Mkuu Three different people can witness the same event and each comes up with a different account of how it occurred!.
Wanachosema ni kwamba
1. Kwa Kila project ya Tanganyika (mambo yasokuwa ya Muungano) Tanganyika haihitaji ridhaa ya Wazanzibar japokuwa kwa kila project ya Zanzibar, Zanzibar inahitaji ridhaa ya Tanganyika ( mfano - OIC)
2. Kwa kila mpango wa project ya Tanganyika (mambo yasokuwa ya Muungano) Tanganyika imetumia jina la Tanzania kuvuta mikopo nje, kwa sababu Kimataifa nchi za Tangayika wala Zanzibar haziwezi kuvuta mikopo kwa sababu hazitambuliwi kama ni Taifa. nakuomba ufahamu tu ya kwamba lengo la TAIFA huru kuwa na kiti UN ni kutambuliwa kama TAIFA huru lenye serikali halali na hivyo kufungwa ktk sheria za Kimataifa katika maswala ya mawasiliano, trade, mikopo, na misaada ambayo mashirika ya Kimataifa yanapewa guarantee ya kuaminiwa.
Hivyo basi utakapo kuwa na serikali ya 3, hiyo ya Tanganyika bado nchi hii itahitaji kutumia jina la Tanzania ktk ushirika wake Kimataifa na mashirika ya nje. Na hivyo itaendelea kulivaa koti la Muungano kwa kutumia tena jina la Tanzania ktk mambo yasokuwa ya Muungano (yawe 7, 11 au 22). Hivyo muundo wa serikali 3 bado hautaondoa tatizo hilo bali Tanganyika itakuwa imelivua koti na kuliweka begani (kuondoa kero) ili upepo upite, lakini kama MAMBO YOTE YATAKUWA YA MUUNGANO tutalivua koti hilo -hakuna Utanganyika wala Uzanzibar kimataifa, hivyo kila jambo litahusu pande zote 2 (TANZANIA) na kupata ridhaa ya bunge la JMT.
Hii itasaidia kuondoa mamlaka kamili kwa viongozi wa serikali za Tanganyika (JMT) kuweka mikataba ya Tangayika chini ya meza, tena basi sio kwa Tanganyika ila kwa wao wenyewe kujilimbikiza utajiri kwa kutumia siri ya nchi. Miradi yote itajadiliwa na wizara kwa faida ya Tanzania, itapitishwa na bunge maana hakuna siri ya miradi ya uzalishaji, ushirika wa wabunge wa pande zote 2 (Utawla na Upinzani) watakuwa na nguvu ya kiitikadi kupinga ama kukubaiana na uwekezaji badala ya Uzanzibar na Ubara na mwisho wa siku ktk mapato ya mradi mzima kodi ya mapato (income tax) itawekwa ktk mafungu mawili, moja ya nchi (VAT) na nyingine ya Taifa ndio kusema kama ni asilimi 30, basi 20 ya Taifa na 10 ni ya nchi. Na ktk nchi, kila mkoa au jimbo litafaidika tena kwa asilimia toka ile asilimia 10. Haiwezekani gas itoke Mtwara waachwe watupu na visima vya maji, pasipo guarantee ya mapato ya kodi toka uwekezaji jimboni hapo.
Haya ni mapendekezo yangu ambayo hata nchi za magharibi wanatumia. kama wewe uanvyodai umewahi kufika Ontario, Canada basi bila shaka unaelewa ndani ya kodi ya HST (13%) kuna kodi 2 za PST (5%)ya jimbo na GST (8%) ya Taifa. Hivyo kila jimbo la Canada linapanga PST yake kuvutia uwekezaji sehemu hiyo kulingana na mahitaji yao lakini kodi ya GST imesimama pale pale kwa majimbo yote. Halafu kuna kodi za Mafuta ambazo kila jimbo linapanga kutokana na gharama za uagizaji, usafiri n.k hivyo bei ya mafuta inatofautiana kwa kila jimbo. yet kila Jimbo hadi taifa wanafaidika na uwekezezaji japo mafuta yanatoka Alberta! Na ndio maana Alberta sasa hivi ni jimbo tajiri kuliko majimbo yote Canada na hawana kinyongo ku share pato lake na majimbo mengine ya Canada kwani hata wao wanafaidika na rasirimali toka majimbo mengine ikiwa ni pamoja na nguvu za umeme wa nuklia toka sehemu nyinginezo.
Kwa hiyo Uwe na tanganyika anma laa maadam mambo yasokuw aya muungano yatakuwepo Tanganyika haitaweza kulivua koti kwa sababu Tanganyika sio TAIFA na haitambuliwi na Umoja wa Mataifa, njia pekee ya kuondokana na adha hii ni kuyafanya mambo yote yawe ya Muungano japo Wazanzibar hawataki na Watanganyika wanataka kujitenga. hatuwezi kukubali kushindwa na hoja za watu wachache wenye nia mbaya na Muungano wetu, njia pekee ya kuwakomoa wote hawa wenye fikra za Ubinafsi na kugawana mbao ni kuyafanya mambo yote yawe ya nmuungano kisha zitungwe sheria mpya za kodi - Tax income act ambayo itawezesha kila jimbo hadi taifa kufaidika na mapato haya.
Najua bado hujanielewa na hutaki kunielewa....
Point ya kwanza, ni kweli, lakini kumbuka kuwa Tanganyika ilitoa utaifa wake na kuukabidhi kwa Tanzania, kwa mujibu wa maneno yako mwenyewe.
Huwezi kulaumu Tanganyika kutodai ridhaa kwa mambo ya muungano. Tayari ni loser kwa kupoteza ID yake.
Znz ambayo ni semi autonomy inapaswa kuomba ridhaa kutoka Tanzania kwasababu ndani ya Tanzania znz imo.
Tanzania ndiyo imevaa Tanganyika na si kinyume chake. Kwa msingi huo aliyepoteza ID yake analaumiwaje?
Ni kwa njia gani Tanganyika ingeweza kupata ridhaa ikiwa yenyewe ilikasimu madaraka kwa Tanzania?
Point ya pili, Tume ya Warioba imeweka wazi, erikali washirika watapata dhamana ya mikopo kupitia serikali kuu.
maana yake ni kuwa Tanganyika itavua koti na kuwa sawa na znz mbele ya serikali ya shirikisho.
Hili linasisitiza umuhimu wa kutenga nchi hizi katika majukumu yake.
Mkuu huwezi kuwa na S2 ukawataka Watanganyika wapate ridhaa znz!
Tanzania imo Tanganyika na ZNZ hivyo huwezi kutenga znz na Tanganyika ukiwa na Tanzania bila Tanganyika. Ndivyo logic ilivyo.
Point ya tatu, njia pekee ya kuleta maridhiano kwa mujibu wako ni kufanya mambo yote ya muungano.
Well, hilo wznz hawataki miaka nenda rudi na ndicho chanzo cha wao kuondoa jambo moja baada ya jingine.
Kwa mfano, hatujavuna mafuta na gesi nini kiliwasukuma kuyaondoa. Nini kimewasuklumua kuondoa shirika la viwango, nini kimewasukuma kuondoa baraza la mitihani. Ukiangalia wanaondoa hata mambo ambayo ni huduma tu kwasababu ya uzanzibar.
Kuna sababu gani za kuwa HESLB na ZHESLB? Kuna ulazima gani?
Utaona wazi kuwa kinachowasukuma wznz ni umimi na ubinafsi. Ni kitu kinaitwa narcissism ili kizae Nepotism.
Narcissism and Nepotism ya wznz ndio imezaa loneliness ya Watanganyika na uprising.
Kwa miaka 50 Watanganyika waliridhika lakini sasa wamechoka.
Katiba ya znz ya 2010 imeundwa katika misingi ya proud, narcissism, Nepotism na 'superiority complex'.
Walidhani kuwa wao ni stake holder wakubwa katika muungano ili hali ni minority at any parameter you may want to use.
Kwa hiyo lazima kwanza ulaani matatizo yaliyosababishwa na znz, halafu ndipo ushauri the way forward.
Hatuwezi kuwa na mambo ya pamoja kama katiba ya znz ya 2010 ikiwa hai.
Suala la harmonized tax ndilo wznz hawataki kulisikia. Wanadai wanaibiwa, leo vipi tunaweza kuwa na kodi ya pamoja?
Mkuu hapa huoni unazungumzia impossible. Hoja yako ina mantiki sana na mfano uliotoa ndio hasa inavyopaswa kuwa, tatizo la wznz ni uwezo wa kutambua. Utawezaje kumshawishi kuwa bajeti yake ya 400B ingekuwa na maana kama angekubali kodi iwe ya pamoja. Ni hesabu tu na wao hawatumii hizo. Unaona hata msomi wa Ph.D bado hawezi kuliona, mvuvi utamshawishi nini.
Hatuwezi kuwa na mambo ya pamoja kama kujivunia uzanzibar ndiyo mantra. Unapojivunia uzanzibar tayari unamshawishi Mtanganyika naye ajivunie Utanganyika na ndicho kinachotokea. Katika mazingira hayo hakuna consensus tena lazima tukubali.
Misingi ya muungano imevunjwa na wznz na hakuna namna tunaweza kuirudisha Tanganyika katika chupa.
Mvinyo umefunguliwa na sasa watu wasubiri kileo na ulevi. Who is to blame, absolutely znz.
Na mwisho, huwezi kujenga utaifa mmoja ukiwa na utaifa mdogo ndani yake. Nipe mfano mmoja tu duniani ambapo nchi moja ina utaifa mdogo ndani yake. ZNZ kupitia katiba ya 2010 ni taifa, ni nchi na kila kitu, hatuwezi kuishi katika mazingira hayo. Kutokana na utaifa mdogo,sasa wanataka kuwa taifa kubwa kwa kudharau katiba. This is too low and too hard to swallow. Tupeni nafasi tujadili umasikini wa wataanganyika na si jinsi ya kuwafurahisha wznz.
Taifa letu halikupigania uhuru in order to appease zanzibar