UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

Source please!
Ila siyo mbaya kama itatokea.

Wabunge wa CCM wanazungumza hili, wajumbe wa CCM nec wanazungumza hili, Watu wa karibu na rais kikwete na familia wanazungumza hili, Watu walio karibu na mbatia, Mbowe na Lipumba wanazungumza hili. Awamu ya nne Watu wa aina hii wanazungumza wazi kwenye vijiwe vyetu vya kuhawa, sio Kama zamani.

Isitoshe, hata Mbowe na Lipumba wamekiri kwenye media (gazeti la ----- la Leo).

Sio Mbaya Kama itatokea maana yake nini? Jadili hoja - je ni sahihi kikwete to retreat au sio sahihi? Je how should ukawa respond?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tunarudia ,wapinzani walipokwenda IKULU hawakuambulia chochote zaidi ya kunywa juisi ya maembe.

Safari hii hawataambulia hata juice.

Unadhani mwenye duka siyo mfanya biashara? Kwamba anagawa juice tuu?

Sana sana atawapa kipande cha sababu ya Mshindi wakaoge.

Maana maji ukiyavulia nguo, huna budi kuyaoga.

Simlamu Lipumba kutuma mwakilishi b'se ataendaje dukani uchi wakati tayari keshayavulia maji nguo?
 
Hili nalo neno, neno zito.
 
Mkuu Nguruvi3 kuna kitu kimoja ambacho kidogo kina tatizo kuhusu UKAWA. Sijui kama watarudi wakiwa na msimamo mmoja kama walioondoka nao, au watarudi kama wakiwa ------------.

So far UKAWA kama suala la serikali 3, yaani kama CCM itaendelea kuhadaa watu kuwa ndio zinazofaa, na UKAWA wakaingia kwenye mkumbo huo, basi watakuwa wamelambishwa asali.
 
Nkaubaliana na Mag3 hapo juu kuwa Mkandara haeleweki ingawa anashangaa kwanini hatumwelewi.

Mkuu kwanza ukaazi wa Quebec au majimbo mengine sijui unazungumziaje kisiasa.
Unaweza kuhama kutoka Ontari ukaenda Alberta na kupiga kura kama ulivyo na haki ya kuchaguliwa. Ukaazi umewekwa kwasababu za mambo kama health care, haina maana ukienda Quebec unakosa haki kama raia wa Canada.

Nadhani unajaribu sana kutumia mifano ya huko uliko pengine ukidhani hatuna ufahamu huo.

Pili, unajichanganya sana unaposema undugu wetu ni wa karne. Undugu huo upo kwa Kenya, Msumbiji na Malawi kwa uchache. Hatuna muungano lakini tunaishi vema tu bila shaka.

Zanzibar hawapaswi kumwekea Mtanganyika kitambulisho cha ukazi. Wala hawapaswi kutangaza kuwa wao ni TAIFA nje ya hili tulilo nalo. Sasa wametangaza kuwa ni nchi ikiwa na kila kitu.

Hadi hapo mkuu muungano hakuna, unachotetea ni masilahi ya znz tu.

Nikupe mfano wa juzi. ZNZ wamepewa bilioni 15 zaidi mwaka huu kwasababu ya kodi ya wafanyakazi wa muungano wanaoishi Zanzibar. Wafanyakazi hao wanalipwa na Tanganyika kwasababu znz haina mchango na wala haijachangia takribai miaka 20 sasa.

Kwa maneno mengine, fursa za wznz kuishi Tanganyika ni pamoja na ajira za mambo yasiyowahusu. Na bado tunalipa mishahara hadi mawaziri wao wasiotuhusu.
Sasa tunawazawadia pesa za ili kuwatengenezea ajira.

Wale wabunge 81 wanaolipwa na Tanganyika, znz ina mchango gani.

Labda ueleze umma, hivi Mtanganyika anafaidika na nini na muungano huu zaidi ya mzigo wa gharama. Huenda kuna kitu hatuelewi.

Znz hawataki mambo yote yawe ya muungano ndiyo maana wanayanyofoa.
Wanachotaka ni jina ili wakija wadai kwa mgongo wa Tanzania.
Unapolaumu Tanganyika hutendi haki hata kidogo.

Mambo yote unayosema ni ya muungano huko nyuma umesema ni ya kinyemela na kuwaumiza wznz. Leo unasema yote ni ya muungano!

Hapa ndipo naungana na Mag3 kuhoji kama kweli mkuu unamahali pa kusimamia au ni shoot any moving object.

Kama wznz wameondoa mambo mengi, sisi tunasema basi 7 yawe yetu.
Kama hawataki hatuna sababu za kuwazuia, tunawaacha waendelee na mipango ya TAIFA lao.

Kwani mkuu, tukivunja jahazi na kugawana mbao kuna tatizo gani kwa Tanganyika, na pili, kwa znz?
Mkuu unazidi kulikoroga sasa nitakujibu kwa ufupi zaidi. Huwezi kutoka Ontario ukaenda kupiga kura Quebec pasipo wewe kuwa mkazi wa Quebec. Nilikwambia pia ya kwamba huwezi kwenda Quebec au jimbo lolote kugombea uongozi ikiwa wewe sii mkazi wa jimbo hilo wenzatu hawana makabila wala Uzawa isipokuwa ni raia na unaishi wapi.

Tena huko kuna record ya kila raia kiasi kwamba hata wanapokuja mlangoni wanajua nyumba hiyo wnaishi raia wangapi na majina yao. wanajua hadi wahamiaji wakazi wasokuwa na right ya kupiga kura huwezi kujipachika ati ukatoka Ontario kwenda kupiga kura Quebec. Tena basi kama hukujiandikisha kupiga kura itabidi uonyeshe vitambulisho vyote kuhakikisha wewe ni raia na mkazi wa nyumba au apartment uloitaja.

Acha hizi habari za kudhani dhani wakati hujui mfumo wa S3 unafanya kazi vipi.

2. Kuna tofauti kubwa sana baina ya MAMBO ya Muungano (NCHI) na Utekelezaji wa ShuGHULI za serikali (SERIKALI). Mambo ya muungano ni kuashiria Je, kuna MAMBO gani vimewaunganisha ili kuunda Taifa moja, kisha SHUGHULI za muungano ni mfumo wa utekelezaji wa shughuli zake hivyo ktk mambo ya Muungano wetu tunaweza kuwa pamoja kwa yote (wizara zote) ila ktk utekelezaji wa shughuli zake kila nchi inawajibika kusimamia mamlaka hayo kwa niaba ya Taifa zima, hivyo kuchangia mfuko wa Taifa kwa kila kodi inayopatikana. Serikali huendeshwa na kodi za watu sio serikali zetu zinazo hodhi na kufanya biashara kupitia migongo ya wananchi na mikataba ya 10%. Unaweza kuniuliza hao viongozi wanafaidika vipi ikiwa wao ndio wameleta wawekezaji na kadhalika! wewe mwananchi machinga unachangia nini!

3. Kama wewe huijui Historia ya nchi hizi basi sina sababu ya kuendelea na mjadala maana sii ajabu unajiuliza hata faida ya mkeo nyumbani ikiwa hana ajira inayoingiza fedha sawa na wewe. Bila shaka atakuwa mzigo kwako na hata watoto wako ni mzigo kama nitafikiria kama wewe..Lakini bahati mbaya fikra zetu hazifanani.
 
Zanzibar si TAIFA la Tanzania? Period. Ukishafahamu hivyo utaelewa ulichosema hakina ukweli. Znz si taifa la Tanzania ni taifa la znz.
Znz si taifa la Tanzania, mkandara ukishafahamu hili utaacha kuandika mambo ya utaifa , shughuli za serikali na kazi za serikali. Znz si sehemu ya TAIFA la Tanzania

Nimekuuliza ili uwe mkazi wa Quebec unaghitaji muda gani ?
 
KINANA NA NAPE MGUU NJIANI
WASHINDWA KUELEZA SULUHU YA MUUNGANO WA S2
WATISHA WANANCHI KUHUSU AMANI NA UTULIVU

Katika mazingira ya kawaida CCM walibaki bungeni (BMLK) kujadili rasimu ya katiba.
Tofauti na mategemeo ya wengi rasimu haikujadiliwa bali mipasho na matusi.

Kulikuwa na njia mbili za CCM kuijadili katiba
1. Kueleza kwanini wanataka S2
2. Kueleza kwanini S3 zina matatizo
Hawakufanya hayo, siku zaidi ya 10 zikapotea na leo ukiulizia nini kilijadiliwa, hakuna jibu.

CCM na akina Nape wameondoka na kuzunguka mikoani kueleza uzuri wa S2.
Katika mikutano yao hakuna hoja ya S2 inayojadiliwa wala ya S3.
Sehemu kubwa ya mikutano ni mashambulizi dhidi ya UKAWA

UKAWA waliondoka bungeni, na CCM wakasema akidi inatosha kuendelea na mchakato.
UKAWA ni mkusanyiko wa watu na CCM ni chama tawala.

Tofauti kati ya makundi haya mawili si rangi au bendera za vyama au chama, bali ni hoja zinazokata kiu ya jinamizi la muungano.

Jinamizi la muungano lina miaka 50 likitishia kila mara kuusuambaratisha muungano.
Katika miaka yote mwaka hu ni mgumu , hali ya muungano ni taabani kuliko wakatoi mwingine wowote.

Ni taabani kwasababu majibu ya tatizo hayajapatikana.
Kinachoelezwa ni uzuri wa S2 bila hoja kwanini ni uzuri.
Ni sawa na kuambiwa nyama ni nzuri bila kujua ni ya ng'ombe, kima au nguruwe.
Kinachosema ni nyama ni nzuri kwakweli.

Tulitegemea CCM ieleze matatizo ya muungano uliopo na suluhu.
Hatutegemei waeleze matatizo ya Zanzibar kwasababu malalamiko ni ya pande zote.

Tena ya Tanganyika ni mazito zaidi yakihusisha kubeba zigo la muungano peke yao.
Wengi walitarajia kusikia nini S2 inafanya, kwanini imeshindwa na itatatua vipi tatizo hilo siku za baadaye.

Ilikuwa ni fursa ya CCM kueleza kwanini wanadhani serikali 3 zitadhoofisha muungano na si utatu wa CCM katika uongozi kama tulivyobainisha hapo juu.

Kinyume chake CCM imebaki kuwashambulia ukawa.
Chama tawala kinaposhindana na kundi la watu bila majibu ni aibu na kushindwa kwa hali ya juu.

Ziara za CCM mikoani ni ushahidi kuwa nguvu ya umma sasa inakielemea chama.
Iwe iwavyo CCM watabadili sheria na kanuni ili waweze kuandika rasimu yao.

Jambo moja lililowazi ni kuwa uhuni huo unaonekane na wananchi na kupitia uhuni huo UKAWA inapata nguvu hata bila mikutano.

UKAWA inapata nguvu kwasababu CCM haijibu hoja za wananchi na wala wananchi hawadhani tatizo la muungano ni UKAWA.

Wananachi wameshasema kupitia rasimu ya Warioba, wanapigwa na butwaa nini wanachoelezwa tofauti na kile walichoeleza.

Wananchi wanahoji, iweje tume iliyoundwa na mwenyekiti wa CCM kama Rais ikose kuaminiwa na CCM hiyo hiyo?

Lakini pia wana maswali, endapo sera za CCM ni serikali 2 iweje CCM izungumzie yale ya tume ya Warioba ili hali ilisharidhia uundwaji wake na matokeo ya tume?

CCM ilitoa maoni mbele ya tume ya Waioba. Wananchi wanashangaa iweje ilikwenda mbele ya tume ili hali ilijua wazi kuwa sera yake ni S2 na kwamba uwezekano wa tume kuja na majibu tofuati ulikuwepo.

Mwisho wa siku mikutano ya CCM itabaki kuwa aibu kwa wapiga debe kama Nape na Kinana.
Kumbu kumbu zinaonyesha wameshawahi kuchapwa vibao hadharani kwa hoja ya mawaziri mizigo, na kwa mwendo uliopo JK atawakung'uta tena vibao hadharani.

Atawachapa vibao kwasababu serikali yake haina pa kutokea.
Hakuna katiba ya wananchi kama UKAWA hawatarudi bungeni.

Ndilo linaisukuma serikali kutumia baadhi ya watu wenye ushawishi kuwataka UKAWA warudi mezani ili kupata juisi ya maembe kama ilivyozoeleka.

Mwisho wa siku lolote litakalotokea, Kiwete atabeba lawama.

Jaribio la kutumia jeshi limeshindikana kutisha watu, leo Nape anajaribu kutumia amani na utulivu kutoweka kwa kutumia UKAWA

Hao wananchi wana amani na utulivu gani kwasasa ikiwa hawawezi kununua asprin hata kabla UKAWA haijaundwa.

Amani na utulivu si ukimya ni hali ya utengamano kutokana na uwepo wa haki na upendo.

Nape amani na utulivu si wewe kutembea na VX wazazi wakijifungulia juu ya matenga ya baiskeli.
 
MBUNGE KEISSY WA NKASI: KAWAAMBIA WZNZ WALICHOKIFANYA
WAZANZIBAR WAMETUKANA KATIBA YA JMT,KEISSY KASISITIZA TU

Bungeni jana kulizuka timbwili la mbunge wa Nkasi (CCM) kuwaambia wazanzibar ukweli jua likiangaza, mbele ya Radio na TV.

Kilichoamsha hasira za wazanzibar ni kuambiwa wao ni mzigo, wanadai bila mchango wowote katika JMT na kuwapa chaguo la ‘njia nyeupe'

Kabla ya hapo, mbunge wa znz alisimama na kusema kati ya mbalozi 34 ni 3 kutoka znz.

Huo ni uonevu na kwamba Zanzibar ni koloni la Tanganyika.

Mbunge wa znz aliyasema hayo bila kufikiria neno ukoloni ni tusi kwa Watanganyika walioelemewa na mzigo wa znz, na omba omba isiyokwisha .

Hoja kubwa ya wznz ni kauli za Keissy kuwadhalilisha. Wznz wana hulka ya kudhani wao ni bora na wanaweza kusema chochote lakini ni kosa kuwaambia ukweli.

Alichosema Keissy ni kweli. Znz haina mchango wa aina yoyote kuendesha wizara ya mambo ya nje. Na wala haina haki ya kudai nafasi sawa za mabalozi.

Wanadai kitu gani wasichojua kinaendeshwa vipi na gharama zipi?

Hoja ya mabalozi ni ya kipuuzi sana. Balozi hawakilishi kabila au jimbo, anawakilisha nchi. kudhani ni mznz na si mtanzania au Mtanganyika na si mzanzibar ni elimu mbovu sana isyohitaji kujadiliwa

Pili, mabalozi ni wafanyakazi wa umma, duru hatuelewi ni vipi uwepo wa balozi mzanzibar unaweza kupunguza adha za mvuvi na mgema kule znz.

Hizi ni fikra chafu zinazopaswa kukemewa. Waziri au balozi anamalizaje shida za wananchi wanaomzunguka?

Tatu, hao wznz wanaodai nafasi bungeni walipaswa wajiangalie kwanza.

Wabunge wa znz baadhi yao wanawakilisha wananchi 10,000 na wa juu zaidi ni 30,000.

Mbunge wa Nkasi anawakilisha idadi nzima ya wznz.

Mfuko wa bunge na masilahi yote, wabunge wanapewa sawa.

Ilibidi tuangalie usawa huo kwanza kabla ya kuangalia mabalozi 30.

Usawa upi wa uwakilishi wa watu 5,000 na mwingine 1,000,000?

Hili linadhihirisha, ubinafsi, umimi na ‘nataka' ya wznz.

ZNZ walioondoa mambo ya muungano ya mkataba wa 1964 kama bandari, anga n.k walikuwa anatengeneza njia.Wamekiuka katiba ya JMT, wanatengeneza njia.

Kuifanya katiba yao kuu juu ya JMT wanatukana Tanganyika na wanatengeneza njia

Alichosema Keissy ni kuwa njia ipo tena nyeupe waliyotengeneza, wana chaguo, kubaki au njia nyeupe.sasa tusi lipo wapi?

Njia ni nyeupe kwasababu mzigo ni mzito, unapoambatana na hoja za mabalozi, wakuu wa majeshi inasikitisha.

Kwamba, tatizo la wznz si uchumi wa JMT ni nafasi za kazi.

Baada ya kupewa asilimia 21 ambayo hawana haki wala hawastahili kwa kiasi hicho, sasa wanazidi kwenda mbali na kuomba hata kisicho chao.

Waombe wakichangia, kuwa omba omba tu kwa malalamiko Watanganyika wamechoka.

Keissy kawaambia mchana, wamechokwa na sasa ni bzamu yao kuamua.

Njia nyeupe

Tusemezane

TULIONYA UKAWA, KUWENI MAKINI
ZIPO DALILI ZA KUBABAIKA

Kama mtakumbuka, mwanzo wa bandiko tuliwaonya ukawa kuhusu subira CCM wamalize bunge lao ili kupeleka kesi kwa wananchi. UKAWA wakasubiri na sasa ni mtifuano huko mitaani.

Tuliwaambia ukawa, jambo la muhimu si kueleza ubaya wa muungano au tatizo la muungano.
Kilichotakiwa ni kuifahamu jamii na tatizo la mwanzo kabla ya kuingia katika mada.

Watanzania wengi wanaelewa katiba ni kitabu anachoshika rais akiapa.
Hawana ufahamu katiba inaathiri maisha yao pale pale waliposimama.
Na wala hawaelewi kuwa matatizo wanayoyakabili sehemu kubwa ni ubovu wa katiba.

Kwa mfano, wizi uliokubuhu ni matokeo ya katiba inayotoa nafasi kutenda hayo.
Kwamba, mtu mmoja kwa nguvu za ajabu na anaweza kuuza reli inayowasaidi wananchi kwa wahindi wang'oe kama vyuma chakavu.
Kwamba, shirika kama la UDA lililoanzishwa kwa kodi zao linaweza kuuzwa kihasara tu bila mtu kuhoji au kuhojiwa.

Kwamba, haki zao za msingi za elimu, afya a ulinzi lazima zilindwe kwa kutumia katiba.
Hivyo umuhimu wa katiba inayogusa maisha yao ni mkubwa sana. Hilo lilikuwa la kwanza kufanya

Suala la pili, ilikuwa kuonyesha namna ambavyo fursa yao ya kuandika katiba kwa maoni yao inavyovurugugwa na kundi la watu wachache wenye nia ya kulinda maislahi yao kiuchumi na kwamba, katiba tarajiwa si ile waiyoitaka.

La tatu, ilikuwa kuwaeleza kwanini wanagomea bunge, ni sababu zipi za msingi .
Hapa ni pamoja na kueleza jinsi ambavyo utangamano wa nchi mbili unavyoweza kuzaa matatizo mbele ya safari endapo 'will' ya watu haitaheshimiwa.

Walipaswa kuonyesha mgogoro unaohusu Tanganyika na kwanini kuna malalamiko kama ambavyo yapo znz.
Wahoji iweje miaka 50 hakuna ufumbuzi, leo waambiwe ufumbuzi umepatikana jana kuamkia leo?

Halafu, wapendekeza namna ya kuondoa mitafaruku inayolenga kulivuruga taifa au basi kama inabidi kuondoa tatizo kabisa.
Hata mguu wenye kidonda kisichopona dawa ni kuukata usiumize mwili kuliko kuwekea dawa ya GV

Na mwisho kuwaomba wananchi wawaunge mkono katika kulinda demokrasia, kusimamia haki na kupata nyaraka inayogusa maisha yao ya leo na miaka ijayo bila kujali uwanda wa kisiasa (political spectrum)

Inashangaza kuona UKAWA wakiingia katika mikuatano kama mbuzi walioachiwa mazizini kujitafutia malisho.
Kila mtu akisema lake na hakuna common ground.
Haina maana kwa Lissu kusimama na kuwapendeza wznz badala ya kueleza kiini cha matatizo.
Tatizo si wznz ni tatizo la upande wa pili pia.

Leo wananchi wa Tanganyika wanalalamika kubeba mzigo wa muungano.
Wanalalamika kwa upendeleo uliokithiri kwa wznz kana kwamba ukiwa mznz wewe ni rais wa daraja la kwanza.

Lissu anaposema Tanganyika inawaonea kwa misaada, bado hajaeleza tatizo kwa ujumla wake.
Tena anafanya hivyo akiwaficha Watanganyika ukweli juu ya mzigo mzito waliobeba wa madeni ya ndani, nje na fursa za kipekee zinazotokana na Uzanzibar na wala si Utanzania.

Tundu haelezi tatizo la katiba ya zanzibar ya 2010 na wala utegemezi wa kiuchumi ambao sasa wznz wanaugeza kama haki. Inapofikia mahali ambapo wznz wanaweza kuamua mswada unaohusu mambo ya Shinyanga na Lindi, hapo kuna tatizo.
Haionekani Kinara Lissu kuelewa mkakati.

Ndivyo ilivyo kwa Ukawa, leo utasikia hili kesho utasikia lile. Hakuna message consistent katika wiki moja.
Makosa hayo yanatumiwa vema na CCM ambao wao kwa kugundua udhaifu wa Ukawa, wamejikita kuwaeleza wananchi kwa lugha wanazoelewa. Kuwalaghai kuwa katiba haileti shule au hospitali huku wakipita kukagua maeneo hayo.

Kuna upungufu wa message kutoka ukawa na ndio maana tulianza kwa kusema 'ukawa wanababika'
Katika kubabaika si ajabu wakajikuta mbela ya glasi za juisi ya maembe kama ilivyokuwa huko nyuma.
Yes, wanaweza kwenda kwasababu haionekani kama wana mkakati thabiti.

Tusemezane
 
Tuliwaambia ukawa, jambo la muhimu si kueleza ubaya wa muungano au tatizo la muungano.
Kilichotakiwa ni kuifahamu jamii na tatizo la mwanzo kabla ya kuingia katika mada.

Watanzania wengi wanaelewa katiba ni kitabu anachoshika rais akiapa.
Hawana ufahamu katiba inaathiri maisha yao pale pale waliposimama.
Na wala hawaelewi kuwa matatizo wanayoyakabili sehemu kubwa ni ubovu wa katiba.
swadakta haya ndio maneno toka kwa mwananchi mwenye nia ya dhati kuitaka katiba Mpya ya JMT.
 
Mchambuzi,
Dah kumbe ndio hivi mimi sikujua hili.kumbe Ukawa ni Chadema kwa bara sio umoja wa wajumbe, haya sasa mimi nayepingana na UKAWA pia nipo ni kundi la nani la ACT au sio? Mkuu ieleweke nachopinga mimi sio umoja wa UKAWA ila fikra za kuunda serikali 3 wakiacha mambo ya muungano kuwa 7 badala ya mambo yote yawe ya Muungano.

Kama hivi leo tuna mambo 22 ya Muungano na yale ya Bara yanaendeshwa chini ya muundo huu wa seriikali 2 tusiidai Tanganyika kwa miaka 50, Je inashindikana nini kuwa na yote ya Muungano kuziba kabisa midomo yahawa kina Jussa maana wao ndio wanataka kila siku mambo ya muungano tupunguze, nanyi mnaafikiana nao. Leo tuna saba, kesho yatakuwa matano, na kisha mawili na mwisho hakuna kitu hudhani kwamba hawa jamaa hawakuwa na mwisho hadi waone Muungano umekufa!.

Hili ndilo tatizo langu kubwa na UKAWA ktk mapendekezo ya rasimu ya Warioba. Tulichoomba sisi wananchi ni katiba mpya inayokwenda sambamba na transformation ya TAIFA letu Kiuchumi na kisiasa ili kukidhi mahitaji yetu, jambo ambalo lilitakiwa toka mwaka 1993 na sii swala la kero za Muungano wetu maana mamlaka ya utekelezaji shughuli za serikali ni i za serikali, kila jimbo, kila mkoa na kila wilaya wanayo haki ya kupewa mamlaka hayo ndani ya mfumo huu wa Kibepari..muhimu la lazima kwa serikali zote 2 chini ya muundo wowote na haikomei kwa serikali hiz bai huenda hadi kwa Magavana, Mayor na serikali za mitaa wote wanahitaji mamlaka kamili kwa shughuli zao na sii mlolongo wapaper work na ofisi, hii inaoleta Urasimu na ucheleweshaji wa maendeleo.
Mkuu Mkandara, hakuna serikali 2. Huwezi kuwa na SMZ na JMT ambayo znz imo ukasema ni 2. Hapa ni pana kutatiza sana ima kwa kuogopa ukweli au kwa kutofahamu.
Ukisema JMT tayari umeshaondoa serikali ya pili. Hakuna serikali ya pili ya JMT.
Serikali 2 ni ya Tanganyika na Zanzibar halafu kuna ya JMT

Mkandara, Warioba amesikiliza maoni ya watu. Moja ya malalamiko ya wznz ni Tanganyika kuvaa koti la muungano.
Yaani yalipongezwa mambo hadi 22 hakuna faida kwa Tanganyika, aliyefaidika ni mzanzibar.
Mznz kasema mambo yaliyoongezwa ni kinyemeala na wewe umemuunga mkono. Inashangaza leo unaposema eti mambo yote ni ya muungano. Ni ya muungano vipi wakati wznz unaowatetea hawataki iwe hivyo?

Halafu unasema kuna mambo yameongezwa kinyemela, back and forth, huwezi kuwa na mambo ya muungano halafu ukasema yameongezwa kinyemela.

Ni jambo la kusikitisha kuona Mtanganyika kama wewe upo tayari kuuza utaifa na rasilimali za nchi yako bila hoja za msingi.

Huwezi kuwa na ka nchi kama znz kakapanga namna Tanganyika inavyojitawala.
Leo tunapeleka miswada ikatiwe sahihi na BLW la watu 50, wote wakiamini na akili zao zikifiri kwa bidii kabisa mabalozi ndio tatizo la nchi hii. Real! hawa ndio watu wakaupitia miswada yetu! hawa!

Mkuu Mkandara, wznz wanasema wanataka mamlaka kamili. Tulianza na mambo 11 yakafikia 22,wznz hawataki. Leo wewe unakuwaje mznz kuliko wznz wenyewe? hawataki, tunajaribu 7 kama hawataki njia nyeupee

Na mwisho waeleze watu, serikali 2 zinafanyaje kazi kuondoa malalamiko, kwanza kwa znz, na pili kuwajibisha znz iwe na jambo la maana katika maendeleo, kuchangia na kubadili mawazo ya mabalozi 3.
Tueleze nani anasimamia rasilimali za Tanganyika, na kwanini unadhani cha Mtanganyika ni cha wote cha mzanzibar ni chao peke yao. Haki hiyo inatolewa kwa msingi gani.

Hebu eleza umuhimu wa znz kwetu, maana wengine kwa kusikia wenzetu wanashida ya mabalozi 3, tunadhani kifikra tupo katika muungano na watu tofauti kabisa.
 
Mkuu Mkandara, hakuna serikali 2. Huwezi kuwa na SMZ na JMT ambayo znz imo. Hapa ni mhalai pana kutatiza sana ima kwa kuogopa ukweli au kwa kutofahamu.
Ukisema JMT tayari umeshaondoa serikali ya pili. Hakuna serikali ya pili ya JMT.
Serikali 2 ni ya Tanganyika na Zanzibar halafu kuna ya JMT

Mkandara, Warioba amesikiliza maoni ya watu. Moja ya malalamiko ya wznz ni Tanganyika kuvaa koti la muungano.
Yaani yalipongezwa mambo hadi 22 hakuna faida kwa Tanganyika, aliyefaidika ni mzanzibar.
Mznz kasema mambo yaliyoongezwa ni kinyemeala na wewe umemuunga mkono. Inashangaza leo unaposema eti mambo yote ni ya muungano. Ni ya muungano vipi wakati wznz unaowatetea hawataki iwe hivyo?

Hafu unasema kuna mambo yameongezwa kinyemela, back and forth, huwezi kuwa na mambo ya muungano halafu ukasema yameongezwa kinyemela.

Ni jambo la kusikitisha kuona Mtanganyika kama wewe upo tayari kuuza utaifa na rasilimali za nchi yako bila hoja za msingi. Huwezi kuwa na ka nchi kama znz kakapanga namna Tanganyika inavyojitawala.
Leo tunapeleka miswada ikatiwe sahihi na BLW la watu 50, wote wakiamini na akili zao zikifiri kwa bidii kabisa mabalozi ndio tatizo la nchi hii. Real! hawa ndio watu wakaupitia miswada yetu! hawa!

Mkuu Mkandara, wznz wanasema wanataka mamlaka kamili. Tulianza na mambo 11 yakafikia 22,wznz hawataki. Leo wewe unakuwaje mznz kuliko wznz wenyewe? hawataki, tunajaribu 7 kama hawataki njia nyeupee

Na mwisho waeleze watu, serikali 2 zinafanyaje kazi kuondoa malalamiko, kwanza kwa znz, na pili kuwajibisha znz iwe na jambo la maana katika maendeleo, kuchangia na kubadili mawazo ya mabalozi 3.
Tueleze nani anasimamia rasilimali za Tanganyika, na kwanini unadhani cha Mtanganyika ni cha wote cha mzanzibar ni chao peke yao. Haki hiyo inatolewa kwa msingi gani.

Hebu eleza umuhimu wa znz kwetu, maana wengine kwa kusikia wenzetu wanashida ya mabalozi 3, tunadhani kifikra tupo katika muungano na watu tofauti kabisa.
Mkuu wangu nikwambie nini uweze kuelewa... kwanza nini maana ya Tanganyika kuvaa koti la Muungano?.. maana muhimu ufahamu hili kwanza kabla hujarukia hoja ambazo hazifanani na madai. Acha hizi habari za kusikia wadhungu wanasema -Three different people can witness the same event and each comes up with a different account of how it occurred!.

Wanachosema ni kwamba
1. Kwa Kila project ya Tanganyika (mambo yasokuwa ya Muungano) Tanganyika haihitaji ridhaa ya Wazanzibar japokuwa kwa kila project ya Zanzibar, Zanzibar inahitaji ridhaa ya Tanganyika ( mfano - OIC)
2. Kwa kila mpango wa project ya Tanganyika (mambo yasokuwa ya Muungano) Tanganyika imetumia jina la Tanzania kuvuta mikopo nje, kwa sababu Kimataifa nchi za Tangayika wala Zanzibar haziwezi kuvuta mikopo kwa sababu hazitambuliwi kama ni Taifa. nakuomba ufahamu tu ya kwamba lengo la TAIFA huru kuwa na kiti UN ni kutambuliwa kama TAIFA huru lenye serikali halali na hivyo kufungwa ktk sheria za Kimataifa katika maswala ya mawasiliano, trade, mikopo, na misaada ambayo mashirika ya Kimataifa yanapewa guarantee ya kuaminiwa.

Hivyo basi utakapo kuwa na serikali ya 3, hiyo ya Tanganyika bado nchi hii itahitaji kutumia jina la Tanzania ktk ushirika wake Kimataifa na mashirika ya nje. Na hivyo itaendelea kulivaa koti la Muungano kwa kutumia tena jina la Tanzania ktk mambo yasokuwa ya Muungano (yawe 7, 11 au 22). Hivyo muundo wa serikali 3 bado hautaondoa tatizo hilo bali Tanganyika itakuwa imelivua koti na kuliweka begani (kuondoa kero) ili upepo upite, lakini kama MAMBO YOTE YATAKUWA YA MUUNGANO tutalivua koti hilo -hakuna Utanganyika wala Uzanzibar kimataifa, hivyo kila jambo litahusu pande zote 2 (TANZANIA) na kupata ridhaa ya bunge la JMT.

Hii itasaidia kuondoa mamlaka kamili kwa viongozi wa serikali za Tanganyika (JMT) kuweka mikataba ya Tangayika chini ya meza, tena basi sio kwa Tanganyika ila kwa wao wenyewe kujilimbikiza utajiri kwa kutumia siri ya nchi. Miradi yote itajadiliwa na wizara kwa faida ya Tanzania, itapitishwa na bunge maana hakuna siri ya miradi ya uzalishaji, ushirika wa wabunge wa pande zote 2 (chama tawala na Upinzani) watakuwa na nguvu ya kiitikadi kupinga ama kukubaliana na uwekezaji badala ya Uzanzibar na Ubara na mwisho wa siku ktk mapato ya mradi mzima kodi ya mapato (income tax) itawekwa ktk mafungu mawili, moja ya nchi (VAT) na nyingine ya Taifa ndio kusema kama ni asilimi 30, basi 20 ya Taifa na 10 ni ya nchi. Na ktk nchi, kila mkoa au jimbo litafaidika tena kwa asilimia toka ile asilimia 10. Haiwezekani gas itoke Mtwara waachwe watupu na visima vya maji, pasipo guarantee ya mapato ya kodi toka uwekezaji jimboni hapo.

Haya ni mapendekezo yangu ambayo hata nchi za magharibi wanatumia. kama wewe uanvyodai umewahi kufika Ontario, Canada basi bila shaka unaelewa ndani ya kodi ya HST (13%) kuna kodi 2 za PST (5%)ya jimbo na GST (8%) ya Taifa. Hivyo kila jimbo la Canada linapanga PST yake kuvutia uwekezaji sehemu hiyo kulingana na mahitaji yao lakini kodi ya GST imesimama pale pale kwa majimbo yote. Halafu kuna kodi za Mafuta ambazo kila jimbo linapanga kutokana na gharama za uagizaji, usafiri n.k hivyo bei ya mafuta inatofautiana kwa kila jimbo. yet kila Jimbo hadi taifa wanafaidika na uwekezezaji japo mafuta yanatoka Alberta! Na ndio maana Alberta sasa hivi ni jimbo tajiri kuliko majimbo yote Canada na hawana kinyongo ku share pato lake na majimbo mengine ya Canada kwani hata wao wanafaidika na rasirimali toka majimbo mengine ikiwa ni pamoja na nguvu za umeme wa nuklia toka sehemu nyinginezo.

Kwa hiyo Uwe na tanganyika anma laa maadam mambo yasokuw aya muungano yatakuwepo Tanganyika haitaweza kulivua koti kwa sababu Tanganyika sio TAIFA na haitambuliwi na Umoja wa Mataifa, njia pekee ya kuondokana na adha hii ni kuyafanya mambo yote yawe ya Muungano japo Wazanzibar hawataki na Watanganyika wanataka kujitenga. hatuwezi kukubali kushindwa na hoja za watu wachache wenye nia mbaya na Muungano wetu, njia pekee ya kuwakomoa wote hawa wenye fikra za Ubinafsi na kugawana mbao ni kuyafanya mambo yote yawe ya nmuungano kisha zitungwe sheria mpya za kodi - Tax income act ambayo itawezesha kila jimbo hadi taifa kufaidika na mapato haya.

Najua bado hujanielewa na hutaki kunielewa....
 
Mkuu Three different people can witness the same event and each comes up with a different account of how it occurred!.

Wanachosema ni kwamba
1. Kwa Kila project ya Tanganyika (mambo yasokuwa ya Muungano) Tanganyika haihitaji ridhaa ya Wazanzibar japokuwa kwa kila project ya Zanzibar, Zanzibar inahitaji ridhaa ya Tanganyika ( mfano - OIC)

2. Kwa kila mpango wa project ya Tanganyika (mambo yasokuwa ya Muungano) Tanganyika imetumia jina la Tanzania kuvuta mikopo nje, kwa sababu Kimataifa nchi za Tangayika wala Zanzibar haziwezi kuvuta mikopo kwa sababu hazitambuliwi kama ni Taifa. nakuomba ufahamu tu ya kwamba lengo la TAIFA huru kuwa na kiti UN ni kutambuliwa kama TAIFA huru lenye serikali halali na hivyo kufungwa ktk sheria za Kimataifa katika maswala ya mawasiliano, trade, mikopo, na misaada ambayo mashirika ya Kimataifa yanapewa guarantee ya kuaminiwa.

Hivyo basi utakapo kuwa na serikali ya 3, hiyo ya Tanganyika bado nchi hii itahitaji kutumia jina la Tanzania ktk ushirika wake Kimataifa na mashirika ya nje. Na hivyo itaendelea kulivaa koti la Muungano kwa kutumia tena jina la Tanzania ktk mambo yasokuwa ya Muungano (yawe 7, 11 au 22). Hivyo muundo wa serikali 3 bado hautaondoa tatizo hilo bali Tanganyika itakuwa imelivua koti na kuliweka begani (kuondoa kero) ili upepo upite, lakini kama MAMBO YOTE YATAKUWA YA MUUNGANO tutalivua koti hilo -hakuna Utanganyika wala Uzanzibar kimataifa, hivyo kila jambo litahusu pande zote 2 (TANZANIA) na kupata ridhaa ya bunge la JMT.

Hii itasaidia kuondoa mamlaka kamili kwa viongozi wa serikali za Tanganyika (JMT) kuweka mikataba ya Tangayika chini ya meza, tena basi sio kwa Tanganyika ila kwa wao wenyewe kujilimbikiza utajiri kwa kutumia siri ya nchi. Miradi yote itajadiliwa na wizara kwa faida ya Tanzania, itapitishwa na bunge maana hakuna siri ya miradi ya uzalishaji, ushirika wa wabunge wa pande zote 2 (Utawla na Upinzani) watakuwa na nguvu ya kiitikadi kupinga ama kukubaiana na uwekezaji badala ya Uzanzibar na Ubara na mwisho wa siku ktk mapato ya mradi mzima kodi ya mapato (income tax) itawekwa ktk mafungu mawili, moja ya nchi (VAT) na nyingine ya Taifa ndio kusema kama ni asilimi 30, basi 20 ya Taifa na 10 ni ya nchi. Na ktk nchi, kila mkoa au jimbo litafaidika tena kwa asilimia toka ile asilimia 10. Haiwezekani gas itoke Mtwara waachwe watupu na visima vya maji, pasipo guarantee ya mapato ya kodi toka uwekezaji jimboni hapo.

Haya ni mapendekezo yangu ambayo hata nchi za magharibi wanatumia. kama wewe uanvyodai umewahi kufika Ontario, Canada basi bila shaka unaelewa ndani ya kodi ya HST (13%) kuna kodi 2 za PST (5%)ya jimbo na GST (8%) ya Taifa. Hivyo kila jimbo la Canada linapanga PST yake kuvutia uwekezaji sehemu hiyo kulingana na mahitaji yao lakini kodi ya GST imesimama pale pale kwa majimbo yote. Halafu kuna kodi za Mafuta ambazo kila jimbo linapanga kutokana na gharama za uagizaji, usafiri n.k hivyo bei ya mafuta inatofautiana kwa kila jimbo. yet kila Jimbo hadi taifa wanafaidika na uwekezezaji japo mafuta yanatoka Alberta! Na ndio maana Alberta sasa hivi ni jimbo tajiri kuliko majimbo yote Canada na hawana kinyongo ku share pato lake na majimbo mengine ya Canada kwani hata wao wanafaidika na rasirimali toka majimbo mengine ikiwa ni pamoja na nguvu za umeme wa nuklia toka sehemu nyinginezo.

Kwa hiyo Uwe na tanganyika anma laa maadam mambo yasokuw aya muungano yatakuwepo Tanganyika haitaweza kulivua koti kwa sababu Tanganyika sio TAIFA na haitambuliwi na Umoja wa Mataifa, njia pekee ya kuondokana na adha hii ni kuyafanya mambo yote yawe ya Muungano japo Wazanzibar hawataki na Watanganyika wanataka kujitenga. hatuwezi kukubali kushindwa na hoja za watu wachache wenye nia mbaya na Muungano wetu, njia pekee ya kuwakomoa wote hawa wenye fikra za Ubinafsi na kugawana mbao ni kuyafanya mambo yote yawe ya nmuungano kisha zitungwe sheria mpya za kodi - Tax income act ambayo itawezesha kila jimbo hadi taifa kufaidika na mapato haya.

Najua bado hujanielewa na hutaki kunielewa....
Point ya kwanza, ni kweli, lakini kumbuka kuwa Tanganyika ilitoa utaifa wake na kuukabidhi kwa Tanzania, kwa mujibu wa maneno yako mwenyewe.

Huwezi kulaumu Tanganyika kutodai ridhaa kwa mambo ya muungano. Tayari ni loser kwa kupoteza ID yake.
Znz ambayo ni semi autonomy inapaswa kuomba ridhaa kutoka Tanzania kwasababu ndani ya Tanzania znz imo.
Tanzania ndiyo imevaa Tanganyika na si kinyume chake. Kwa msingi huo aliyepoteza ID yake analaumiwaje?
Ni kwa njia gani Tanganyika ingeweza kupata ridhaa ikiwa yenyewe ilikasimu madaraka kwa Tanzania?

Point ya pili, Tume ya Warioba imeweka wazi, erikali washirika watapata dhamana ya mikopo kupitia serikali kuu.
maana yake ni kuwa Tanganyika itavua koti na kuwa sawa na znz mbele ya serikali ya shirikisho.
Hili linasisitiza umuhimu wa kutenga nchi hizi katika majukumu yake.

Mkuu huwezi kuwa na S2 ukawataka Watanganyika wapate ridhaa znz!
Tanzania imo Tanganyika na ZNZ hivyo huwezi kutenga znz na Tanganyika ukiwa na Tanzania bila Tanganyika. Ndivyo logic ilivyo.

Point ya tatu, njia pekee ya kuleta maridhiano kwa mujibu wako ni kufanya mambo yote ya muungano.
Well, hilo wznz hawataki miaka nenda rudi na ndicho chanzo cha wao kuondoa jambo moja baada ya jingine.

Kwa mfano, hatujavuna mafuta na gesi nini kiliwasukuma kuyaondoa. Nini kimewasuklumua kuondoa shirika la viwango, nini kimewasukuma kuondoa baraza la mitihani. Ukiangalia wanaondoa hata mambo ambayo ni huduma tu kwasababu ya uzanzibar.
Kuna sababu gani za kuwa HESLB na ZHESLB? Kuna ulazima gani?

Utaona wazi kuwa kinachowasukuma wznz ni umimi na ubinafsi. Ni kitu kinaitwa narcissism ili kizae Nepotism.
Narcissism and Nepotism ya wznz ndio imezaa loneliness ya Watanganyika na uprising.
Kwa miaka 50 Watanganyika waliridhika lakini sasa wamechoka.

Katiba ya znz ya 2010 imeundwa katika misingi ya proud, narcissism, Nepotism na 'superiority complex'.
Walidhani kuwa wao ni stake holder wakubwa katika muungano ili hali ni minority at any parameter you may want to use.

Kwa hiyo lazima kwanza ulaani matatizo yaliyosababishwa na znz, halafu ndipo ushauri the way forward.
Hatuwezi kuwa na mambo ya pamoja kama katiba ya znz ya 2010 ikiwa hai.

Suala la harmonized tax ndilo wznz hawataki kulisikia. Wanadai wanaibiwa, leo vipi tunaweza kuwa na kodi ya pamoja?
Mkuu hapa huoni unazungumzia impossible. Hoja yako ina mantiki sana na mfano uliotoa ndio hasa inavyopaswa kuwa, tatizo la wznz ni uwezo wa kutambua. Utawezaje kumshawishi kuwa bajeti yake ya 400B ingekuwa na maana kama angekubali kodi iwe ya pamoja. Ni hesabu tu na wao hawatumii hizo. Unaona hata msomi wa Ph.D bado hawezi kuliona, mvuvi utamshawishi nini.

Hatuwezi kuwa na mambo ya pamoja kama kujivunia uzanzibar ndiyo mantra. Unapojivunia uzanzibar tayari unamshawishi Mtanganyika naye ajivunie Utanganyika na ndicho kinachotokea. Katika mazingira hayo hakuna consensus tena lazima tukubali.

Misingi ya muungano imevunjwa na wznz na hakuna namna tunaweza kuirudisha Tanganyika katika chupa.
Mvinyo umefunguliwa na sasa watu wasubiri kileo na ulevi. Who is to blame, absolutely znz.

Na mwisho, huwezi kujenga utaifa mmoja ukiwa na utaifa mdogo ndani yake. Nipe mfano mmoja tu duniani ambapo nchi moja ina utaifa mdogo ndani yake. ZNZ kupitia katiba ya 2010 ni taifa, ni nchi na kila kitu, hatuwezi kuishi katika mazingira hayo. Kutokana na utaifa mdogo,sasa wanataka kuwa taifa kubwa kwa kudharau katiba. This is too low and too hard to swallow. Tupeni nafasi tujadili umasikini wa wataanganyika na si jinsi ya kuwafurahisha wznz.

Taifa letu halikupigania uhuru in order to appease zanzibar
 
Nguruvi3,
Unaposema Tanzania imevaa koti a Tanganyika una maana gani? ikiwa Tanganyika imo ndani ya Tanzania itakuwaje koti livaliwe ndani au una maana fulana?. Na hii sio swala la kuonekana nje utanashati bali matendo ya mtu huyu ambaye anajumulikana kama Tanzania kumbe ni Tanganyika kwa kila anappochukua mikopo nje. Zanzibar hawana uwezo huo bila kupitia kwa Tanganyika ndio maana nikakupa mfano wa mke na Mume, lakini bado hujaelewa.

Unapopigania wewe ni Tanganyik akuwa na Identity yake kama Zanzibar lakini huu ni ujinga ikiwa tanganyika inajulikana au laa wakati mambo yake yanakwenda. Hii ndio kusema tunakuwa kama wale Mapedejee wanaorusha mifedha ktk miduara au Gwasuma watajwe majina yao wajulikane. Tusitake kufikiri kama wao ama kutazama picha nzima kwa jicho la Utanganyika kwa sababu tu wao wamechoka na vitendo vya CCM. Kwa unapozungumzia Bara ni sawa na kuitukana CCM na kweli sisi ndio tunaoibeba CCM.

Ili wao wapate kuendesha shughuli zao ni lazima watumie Uzanzibar kwa sababu Tanganyika inaendesha shughuli zake bila ridhaa ya bunge la Tanzania wakidai kuwa ni siri ya taifa, hizi siri za uendeshaji serikali ya Tanganyika ktk mikataba yake unatoka wapi? mikataba hadi inawekwa hotelini bado mnadai kuwa Tanganyika haipo!. Lini tutakuwa na UWAZI na UWAJIBIKAJI ikiwa maswala yote ya yanawekwa ktk usiri ambao hatufahamu isipokuwa uongozi wa CCM?..

Pili, unaposema serikali hizi zitapata udhamana toka serikali kuu, udhamana upi kwa Tanganyika utakao kuwa tofauti na uliopo?. Ikiwa serikali kuu ina mambo 7 tu yasohusiana na uwekezaji, itaweza vipi kuidhamini Tanganyika au Zanzibar ktk maswala ya mikopo ilihali maswala hayo sii ya muungano? Serikali kuu itaweza vipi kudhamini kitu wasichokijua undani wake, faida zake, uwezo wa kurudisha mikopo hiyo ikiwa haya sii mambo ya muungano? ni kwa sheria ipi hiyo serikali kuu yenye mambo 7 itaweza kudhamini maswala ambayo hayawahusu na sii ya muungano maana huko ndiko kwenye uzalishaji na mapato!...
 
Mkuu Mkandara
Ninaposema Tanzania imevaa koti la Tanganyika nina maana rasilimali za Tanganyika zimegeuzwa kuwa za Tanzania.
Nina maana mzigo wa Tanzania ameubeba Mtanganyika kwa jina la Tanzania. Hilo lipo wazi kwa kile kigezo cha uchumi.

Kuhusu mikopo, waziri wa znz anasema 88% ya deni lao limedhamiwa na Tanzania iliyovaa koti la Tanganyika. In other words kila sh 100, sh 88 amedhamini Mtanganyika kwa jina la Tanzania.

Tuonyeshe mahali katika bajeti ya znz ya bilioni 710 panapoonyeshwa kuwa kuna fungu la kulipa hiyo 88 au 12%
Jibu ni hakuna na deni hilo atalimeza Mtanganyika kwa jina la Tanzania.

Kuhusu Utanganyika, hilo nalo nasema ili kutokuwa na malalamiko na kuwapa wznz nafasi nzuri ya kukopa bila kupitia Tanzania, tunataka S3. Hapo hakutakuwa na malalamiko kwa sababu znz watakwenda Paris na Washington kupata mikopo na misaada yao kwa uhuru. Tanganyika nao watakwenda huko kwa njia zao.

Na mwisho, nimeeleza kuwa kuna deni la ndani na la nje.
Unapoangalia mikopo na misaada, Mkandara unafumba macho kabisa kuangalia ni kiasi gani znz inatumia kwa deni la ndani.

Hebu tueleze kwa znz, bajeti ya ulinzi na usalama, mambo ya ndani, mambo ya nje, elimu ya juu, wizara za muungano, zn inatumia kiasi gani cha bajeti yake.

Pili, znz ikipata huo uwezo wa kukopa na misaada, je suala la Tanzania litahudumiwaje. Nina maana mikopo na misaada ya Tanzania itahudumia Tanzania, je ile ya znz itakuwa na mchango gani kwa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:

Rasilimali zipi? ebu nambie wewe Mtanganyika unanufaika vipi na hesabu kubwa ya watu wasiolipa kodi? unanufaika vipi na ardhi kubwa inayoizwa kwa wageni? Unanufaika vipi na dhahabu za Geita na Bulyanhulu? hiyo gas ya Mtwara, Uranium ya Iringa na kadhalika! Je, Huyo Mzanzibar ananufaika vipi!.. Badala ya wewe kutazama katiba iliyopo ili ikuwezeshe wewe kufaiodika na rasilimali hizi unaitazama Zanzibar na kutaka ardhi kule ili iweje?.

Hakuna kitu Tanganyika, hapa tuna tanzania tu na serikali yake ya JMT ambayo inaendesha mambo ya Tanganyika. Hivyo Tanganyika inapolivaa koti la Muungano ni muhimu ufahamu kinachosemwa hapa kinahusu nini na sii kuvumbua yako..Ni katiba hii ya mwaka 1977 inayotuongoza sote hivyo unapokuja na maswala ya Utanganyika wakati haipo, basi kesho utakuja na maswala ya Usukuma na Ukurya kutuondoa hata sisi Wakerewe wa visiwani tusokuwa na maliasili na rasilimali kama zenu. Acheni hizi habari za kuvaa koti kwa kutazama una nini mfukoni bali tazama fursa zilizopo wewe kama Mtanganyika unakwamishwa vipi?
Kuna haja kubwa sana ya Kutoa elimu ya URAIA maanake naona watu wameanza kughiribiwa na hii Ukawa!
 
Tena hapa unanisaidia sana. Tulisema ili mzanzibar anufaike ni lazima tuwe na kila jambo la pamoja.
Waliposikia kuna madebe 300 ya mafuta baharini wakakimbi kuondoa jambo hilo katika muungano bila kushaurina nasi.
Wanahitaji kufaidika na dhahabu au gesi ya Mtwara kwa lipi? Hivi huoni ubinafsi na uchoyo wao ndio unao uongelea?

Waliposikia bandari huru, wakaondoa katika mambo ya muungano, kwa kiburi chao kisicho na ilim hawakushaurina na Tanganyika. Kwa bahati mbaya hawajui kuwa jiografia haiwapendelei. Bandari huru ya Tanganya pale Mwambani inapanda.
Wao yao watafanya biashara na Kenya, Comoro na kwingine.

Rasilimali za Tanzania ziache zifisadiwe na Watanganyika. Cha wa Tanganyika si shamba la bibi.
Hawa wazanzibar ni watu wa nchi nyingine. Tunapoongelea ufisadi na rasilimali siyo sehemu ya matatizo yao. W
ana nchi, serikali na kila kitu, hatuhitaji kuwaingilia.

Uzanzibar na Utanganyika umeletwa na Wazanzibar . Katiba ya 2010 inawatambua kama Wazanzibar.
Hakuna, narudia,hakuna hata neno moja linalomtambulisha mzanzibar kama Mtanzania.
Hatuna sababu ya kuwanyima fursa ya kujivunia utaifa wao. Na hakuna sababu ya kutojivunia Utanganyika wetu.

Unachotaka ni tuwe na Tanzania ambayo znz ipo kuchota. Sisi tunasema hapana! mwisho wa kutumia jina kuchota sasa basi.
Na njia nyepesi ni kutenga mambo, yale ya Tanzania, Tanganyika na Zanzibar. Hiyo itasaidia sana kuvua koti.
Koti tulilovaa halitusitiri chochote, ni mzigo sasa tunataka t-shirt tu. Koti lipi kwa uchumi wa znz?

Katiba ya 1977 inaongoza Watanganyika. Wazanzibar hawaitaki. Wameidhalilisha, wameivunja na hawaitambui.
Wangekuwa wanaitambua ile ya 2010 isingesomeka kama ilivyo.

Wangekuwa wanaitambua wasingekuwa na unilateral decisions ambazo mwisho zinawaumiza.
Bandari huru imewasaidia nini hadi sasa? Mafuta yamepatikana na kuwasaidiaje?
Tunavuna gesi wao wanavuna nini. Tayari wameshajenga mpaka, si wenzetu ni raia wa nchi jirani ya znz. Ni suala la muda tu!

Elimu ya Uraia ingeanzia zanzibar na kuja Tanganyika. Huko ndiko wana nchi na kila kitu. Tanganyika tunahitaji nchi yetu kwanza halafu elimu ya uraia. Muhimu kwanza ni Utanganyika hayo mengine yatafuata.

Mtanganyika hahitaji fursa zilizozibwa kule znz. Lakini pia hahitaji kuibiwa zaidi.
Tunataka tutumie tulicho nacho kwa ajili ya watu wetu. Znz hatuhitaji tena, ni nchi ya jirani na tungeomba wapewe passport zao.

Na mwisho Watanganyika ni wamoja. Unajaribu kuwatisha kwa ukabila. Hatujasikia Mmakonde akidai passport.
Hatujasikia Mngindo kachomwa moto Arusha. Wala hatujasikia msukuma kapewa nafasi za upendeleo asilimi 21 na zingine. Wanaotuletea ubaguzi ni wazanzibar, ni muhimu tukawapa nafasi.

Njia rahisi ni Tanganyika kurudi tu, halafu mengine yatafuta. Wewe unaona ukabila wa Tanganyika, hebu angalia video hii hapa halafu urudi tuongee zaidi.

https://www.youtube.com/watch?v=Dtqh8fva8Ro
 
Mkandara
Video hiyo nimekuonyesha makusudi ili usitumie makabila kuwatisha Watanganyika.
Pili, wznz wenyewe wanasema kila jambo limekubaliwa. Asilimia 21, PAYE, Mikopo na kujitafutia misaada.

Kumbuka mikopo wanapata kwa dhamana ya Tanganyika yenye assets. Mikopo hiyo haionyeshwi italipwaje, tunachojua ni kumbebesha Mtanganyika mzigo.

Tatu, Wazanzibar watakapopata mikopo na misaada Wataitumia vipi katika muungano. Kama ni yao, kwanini hii inayokuja kwa Tanzania ikihudumia wao(Ulinzi na usalama na mambo chungu nzima) ibebwe na Mtanganyika peke yake?

Nne, kwavile Tanganyika imevaa koti, hebu tuanze kuangalia mambo kwa undani zaidi.
Mkandara, naomba unipe bajeti ya Zanzibar ya ulinzi na usalama, na mambo ya ndani ya mwaka 2014/2015 . Hivyo viwili tu.
Halafu tutaendelea
 
Mkuu nimeisikiliza video hiyo kwa umakini na sielewi unachodai wewe zaidi ya kwamba Mtoa hotuba anaamini ktk serikali 2. Na zaidi ya hapo kaonyesha wazi kwamba serikali hii inaendelea kufanya makosa yale yale ambayo hayawezi kuondoa mapungufu ya Katiba bali kuondokana na kero zilizopo.

Na unafanya makosa yale yale unapotumia neno Tanganyika kwa sababu hakuna kitu Tanganyika ila kuna JMT ambayo ndio mdhamini wa mikopo ya Kitaifa. Na mikopo yote hutazamwa yenyewe ni jinsi gani itarudisha gharama za uwekezaji (mikopo) na hivyo dhamana ya JMT inatokana na kutazama faida ya uwekezaji wenyewe kama inavyofanyika leo hii wewe uktaka mkopo benki haitazami nyumba yako bali matarajio ya uwekezaji wako (business plan). Kwa maana hiyo huyu mjumbe hafahamu au anafahamu kuwa ni viongozi wa Zanzibar watakao faidika kama ilivyo kwetu ni viongozi wa CCM (Tanganyika) ndio wanafaidika na miradi ya uwekezaji kwa dhamana ya JMT. Huku ndio kuvaa koti mkuu wangu yaani unafaidika wewe kwa jina la JMT au Utanganyika/Uzanzibar. Hizi ndio Siasa za Bongo!

Tazama na soma miradi ya makaa ya mawe, tazama miradi ya dhahabu, gas na kadhalika wewe Mtanganyika unafaidika vipi? Hawa wanasiasa wanaowadanganyeni nyie na kuwatia upofu mnawasikiliza wa nini wakati wanacholilia wao sii kuiwezesha Zanzibar ama Tanganyika bali kuzinufaisha nafsi zao na utajiri uliopo. Sasa Hata kama Zanzibar wamepewa fursa hizo pasipo mambo haya kuwa ya Muungano ina maana Maalim Sief au Karume wanaweza kufanya makubalianao na shirika la Arabuni kujenga bandari ambayo yeye ana share na likapitishwa kwa sababu ni SIRI ya nchi. Wewe na mimi tusiweze kupinga na pia hatua hiyo ikapingana na uwekezaji wa bandari za Bagamoyo na Dar. es salaam maana hili sio swala la Taifa.

Hakuna njia pekee ya kumaliza mgogoro huu isipokuwa kuweka mambo yote kuwa ya Muungano hivyo kama inajengwa Bandari zanzibar ya Kitaifa na kuifanya Zanzibar freeport basi bara zinaandaliwa usafirishaji wa mali hizo mikoani na nchi za jirani kaa vile kuhakikisha uwanja wa ndege wa Kimataifa unajengwa Bagamoyo kusafirisha mizigo. reli inajengwa kuunganisha Bagamoyo, Tanga, ile ya Kati na Tazara. Hivyo kila plan ya ujenzi wa miundombinu unatazama interest of the nation. haiwezekani kila nchi ijiamulie mambo yake kana kwamba hatukuungana.

Na kwa bahati mbaya sana hadi sasa hivi tuna gonjwa la kifikra na mwamko juu ya interest of Tanganyika na Interest of Zanzibar ndani ya Muungano. Wewe na hao UKAWA mnaendelea kuthamini interest of Tanganyika na hao Wazenji vile vile pasipo kujua hapa katikati kuna Politicians ambao wanajua wazi kwamba hakuna mtu kati yao anayetetea interest za Tangianyika wala Zanzibar ila interest zao wenyewe wakitumia jina la Utanganyika na Uzanzibar. Mjinga nani hapa mkuu wangu?.

Halafu unauliza bajeti ya Zanzibar ktk Ulinzi na Usalama wakati hili ni swala la Muungano? sikuelewi hata kidogo maana askari wetu wote wanaishi kutokana na kodi za wananchi. Na huyo mwananchi ni Mzanzibar na Mtanganyika bila kujali anaishi wapi maana katiba ya sasa inasema tuna nchi MOJA, Taifa MOJA ila serikali 2. Ina maana sisi sote ni raia wa Tanzania na inapofika swala la Ulinzi na usalama sisi ni kitu kimoja. Mikopo ya nje iwe vifaru, bunduki au ndege za kivita hailipwi kwa fedha taslimu, dhahabu au Almasi tunayozalisha.

Kwanza hivi vitu sio vyetu sisi tunapewa ruzuku tu hatuna mamlaka ya kuuza, Hiyo Tanganyika haina kitu kama Prof. Muhongo anavyowabeza wananchi basi ndio Tanganyika yenyewe ilivyo, haina uwezo wa kununua hata ndege ya Abiria leo uweze vipi kumudu ndege za kivita! Hivyo tunalipa madeni ya mikopo kwa mikataba ambayo inatulazimu sisi kuwauzia mali zetu kwa bei waloipanga wao, ama kukubali mikataba mibovu ya uwekezaji kama hii tunayoiona. Unafikiri yale maua ya Arusha yanaweza kununua vifaa vya kivita ama kuwalisha askari wetu!..Kwanza nambie wee hivi deni la taifa (external debt) limefika kiasi gani? I don't think you have any clue tumekopa vitu gani? na nani atalilipa au litalipwa vipi?

Kwa hiyo Mtanganyika mtumishi wa serikali anayeishi Zanzibar hahesabiwi kama ni Mtanganyika ktk kodi au Mzanzibar anayeishi bara hahesabiwi kama ni Mzanzibar bali MTANZANIA. Ila inaonyesha kufuatia fikra hizi za kugawana umaskini tunaelekea ktk kuondoa UTAIFA wetu kutokana na madai ya mamlaka. Kama watu hawaelewi maana ya mamlaka ya kuendesha shughuli za serikali wakazichambua kama ni Utaifa hili kosa la nani lkama sii Ujinga wa kutokuwa na elimu ya Uraia?

The only option ni:-
1. kufuta sehemu ya 2 ya katiba ibara ya 3 ili kuondoa mambo yasokuwa ya Muungano, kisha kuzipa mamlaka kamili serikali zetu kuendesha shughuli za maendeleo. Serikali kuu ni mdhamini mkuu wa mambo yote ya maendeleo ktk mawasiliano ya kisiasa na kibiashara na nchi za nje na - for the interest of the NATION.

2. Madaraka mikoani yarudishwe ili kila Mkuu wa mkoa (RC) awe ndiye Governor wa shughuli hizo na achaguliwe na wananchi toka vyama vya siasa/independent na mwenye CV inayokubalika. Kila mkoa uwe na mamlaka yake ya Kimkoa ktk mpangilio unaoshuka wilaya hadi kata kwa maendeleo ya mkoa mzima, hivyo kuondoa Utanganyika na Uzanzibar ili kila mkoa unatazama rasilimali zake ktk kupanga na kuchagua maendeleo yake. Tukiwa na mamlaka mikoani Utanganyika na Uzanzibar utakufa wenyewe!.

3. Mchango wa kodi kwa kila nchi utakuwa na sehemu 3. Ya kwanza ni Kodi ya Mkoa, 2. kodi ya nchi na 3. Kodi ya Taifa hivyo kila mkoa, nchi na Taifa zitafaidika na tozo kila pahala penye exchange ya ununuzi na hizo hivyo kuondoa Utanganyika na Uzanzibar maana mamlaka yanaanzia mikoani na kwenda juu had serikali kuu.

4. Maadam serikali ya Tangayika imeweza kuendesha shughuli zake ndani ya serikali ya JMT, hakuna sababu ya kuzaliwa Tanganyika leo hii wakati wananchi tunahitaji katiba mpya kabla ya mwaka 2015, ili kuondokana na mfumo wa utawala wa chama kimoja kushika hatamu. Maadam CCM ina nguvu zote za dola ina mapandikizi sehemu zote za Utawala basi itaendelea Kushinda kiti cha Uraia na hivyo ina maana hata kama CUF au Chadema wakishinda asilimia kubwa ya bunge bado rais ana nguvu kubwa kiutawala ambayo inakiweka chama tawala ktk uendeshaji wa shughuli zote za maendeleo nchi iwe Tanganyika au Zanzibar.

Kumbuka tu umuhimu wa kuendesha shughuli za maendeleo kuwekwa ktk serikali ni kutambua kwamba serikali hutokana na chama kilichoshinda uchaguzi wa jimbo, wilaya au mkoa na hivyo hawa kupewa mamlaka hayo. Ukiidai demokrasia pasipo kuziwezesha serikali kuendeshwa na chama kilichoshinda ni kujidanganya wenyewe na hili neno Demokraisa maana demokrasia sio kumwezesha mtu agombee ubunge au urais bali ni kuiwezesha itikadi, sera na ilani walochagua wananchi kuendesha shughuli za maendeleo yao. Sio hivi leo Chadema wameshinda mikoa ya Arusha, Mwanza na Mara lakini ni serikali ya CCM yenye itikadi potofu, sera za kuungaisha na ilani zisizokubalika inayoendesha shughuli za maendeleo ya mikoa hiyo!

Hii ndio sababu tunahitaji Katiba mpya, na sio Muungano mpya!
 
Mkuu Mkandara
Nimekuwekea video ili uache utaratibu wako wa kuwatisha Watanganyika ni wamoja ndani ya muungano, nje ya hapo wataanza Ukurya na Unyakyusa. Nimekuweke uone hali ya Zanzibar kama alivyosema Yahaya Kassimu. ''muungano ukivunjika na ninyi manrudi kwenu,pale mnapaita tu, Wallahi mtaondoka'' .
Je, huoni tatizo hapo? Ni akina nani wataondoka.

Pili, nimekuwekea usikilize wakikiri kuwa ndani ya muungano wanapata kila wanachodai.
Wewe unapata wapi ushujaa wa kusema wanaonewa ikiwa wao wenyewe wanasema hakuna uonevu.

Tatu, maelezo yako umekubaliana na Warioba. Usichokitaka ni jina Tanganyika.
Unaposema tumeweza kuendesha S2 bila matatizo unajidanganya.
Suala la muungano lina mtatizo na wewe ndiye muumini wa Tanganyika kuvaa koti.

Huwezi kuwa na JMT ndani yake Tanganyika ikafanya kazi. Haliwezekani,ndilo tatizo la miaka 50. Utatengaje shughuli za waziri au katibu mkuu katika kushughulikia Tanzania na Tanganyika.
Hesabu zinakataa, mantiki hairuhusu. Unagoma tu lakini unaelewa ukweli.

Muundo uliousema ndio waWarioba, kinachokutisha ni kuzinduka kwa Tanganyika. Unafahamu uwepo wa Tanganyika utaondoa loophole za kutumia herufi ZAN katika kuiba, kudoea. Hilo ndilo linakutesa, na umeshalisema hapa JF(Kumbu kumbu ipo). Unakumbuka kauli ya ''wazanzibar hawajui, wataumia sana Tanganyika ikirudi""

Kuhusu ulinzi na usalama, nimekuuliza makusudi ili kukuonyesha misaada na mikopo si muhimu kuliko wanachokipata. Hawana bajeti ya ulinzi na usalama ambayo kwa bilioni 400 ingechukua zaidi ya Bilioni 150. Ukiweka na wizara zingine wasiokuwa nazo, znz ingebaki bila bajeti ya kulipa mshahara wa sheha.
Leo yote hayaonekani kinachoonekana ni pesa kutoka Washington.

Nikupe mfano kwa hili, kuna mtu alikuwa anamuomba mwenyezi mungu amsaidie kupata kazi.
Amesali usiku kucha kwa miaka 2 bila kupata kazi.Kwa miaka 2 alikuwa na afya akitembea kutafuta kazi.

Baada ya miaka 2 akaacha kumuomba mungu kwasababu hajamsaidia katika maombi ya kupata kazi. Akasema hakuna haja ya kuendelea na swala au maombi yake.

Masikini ya mungu, kumbe huyu jamaa hakujua mungu alikuwa anasikiliza na kujibu swala na maombi yake. Kwa miaka 2 hakuugua hata siku moja. Kuna uwezekano angepata kazi na kuugua kipindi hicho na pesa zote za mshahara kuishia katika matibabu. Mungu alimsaidia kumwepusha na maradhi kwasababu maradhi ndilo tatizo lililomkabili, si kazi.

Mfano huo ni sawa na wazanzibar,wanaona kukopa washington ni fahari kama yule mtu aliyekuwa anatafuta kazi. Hawajui kuwa kutokuwa na bajati za ulinzi na usalama, mambo ya ndani, mambo ya nje, elimu na mzigo wa kubeba muungano ni mkubwa kuliko kupata pesa kutoka kwa Christine Lagard zenye riba. wapo mgongoni wakiendelea na safari na hawaoni, wanachotaka ni kutembea chini waonekane wanaweza.

Muda umefika, wapewe nafasi ya kukopa IMF na kupata misaada kutoka Uarabuni na Ulaya bila kikwazo. Wapewe mamlaka za kumiliki wizara zao, wapewe kila wanachokitaka.
Sisi tunaizindua Tanganyika, ni nafuu kuzuia pesa zetu kwenda znz kuliko kuwakataza kukopa.

Tanganyika ni muhimu kwa wakati huu kuliko wakati mwingine.
Hakuna wa kuizuia, wapo wa kuichelewesha. Tanganyika itazinduka katika meza ya majadiliano au kinyume chake wazanzibar watalipa gharama kubwa kuizindua.

Hakuna kurudi nyuma ni Tanganyika tu. Hilo litatokea iwe mwaka huu au kesho lakini lazima litokee na wznz waelewe hivyo.

Likitokea mezani ni nafuu kwao, wakisubiri tuwatake waizindue Tanganyika wataumia sana.
 
Back
Top Bottom