Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Duh, mnanikumbusha mbaaali kweli kweli...miaka ilee! Alikuwepo mzee mmoja wa Kimasai ndani ya Bunge la Kenya aliyekuwa akijikongoja kwa fimbo yake ya kutembelea. Siku moja alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na mwenzake lakini kila alivyojitahidi kumfafanulia mwenzie aweze kuelewa, ndivyo mwenzake alivyozidi kuwa mkaidi. Ilifikia mahali mzee wa watu akaamua kutumia njia moja tu kufikisha ujumbe wake; fimbo yake ya kutembelea! Kila point aliyotamka alihakikisha inaambatana na kipigo kichwani kwa mbunge mwenzake kwa kutumia hiyo hiyo fimbo! Ilikuwa ni burudani ya aina yake.
That aside, mimi naomba tu nimuulize Mkandara swali moja tu; mara nyingi nimemuona, katika kutetea Muungano tulio nao akiufananisha na ndoa na si mara moja. Sasa Mkuu hii analogy ya ndoa inanipa taabu kidogo; unaweza kuielezea kwa kifupi tu; hii ndoa ni ya aina gani na nani wameoana/waliooana! Nimekuwa nikisikia madai ya ajabu ajabu k.m. mume anayeshindwa kuwahudumia wake wawili atawezaje watatu...!