Kwanini miaka 50 iliyopita (1964), muundo bora ulioneka kuwa ni ule wa United Kingdom (unitary system), na miaka 50 baadae, muundo bora usiwe wa shirikisho kama USA? Mwalimu alitamka wazi kwamba tumeazima mfumo wa UK. Kwa maana nyingine - kwanini tulikuwa tayari kumuiga UK miaka mitatu baada ya uhuru, lakini miaka 50 baadae kuiga Federation - kwanini tusiwe tayari?
Mkuu
Mkandara, kama muundo wa shirikisho haufai leo, kwanini miaka 20 iliyopita ulionekana kufaa? Baada ya kiwewe cha ujio wa vyama vingi vya siasa nchini, ikawa wazi kwamba uchaguzi mkuu 1995 ungeweza zaa rais wa zanzibar toka cuf na rais wa muungano toka ccm, huku nchi ikiwa na makamu wa rais kutoka cuf (rais wa znz). Jaji bomani akateuliwa kutatua hilo, ndio akapendekeza mfumo wa mgombea mwenza huku akiitaja "marekani", na hili ni shirikisho unalosema halitufai. Hivyo ndivyo mgombea mwenza wa kwanza - marehemu Dr Omar Juma akapatikana, na ccm kupumua - japo kwa muda. Hata Dr Shein, na Bilal, wao ni makamo wa Rais kishirikisho. Ni mfumo ule ule uliopendekezwa na mkataba wa muungano (1964) huku utekelezaji wake ukiwa na kasoro.
Pia unashambulia sana neno "shirikisho" bila kujua you are shooting on your own foot. Maana rahisi ya shirikisho ni hii:
Hivi hauoni tuki - relate hii definition na muungano uliopo, si tuna central government (serikali ya muungano) na zanzibar kama "a constituent political unit" tayari? Hivi hamuoni kwamba kwa miaka 50, tuna:
Rasimu ya katiba inachofanya ni kuleta the other constituent political unit iwe wazi, isiwe chini ya Carpet (Tanganyika). Basi.
Huwa sipendi kutumia mifano ya ndoa na familia kama ulivyozoea, lakini niseme tu kwamba - Tanganyika mnamficha ndani ya nyumba wageni wasimuone kwa vile ni kichaa na ni nyie mlimroga. Lakini kelele zake haziachi sikika.
Hivi mna akili sawa kweli kukaa kwenye zile kamati kumi na mbili na kuja eti na maoni ya wengi kuondoa neno "shirikisho" kwenye sura ya kwanza, na kuunguza fedha za walipa kodi wakati in practice, kwa miaka 50, Tanzania ni shirikisho la serikali mbili?
Hakika mtaumbuka sana. Ni suala la muda tu.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums