kwani muungano wetu umetokana na WATU na sii Karume au Nyerere hawa wamewezesha tu kuwepo kwa Muungano wa nchi. Udugu wetu umekuwepo toka karne ya kwanza..
Na ndio sababu kubwa mimi napingana na rasimu kwa sababu inachofanya ni kugawa nchi sehemu 3 lakini bado inaendeleza ya S2. Kama vile mkoa wa Arusha unaugawa na kuwa Kuunda Manyara. Hatua hiyo haibaidlishi kitu zaidi ya kuongeza wakuu wa mkoa, wilaya na kadhalika! pia kuwapa nafasi viongozi mafisadi nafasi zaidi ya kufisadi.
Mkuu kwani huo ukaazi unapatikanaje huko ? Maana huwezi kusema ukaazi bila kuwa na muda. Hebu tupe habari kidogo.Huwezi kwenda Quebec kugombea Uongozi wa serikali ya Quebec kama wewe sii Mkazi wa Quebec. Vivyo hivyo ktk majimbo mengine ila unaweza kuwa kiongozi ktk serikali kuu inayounganisha majimbo yote na kwa mambo yote ni ya Muungano, isipokuwa kila mmoja wenu atakuwa ktk nafasi yake ya kazi, mahala pake na kadhalika. Mkuu ndio maana nasema nyie mnataka muundo wa S3 wakati hamjui muundo huo ni utawala wa aina gani na unaendeshaje shughuli zake ili wapate kufanikiwa.
Ndani ya serikali ya Zanzibar kuna viongozi kibao wenye asili ya Bara yaani Watanganyika lakini maadam ni wakati wa Zanzibar wanahesabuiwa kama Wazanzibar. Na huku bara wapo Wazanzibar wanaoishi Bara na wanahesabiwa kama Watanganyika kwani muungano wetu umetokana na WATU na sii Karume au Nyerere hawa wamewezesha tu kuwepo kwa Muungano wa nchi. Udugu wetu umekuwepo toka karne ya kwanza..
Na ndio sababu kubwa mimi napingana na rasimu kwa sababu inachofanya ni kugawa nchi sehemu 3 lakini bado inaendeleza ya S2. Kama vile mkoa wa Arusha unaugawa na kuwa Kuunda Manyara. Hatua hiyo haibaidlishi kitu zaidi ya kuongeza wakuu wa mkoa, wilaya na kadhalika! pia kuwapa nafasi viongozi mafisadi nafasi zaidi ya kufisadi.
Source please!KIWEWE CHA RASIMU CHAZIDI KUITESA SERIKALI NA RAIS
UKAWA WAFIKIWA NA SERIKALI ILI WARUDI BUNGENI
WAJUMBE WATUMWA KUONANA NA lLIPUMBA, MBOWE NA MBATIA
UKAWA WAANZA KUBABAIKA, WAFIKIRIA KURUDI KUNYWA JUISI TENA.
Wanaduru
Taarifa zilizopo Rais kuwafikia viongozi wa UKAWA ili kupata mufaka wa kurudi bungeni.
Pamoja na jitihada za kuwatuma akina Nape ili kupotosha, ukweli ni kuwa bila wapianzani rasimu itakuwa ya CCM na ingeweza kuandikwa Lumumba.
Taswira nje ya nchi inapoteza ung'avu wananchi wakionekana kuunga mkono UKAWA.
Wasomi na wenye weledi na ushawishi wameonekana kutoridhishwa na uhuni wa bunge.
Hali hiyo imeongeza pressure kwa serikali ambayo si tu itaonekana kushindwa kuendesha mambo ya taifa, bali pia kulitia taifa gaharama nyingi.Bajeti ya bunge la katiba haipo na 'waliotoa' wanafuatilia mchakato mzima.
Serikali alidhani ilikuwa ni tisha toto na UKAWA wangerejea baada ya muda.
Hali haionekani kutengamaa na hilo linazidi kumweka serikali katika wakati mgumu.
Kuna taarifa za viongozi wa UKAWA kufikiwa kwenda kunya Juisi pale magogoni.
Ni mazungumzo yale yale ya kunywa juisi na kuwafariji kama ilivyozoeleka
Tunarudia , mara zote wapinzani walipokwenda IKULU hawakuambulia chochote zaidi ya kunywa juisi ya maembe. Kuna nyakati Rais aliwapiga makofi kwa kujadiliana mamboili hali alishasaini kile walichokipinga.
Mbowe anafahamu, jumatatu akiahirisha maandamano ya kupinga ubabe ili kuonana na JK, jumatatu hiyo hiyo JK akasiani mswada uliopitishwa na wabunge 100. Mbowe aliambulia Juisi tamu sana
Kuna habari pia kuwa Mh Profesa Lipumba amekataa kuonana na rais isipokuwa anaweza kufanya hivyo kupitia wawakilishi.
Duru za siasa tunapenda kuwashuri UKAWA kama ifuatavyo
1. Mbinu za kuwagawa zinaendelea hivyo lazima muwe macho.
Kitendo cha kuonana na viongozi tofauti ni dalili za kuendelea kuwagawa.
Msimamo wa Lipumba utakapotofautiana na Mbowe au Mbati, huo ndio mwisho wa UKAWA.
2. Rais Kikwete alisema 'UKAWA' wapo likizo na ni suala la muda tu watarudi
3. Akina Nape wanapita kuwashambulia kwa kuchukua posho , kumezuka kundi la washabiki wanaotaka muende mahakamani. Kundi hili linajenga hoja dhaifu ili kumkingia kifua Rais ambaye:
a. Amewadhalilisha ninyi kuwepo likizo
b. Ameleta mtafaruku kuhusu jeshi letu
c. Ametuma mawaziri kwenda maeneo ya dini kuchoche vurugu
3. Historia haionyeshi kuwa kukutana na Rais kumewahi kubadilisha hali yoyote zaidi ya glass za juisi
4. Kitendo cha ninyi kukataa kuonana na Rais lakini mkitaka muonane na wawakilishi wake ni cha kushangaza na kutisha.
Rais atatumia mwanya huo kuwananga siku za baadaye akitumia wawakilishi mlio onana nao.
Hapa mtakuwa mnajikaanga kwa mafuta yenu.
NNI MKIFANYE KAMA MNEOMBA USHAURI
1. Kwanza ni serikali na rais kuomba radhi kwa dhalili, uchochezi wa kidini na kuliingiza jeshi pasipohusika
2. Kwamba, mtarejea katika bunge la katiba kwa masharti haya
a) Rasimu ya tume ijadiliwe kama ilivyoletwa na kusainiwa na rais.
b) Maboresho ya rasimu yazingatie framework ya rasimu original
c. Uwepo usawa katika mijadala na uendeshaji wa bunge kwa kufuata kanuni na sheria
d. Kuzuia aina yoyote ya rasimu nje ya ile ya Warioba.
UKAWA wakiurudi mezani kabla ya madai,watambue wameuza ghala la silaha.
Hakuna namna umma utawaelewa kwa kuongea na Rais yule yule aliyesema muundo wa muungano ni S2. akatishia nchi kupinduliwa na jeshi na kutuma mawaziri katika makanisa kushindilia hoja za uchochezi.
UKAWA, mkienda kama mnakwenda kwenye ngoma ya mkole kumnema bibi harusi mumekwisha.
Dalili za kuanza kubabaika ni pamoja na hili la kukubali wawakilishi.
Jiandaeni kwa juisi ya maembe, kuna kila dalili mumeshaanza kubabaika.
Tusemezane
Mwigulu Nchemba Kobello Nape Nnauye Mkandara EMT Mchambuzi Alinda Ngongo Bongolander Kichuguu @J.Mnyika Anna Tibaijuka Mzee Mwanakijiji Alinda gfsonwin Mkuu wa chuo Tumaini Makene mohamed mohamed Mtoi Paul Makonda Ezekiel Maige @