UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

Ukishamsoma Mkandara aliyeandika leo utajiuliza kama ndiye yule aliyeandika maneno haya wiki mbili zilizopita Kwa ufupi, Mkandara wa wiki mbili zilizopita alituambia Tanganyika imevaa koti la muungano na kuwanyonya wazaznibar. Leo Mkandara anasema znz waliondoa baadhi ya mambo kwavile Tanganyika iliyaondoa kwanza katika muungano! Angali contradiction hiyo, halafu anasema ' Hatuwezi kuwa na serikali 3 kwasababu zitakuwa ni dhaifu' hasa ile kuu. Wakati huo huo wiki iliyopita alisema serikali kuu ya sasa inainyonya znz. Hivi unawezaje kuwa na serikali kuu inayonyanya leo kesho ukadai muundo huo huo ni mzuri?

Mkandara, my dear friend !

Mkuu katika mapambano haya, hata wale uliodhani ni werevu na silaha ya ushindi kwa umma ndipo sura halisi za akina Mkandara utaziona hivi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu katika mapambano haya, hata wale uliodhani ni werevu na silaha ya ushindi kwa umma ndipo sura halisi za akina Mkandara utaziona hivi.
Tatizo lenu mnasoma pasipo kufahamu. Na katika mambo makubwa binadamu tunayaomba kwa mola ni kutujalia KUFAHAMU yaani unayoyaona, kuyasoma, kusasikia na kuyagusa unayafahamu na sii kuyakairi kama tu Mmatumbi mimi napoitazama sinema ya kihindi.
Nguruvi3 mgumu sana wa kuchambua mada, maana haelewi nachozungumzia hata baada ya kumwambia mara 100 kitu kile kile. Tanganyika imevaa kweli koti la Muungano na JK ktk Hotuba yake alitudhihirishia aliposema Reli inawahusu vipi Zanzibar, ati hawaihitaji usafiri wa reli wakati reli hiyo ilipatikana kwa mkopo wa jina la JMT tena basi Abrahaman Babu akiwa mhusika mkuu. Kwa nini reli hiyo isiwafaidishe Wazanzibar pia ila wepesi sana kusema Znz wakipata mafuta au gas ni ya JMT kwa sababu Znz sio nchi bali koti tu, nchi ni moja.

Leo Dhahabu ya Geita na Bulyanhulu haiwahusu Zanzibar lakini tumedai Mafuta yakipatikana Pemba yatakuwa na Muungano na kuanzisha kero mpya kijinga kabisa. Ikiwa kweli Zanzibar haipati kitu tokana na makusanyo ya kodi za dhahabu kwa kutmia jina la JMT inaingia akilini? Je tukiwa na serikali 3 Zanzibar watapa kitu ama ndio muundo mpya wa Chako chako, changu changu. Je hii itaondoa kero au malalamishi inawezekana lakini kuna Muungano hapo au ndio yaleyale yashirikisho la EAC.

Wanachodai Zanzibar ni haki yao chochote kinachoingia ama kutoka mfuko wa JMT wanahusika moja kwa moja maana ni Partners wetu pale jina la Muungano linapotumika. Sisi tunalivaa koti tunapolihitaji na kulivua pale hatulihitaji. Nyericko sura yangu halisi wewe huwezi kuielewa kwa sababu wewe ni mshabiki, wewe unaijali Chadema kuliko maslahi ya Taifa na uko radhi nchi hii igeuzwe jangwa lakini Chadema ipone. Kama kweli wewe mwenrevu kiasi hicho mbona sikukusikia ktk matusi ya TL au kwa sababu Nyerere na Karume sio Chadema?

Niliwahi kusema sii Mbowe wala Zitto walonipeleka Kujiunga na Chaderma isipokuwa tumaini niloliweka juu ya chama hicho na mwelekeo wake lakini toka wahuni walipoingia nimekosa amani na chama hiki maana hawakijengi chama bali wanakibomoa kwa fikra kwamba wao wamesoma saaana na wanajua saaana kuliko watu wote! Ikiwa viongozi hawana NIdhamu kweli tumebakiwa na chama au magumashi!
 
Mkuu Mkandara, umejaribu sana kukwepa maswali na nadhani tukubaliane kuwa huna majibu.

1. Kuingiza mambo ya katiba katika nyumba za imani na ibada ni upuuzi na wendwazimu.
Afrika ya kati, Nigeria wanajua hilo

2. ZNZ iliandika katiba kwa kiburi tu na wala si kushauriana.
Kama ni kushauriana basi ni kinyume cha sheria. Sheria za bunge hufutwa na bunge si watawala. Kama ni watawala mbona hakuna decree?
Ujeuri wa znz haukuanzia katika katiba, ni pamoja na kukataa kulipa madeni yake kwasababu ya kiburi tu, watautafanya nini!

a) Kama unakubali kuna mambo 11 yaliyoongezwa kinyemela na kufikia 22, unachaokataa ni kitu gani Warioba na tume kuyapunguza hadi 7. Hivi unapaswa kumuunga mkono au kukataa!

b) JK ametoa tarehe na moja ya mambo yaliyoongezwa alisaini Karume. Unyemela upo wapi.

c) Hayo yaliyoongezwa ni mangapi Tanganyika inafadika nayo.
Elimu ya juu kwa mfano, Tanganyika inafadikaje

2. Kuhusu kuvaa koti la muungano
Kama hayo ni madai ya znz na kwamba asilimia 40 ya misaada inaishia Tanganyika, hivi huoni ni vema tukawa na serikali 3 ili kila mmoja akope kwa nguvu yake na alipe kwa nguvu yake.
Mkuu hapa humuungi mkono Warioba. Unachokataa ni kitu gani hasa.

Unapoongelea misaada asilimia 40, usisahau deni la ndani na usisahau kuwa miaka zaidi ya 20 znz haina mchango na inachota tu.

Kama inachota kwanini uone asilimia40 ya misaada na usione kama ndiyo sehemu ya misaada.
Mkuu sisi tunasema hutuhitaji kuinyonya znz, tunataka Tanganyika, wewe unayesema inanyonywa unataka iendelee kujibanza kama ulivyosema bandiko hapo juu.
Mkandara , znz haina mchango wowote wa ustawi wetu hilo kubali.
Wao wanatuhitaji, nieleze sisi tunawahitaji kwa lipi.

3. Vyanzo vya mapato vya serikali ya sasa unayoiita JMT ambayo haina mchango wa kicuhumi kutoka znz ni Tanganyika.

Mfanyakazi, mkulima, na mvuvi wa ukerewe analipa kodi ili ziende kuendesha serikali ambayo haimhusu.

Kumkamua Mtanganyika ahudumie serikali ya nchi jirani ni kiwango cha chini sana cha fikra.

Mnaogopa kusema kuwa uwepo wa Tananyika utalazimu znz ichangie.
Mnatumia hoja za serikali haina vyanzo vya uhakika. Ni kumuumiza Mtanganyika eti alipe kodi uendesha serikai ya nchi jirani wakati nchi hiyo ina vyanzo vyake.

Tukubaliane kuwa mnachosema chanzo cha uhakika ni pesa za Mtanganyika.

Katika shirikisho mnafahamu znz italazimika kulipa, hilo ndilo mnaita shirikisho hafifu.
Kwamba ili shirikisho liwe na nguvu ni lazima Mtanganyika kupitia serikali 2 aminywe ili hali mznz anasubiri vyeo na ajira.

Mkuu Mkandara ifike mahali uwaonee huruma wavuvi wa Ukerewe.
It is immoral kutoza kodi ili ziende kuendesha mambo nchi jirani.

Mvuvi wa ukerewe anafadika na nini kutoka SMZ?
Lini znz yenye choyo hata ya ukaazi itamjali mvuvi huyo.

Tuache kuumiza watu wetu bila sababu. Narudia it is immoral kumtoza kodi mbeba mizigo pale ubungo ili iende kumhudumia mznz. Ni jambo la kusikitisha sana unasimamia uhuni huo.

4. Miaka 50 serikali 2 hazina suluhu. Leo unatuaminisha kero zimebaki 6. T
ena ili kuonyesha usanii na jinsi ulivyoingia mkenge wewe unasema kero ni 6, leo waziri wa serikali muungano Samia Suluhu amesema zimebaki 3(Habri leo gazeti)

Kwamba wiki 2 wameweza kutatua kero 3, wakati miaka 50 na tume 10 hawakuweza kupata suluhu.

Huu usanii Mkandara anaupa baraka kama utatuzi na anakubali kudanganywa akijua anadanganywa.

Mkandara, wakati wa kutatua hizo kero iliyokuwepo ni JMT ambayo znz ipo na SMZ.
Hivi huoni tatizo hadi hapo.

Kwamba mwenye malalamiko ni Idd Seif makamu wa wa kwanza SMZ, anayesuluhisha na Gharibu Bilal.Bado Mkandara anategemea Mtanganyika amenufaika.

Kero zilizopo ambazo zimebaki 3 kwa maajabu ya mola kwa siku 10 tu ni zile za znz.
Kwa maana nyingine ili kuondoa kero hizo Mtanganyika ameumia sana.
Kuwapa bajeti zaidi na pesa zsizio na audit.
Kufuta madeni ya huduma zao na kuendelee kuwapa raha, wavuvi wa ukerewe wakikereheka

Leo wamepewa 21 percent ya ajira za muungano. Ajira ambazo hawana mchango, na pili haziwahusu.

Hivi waziri wa afya anasimamia nini maana afya si jambo la muungano
Hivi bodi ya NECTA ilio na wznz inasimamia nini wakati si jambo la muungano. n.k

Leo kuna vilaza wa wznz waliopata division 4 ya znz, hawa wanapewa mikopo ya elimu ya juu huku watoto wa Kitanganyika ambao baba na mama zao wamebeba muungano, wanalipa kodi watoto wao wakihangaika.

Hakuna mtoto wa Tanganyika anayeweza kupewa mkopo wa elimu ya juu znz.
Mkandara anawatetea kwa misaada asilimia 40 na kufumbia macho ukupe na utegemezi wa wznz.

Mkuu Mkandara, njia muafaka ni kuhakikisha kila upande japo unaridhika. T
anganyika ipewe nafasi yake bila kubeba mizigo ya jirani, znz ibebe mizigo yake.
Yale ya pamoja tubebane. Warioba kasema ni 7 tu.

Kinyume na majadiliano, kutazuka tatizo kubwa sana.
Nje ya majadiliano kutaongeza chuki. Ingawa znz ilishajenga chuki, chuki ya Watanganyika ambao sasa wametambua kuwa wanauziwa mbuzi wa gunia, na kwamba koba waliloambiwa lina dhahabu kumbe limejaa samadi watazihamishia kwa wznz.

Kama hakuna control kuanzia sasa, basi hata kulazimisha serikali 2 Mkandara na wabunge wa CCM wanachokifanya kutazaa tatizo kubwa.
Huenda muungano ukafa si kwa maridhiano bali kufukuzana kwa pinde na mishale.

Ni vema umma ukasikilizwa, nje ya meza ya majadiliano kifo cha muungano kipo wazi kabisa.
Na nje ya meza ya majadiliano watakaochukua mjadala ni watu wa kutaani.

Hapo utaelewa unachokifanya na CCM ni kosa la karne.
Narudia tena, out of control ni rule of the jungle, ikifika hapo watu watashika tama.
Hii fursa inachezewa itakaporudi itakuwa juu ya maji, maziwa au damu.

Tusemezane
 
Tatizo lenu mnasoma pasipo kufahamu. Na katika mambo makubwa binadamu tunayaomba kwa mola ni kutujalia KUFAHAMU yaani unayoyaona, kuyasoma, kusasikia na kuyagusa unayafahamu na sii kuyakairi kama tu Mmatumbi mimi napoitazama sinema ya kihindi.
Nguruvi3 mgumu sana wa kuchambua mada, maana haelewi nachozungumzia hata baada ya kumwambia mara 100 kitu kile kile. Tanganyika imevaa kweli koti la Muungano na JK ktk Hotuba yake alitudhihirishia aliposema Reli inawahusu vipi Zanzibar, ati hawaihitaji usafiri wa reli wakati reli hiyo ilipatikana kwa mkopo wa jina la JMT tena basi Abrahaman Babu akiwa mhusika mkuu. Kwa nini reli hiyo isiwafaidishe Wazanzibar pia ila wepesi sana kusema Znz wakipata mafuta au gas ni ya JMT kwa sababu Znz sio nchi bali koti tu, nchi ni moja.

Leo Dhahabu ya Geita na Bulyanhulu haiwahusu Zanzibar lakini tumedai Mafuta yakipatikana Pemba yatakuwa na Muungano na kuanzisha kero mpya kijinga kabisa. Ikiwa kweli Zanzibar haipati kitu tokana na makusanyo ya kodi za dhahabu kwa kutmia jina la JMT inaingia akilini? Je tukiwa na serikali 3 Zanzibar watapa kitu ama ndio muundo mpya wa Chako chako, changu changu. Je hii itaondoa kero au malalamishi inawezekana lakini kuna Muungano hapo au ndio yaleyale yashirikisho la EAC.

Wanachodai Zanzibar ni haki yao chochote kinachoingia ama kutoka mfuko wa JMT wanahusika moja kwa moja maana ni Partners wetu pale jina la Muungano linapotumika. Sisi tunalivaa koti tunapolihitaji na kulivua pale hatulihitaji. Nyericko sura yangu halisi wewe huwezi kuielewa kwa sababu wewe ni mshabiki, wewe unaijali Chadema kuliko maslahi ya Taifa na uko radhi nchi hii igeuzwe jangwa lakini Chadema ipone. Kama kweli wewe mwenrevu kiasi hicho mbona sikukusikia ktk matusi ya TL au kwa sababu Nyerere na Karume sio Chadema?

Niliwahi kusema sii Mbowe wala Zitto walonipeleka Kujiunga na Chaderma isipokuwa tumaini niloliweka juu ya chama hicho na mwelekeo wake lakini toka wahuni walipoingia nimekosa amani na chama hiki maana hawakijengi chama bali wanakibomoa kwa fikra kwamba wao wamesoma saaana na wanajua saaana kuliko watu wote! Ikiwa viongozi hawana NIdhamu kweli tumebakiwa na chama au magumashi!
Tueleze sisi wagumu wa kuelewa. Kama Tanganyika imevaa koti la muungano, ni vipi tulivue koti hilo ili kusiwe na malalamiko ya koti.

Tuanzie hapo
 
Mkandara narudia tena
Warioba na tume wamesema kuwa ili kuondoa reli, dhahabu n.k. katika mambo yasiyo ya muungano Tanganyika irudi.

Huwezi kuondoa mambo yasiyo ya muungano ukawapa Kenya wayashughulikie.
Warioba kasema ili kuondoa Tanganyika isivae koti haramu la Tanzania, tuwe na Tanganyika, znz na shirikisho.

Mkandara, wewe model yako unayoshauri ni ipi tofauti na ya Warioba?

Hapa hakuna maneno ya ujamaa au ujima, ni swali na jibu.
Tuonyeshe unapendekeza serikli 2 na zifanye shughuli kwa utaratibu gani.
 
Mkandara, halafu pia ueleze wana jamvi hivi mchango wa znz ni jina tu.
Kama Tanganyika ikichangia jina (kumbuka ni Tz na znz) huo muunano unaendeshwaje?

Uhalali wa znz kuchota tu unapatikana kwa jina?
Na kwanini Mtanganyika mwenye jina pia asione kaumizwa.
 
Mkandara

Kwanza niondoe upotoshaji ulioufanya dhidi yangu, mimi sio shabiki wa Chadema bali ni muumini wa itikadi ya Chadema,

Pili, hebu tusaidie kujua namna Tanganyika itakavyovua koti la Muungano bila kuathiri dhana ya muungano huu.

Tatu, nitajie matusi mawili tu ya Tundu Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara narudia tena
Warioba na tume wamesema kuwa ili kuondoa reli, dhahabu n.k. katika mambo yasiyo ya muungano Tanganyika irudi.

Huwezi kuondoa mambo yasiyo ya muungano ukawapa Kenya wayashughulikie.
Warioba kasema ili kuondoa Tanganyika isivae koti haramu la Tanzania, tuwe na Tanganyika, znz na shirikisho.

Mkandara, wewe model yako unayoshauri ni ipi tofauti na ya Warioba?

Hapa hakuna maneno ya ujamaa au ujima, ni swali na jibu.
Tuonyeshe unapendekeza serikli 2 na zifanye shughuli kwa utaratibu gani.
Nimeshasema ya kwamba kuiweka reli kuwa sii ya Muungano ndio chanzo cha mapungufu ya Muungano wetu kwa sababu hili neno mambo yasiyokuwa ya Muungano ni lugha chafu na kukosa nidhamu. Uhalali wa serikali za muungano ni MAMLAKA ya shughuli za serikali kuwa sii ya muungano kwa maana ya kwamba kila nchi nitashughulika kuendesha serikali yake ndani ya Muungano ambao ni serikali kuu yenye wizara zote. Nitarudia tena kusema hivi hakuna nchi au Taifa duniani ambalo linaweka wizara nzima ya Usafiri kuwa sii ya mambo ya Muungano na hivyo hata mapato yake hayawahusu washirika - HAKUNA ila Tanznaia nyumba ya umaskini. Kilichopo ni mamlaka ya kusimamia shughuli hizo na baadhi ya sheria ndizo huwa sii za muungano japo nyumba ni moja.

Hivyo kama Bara tuna reli pato lake linakuwa asilimia 40 kwa bara na ile 60 kwa JMT kiasi kwamba Znz watafaidika toka ktk asilimia ile 60. Kinachofanyika ktk mamlaka haya ni kugawana majukumu ya kazi na ukusanyaji kodi kurahisisha kazi na ufanisi na sii kugawana umaskini ati kila mtu na chake.

Ni kama vile unavyoweza wewe unagawana majukumu na Mkeo ndani ya nyumba, hii haina maana hata mapato ya majukumu hayo hayamhusu mwenza. Hii ni tabia ya kishenzi ambayo wapo wanaume huwanyanyasa wake zao na kuwakwaza kwa kusema hili gari ni langu, hii nyumba yangu wewe kuhuja na kitu hapa ili mradi kuweka mipaka mkeo ajue hana kitu ndani ya ndoa. Lugha mnayoitumia ni sawa na kumwambia mkeo wewe umeleta nini ndani ya ndoa hii! huu ni uchenzi mkuu wangu na sidhani kama unafanya hivo!.

Sijui kama umenielewa maana kama hujaishi nchi zenye Muungano uwe wa federation au Kisiasa huwezi kuelewa mamlaka haya hugawanywa vipi. Kila nchi nilowahi kuitembelea utakuta shughuli zote za serikali hufanywa na nchi husika ambayo ni sehemu ya Utaifa wao hivyo pato lolote linalopatikana linawahusu washuirika pia japo kwa asilimia ndogo wakati huo huo ncjhi ilikuwa na mali hiyo hufaidika kwa asilimia 40 kama nilivyotolea mfano huko nyuma.

Labda nikupe mfano, Katika nyumba yako wewe unaweza kutokuwa unatayarisha chakula, hufui nguo, na maangalizi mengine ya nyumbani lakini wewe ndiye unayefanya kazi na kulisha familia. Isije kuwa kwa sababu hiyo ukasema gari unaloendea kazini ni lako mkeo hana mamlaka nalo, hii ni lugha chafu inayoharibu unyumba hasa pale mkeo anapodai kwa nini gari hilo lisiwe la wote. Hivyo Warioba na kundi lake wamekosea pale wanapotaka kuirudisha Tanganyika ili tugawane kwa uuwiano mambo yasokuwa ya Muungano kama vile tunagawa kila mtu na chake ila tukutane kwa shirikisho kitandani. Hii ndoa kweli?

Sipingi serikali 3 wala sina tatizo na badiliko lolote la muundo wa serikali isipokuwa mapendekezo ya Warioba kuirudisha Tanganyika ni kuelekea ktk divorce maana hii ni clear separation na tunaisoma ktk kila mstari wa mapendekezo. Model yangu nimeisema sana bado hunielewi na nadhani hutanielewa ila labda kwa wasomaji wengine. Muundo bora ni sawa na ule wa USA au Canada lakini sio kwa leo wala kesho, tupate kwanza Katiba Bora itakayo vunja mizizi yote ya ukosefu wa Uzalendo a kuendelea kutumia katiba ya CCM ya mwaka 1977mwaka hadi mwaka tukifanya marekebisho tu. Huu sii wakati wa kudai serikali 1, au 3 aidha tumechelewa ama tusubiri kwanza baada ya katiba mpya ipatikane na tuvunje zile itikadi za UCCM kuwa wameshika Hatamu.

Tunataka serikari 3 lazima iwe ktk mamlaka ya kuendesha shughuli za serikali kama vile tuna serikali moja ya Muungano ila imegawanyika ktk nchi 2. Hiyio nyumba nilozungumzia hapo juu ndio JMT. Dhahabu ya Geita lazima iwanufaishe Zanzibar kama vile sisi tutanufaika na Mafuta, Gas au karafu ya Zanzibar japo kidogo toka ile asilimi 60 walochangia ktk mfuko wa Taifa. Na hii ni kwa wizara zote, taasiasi zote, biashsra zote mchango ni huo huo hakuna Unafuu.

Na ikiwa Zanzibar watachangia mil 2 ktk mfuko wa Taifa wakati wao ni mil. 2 msifikiri ya kwamba mbona Tanganyika inachangia mil 40? hawa wanatunyonya pasipo kuzingatia kwamba Bara kuna watu mil. 45 hivyo Znz Wamechangia zaidi yetu kiasimilia. Watu mnachanganyikiwa na jambo dogo sana mkaacha makubwa ambayo hadi leo CCM imekuwa ikiyatumia kupata ushindi, kuongoza nchi kwa mabavu na kadhalika.

Serikali 3 haiwezi uondoa mabavu ya CCM hata kidogo kwa sababu Mamlaka hayo anayoyataka Warioba ni kuzitenganisha nchi tu wakati CCM itaendelea kumiliki nguvu zake pande zote mbili maana hakuna kitakacho badilika. Mfumo wa Kinafiki wa kujenga WAHESHIMIWA utaendelea kuwepo iwe tuna Tanganyika au laa. Na kinachonifanya nipingane na Warioba zaidi ni kwamba yeye kapewa kazi ya kuratibu Katiba MPYA hivyo malengo ni kukusanya mawazo ya wananchi kuhusiana na katiba ya nchi ilokuwa na mapungufu ktk mahitaji ya wananchi. Sasa yeye na kamati yake badala ya kutafuta utunzi wa Katiba wametuingia choo cha kike kuanza kujadili Muungano wetu.

Kama swala lingekuwa kuunda katiba ya Tanganyika basi hoja nyingi za Warioba ningekubaliana nazo isipokuwa hawa watu wamepewa kazi ya Katiba ya Muungano.

Wamepewa kazi ya kuratibu na kutunga mwongozo wa malezi bora ya mtoto alozaliwa, kina Warioba wanarudi na kusema Aaah mbona mtoto huyu alizaliwa nje ya ndoa? ni mtoto wa Haramu huyu hafai ni lazima kwanza tuirudishe ndoa yao kwa Ubatizo, wakati swala hapa ni malezi ya mtoto.

Kama kweli kulikuwa na uharamu basi ulifanywa na wazazi ambao kwa maridhiano yao walikubali kulala na kutunga mimba ya mtoto huyu Tanzania - Uharamu wake unatoka wapi?. Kumuadhibu mtoto huyu Tanzania kwa sababu mnafikiri Nyerere na Karume walikwenda kinyume cha sheria na sijui sheria ya nani ni kutafuta majanga zaidi.
 
Mkandara

Kwanza niondoe upotoshaji ulioufanya dhidi yangu, mimi sio shabiki wa Chadema bali ni muumini wa itikadi ya Chadema,

Pili, hebu tusaidie kujua namna Tanganyika itakavyovua koti la Muungano bila kuathiri dhana ya muungano huu.

Tatu, nitajie matusi mawili tu ya Tundu Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere.
Swali lako la Pili linajibu swala lako la kwanza ... Ni mshabiki tu ambaye hataona matusi aloyafanya TL. na vigumu wewe kukubali kwa sababu shabiki ni sawa na nyani asoweza kuona makalio yake!
 
Ombi langu kwa Mh. James Francis Mbatia, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na Mh. Freeman Aikaeli Mbowe na wote wale wanaowaunga mkono ndani ya Bunge Maalum La Katiba; jahazi la taifa linaenda mrama na kwa sasa makasia yako mikononi mwenu, ni jukumu lenu kutuvusha salama sisi wananchi. Hao manyang'au ya CCM hayana nia wala sababu za kuheshimu maoni ya wananchi na mkilegeza tu juhudi zenu katika kuliokoa taifa, tumezama. Tafadhalini msituangushe...mkifanya kosa, historia itawahukumu.

Mkuu Mag3, hao wanasiasa uliowataja laiti wasingejichukulia uongozi wa UKAWA inawezekana kabisa hoja za msingi juu ya Katiba kutoka makundi ya wachache zingepewa uzito unaostahili. Wanasiasa hao wote ni wabahatishaji (opportunists), mapandikizi na ambao kwa kiasi kikubwa ni sababu ya upinzani legelege baada ya miaka zaidi ya 20 ya vyama vingi.

Watch this space; labda wakae pembeni tusikie sauti kutoka kwa watu tofauti, UKAWA huenda imeshajifia yenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Swali lako la Pili linajibu swala lako la kwanza ... Ni mshabiki tu ambaye hataona matusi aloyafanya TL. na vigumu wewe kukubali kwa sababu shabiki ni sawa na nyani asoweza kuona makalio yake!

Mkandara

Ni wewe kweli au??
 
Last edited by a moderator:
Swali lako la Pili linajibu swala lako la kwanza ... Ni mshabiki tu ambaye hataona matusi aloyafanya TL. na vigumu wewe kukubali kwa sababu shabiki ni sawa na nyani asoweza kuona makalio yake!

Ipi tofauti kubwa iliyopo kati ya aliyosema lissu na aliyosema PIUS MSEKWA kwamba mwalimu aliamka na kutoa tu amri ya kuifutilia mbali Tanganyika bila ya kufuata utaratibu na sheria?

Kwanini hamsemi MSEKWA kamtusi mwalimu nyerere?

Double standards!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
3 days to go......JK akipiga jaramba huku akiendelea kusaidiwa na mjadala wa Dodoma ambao bado umebakia kuwa attention ya wananchi hadi sasa.......Wengine ni kama tunasubiri miujiza ya steringi kutokufa hadi mwisho wa filamu......

Mkuu Nguruvi3 ameandika mambo mazito na muhimu sana, Dhamira chafu tu ndio inayoweza kupinga maono yake.
 
Last edited by a moderator:
Ipi tofauti kubwa iliyopo kati ya aliyosema lissu na aliyosema PIUS MSEKWA kwamba mwalimu aliamka na kutoa tu amri ya kuifutilia mbali Tanganyika bila ya kufuata utaratibu na sheria?

Kwanini hamsemi MSEKWA kamtusi mwalimu nyerere?

Double standards!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi pengine huelewi maana naposema matusi kwa sababu hapa tuna deal na ukweli zaidi ya fikra za mtu ama taarifa. Katika kuunda Mungano kiongozi yeyote anaweza kuamka asubuhi akaamua jambo lolote na kukawa na ukweli lakini tunapozungumzia swala la Muungano hakuna Formula ya Kisheria. Kikubwa ni makubaliano iwe kwa maandishi ama kauli na yanaweza fikiwa kwa njia tofauti.

Kwa TJ kusema Muungano wetu ni batili na hata hati ya Muungano ni feki na kuwatuhumu viongozi hawa kwa kula njama ni utovu wa nidhamu hasa ktk nchi ambayo tayari imekwisha tambuliwa na Umoja wa Mataifa. Kama nilivyosema hakuna formula ya kuunda Muungano ama nchi kwa sababu Sisi tulikuwa koloni la Mjarumani paspo rishaa ya wananchi na tukawa chini ya Muingereza na hata Uhuru wetu hapakuwa na ridhaa ama sheria inayotakiwa kufuatwa ktk kutoa Uhur wa nchi. Kuna nci zilipigana viya kuupata Uhuru wake huwezi kusema haikuwa halali ama kufuata sheria hakuna kitu hicho.

Nitarudia kusema kwa mfano, wewe unaweza tunga mimba kwa mapenzi ya siku moja tu na watu wakalizungumzia hilo lakini yule atakaye sema ulim rape mwanamke na kupata mimba hili ni tusi ikiwa wewe unaamini yalikuwa makubaliano baina yenu japo kwa siku moja. Sijui umenielewa! Kilichoniudhi zaidi kuhusu TL ni kuyasema hayo mbele ya baraza la kutunga katiba ambayo yeye mwenyewe haoni Uhalali wa kuwepo nchi hii ya tanzania ilomsomesha na kumpa nafasi hata ya kuwa Mbunge aloapa kuilinda nchi hii leo huyu mjumbe wangu anakuja na matusi mazito juu ya nchi yangu niiipendayo kwa kuiita FAKE. Mpuuzi sana huyu tena ni mtu wa kujisikia saana kuwa yeye mbora sana kumbe mara kibao huzungumza madudu...

Yericko Nyerere,
Mkuu wangu ni mimi tena inabidi tuonane maana nipo mujini labda utanielewa vizuri zaidi tukiwa ana kwa ana. Upuuzi unaoendelea Bungeni ni upotoshaji ambao unatuweka ktk nafasi mbaya sana kisiasa. Kumbuka mimi hutazama mbali zaidi ya kile mnachokitazama kwa maana Mdanganyika maisha yake ni ya siku kwa siku. Ushindi wa Bungeni dhidi ya CCM sio Ushindi wa Mtanzania ikiwa tunaiweka nchi yetu ktk hatari kubwa. Hii habari ya kuungana na kina Jussa imetoka wapi? au kwa sababu mnafikiri kuunda umoja ktk katiba inapoteza ukweli kwamba hawa watu wanatupiga vita nje. Hii ni mada yao na sisi tunasherehekea kwa kuvikwa kofia ya mtungo!

Mimi siku zote sina ushabiki, Zitto akiboronga nilimvaa bila kusita, iwe JK, Mbowe Dr. Slaa, Sheikh Mkuu, Mchungaji na wengineo kwa sababu neno moja jukwaani linaweza kabisa kuliweka Taifa ktk nafasi mbaya sana hata kama ni mawazo ya mtu binafsi. Utumiaji lugha chafu au mabavu pale pasipostahili sikubaliani nako ikiwa haijengi chama au Taifa. Majuzi tu waziri mmoja wa CCM kenda kanisani na kubwabwaja Udini, kitendo kile kama kuna mwana CCM amekisifia ama Kushabikia basi ujue huyu mtu ana matatizo, ni Mshabiki maana kwao washabiki hawana itikadi isipokuwa ugonjwa wa kupenda iwe ni Arsenal sijui ManU hushindwa kwa njama tu za marefa. Utanisamehe lakini nakusoma sana hapa na Tweet hujifichi una watu wako.

Kifupi mimi nitasema tena nachokitaka ni Katiba mpya hii habari ya serikali 3 ni kupoteza muda maana huko hakuna dawa ya mapungufu ya Muungano. Kero zote za Muungano ni matokeo ya sisi kulimbikiza mapungufu ya Muungano kwa kuendelea kutumia katiba ya CCM ambayo ina mfumo wa Ujima ndani yake.

Tanganyika sii tu tumevaa koti la Muungano hata CCM imevaa koti na hivi sasa mwanasiasa yeyote anayeinukia kupambana na katiba ile huwekwa sawa akapewa nafasi ya uongozi kupoza kelele za mlangoni. Hii tabia ya kina Maalim Seif Hamad sintokubaliana nayo hata kidogo maana hawa wajumbe wetu, viongozi wetu wanachota mabillioni kwa kusema tu majuklwaani ilihali wananchi wanashinda siku nzima kwa mlo mmoja..
 
Muundo bora ni sawa na ule wa USA au Canada lakini sio kwa leo wala kesho, tupate kwanza Katiba Bora itakayo vunja mizizi yote ya ukosefu wa Uzalendo a kuendelea kutumia katiba ya CCM ya mwaka 1977mwaka hadi mwaka tukifanya marekebisho tu. Huu sii wakati wa kudai serikali 1, au 3 aidha tumechelewa ama tusubiri kwanza baada ya katiba mpya ipatikane na tuvunje zile itikadi za UCCM kuwa wameshika Hatamu.

Kwanini miaka 50 iliyopita (1964), muundo bora ulioneka kuwa ni ule wa United Kingdom (unitary system), na miaka 50 baadae, muundo bora usiwe wa shirikisho kama USA? Mwalimu alitamka wazi kwamba tumeazima mfumo wa UK. Kwa maana nyingine - kwanini tulikuwa tayari kumuiga UK miaka mitatu baada ya uhuru, lakini miaka 50 baadae kuiga Federation - kwanini tusiwe tayari?

Mkuu Mkandara, kama muundo wa shirikisho haufai leo, kwanini miaka 20 iliyopita ulionekana kufaa? Baada ya kiwewe cha ujio wa vyama vingi vya siasa nchini, ikawa wazi kwamba uchaguzi mkuu 1995 ungeweza zaa rais wa zanzibar toka cuf na rais wa muungano toka ccm, huku nchi ikiwa na makamu wa rais kutoka cuf (rais wa znz). Jaji bomani akateuliwa kutatua hilo, ndio akapendekeza mfumo wa mgombea mwenza huku akiitaja "marekani", na hili ni shirikisho unalosema halitufai. Hivyo ndivyo mgombea mwenza wa kwanza - marehemu Dr Omar Juma akapatikana, na ccm kupumua - japo kwa muda. Hata Dr Shein, na Bilal, wao ni makamo wa Rais kishirikisho. Ni mfumo ule ule uliopendekezwa na mkataba wa muungano (1964) huku utekelezaji wake ukiwa na kasoro.

Pia unashambulia sana neno "shirikisho" bila kujua you are shooting on your own foot. Maana rahisi ya shirikisho ni hii:
A system of government in which power is divided between a central authority and constituent political units.

Hivi hauoni tuki - relate hii definition na muungano uliopo, si tuna central government (serikali ya muungano) na zanzibar kama "a constituent political unit" tayari? Hivi hamuoni kwamba kwa miaka 50, tuna:
Shirikisho la Serikali Mbili????

Rasimu ya katiba inachofanya ni kuleta the other constituent political unit iwe wazi, isiwe chini ya Carpet (Tanganyika). Basi.

Huwa sipendi kutumia mifano ya ndoa na familia kama ulivyozoea, lakini niseme tu kwamba - Tanganyika mnamficha ndani ya nyumba wageni wasimuone kwa vile ni kichaa na ni nyie mlimroga. Lakini kelele zake haziachi sikika.

Hivi mna akili sawa kweli kukaa kwenye zile kamati kumi na mbili na kuja eti na maoni ya wengi kuondoa neno "shirikisho" kwenye sura ya kwanza, na kuunguza fedha za walipa kodi wakati in practice, kwa miaka 50, Tanzania ni shirikisho la serikali mbili?

Hakika mtaumbuka sana. Ni suala la muda tu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi, inaonekana pamoja na usomi wake wote, Mkandara hajui hata mfumo tulio nao hivi sasa unafanyaje kazi. Ngoja nimpe A,B,C ya tunaouita mfumo wa serikali mbili ndani ya nchi mbili...tunazo mamlaka tatu;

  1. Kuna mamlaka inayosimamia mambo ya Muungano.
  2. Kuna mamlaka inayosimamia mambo yasiyo ya Muungano kwa Zanzibar
  3. Kuna mamlaka inayosimamia mambo yasiyo ya Muungano kwa (Tanganyika) Tanzania bara.
Mtizamo wa watu kama Mkandara naufananisha na msimamo wa Wamarekani wasiompenda Obama. Utawakuta wakipinga kinachoitwa Obama care huku wakiisifia ACA, Affordable Care Act bila kujua ni kitu hicho hicho. Saha hapa mtu anakiri kwamba mamlaka ziko tatu lakini hapo hapo anapinga serikali tatu bila kujua kwamba ni kitu kile kile. Inaonekana wasichotaka kukisikia ni maneno serikali ya Tanganyika na wakati huo huo hawaoni tatizo kuitaja na kuitetea serikali ya Zanzibar; eti serikali ya Zanzibar ikae na serikali ya Muungano ili waongee nini? Mambo ya Zanzibar, ya Muungano ama ya Tanganyika? CCM ilijiunga na CUF kuunda serikali lakini leo Chadema ikijiunga na CUF hiyo hiyo kudai katiba ya wananchi, huo umoja unatiliwa shaka na kuhusishwa na ugaidi/usultani! Akili gani hizi?

Mkandara, ukweli ni kwamba hapa hatuna Muungano, tuna shirikisho, period. Hatuwezi kuwa na Muungano tukawa na serikali mbili, tatu, nne, tano na kuendelea! Matapeli wa kisiasa ndio wanataka watuaminishe kuwa tuna Muungano wa serikali mbili wapate pa kuficha uovu wanaoutendea Tanganyika, wapate kichaka cha kufujia rasilimali za Watanganyika na wapate kambi ya kuendeshea ufisadi kwa kung'ang'ania madaraka. Sasa ilichofanya Tume ni kuuambia utawala kuwa mbinu zao chafu wananchi wamezishtukia, Watanganyika kama walivyo Wazanzibar wamechoka kudhulumiwa kwa kivuli cha Muungano. The good news kwao ni kwamba wapo watu kama wewe, tena wasomi, mko tayari kutumiwa/kutumika kutetea hiyo hali; the bad news kwenu ni kwamba wananchi walio wengi wameamka na kwa sauti kubwa wamesema imetosha.
 
Kwanini miaka 50 iliyopita (1964), muundo bora ulioneka kuwa ni ule wa United Kingdom (unitary system), na miaka 50 baadae, muundo bora usiwe wa shirikisho kama USA? Mwalimu alitamka wazi kwamba tumeazima mfumo wa UK. Kwa maana nyingine - kwanini tulikuwa tayari kumuiga UK miaka mitatu baada ya uhuru, lakini miaka 50 baadae kuiga Federation - kwanini tusiwe tayari?

Mkuu Mkandara, kama muundo wa shirikisho haufai leo, kwanini miaka 20 iliyopita ulionekana kufaa? Baada ya kiwewe cha ujio wa vyama vingi vya siasa nchini, ikawa wazi kwamba uchaguzi mkuu 1995 ungeweza zaa rais wa zanzibar toka cuf na rais wa muungano toka ccm, huku nchi ikiwa na makamu wa rais kutoka cuf (rais wa znz). Jaji bomani akateuliwa kutatua hilo, ndio akapendekeza mfumo wa mgombea mwenza huku akiitaja "marekani", na hili ni shirikisho unalosema halitufai. Hivyo ndivyo mgombea mwenza wa kwanza - marehemu Dr Omar Juma akapatikana, na ccm kupumua - japo kwa muda. Hata Dr Shein, na Bilal, wao ni makamo wa Rais kishirikisho. Ni mfumo ule ule uliopendekezwa na mkataba wa muungano (1964) huku utekelezaji wake ukiwa na kasoro.

Pia unashambulia sana neno "shirikisho" bila kujua you are shooting on your own foot. Maana rahisi ya shirikisho ni hii:

Hivi hauoni tuki - relate hii definition na muungano uliopo, si tuna central government (serikali ya muungano) na zanzibar kama "a constituent political unit" tayari? Hivi hamuoni kwamba kwa miaka 50, tuna:

Rasimu ya katiba inachofanya ni kuleta the other constituent political unit iwe wazi, isiwe chini ya Carpet (Tanganyika). Basi.

Huwa sipendi kutumia mifano ya ndoa na familia kama ulivyozoea, lakini niseme tu kwamba - Tanganyika mnamficha ndani ya nyumba wageni wasimuone kwa vile ni kichaa na ni nyie mlimroga. Lakini kelele zake haziachi sikika.

Hivi mna akili sawa kweli kukaa kwenye zile kamati kumi na mbili na kuja eti na maoni ya wengi kuondoa neno "shirikisho" kwenye sura ya kwanza, na kuunguza fedha za walipa kodi wakati in practice, kwa miaka 50, Tanzania ni shirikisho la serikali mbili?

Hakika mtaumbuka sana. Ni suala la muda tu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Sijakuelewa kabisa... Wapi Nyerere alisema muundo wa muungano wetu umeiga mfumo wa UK? na unafanana vipi? Ukinambia USSR nitakubali lakini UK sidhani na hata hivyo tumekuwa na central Government miaka 12 baada ya muungano. Nijuavyo hakuna uuwiano waaina yoyote baina ya muungano wetu na ule wa UK maana sisi hatujawahi kuwa na mfano wa King Henry.

Na kwa nini tufuate mfano wa US leo hii ikiwa wao toka waungane hawajabadilisha muundo leo zaidi ya miaka 200. UK, US Canada na nchi nyingine zote zina muundo ule ule uloasisiwa na viongozi wao kwa miaka zaidi ya 200, sisi miaka 50 tu tunaanza kuchoka. Huoni kaa tuna matatizo?

Ni nani alosema muundo wa shirikisho ulifaa baada ya ujio wa vyama vingi vya siasa nchini? Wale wote walisema ama kuona shirikisho linafaa ni kutokana na kero za muungano na sii mapungufu ya muungano. Na kama nilivyosema Wadanganyika mna deal sana na kerio ambazo ni matokeo ya kulimbikiza mapungufu hadi yanapokuwa kero ndio mna react.

Haya maswala ya Urais wa Zanzibar na JMT ni ulafi wa viongozi wenyewe na sii ridhaa ya wananchi. Wanaosema kuhusu rais wa Zanzibar awe hivi ama vile ni hao hao wanaotaka kugiombea Urais kesho, sioni sababu ya kuwa na rais wa Zanzibar na JMT ikiwa kweli viongozi wetu wana Uzalendo wa kweli.

Yote hii inatokana na roho zetu mbaya na unafiki ndio maana Znz wanaweka madai yao kinafiki. Hivi kweli wewe unaamini rais wa Tanzania akiwa Mzanzibar ataipendelea Zanzibar kuliko Bara? hivi kweli tukiandika katiba bora yenye uwazi na uwajibikaji kuna haja ya kuwa na uuwiano wa viongozi kutokana na nchi au majimbo! Kama huu sii ukabila ama Ubaguzi ni kitr gani? Hivi kweli wewe unaamini JK kwa sababu ni Mbara basi anaipendelea Bara kuliko Zanzibar na akija Dr A mwinyi ataipendelea Znz kuliko bara? basi sisi waafrika tuna matatizo maana mifano hii iko Afrika tu.

Hizi fikra za kwamba Mzanzibar ataiopenda zanzibar zaid ya bara ni fikra za wale wasiopenda Muungano wetu kwa sababu huko mnakotaka kuiga hakuna kiongozi anayefagilia kwao kwanza Obama ni rais wa Marekani ni rais wa wote sii wa Illinois ala Kenya na ndio maana Kenya wanashindwa kumuelewa. Prime minister wa Canada ni Prime minister wa wote hakuna anayejali katoka mkoa gani au kijiji gani..Ndio kusema sisi tunaofikiria Ukabila, na asili zetu inatufanya kuwa - MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO.
 
Basi ndio maana uelewa wako ni mdogo sana. Yani muungano ulioshinikizwa na UK na USA uige mfumo wa Soviet wakati USA na UK waliingilia kati muungano kwa nia ya kudhibiti soviet na communism? Rudi ukafanye utafiti vizuri. Kuna mahali Nyerere amenukuliwa wazi akisema mfumo wetu tumeiga ule wa United Kingdom. Nina vitabu vingi sana nasoma, nikipata the exact source nitakuletea hapa.
Na kwa nini tufuate mfano wa US leo hii ikiwa wao toka waungane hawajabadilisha muundo leo zaidi ya miaka 200.
Kwanini tulifuata mfano wa UK ambayo haina written constitution?
UK, US Canada na nchi nyingine zote zina muundo ule ule uloasisiwa na viongozi wao kwa miaka zaidi ya 200, sisi miaka 50 tu tunaanza kuchoka. Huoni kaa tuna matatizo?
Mwenye tatizo ni wewe ambae hauelewi kwamba UK ambayo tumemuiga, muungano wake na Ireland ukafa 1922 kwa sababu hizi hizi za muungano wa mabavu, UK ikaingia katika fujo za kigaidi baada ya ireland kaskazini kuchoka kabla ya England kuwapa fiscal and political autonomy ambayo hata sisi Tanganyika ndio hiyo tunaitafuta; na mwakani, Scotland wanapiga kura ya maoni kuamua kubaki au kutoka kwenye muungano na England. Unashangaa sisi miaka hamsini tu tumechoka? Nyinyi ndio wenye hoja kwamba 80pct ya watanzania wamezaliwa ndani ya muungano, hivyo hawaifahamu na hawana haja na serikali ya tatu. Scotland waliungana na England miaka 400 iliyopita, na leo, wanaodai autonomy, sio tu kwamba 100pct yao wamezaliwa ndani ya muungano, bali hata bibi, babu, nyanya, vitunguu na karoti zao.

Jifunze kutafiti. England sasa inaangalia uwezekano wa federation yake na wales na scotland kama solution. Unitary system ni TATIZO kwa uchumi, amani, na utulivu.

Ni nani alosema muundo wa shirikisho ulifaa baada ya ujio wa vyama vingi vya siasa nchini?

Jaji Bomani baada ya kupewa kazi hiyo na Nyerere kutatua suala la CUF kushinda znz na CCM bara kufuatia mfumo wa vyama vingi. Makamu wa rais kuanzia marehemu Dr Omar Juma hado leo Dr. Billal ni Makamu wa kishirikisho, na Jaji Bomani aliweka hilo wazi.

Wale wote walisema ama kuona shirikisho linafaa ni kutokana na kero za muungano na sii mapungufu ya muungano.
Hapa unajichanganya tu. "Kero za muungano", "mapungufu ya muungano", same difference?

Na kama nilivyosema Wadanganyika mna deal sana na kerio ambazo ni matokeo ya kulimbikiza mapungufu hadi yanapokuwa kero ndio mna react.
Unaendelea kujichanganya - kero na matokeo ya mapungufu ndio kitu gani? By the way, wengi wetu sio "wadanganyika" tena bali sasa ni "watanganyika" kabla ya Utanzania. Kauli mbiu yetu kuelekea kura ya maoni ni: "Tanzania kwanza, Tanganyia KABLA"

Haya maswala ya Urais wa Zanzibar na JMT ni ulafi wa viongozi wenyewe na sii ridhaa ya wananchi. Wanaosema kuhusu rais wa Zanzibar awe hivi ama vile ni hao hao wanaotaka kugiombea Urais kesho, sioni sababu ya kuwa na rais wa Zanzibar na JMT ikiwa kweli viongozi wetu wana Uzalendo wa kweli.

Yote hii inatokana na roho zetu mbaya na unafiki ndio maana Znz wanaweka madai yao kinafiki. Hivi kweli wewe unaamini rais wa Tanzania akiwa Mzanzibar ataipendelea Zanzibar kuliko Bara? hivi kweli tukiandika katiba bora yenye uwazi na uwajibikaji kuna haja ya kuwa na uuwiano wa viongozi kutokana na nchi au majimbo! Kama huu sii ukabila ama Ubaguzi ni kitr gani? Hivi kweli wewe unaamini JK kwa sababu ni Mbara basi anaipendelea Bara kuliko Zanzibar na akija Dr A mwinyi ataipendelea Znz kuliko bara? basi sisi waafrika tuna matatizo maana mifano hii iko Afrika tu.

Hizi fikra za kwamba Mzanzibar ataiopenda zanzibar zaid ya bara ni fikra za wale wasiopenda Muungano wetu kwa sababu huko mnakotaka kuiga hakuna kiongozi anayefagilia kwao kwanza Obama ni rais wa Marekani ni rais wa wote sii wa Illinois ala Kenya na ndio maana Kenya wanashindwa kumuelewa. Prime minister wa Canada ni Prime minister wa wote hakuna anayejali katoka mkoa gani au kijiji gani..Ndio kusema sisi tunaofikiria Ukabila, na asili zetu inatufanya kuwa - MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO.

Hizi ni porojo tu zenye lengo la kutuondoa kwenye mada. Nguruvi3 alizijadili sana. Nitazijadili tena kwenye uzi ninaoandaa sasa na nitakualika.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Sijakuelewa kabisa... Wapi Nyerere alisema muundo wa muungano wetu umeiga mfumo wa UK? na unafanana vipi? Ukinambia USSR nitakubali lakini UK sidhani na hata hivyo tumekuwa na central Government miaka 12 baada ya muungano. Nijuavyo hakuna uuwiano waaina yoyote baina ya muungano wetu na ule wa UK maana sisi hatujawahi kuwa na mfano wa King Henry.

Na kwa nini tufuate mfano wa US leo hii ikiwa wao toka waungane hawajabadilisha muundo leo zaidi ya miaka 200. UK, US Canada na nchi nyingine zote zina muundo ule ule uloasisiwa na viongozi wao kwa miaka zaidi ya 200, sisi miaka 50 tu tunaanza kuchoka. Huoni kaa tuna matatizo?

Ni nani alosema muundo wa shirikisho ulifaa baada ya ujio wa vyama vingi vya siasa nchini? Wale wote walisema ama kuona shirikisho linafaa ni kutokana na kero za muungano na sii mapungufu ya muungano. Na kama nilivyosema Wadanganyika mna deal sana na kerio ambazo ni matokeo ya kulimbikiza mapungufu hadi yanapokuwa kero ndio mna react.

Haya maswala ya Urais wa Zanzibar na JMT ni ulafi wa viongozi wenyewe na sii ridhaa ya wananchi. Wanaosema kuhusu rais wa Zanzibar awe hivi ama vile ni hao hao wanaotaka kugiombea Urais kesho, sioni sababu ya kuwa na rais wa Zanzibar na JMT ikiwa kweli viongozi wetu wana Uzalendo wa kweli.

Yote hii inatokana na roho zetu mbaya na unafiki ndio maana Znz wanaweka madai yao kinafiki. Hivi kweli wewe unaamini rais wa Tanzania akiwa Mzanzibar ataipendelea Zanzibar kuliko Bara? hivi kweli tukiandika katiba bora yenye uwazi na uwajibikaji kuna haja ya kuwa na uuwiano wa viongozi kutokana na nchi au majimbo! Kama huu sii ukabila ama Ubaguzi ni kitr gani? Hivi kweli wewe unaamini JK kwa sababu ni Mbara basi anaipendelea Bara kuliko Zanzibar na akija Dr A mwinyi ataipendelea Znz kuliko bara? basi sisi waafrika tuna matatizo maana mifano hii iko Afrika tu.

Hizi fikra za kwamba Mzanzibar ataiopenda zanzibar zaid ya bara ni fikra za wale wasiopenda Muungano wetu kwa sababu huko mnakotaka kuiga hakuna kiongozi anayefagilia kwao kwanza Obama ni rais wa Marekani ni rais wa wote sii wa Illinois ala Kenya na ndio maana Kenya wanashindwa kumuelewa. Prime minister wa Canada ni Prime minister wa wote hakuna anayejali katoka mkoa gani au kijiji gani..Ndio kusema sisi tunaofikiria Ukabila, na asili zetu inatufanya kuwa - MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO.
@Mkandara, lazima uelewe tofauti ya confederation, Federation na Union.
Canada haiukuanza na kubaki na mfumo huo kwa miaka zaidi ya 150. Rejea kuundwa kwa confedearion na kufikia federation.

Uwepo wa muungano wa aina yoyote kwa miaka 200 au zaidi hauna maana hakuna matatizo.
Canada wana tatizo na Quebec katika mfumo uliodumu zaidi ya miaka 150.
Mwaka jana Puerto Rico walikuwa na kura ya maoni kuamua wabaki na USA au waondoke

Sisi tuna Union ambayo ukiiangalia kwa macho angavu si sawa na fedeation.
Kulinganisha vitu hivyo kwa simple 200 years ni kulinganisha chenza na chungwa.
Chungwa na Chenza ni tofauti, ni rahisi sana kwa asiyevitambua kudhani is one and the same.

Hakuna kitu kinaitwa mapungufu au kero.
Hayo ni maneno ya wana siasa kuwababaisha watu, wengine huko hatupo.
Tunachojua ni kuwa kuna matatizo yanayotokana na muundo wa muungano.

Matatizo hayo sasa yamepamba moto kwa pande zote yakichaguzwa zaidi na hoja za uchumi.

Huwezi kuwa na znz pekee na znz katika JMT wakati huna mshirika mwingine katika JMT
Huyo mshirika mliyembatiza jina la bara au Tanzania bara historia yake haina miaka zaidi ya 50. Leo Tanganyika inaambiwa ifutwe ili kupisha mazingaombwe yafanyike.

Serikali 2 hazijatatua matatizo kwa miaka 50.
Narudia tena jana Samia Suluhu amesema zimebaki kero 3.
Iweje kero za miaka 50 zitatuliwe kwa wiki mbili baada ya htuba ya JK
Hizo kero zilizotafutiwa majawabu zinahusu Tanganyika?

Hapo nyuma umekiri uwepo wa Tanganyika(nukuu ipo) sasa katika kutatua kero nani alikuwepo kusimamia Tanganyika?

Hapo kuna ku solve tatizo kweli! S2 zikishalazimishwa maana yake ni kumwaga mtama kwa kuku, Watanganyika kama walivyosimama kudai nchi yao mbele ya mkoloni watairudisha tu.
Hapo ndipo tatizo litakapokuja.
Rule of the jungle, naomba mungu asaidie tusifike huko maana ni hatari kubwa!

Mkandara katika bandiko moja(nukuu ipo) anasema serikali ya shirikisho lazima isimamie mambo yoote. Bandiko linalofuata anasema Tanganyika imechukua mambo ya znz kwa koti la muungano. Bandiko lingine anasema ni vema tukatenga ya muungano na ya znz.

Mkandara anasema znz inaumia kutokana na muungano, wkati huo huo anasema kwa mfumo wa shirikisho znz itaumia sana. Hivi kama wanaumia na muungano, shirikisho linawaumiza vipi zaidi ya maumivu wanayoishi nayo.

Mkandara, znz imepewa fursa ya kuondoka katika maumivu, tunawasikia bungeni wakitaka serikali 2.
Hao ni wznz wenyewe, wengine akina Mansour wanataka muungano kwa video za majuzi tu.
Leo mwenye maumivu anang'an'gania kubanwa!

Hao ni wznz wenye nchi yao, wewe Mkandara una uchungu gani zaidi kuliko ule wa wakerewe wanaolipa kodi kwenda nchi jirani.

Tukamuuliza yasiyo ya muungano yaende wapi, hana jibu.

Kwavile hana msingi wa hoja anayotetea Mkandara anabadilisha position kila asubuhi.
Angalia mabandiko niliyomnukuu hapo juu

Hakuna haki, usawa wala wajibu kama znz itakuwa na sehemu mbili.
1. Changu ni changu kama wanavyoweka vikwazo kwa Watanganyika wakienda kwao
2. Chako ni changu kama wanavyokuja bara na kufadika na rasilimali wasizojua zinapataikanje isipokuwa kwa jina lao tu.

Tunataka Tanganyika kwa Watanganyika. Hutahitaji kunyonya ng'ombe asiye na chuchu!
 
Mkuu Mkandara anasema kazi ya Warioba ilikuwa kuratibu mawazo ya wananchi .
Anachosahau ni kuwa kuratibu mawazo ni pamoja na kuyafanyia kazi.

Mkandara amesahau kilichomkuta Sitta hadi mswada ukabadilishwa.

Ninamshangaa mwenzetu kwasababu wananchi hawajawahi kuulizwa kuhusu muungano, leo Mkandara anataka waboreshe kitu wasichokijua.

Mkuu Mkandara niembie lini na wapi mwananchi alishiriki kutengeneza muungano hadi ifike mahali tumombe aboreshe muungano huo

Ukimsoma Mkandara anasema federal gov kila mmoja anachangia serikali kuu. Ndivyo Warioba amesema.

Mkandara anasema serikali kuu ichangiwe kwa maana dhahabu ya Geita imnufaishe mzanzibar na mafuta na gesi ya znz yamnufaishe Mtanganyika.

Hivyo ndivyo ilivyo hadi sasa kuwa dhahabu ya Geita inalipia ulinzi na usalama wa mznz. Tatizo ni kuwa mznz keshaondoa mafuta na gesi, hataki tena liwe la muungano. Swali kwa Mkandara katika mazingira ya ubinafsi na uchoyo wa mznz inawezekanje kuwa na model ya Canada?

ZNZ hawataki kuwa na mambo ya muungano, wanataka wawe na yao.

Tumekubali na kusema yawe 7 kama muungano unatakiwa kuwepo.
Na katika hayo hayo 7 tuchangie kila mmoja kwa uwezo wake.

Hii habari ya znz kutumia jina la Tanzania kuwalipia madeni sasa mwisho.
Ni kutokana na ubwerere huo wznz hawajali muungano, wana kiburi na jeuri hata za kuamua nini tufanye na nini tusifanye.

Mkuu Mkandara, hivi kwenda kuomba watu 50 wa BLW kujenga vyoo vya shule zetu tunahitaji mhuri wa znz?

Tunahitaji mhuri wa kitu gani ikiwa sisi ndio wenye hizo resource?
Kwamba tuwe na rasilimali zetu wakati wa kuzitumia tuwaombe wznz. Please!

Tunataka Tanganyika kwa ajili ya Watanganyika.
Wakitaka yawe 7 kama hawataki 7 tuvunje jahazi, tutagawane mbao na misumari. Hatupo tayari kubebe furushi lisilo na tija tena!

CCM wakilazimisha, basi tutaikomboa Tanganyika.
Tutakwenda Oxford kutafuta vitabu vilivyomuondoa mwingiereza Tanganyika.

Nina hofu sijui kama kila mmoja atakuwa na subira za kusoma vitabu kwanza!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom