Kiukweli mkuu hujibu swali...
Sidhani kama hili swali la serikali 2 zitasaidiaje Tanganyika kuvua koti la muungano linajibiwa kwa sentensi 20. Unachojitahidi kueleza wewe ni kwa nini huoni umuhimu wa serikali 3.
Lakini ni kwa vipi serikali 2 zitatatua tatizo, kiukweli hata hujagusia kabisaa...
Mkuu wangu wewe unashindwa kuliona tatizo kwa sababu mnatazama KERO badala ya Mapungufu yaliyomo ktk mfumo tulokuwa nao wa kiutawala. Ni mfumo wa kiutawala ndio unaweza leta maendeleo ama kutoyaleta kwani hoja kubwa ya Wazanzibar ni MAENDELEO ktk visiwa vyake na ndipo kero zilipokuja baada ya wao kutopewa kipaumbele kwa miaka 30, japo nyie kizazi kipya mnadai miaka 50 serikali 2 imeshindwa kuondoa kero.
Kwa mwenye weredi ataelewa kwamba sii muundo wa serikali unaoweza kubadilisha maisha ya wananchi isipokuwa tu ikiwa muundo huo utagawa mamlaka ya shughuli za serikali ktk serikali za nci na majimbo. Kosa kubwa la muundo wa serikali 2 ni kulimbikiza shughuli zote za mamlaka ya serikali kuwa chini ya serikali kuu na zile za states ama majimbo wana mamlaka madogo sana ya nayo ni ahadi na kutembeza bakuli kama kanisani. They can't make any decision on behalf of their people without approved by the central government, huu mfumo wa Kiimla ndio tatizo letu na katiba mpya inaweza kabisa kubadilisha hili bila kuwa na mfumo wa S3.
Ndio maana OIC ilipigwa vita bara kwa kutumia jina la JMT, ndio maana Chadema na CUF japo walishinda chaguzi ktk majimbo tofauti hawana mamlaka ya kuendesha shughuli za maendeleo ya majimbo hayo pasipo kuidhinishwa na kukatiwa fungu na CCM (serikali kuu)na kadhalika. Hapo walipo sii Chadema wala CUF wanaweza kuleta maendeleo kwa wananchi, tukiamini hili pasipo mabadiliko tutakuwa tunajidanganya iwe kwa serikali 1,2 au 3.
Sii Zanzibar wala Majimbo wana mfuko wao wa maendeleo kutokana na kodi za wananchi wake, pasipo kupewa toka bajeti ya serikali kuu. Hili ndilo jibu langu hivyo sitetei serikali 2 wala 3 kwa sababu najua wingi ama uchache wa serikali sio tija, huu ni mchezo wa kisiasa ambao CCM na vyama vya Upouinzani pamoja na wahaini wanautumia kupambana wao kisiasa ili kuunda katiba inayowalinda wao kama wanasiasa ama asasi na sii wananchi wa JMT. Maadam tunahitaji katiba ya wananchi swala la Muungano wetu ni la mwanzo na mwisho na halihusiani kabisa na kuandikwa kwa katiba mpya ambayo sisi wananchi tuloiomba ila limeongezwa na wanasiasa kwa sababu zao na faida zao. Sasa mkuu wangu unataka jibu lipi zaidi?
Nirudie Hakuna muarobaini wa matatizo tulokuwa nayo kupitia mabadiliko ya serikali 1, 2 wala 3 kwa sababu mapungufu yetu hayahusiani na muundo wa serikali bali mamlaka ya serikali hizo kiutawala. Badala ya kugawakna kazi (mamlaka) muundo wa serikali 2 umekuwa ukitugawa kwa mambo yasokuwa ya muungano hivyo kila nchi kuendesha wizara zake na kuusanya mapato yake.
Labda niwape tena mifano unaohusiana na maisha yetu. Mkuu mtazamo wangu ni sawa na wewe umeoa mke, lakini mkeo ana biashara zake na wewe una biashara zako, kisha kila mtu anachukua chake na kuchangia mfuko wa familia. Hii siii haba ila tatizo linakuja kuwa wewe ndiye mwenye access na account ya pamoja, fedha za chakula unamgawia mkeo kwa mahesabu makali lakini wewe unaenda nunua suti za bei mbaya toka mfuko wa familia ukidai wewe ndiye mwenye mchango mkubwa ndani ya mfuko ule na zaidi ya hapo fedha zako huzichanganya na zile za pamoja ndio kusema kwamba mkeo akitoa Tsh 200,000 kwa mwezi wakati account ina mil. 3 wewe unahesabu kati ya Mil.3 zile mil.2.8 nyingine ni zako wewe pasipo kujua ama unafanya makusudi ukijua ya kwamba unatakiwa kutenga Tsh 200,000 zenye uuwiano na mkeo kuwa za familia na sii zako. Mkeo pato lake ni Tsh laki 3, Tsh laki2 ni ni asilimia 66.7 ya pato lake hivyo nawe ktk pato lako unatakiwa kuchangia familia asilimia 66.7 ya pato lako.
Pili, katika hizo mil.2.8 unazo dai zako kuna karibu 1.2 (asilimia 40) ulikwenda kukopa fedha benki, ukaweka rehani nyumba ya familia kama dhamana, hivyo hizo Mil 1.2 ulizopewa na benki kama mkopo, sii zako bali za familia,vizuri kushauriana na mkeo jinsi ya kuzitumia kwa faida ya familia. Na hivyo basi mkeo akitaka kununua jiko jipya, shuka mpya, vikombe na vijiko na kadhalika usimnange ukamwambia hatuna fedha maana mlisha gawana, na kudai kuwa yeye ulimpa Laki 3 ni zaidi ya laki 2 alochangia mfuko kwa sababu tu naye ile laki 1 ilobakia nayo yeye pia alikwenda kununua mkoba wa Louis Vuitton badala ya nepi za watoto.
Sijui unanipata? Kama mwananchi hapa ndipo tunatakiwa kukomelea, matumizi mabaya ya viongozi wetu na mamlaka makubwa walopewa hii inatuumiza sisi watoto wa familia hii. Na nimeweza kuyajua haya kwa kujiweka mimi ktk kundi la watoto wako hivyo ni rahisi mimi kuona pande zote mbili badala ya mimi kujitambua kama mtoto wa kiume ni jukumu langu kumtetea baba mwanamme mwenzangu.
Na ndio nikasema ya kwamba inabidi mkuu wangu ujitazame upya kwa sababu fedha zilizopo ktk mfuko wa familia sii zako japo unatazama tu mchango wa mkeo. Kwanza tazama mshahara wako kulinganisha na wake ili ujue ni asilimia ngapi ya mshahara wake hkachangia mfuko wa nyumbani yawezekana yeye katoa zaidi yako maaka mshahara wake ni Tsh laki 3 kutoa laki 2 ni asilimia kubwa kuzidi wewe mwenye mshahara wa laki 5 kisha familia inaendeshwa kwa mikopo ambayo unachukulia kama fedha ni zako uliomba wewe. Hivi kweli kuna kosa kwa mkeo kuhoji mapato na matumizi haya likawa swala la ndoa?
Haya madai ya mkeo yanapozidi yanakuwa KERO na hivyo kwa sababu unaona keor zinazidi ndio unafikia maamuzi ya kuomba kujadili tena ndoa yenu. Hapa ndipo mimi nakataa na mundo wa serikali ktk hoja nzima ya kuandika katiba mpya kuingia swala la muungano. Na inaposhauriwa kufanya ndoa iwe ya makubaliano (Prenuptial agreement) na wengine wakishauri separation ya kindoa kiasi kwamba kila mtu na fedha yake mkutane kitandani tu maana ndoa ni mapenzi na uzazi sii fedha!
Hapa ndipo napowakatatlia nyote iwe S2 au S3 kwa sababu nayaona matatizo yalipoanzia. Matatizo ni mgao wa pato lenu na haiwezekani kuendelea na muundo uliopo wala kugawana kazi na mapato yake kiasi kwamba inakuwa kila mtu atabeba mzigo wake, chake chake changu changu hii sii ndoa tena mkuu wangu bali mnakaribisha kuachana kabisa na umaskini utazidi baina yenu hapatakuwa na mshindi. Jiulize kwa nini CAG anashindwa kukagua mali za viongozi wetu? anashindwa kuhoji hata mishahara ya viongozi wetu? Posho zao na kadhalika hii ni kutokana na katiba iliyopo inawalinda na sio kuwepo kwa serikali 2.
Hivyo basi nimeyaona malalamiko ya Wazanzibar kama ya mkeo na kuyaelewa na nikajua wapi wewe kama mume ulikosea na unendelea kukosea unapotazama mahitaji yako binafsi ukasahau kwamba huyu ni mkeo. Anapopendeza yeye ndio unavyosifiwa wewe na nyumba yenu sii tu kwamba kuvaa suti kwako ndio sifa! Na ndio kikashauri kuwepo na miiko na maadili kujenga vipaumbele ktk kuijenga familia kwa mazuri na sii mavazi.
Namalizia kusema ya kwamba nimeandika mengi sana kuhusu Mchango wangu ktk uandishi wa katiba mpya na kama hadi sasa hivi hamunielewi na bado mnataka kuendelea na hizo serikali 3 Endeleeni siwakwazi wala sintoendelea kubishana juu ya hili. Alonielewa kanielewa na asiyetaka kukubaliana nami sawa vile vile kwa sababu ni haki yao kufikiri wanavyofikiria.