UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

Uzuri wa siasa za Tanzania, kila mtu ni political analyst!

Karibuni kwenye political ground zero ili mzionje siasa zilizo halisi na siyo hizi za kudonoa kupitia keyboard/keypad kwenye mitandao.

Hata Katibu wenu Mkuu, Dkt. Slaa alishawakaribisha katika andiko lake hili,

Kujenga hoja katika mlengo wa siasa za probability zenye matokeo ya aina mbili hakuhitaji kisima kirefu cha fikra!
Kama probability hizo zina reproducible results zinapaswa kuangaliwa kwa jicho pevu.

Unachotaka kusema hapa ni kuwa watu wasitoe maoni yao kwa kuangalia kwa upana.
Pengine unashauri wakae kimya kama ilivyokuwa hapo awali, nyakati za zidumu fikra.

Mkuu, kila lililosemwa lililtokea, linatokea au litatokea. Tunajua si jambo rahisi kumridhisha kila mtu hata hivyo wazungu wanasema 'if you wanna please everybody you will end up pleasing nobody''

Tunafahamu maumivu ya sindano, lazima tukubali ni dawa.

Zama hizo ilikuwa si rahisi kwasababu nchi ilikuwa na uongozi na viongozi.

Siku hizi huhitaji hata probability, ni kikombe cha chai tu pembeni mwa keyboard utaona kila kitu.

Ni siku hizi ambapo kila mwenye suti na tai anataka kuwa Rais, unahitaji probability gani kujua nchi ipo halijojojo?

Sisi tusioweza kucheza uwanjani hatakutazwi kushangilia au kuzomea as long as kuna fyongo uwanjani.

Tunasubiri Mh Lusinde atangaze nia ya kuwania urais. Hilo nalo linahitaji probability!!!!
The bar is too low, every tom and dick would like to reach.

Hatutaona huruma au kumuonea mtu, tutapiga misumari pale inapopaswa.

Tusemezane
 
Uzuri wa siasa za Tanzania, kila mtu ni political analyst!

Karibuni kwenye political ground zero ili mzionje siasa zilizo halisi na siyo hizi za kudonoa kupitia keyboard/keypad kwenye mitandao.

Hata Katibu wenu Mkuu, Dkt. Slaa alishawakaribisha katika andiko lake hili,

Kujenga hoja katika mlengo wa siasa za probability zenye matokeo ya aina mbili hakuhitaji kisima kirefu cha fikra!

Hauitaji kuingia kwenye maji ya moto kujua ni maji ya moto au kuwaambia wengine kuwa hayo ni maji ya moto. Huitaji kuwa ndani ya siasa kutolea maoni siasa na ukawa sahihi. Ingekuwa hilo ni kweli (kuwa lazima uingie so called ground zero) watu wengi wangekuwa hawatolei maoni siasa za nchi kama ya Marekani kwani wengi labda hata kukanyaga miguu huko hawajawahi. Siasa za Tanzania hazifanywi gizani kiasi kwambawalioko gizani tu ndio wanajua nini kinaendelea.
 
Mkuu, tatizo ni kuwa huko gizani wanakanyagana, ukimulika tochi wanalalamika kwanini unaleta 'probability za wao kuonekana''

Wanachotaka tujipange barabarani ili waje na tai zao wakaiahidi kutuletea maendeleo.
Makontena yapo bandari, pesa za kukomboa wanazo, usafiri wa kuyaleta makontena yaliyosheheni ubuyu wa maendeleo wanazo.

Tunapohoji iweje wawe na uwezo huo halafu washindwe kulipia hoteli ya sh 30,000 Dodoma, wadai laki 2 za kukaa katika viti vyao vya kazi, tunaambiwa tuache probability.

Hotuba ya JK na mchakato mzima hauhitaji probability, ni kitu kilichoonekana kufeli bila cert ya VETA.

Tukisema tunaambiwa probability hazifai, wanachotaka kusikia ni CCM oyee! nasi tuitikie kwa nguvu.
Wao wanachupa za maji ya Kilimanjaro sisi tunagombana visimani kutia vinywa vyetu kupooza makoo ya kusema Oyee!

Hivi kunahitajika probability yoyote kujua kuwa watu wapo Dodoma kukusanya posho na si vinginevyo

Tutasema na kuwamulika huko walikojificha, kukaa kimya ni kubariki uhuni na uhalifu wa kisiasa.

Wameshindwa uchumi, wamefeli katiba na sasa hawawezi hata kulaani ajali za mabasi. Tunahitaji probability ya kujua nchi inakwenda kwa solar energy!
 
Nakubaliana nanyi kuwa uchambuzi wa mambo ya siasa hauhitaji uwe kiongozi au mwanasiasa.

However, uchambuzi wa mambo ya siasa ukishakuwa umejikita kwenye mahaba au chuki kwa upande fulani, uchambuzi huo mara nyingi, kama siyo mara zote huwa hauna maana.

Mfano mzuri ni msissitizo wenu kuwa CCM imefeli, wakati ni wazi kuwa CCM imefanikiwa kimkakati kwenye kila kitu. Mchakato huu wa Katiba mpya ni kielelezo kizuri cha jinsi UKAWA walivyopoteza dira. Kila issue ambayo UKAWA imepigania, imeishia ukingoni.

Mnachoshindwa kwenye siasa zenu ni kutofanya maamuzi juu ya common denominator, ambayo ni wananchi. mnaposita kuwapa nguvu wananchi juu ya mustakabali wa taifa lao kwa kupitia refferrendum, ndipo mnapojitenga na wananchi na mwisho wake kurudi kwa viongozi wa upande mwingine.

Yapo wapi yale ya kwenda kwa wananchi? ... mbona mnakokwenda sipo?
 
Well, tutaepuka vipi chuki ikiwa watoto wetu wanakaa juu ya matofali ili hali baba na mama zao wapo Dodoma wakikusanya posho?

Tutaepuka vipi chuki kama nchi inakwenda kama boya baharini nasi tukiwa tumo ndani?
Tunaepeuka vipi chuki kama viongozi wametugeuza mazezeta, wanatutenda wanavyojua? n.k.

Tutapekuaje chuki kma wakunga wanazalisha bila gloves wakati bilioni 8 zimetumika kujenga viti?
Mbona wanapofanya mikutano yao ya chama hufanyia kizota na Diamond, leo nini kimebadilika?

Ni heri basi ya chuki kuliko hasira, maana kungekuwa kwingine tusingekutana katika keyboard bali misituni tukiwa na magodoro vichwani,wakina mama wamevimba miguu, na brazamen wakichimba makaburi on the run.

Kuhusu CCM kufeli, hilo ni mtazamo wa kila mmoja. Mfano, kama watu wanakufa katika ajali na CCM iliyo na serikali haijishughulishi wala kusikitika inawezekana ni ''pass'' kwa wale wanaotaka idadi ya watu wapungue.

Kwa wale wanaoona mbali zaidi ya pua zao huko ni kufeli.
Kwahiyo uzuri wa jambo upo machoni mwa mtazamaji i.e the beauty is on the eye...

Kufeli kwa CCM huwezi kulinganisha na kitu kingine. UKAWA hawjawahi kushika dola, sasa unapowalinganisha na wenye dola unakosea. Kufeli kwa CCM hakupimwi kwa makosa ya UKAWA, bali matokeo ya kazi zao miaka 50 hadi sasa.
Hivyo unapopima UKAWA na CCM ni kuidhulumu CCM. Kipimo cha CCM ni miaka 50, cha UKAWA ni miezi 4.

CCM haijafanya maamuzi kwa ajili ya wananchi. Wanapovua watu magamba kwa maneno si maamuzi.
Wanapowakabidhi hao wenye magamba dhama ya kuandika katiba tena maadili ya uongozi huko ndiko kufeli.
Leo unamkabidhi fisi ulinzi wa bucha na kurudi nyumbani ukisema umefanikiwa?

CCM haijafanya maamuzi ya wananchi, walipowasokomeza wabunge wao matambara na kuzalisha UKAWA ni kufeli.
CCM hawajafanya maamuzi, pale waliposhindwa kubaini katiba iliyotuikifisha hapa haifai tena, hayo si maamuzi ni wehu.

CCM haijafanya maamuzi maana nchi leo inakwenda kwenda, kila siku kama si mzungu ni kalasangi wanakuja na kuchota
CCM haijafanya maamuzi kwa wananchi, hiawezekani kuendelea na bunge lililofeli ukasema ni uamuzi wa wananchi
CCM haiwezi kukana taarifa ya tume zake zenye maoni ya wananchi ukasema ni uamuzi.

Orodha ni ndefu,ninachotaka kukuambia ni kuwa kipimo cha CCM ni maiaka 50, na katiba ni sehemu tu ya kiashirio cha kushindwa kwake. Miaka 50 ni muda mrefu kwa chama kushindwa kusimamia zoezi kama la katiba. Huko ndiko kufeli na wala si kulinganisha na UKAWA.

Kuhusu maoni na uchambuzi, tunafahamu kuwa watu wana mtazamo tofauti. Hilo halituzuii kusema kile tunachotaka kusema, na wala hatulazimiki kusema kile mnachotaka kusikia.

Tulionya wakati JK anateua tume kuwa lazima kura ya maoni kwanza.Miaka 2 baadaye waziri mkuu anasema kile kile.
Tukasema bunge likiwa na wanasiasa litavunjika, sijui kama limevunjika au la.
Tukasema mchakato utaharibiwa na CCM, hatujui kama tulikuwa bias au waongo
Tukasema CCM wataanza kuumana, mbona wang'atana sasa hivi
Tukisema Sitta atavuruga bunge hata kabla ya kuchaguliwa, samahani kwasasa analiendesha vizuri sana.

Tuliyosema yametokea, yanatokea na mengine yapo njiani.
Tuliahidi kukuita siku moja udhihirishe kuwa ni wambea, leo sijui unataka utuambie nini tena.
Tafadhali tafuta neno jingine maana umbea umegeuka kuwa ukweli.

MJINI CHAI
 
Last edited by a moderator:

Mbona mnaogopa hiyo referendum sasa?

Tukasema bunge likiwa na wanasiasa litavunjika, sijui kama limevunjika au la.
Bunge bado lipo.

Tukasema mchakato utaharibiwa na CCM, hatujui kama tulikuwa bias au waongo
Uwongo mtakatifu. UKAWA ndyo walioondoka bungeni, sababu bado hatujui.

Tukasema CCM wataanza kuumana, mbona wang'atana sasa hivi
Wanang'atana wapi? Mbona wanapata wanachotaka?

Tukisema Sitta atavuruga bunge hata kabla ya kuchaguliwa, samahani kwasasa analiendesha vizuri sana.
Lipo poa tu.

Tuliyosema yametokea, yanatokea na mengine yapo njiani.
HAMNA KILICHOTOKEA..

Tuliahidi kukuita siku moja udhihirishe kuwa ni wambea, leo sijui unataka utuambie nini tena.
Tafadhali tafuta neno jingine maana umbea umegeuka kuwa ukweli.

Umbea upo paleale, hamna mtachopata na Status quo will prevail
 
UKAWA WAINGIZWA KINGI BILA KUJIJUA

NJAMA ZA WAGAWE UWATAWALE ZINAFANYA KAZI

JK NA CCM ''OFF THE HOOK''

Baada ya Rais kuvuruga mchakato,imeonekana bunge la CCM linazidi kupoteza uhalali wa kisiasa, mvuto na thamani. Kitendo cha mwanasheria wa Zanzibar kujitoa kamati ya uandishi kimepeleka kishindo kikubwa.

Hata hivyo suala hilo halipewi kipaumbele ili kufifisha hoja na hao watakuwa mashahidi siku za usoni

Mwanasheria mkuu ndiye mshauri wa Rais wa SMZ. Kujitoa kwake ni ashirio zuri sana la hali tete kwasasa na baadaye. Waziri wa sheria alishajitoa. Hivyo SMZ inakuwa haina uwakilishi wa kisheria si kisheria bali kwa uhalali wa kisiasa.

Habari za ndani zinaeleza mwanasheria kashtushwa na uwepo wa rasimu hata kabla ya majadiliano.

Mengi zaidi kuhusiana na mwanasheria yatasikika siku za karibuni.

Mwenyekiti Sitta ameeleza kutoa maelekezo ya jinsi ya kujadili rasimu.
Hii ni mara ya pili akitoa onyo hilo ikiwa ni dalili nyingine ya mambo kuwa na utata.

Katika hatua nyingine, wapinzani wame endelea kukutana na Rais kutafuta muafaka.

Haifahamiki ni muafaka gani ikiwa Rais alishatoa msimamo wa S3 kupatikana atakapoondoka.

Huko nyuma tumetoa angalizo, taasisi muhimu zipo kazini ili kuwafarakanisha UKAWA.
Tulisema njia rahisi ni kuwagawa ili watawalike kwa urahisi.

Mabandiko ya hivi karibuni tumehoji, iweje rais aliyevuruga bunge kwa makusudi awe na jibu tofauti na kile alichokifanya?
UKAWA wamealikwa Dodoma, na duru tukatilia shaka mwaliko ulivyotolewa.

Kwanza, mwaliko umetolewa kupitia kituo cha demokrasia nchini.

Ni kituo hicho ndicho kilimwalika JK katika moja ya mikutano.
JK alitoa hotuba ilyokuwa tamu, imesheheni tamaa za utaifa na kila aina ya wema.

Ghafla JK akatinga bungeni.
kwanza, kaivuruga tume ya Warioba, na pili kachomeka maoni yake ya rasimu inayofanyiwa kazi sasa.

Pili, walioalikwa ni wanachama wa TCD, wakiwemo wapinzani akina Mrema ambao tayari wapo bungeni wakiungana na CCM kuifanyia kazi rasimu ya mafichoni. Yupo pia Memosa Cheyo kama mwenyekiti ambaye kama Kuga Mziray, Hamad Rashid naoye yupo bungeni.
Ni mkusanyiko wa UKAWA na genge la wasaliti wa taifa hili.

Mbinu iliyotumika ni kuwakwepa UKAWA na kuwaingiza akina Mrema na Cheyo kama mpini mahususi wa kuimaliza UKAWA

UKAWA hawakuwa na sababu zozote za kuwashirikisha watu walioko bungeni tayari.

Ilikuwa ni kuwaacha waendelee kujadili rasimu ya CCM kwavile wao walikuwa ndani tayari na hawakuwa na malalamiko.
Tuliwaonya UKAWA kuhusu ushiriki wa watu hawa.

Habari zilizopo, ndani ya TCD kumekuwa na mgawanyiko kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari

Habari hizi si za kupuuzia hata kidogo. Haiwezekani Mrema aliyewalaani UKAWA akawa kambi moja na UKAWA wakabaki salama? Haiwezekani Cheyo akawa na CCM leo, kesho akawa UKAWA, haiingii akilini.

Kitendo cha UKAWA kukubali majadiliano kupitia TCD na si UKAWA kilikuwa ni kosa la kifundi na tulisema

1. Kwanza, JK atawatumia kama mpini wa kubeba shoka linaowakata wenyewe

2. Imepatikana fursa ya wagawe uwatawale kupitia wananchama wa TCD3

3. JK na serikali yake wameweza kupenyeza mamluki ndani ya UKAWA kwa kutumia TCD

Bandiko la jana tumeeleza jinsi JK na serikali yake watakavyojiweka kando na wapinzani kujinyonga kwa kutupiwa kamba

Kama tulivyoandika leo linaweza kutoka tamko linalohusu majadiliano hayo likisomwa na 'wapinzani'
Tusubiri hadi jioni.

Duru tunauliza , UKAWA wakikubali kurudi bungeni, ni ili iweje na kitokee kitu gani?

Wakikubali marekebisho ya katiba kwenda uchaguzi, swali linabaki ni wema gani alio nao JK kwa UKAWA ambao hana kwa taifa hili ?

Tusemezane
 
TULISEMA YATATOKEA, YAMETOKEA, YANATOKEA NA YATATOKEA

TUMEBEZWA NA KUKEJELIWA. SASA UKWELI UPO UNATUTETEA NA KULINDA HESHIMA YA JAMVI

Wanaduru yote tuliyoyasema siku za nyuma katika mabandiko ya duru yanaendelea kutokea.

Tulisema Bunge litavunjika, yametokeA
Tulieleza mbinu za CCM kujinasua, imetokea
Tukaeleza athari za majadiliano na TCD, imetokea
Tukawaasa UKAWA kwa kila hatua, ndivyo imetokea.
Na tulisema hakuna nguvu ya dola iliyowahi kushinda umma, imetokea

Orodha ni ndefu

Tumeitwa wapiga ramli, wavizia probability na wapika majungu. Ushahidi sasa upo wazi

Kuanzia jioni ya leo tutakuwa na mabandiko 4 mfululizio yakichambua hatua zilizofikiwa, athari kwa CCM na UKAWA na nini kinapangwa siku za usoni kwa mbinu na hila.

Tutaendelea.....

cc MJINI CHAI
 
BUNGE LA KATIBA LAFIKA TAMATI KWA AIBU

JK AKWEPA LAWAMA ZA MUDA MFUPI

SAMWEL SITTA ''UNDER THE BUS'' SAFARI YA KIASIASA YAGOTA

UKAWA WAPATA ''NUSU GLASS YA MAZIWA'' WARUHUSU UHARIBIFU

Tunaanza mfululizo wa mabandiko kama tulivyoahidi hapo juu. Tunaangalia hatima ya Bunge la katiba na yatokanyo

Sehemu I

Ile azma ya JK kuwapa Watazania katiba mpya imebaki katika vitabu chakavu vya historia.
Kilichomponza JK ni kutaka kumfurahisha kila mmoja. Mwishowe hakumfurahisha yeyote.
JK alifanya mambo kwa mjaribio, akamtumia mbwa mzee kumfundisha mbinu mpya.

JK alishindwa kusoma nyakati, mazingira na watu.Watanzania wa 1950, 1970,1980 n.k. ni wa vizazi vyenye mahitaji tofauti.

Mwaka 1950 nguvu ilikuwa kumaliza ukoloni. 1960 ni kujenga taifa jipya. 1970 vipaumbele vya jamii. 1
980 mageuzi ya kisiasa. Mwaka 1990 mageuzi ya kiuchumi, mwaka 2000 teknolojia, 2010 Uchumia na Usalama.

Mbinu alizotumia Nyerere kupigania Uhuru, Mwinyi kuleta mageuzi ya kisiasa na kufungua milango ya kiuchumi, Mkapa kuleta mageuzi ya kiuchumi haziwezi kutumika katika mazingira mengine

Wanasema waswahili, kila zama na kitabu chake,ndilo kosa kubwa alilofanya JK.
Mageuzi ya nchi yanahtaji uthubutu bila kujali nani anafurahi nani anakasirika kusimamia kile kilicho bora kwa taifa.

JK alianzisha mchakato akiwa na nia mbili. Kuwafurahisha Watanzania na hata kushangiliwa na Wapinzani.
Na pili, kuwafurahisha wahafidhina wa chama chake kwa kutokwenda kinyume na matakwa yao.

Kuweka mambo hayo mawili katika kikapu kimoja ni sawa na kuweka nazi na mayai kikapu kimoja.
Kilichotokea ni nazi kuvunja mayai, na nazi kuchafuka kwa ute wa mayai mengine yakiwa viza. Ndipo JK alipo leo.

JK ALIPANGA NINI
JK alitumaini mbinu alizotumia Nyerere za kubadili bunge na kutenegeneza katiba kwa njia za mkato ingefanya kazi.
Alitumia mbinu za white paper ya Mwinyi kuhusu vyama vingi ingefanya kazi
Alitumaini Mbinu za Mkapa kuficha taarifa za Nyalali, Kisanga n.k. zingefanikiwa.
Alijifariji tume zilizoundwa hazikuwa na meno na ni nyingi, ya wakati huu isingekuwa tofauti na zilizopita.

Kitu alichosahau ni kuwa kila kitabu na zama zake, mazingira ya watu na nyakati yanabadilika. Hapa ndipo alipokwama.

JK ALIPUUZA DALILI

Dalili za tatizo kubwa la katiba zilikuwa wazi. Mazingira yalihitaji utaratibu mpya wa kujitawala.
Mazingira yalikuwa yanafunguka taratibu ''unfold' kadri wakati ulivyosonga mbele
Nyerere aligundua, akaondolka mapema kabla ya mazingira hayajamkuta au kumpita.

Dalili za awali zilianza kidogo kidogo. Kuchafuka kwa hali ya hewa visiwani, Jumbe ni shahidi.
Kuundwa kwa kundi la G55, machafuko ya 2001 Znz n.k.
Kiu ya katiba mpya inayokidhi mahitaji ya wakati yalichagiza suala la muungano.

JK AJARIBU KUZUIA HOJA YA MUUNGANO

Dalili nyingine ni pale mswada wa sheria ya mchakato ulipochomwa moto, tena Sitta akishuhudia.
Zanzibar kuandika katiba bila ya kumshirikisha, na yeye kubaki akitoa baraka za uhalifu wa katiba

JK akajaribu kuweka mkakati wa muungano kutoguswa kwa namna yoyote ili afurahishe wahafidhina wa CCM , kwa upande mwingine katiba ibebe maudhui ya wananchi. Kachanganya nazi na mayai katika kikapu kimoja.

Duru za siasa tulieleza siku aliptoa hotuba ya kuanza mchakato wa katiba.
Tulieleza wazi kushindwa kwa JK katika hili kwasababu JK alitumia short cut na mbinu za zamani.
Alitumaini uandishi wa katiba kufunikwa kama zilivyofunikwa tume zilizopoita. Mbinu za zamani katika mazingira na kizazi kipya!

Kitendo cha kukwepa taratibu za uandishi wa katiba ndicho kilichagiza 'curiosity' kuhusu muungano.
Kikajenga mazingira ya kuwa na 'vita' ya kutaka muungano ujadiliwe.

Tulionya mapema, tume ya Warioba isingeweza kuzuia wimbi la mageuzi.
Na kwa bahati nzuri au mbaya wimbi hilo lilivuma na kuingia Tanganyika.

Aliyesaidia kulivumisha ni JK kwa kuacha wazanzibar waamue hatima ya muungano bila kujua wadau wa muungano ni Watanganyika, wazanzibar ni waalikwa tu.Hapo ndipo mgogoro huu unaolitesa taifa kwa hasara ulipoanzia.

Halikuwa jambo la siri kufeli kulikuwa dhahiri. Ni Kiburi cha viongozi wa Tanzania wasiojifunza kuhusu jamii wanayoitawala. Wanadhani upo uwezekano wa kutumia mbinu zile zile kwa watu wale wale, na kila mara.

Mchakato umeshindwa, na hili ni kushindwa kwa Rais Kikwete.
Mbele ya safari historia haiwezi kutoa nafasi kwa JK kujisahihisha, historia itaandikwa na sasa inajiandika.

Legacy yake itakuwa kushindwa kuliongoza taifa katika mageuzi muhimu ya karne hii.

Itaendelea sehemua ya II
 
Sehemu ya II

KUTUMIA WANASIASA BADALA YA WASOMI NI ZAO LA KUSHINDWA KWA JK

JK na serikali yake walidhani wataweza kutumia propaganda za wanasiasa, vitisho na uzushi kuwalaghai wananchi.

Mchakato ulipoanza, tulionya mbinu hizo haina nafasi.
Wanasiasa wa CCM ya leo si wale wa CCM ya miaka 20

Hawa wa leo ni walaghai, hawana maono, wapuz na ni wapiga debe wasiojua wanapiga mirindimo gani.

Tulisikia hoja za kuvunjika kwa amani, kupoteza uzalendo, kutokuwepo kwa taifa la Tanganyika, gharama za kuendesha serikali, umoja wa kitaifa, kumaliza kero, kutazama kwa jicho la karibu na maneno ya kipuuzi yasiyo na hesabu.

Kwavile JK amezungukwa na kundi la wachumia tumbo ambao kelele ndio mradi wao, hoja zao zilishindwa mbele ya umma.

Hawakuweza kusoma nyakati na mazingira, wakatumaini zile mbinu zao za zamani zitafanikiwa.

Wananchi na duru walionya, ili katiba iandikwe ni lazima tuwe na muafaka wa kitaifa utakaotengeneza agenda ya taifa ya miongo mingi ijayo. Hilo ni pamoja na kumaliza manung'uniko yaisiyoisha ya muungano.

JK badala ya kusikiliza wananchi, akawasikiliza wanasiasa uchwara waliomzunguka.
Akaunda tume ya kunyamazisha suala la muungano, katoa pipi kwa wazanzibar na hata kuruhusu katiba ivunjwe ili mradi muungano usijadiliwe.

Duru tulisema, katiba inahusu mambo mengi muhimu ya maisha ya wananchi, lakini suala la muungano litakwamisha na hivyo kura ya maoni ni muhimu kwa wazanzibar ili tujue tupo pamoja au wameshatuacha.
Ndivyo ilivyotokea Dodoma leo.Muungano umekwamisha katiba.

KUSHINDWA KWA JK NI KUSHINDWA KWA TAIFA

Rekodi ya Tanzania ni nzuri hadi karibuni. Tuliweza kusuluhisha na kuleta wananchi wa mataifa mbali mbali kwa pamoja kwasababu tulikuwa ni role model. Tulikwenda Burundi tukapewa heshima, kama ilivyo kwa Rwanda, Kenya, Madagascar, Comoro n.k.

Ingawa hayo mengine yamefanyika wakati wa JK, ukweli ni kuwa rekodi ya Tanzania ndiyo iliyotangulia na wala si jina la mtu au watu. Hivyo JK aliheshimiwa kwasababu ya bendera aliyobeba na rekodi yake safi,EAC, SADC, AU, UN n.k.

Leo sijui nani atawasikiliza Watanzania ikiwa wameshindwa kukaa pamoja na kuandika nyaraka yao wenyewe ya kujitawala.

Huko Uingereza sasa ni kicheko maana wanatamani turudi Lancaster house wakatusaidie kuandika katiba.

Si kwamba hatuwezi, bali hatuna uongozi wa kutuwezesha. Hili linaangukia mabegani mwa JK bila kupepesa macho.

Heshima yetu ta kuwaleta pamoja, SWAPO, ANC na PAC, Frontline state, Kibaki na Raila, South South commission, huko ndani ya UN, sauti kwa niaba ya china,Sauti kwa niaba ya Wanyonge sasa imeyeyuka kama bonge la barafu nyikani.

Nani atamsikiliza JK ikiwa yeye ameshindwa kuwaleta watu wa taifa lake pamoja kuandika nyaraka yao?

Hivyo Watanzania waangalie kufeli kwa JK katika kwa namna nyingi
1. Ndani ya nchi, kama kiongozi aliyeshindwa kutuleta pamoja na kutuongoza
2. Nje ya nchi, kwamba sasa ile thamani yetu ya kuwa stable country imetoweka.
3. Majirani wanatungalia kwa mashaka, wenye mitaji wanafunga acount zao.

Hili linaathiri jamii kwa njia nyingi. Leo nani mwekezaji ataleta mtaji wake katika taifa lilisiloweza kukaa pamoja.

Nani atawamini viongozi walaghai mithili ya Lukuvi, Wasira na Samwel Sitta eti alete mitaji yake.

Kuna jambo moja tu tunalopaswa kulikumbuka, haya yametokea wakati wa enzi za JK.

Hii ndiyo itakuwa legacy yake leo na siku za usoni.

Tulisema nini na kimetokea nini?

Itaendelea.....
 
TULISEMA YATATOKEA, YAMETOKEA, YANATOKEA NA YATATOKEA

TUMEBEZWA NA KUKEJELIWA. SASA UKWELI UPO UNATUTETEA NA KULINDA HESHIMA YA JAMVI

Wanaduru yote tuliyoyasema siku za nyuma katika mabandiko ya duru yanaendelea kutokea.

Tulisema Bunge litavunjika, yametokeA
Tulieleza mbinu za CCM kujinasua, imetokea
Tukaeleza athari za majadiliano na TCD, imetokea
Tukawaasa UKAWA kwa kila hatua, ndivyo imetokea.
Na tulisema hakuna nguvu ya dola iliyowahi kushinda umma, imetokea

Orodha ni ndefu

Tumeitwa wapiga ramli, wavizia probability na wapika majungu. Ushahidi sasa upo wazi

Kuanzia jioni ya leo tutakuwa na mabandiko 4 mfululizio yakichambua hatua zilizofikiwa, athari kwa CCM na UKAWA na nini kinapangwa siku za usoni kwa mbinu na hila.

Tutaendelea.....

cc MJINI CHAI
Ndugu,
Naomba ieleweke kuwa CCM na serikali yake imepata kile ambacho ilikuwa inakitaka kwa njia ya mapatano, au mwafaka, kwa maana ya consensus kwa faida ya mstakabali wa Taifa, wakati huo huo vyama vya upinzani na hasa vile vianvyojiita UKAWA vimepata kile ambacho vimekuwa vikitafuta kwa njia ya maelewano kwa maana ya compromise.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya maelewano (compromise) na mapatano au mwafaka (Consensus).

Katika maelewano au compromise, pande zinazokinzana hatimaye zinakubali kwa shingo upande ili kutokukwamisha maamuzi (UKAWA). Pande zote zinapata kidogo na kupoteza kidogo, na kila upande huwa na mkakati wake wa kupata zaidi katika duru ya pili. Kwa hivyo, maelewano kamwe hayawezi kuwa kwa moyo safi. Maelewano au compromise, yanazaa uamuzi legelege.Kikao chao cha kwanza na Rais Kikwete kilionyesha tofauti zao mpaka Rais Kikwete akawaambia wakajipange upya ili warudi na hoja zinazoeleweka.

Mapatano au consensus (CCM + Serikali), kwa upande mwingine, ni maafikiano yanayofikiwa baada ya mjadala mrefu, kila pande akilenga kuthibitisha hoja yake na kwa njia hii kusadikisha wenzake kwamba hoja yake ni sahihi. Baada ya kufikia uamuzi wa mwafaka, kila mmoja anatoka akiwa ameridhika na amefurahi. Hiki ndicho kilichofanyika baina ya CCM na Serikali.

Kuna baadhi ya Watanzania ninaamini wana tabia ya kusahau sahau!.

Hakuna suala jipya lililosemwa na kukubaliwa na Viongozi Wakuu wa Vyama vya siasa vyenye Wabunge vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD). Yaliyosema ni yale yale ambayo Serikali kupitia kwa Rais Kikwete iliyasema na serikali imekuwa ikisisitiza kila mara.

Ikumbukwe kuwa, Rais Kikwete wakati akihutubia maelfu ya wafanyakazi katika siku kuu ya Mei Mosi ambazo Kitaifa zilifanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam alikaririwa akisema,

“Waliomba nyongeza ya muda nikawapa siku 60, ni matumani ya ngu ndani ya siku hizo watafikia maridhiano na kutuletea Katiba bora, hakutakuwa na muda wa nyongeza, tukiongeza zaidi ya hapo itakuwa ni mwaka mzima tunafanya jambo hilo hilo,” alisema Rais Kikwete, ambaye aliongeza siku 60 baada ya bunge hilo kusuasua kutokana na kutawaliwa na malumbano na mabishano, hivyo kushindwa kufikia makubaliano katika masuala kadhaa kabla ya kuanza kujadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

“Tukiongeza zaidi ya hapo ni kazi, itakuwa mwaka mzima tunazungumzie jambo moja watu watachoka kuona jambo hilo hilo, tunataka kuona na kufanya mambo mengine,” alibainisha.

“Wakishindwa kutupa katiba inayopemndekezwa, itabidi tusitishe mchakato hadi mbeleni,”

Alisema iwapo Katiba mpya itashindwa kupatikana kwa kipindi hicho, Katiba ya sasa itaendelea kutumika na mchakato huo utaanza upya mbele ya safari.
Siku 60 alizoziongeza Rais Kikwete kwa Bunge Maalum la Katiba kupitia Tangazo la Serikali (Government Notice) Na 254 lililotolewa tarehe 1 Agosti, 2014. Tangazo hilo linatumika hadi tarehe 4 Oktoba, 2014 ambapo Katiba inayopendekezwa inategemewa kupatikana.

Hii ilikuja baada ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuanza kupiga kelele kuhusu Mchakato wa Katiba na hasa kuhusiana na muda kuingiliana na vipaumbele vingine ambapo Prof. Lipumba alinukuliwa na Gazeti la Mwananchi katika habari hii,

Lipumba: Kuna njama za kumwongezea JK muda - Kitaifa - mwananchi.co.tz
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amedai kuwa amenasa taarifa za siri za kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani.

Profesa Lipumba alisema hiyo inatokana na wasiwasi kuwa mchakato wa Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014 hivyo kutokuwa rahisi kwa uchaguzi kufanyika mwaka 2015.

Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la CUF, Profesa Lipumba alisema kuwa Serikali inataka kuongezewa muda wa kukaa madarakani kwa miaka miwili ikimaanisha kuwa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete itakaa madarakani hadi mwaka 2017.

Hata hivyo, madai hayo ya Profesa Lipumba yamepingwa vikali na Serikali na viongozi wake watatu waandamizi ambapo walijibu walipoulizwa kwa maandishi na mwandishi wetu mjini Dodoma wanakohudhuria kikao cha Bunge.
Kilichosema na Mwenyekiti wa Jukwaa la Demokrasia (TCD), Mh. John Cheyo kimantiki ndiyo hicho hicho kilichosemwa na Prof. Lipumba.

Mh. John Cheyo amekaririwa akisema,

“Pamoja na kazi ya msingi inayofanywa na Bunge Maalum la Katiba, mchakato wa Katiba unaoendelea sasa hauwezi kutupa Katiba itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kuwa muda hautoshi kukamilisha mchakato na kufanya mabadiliko yatakayohitajika ya Sheria, Kanuni na Taasisi mbalimbali zitakazohitajika”, alisema Mhe. Cheyo.
Mhe. Cheyo aliendelea kwa kusema kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mwisho wa mchakato ni kura ya maoni itakayofanyika mwezi Aprili 2015.

“Kama itabidi kura irudiwe kwa mujibu wa Sheria iliyotajwa, kura itarudiwa mwezi Juni au Julai 2015, muda ambao Bunge la Jamhuri ya Muungano linatakiwa livunjwe kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015 na ili Katiba Mpya itumike katika uchaguzi Mkuu utakaokuja, itabidi uhai wa Bunge na Serikali uongezwe zaidi ya 2015, jambo ambalo hatuliungi mkono”, alisisitiza Mhe. Cheyo.
Kwa mtu mwenye upeo mpana ataelewa kuwa kinachofanyika kwenye makubaliano ni kile kile kilichosemwa huko nyuma na Serikali.

Serikali inaongozwa kwa mujibu wa katiba na katika kuongoza, serikali inaangalia kwanza vipaumbele vyake kisheria katika kufikia malengo ya Kitaifa.

Ieleweke kuwa, Rais Kikwete ana nguvu kisheria kuongeza muda wa Bunge Maalum lakini kusogeza mbele vipaumbele vya kisiasa kama Uchaguzi Mkuu vingeiondolea serikali yake uhalali wa kisiasa, hasa ikichukuliwa kuwa Taifa letu kwa sasa lina Katiba ya 1977 na linaendeshwa kwa Katiba hiyo.

CCM iliona kuongeza muda kwa Bunge Maalum na kusogeza mbele Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi wa Rais na Wabunge ni kuwapa wapinzani mpini wa kisiasa hasa ikichukuliwa kuwa kuna vyama vya siasa huwa vinatafuta umaarufu kwa njia ya Maandamano. Kusogeza mbele Uchaguzi Mkuu ni kuvipa vyama hiyo ajenda ya kuingia mitaani kutafuta umaarufu kwa njia ya maandamano.

CCM na Serikali yake wameliona hilo, na kwa maana hiyo, mlango wa kutafuta umaarufu kwa baadhi ya vyama vya upinzani imeufunga wakati huo huo kupitia serikali yake.

Ieleweke kuwa, mchakato wa Katiba unaendelea mpaka tarehe 4/10/2014, Katiba mpya itatungwa na kupendekezwa kwa wananchi. Muda muafaka ukifika, wananchi wataipigia kura kuikubali au kuikataa kama sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyosema.

Serikali endelevu kwa siasa za Tanzania ni ile inayosikiliza sauti ya chama kilichoiunda na kutoa maamuzi katika msingi wa Sera na Ilani ya chama hicho.

CCM na Serikali yake vinaongoza, Vyama vya upinzani vinafuata kwa nyuma.

CCM ilithubutu, ikaweza na sasa inasonga mbele.

Mengine tunawaachia wataalam wa probability and political analyst!
 
Ndugu,
Naomba ieleweke kuwa CCM na serikali yake imepata kile ambacho ilikuwa inakitaka kwa njia ya mapatano, au mwafaka, kwa maana ya consensus kwa faida ya mstakabali wa Taifa, wakati huo huo vyama vya upinzani na hasa vile vianvyojiita UKAWA vimepata kile ambacho vimekuwa vikitafuta kwa njia ya maelewano kwa maana ya compromise.

In other words, CCM ilishajua Kwamba yenyewe Ndio tatizo na ni kikwazo cha kupatikana kwa katiba mpya, ilichokuwa inatafuta (CCM) ni mlango wa kutokea.

Historia ya miaka zaidi ya 20 sasa inaweka Suala Hilo wazi yani - mikakati ya CCM kulinyima taifa katiba ya wananchi (rejea kazi ya tume ya nyalali pamoja na mapendekezo yake ambayo Kama jadi ya CCM, yalitupwa kwenye jalala Kama alivyojadili Nguruvi3.

Katika muktadha wa sasa, CCM ilikuwa Ikitafuta a way to share the blame and burden na ukawa ili chama kisionekane Kama Ndio kikwazo Wakati hivyo ndivyo historia itakavyokuja andika.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya maelewano (compromise) na mapatano au mwafaka (Consensus).

Inakuwaje Leo Ndio CCM inakubali hata kutaja maneno haya Wakati Huko nyuma lugha na matamshi yenu na kina nape, kinana, Wassira, Sitta, lukuvi etc yalikuwa wazi na bayana Kwamba katiba inayotungwa ni I'm yenye kuangalia maslahi ya CCM kwanza? Iweje Leo muanze kutumia lugha na maneno ya wale mliowabeza kwa mfano kina jaji warioba, professor Lumumba n.k? Hawa na Wengine wengi walihimiza sana huu ya umuhimu wa maridhiano huku nyinyi kwenye uongozi wa chama mkukwepa maneno haya Kama ukoma.

Katika maelewano au compromise, pande zinazokinzana hatimaye zinakubali kwa shingo upande ili kutokukwamisha maamuzi (UKAWA).
CCM Ndio iliyokwamisha mchakato wa katiba. Ukawa walichofanya ni kupigania Sheria ya mabadiliko ya katiba isimamiwe na isichakachuliwe na CCM na vikaragosi wao bungeni; ukawa ilichofanya ni kusimamia upande wa wananchi kwa Mujibu wa maoni waliyopendekeza wananchi, of which mmekuwa mkisema Kwamba ni batili na ya kutungwa na tune ya warioba; nikuulize - Kama maoni haya ni ya kutunga, kwanini mnaweweseka na ukawa, kwani msiendelee na katiba yenu huku mkizunguka nchi nzima kueleZea wananchi juu ya dhambi ya tume ya warioba kutungia wananchi maoni, na ukawa kuendeleza dhambi hiyo?

Pande zote zinapata kidogo na kupoteza kidogo, na kila upande huwa na mkakati wake wa kupata zaidi katika duru ya pili. Kwa hivyo, maelewano kamwe hayawezi kuwa kwa moyo safi. Maelewano au compromise, yanazaa uamuzi legelege.

Nikuulize: CCM sasa imeamua kupoteza Kidogo kipi? Na kwa mtazamo wako, ukawa wamepoteza Kidogo kipi?

Kikao chao cha kwanza na Rais Kikwete kilionyesha tofauti zao mpaka Rais Kikwete akawaambia wakajipange upya ili warudi na hoja zinazoeleweka.

Watanzania wengi walichoelewa ni Kwamba rais aliondoka na hoja Kwamba Hana mamlaka ya kulivunja bunge, hivyo ukawa Waende kulifanyia Hilo kazi. Au wewe ulielewa vipi? Na je, rais Hana mamlaka ya kufanya maamuzi Wakati wa dharura? Kinachoendelea bungeni hakitazaa katiba ya wananchi, na kuendelea kutafuna hela za walipa kodi Wakati CCM ikifahamu Hilo ni Jambo ambalo rais anaweza kulifanyia maamuzi Katika Hali ya dharura. Isitoshe, Huko nyuma mliulizwa, je rais alihairisha BLK kupisha bunge la bajeti kwa Sheria Ipi? Hamkujibu.

Mapatano au consensus (CCM + Serikali), kwa upande mwingine, ni maafikiano yanayofikiwa baada ya mjadala mrefu, kila pande akilenga kuthibitisha hoja yake na kwa njia hii kusadikisha wenzake kwamba hoja yake ni sahihi. Baada ya kufikia uamuzi wa mwafaka, kila mmoja anatoka akiwa ameridhika na amefurahi. Hiki ndicho kilichofanyika baina ya CCM na Serikali.
Awali mtazamo wa CCM ulikuwa Kwamba katiba ya wananchi haipatikani nje ya ukumbi wa bunge maalum la katiba, what changed?

Kuna baadhi ya Watanzania ninaamini wana tabia ya kusahau sahau!.
Hakuna upande wenye kusahau mambo Kama CCM. Chama kiliingia kwa Kishindo bungeni na kuichafua tume ya warioba huku ikiivua uhalali wake Mbele ya umma. Huu Ndio ukawa mwanzo wa mchakato wote kuharibika. Tuendelee...

Hakuna suala jipya lililosemwa na kukubaliwa na Viongozi Wakuu wa Vyama vya siasa vyenye Wabunge vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD). Yaliyosema ni yale yale ambayo Serikali kupitia kwa Rais Kikwete iliyasema na serikali imekuwa ikisisitiza kila mara.
Hakuna jipya la kusemwa zaidi ya msimamo ule ule wa kutetea rasimu iliyotokana na wananchi. Wangekuja na Jambo jipya, Hilo lingekuwa ni tatizo.

Ikumbukwe kuwa, Rais Kikwete wakati akihutubia maelfu ya wafanyakazi katika siku kuu ya Mei Mosi ambazo Kitaifa zilifanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam alikaririwa akisema,
Siku 60 alizoziongeza Rais Kikwete kwa Bunge Maalum la Katiba kupitia Tangazo la Serikali (Government Notice) Na 254 lililotolewa tarehe 1 Agosti, 2014. Tangazo hilo linatumika hadi tarehe 4 Oktoba, 2014 ambapo Katiba inayopendekezwa inategemewa kupatikana.

Pia alisema Kwamba iwapo katiba mpya haitapatikana ndani ya kipindi hicho, katiba ya sasa/iliyopo (1977), itaendelea kutumika na Ndio hiyo hiyo itakayotumika kwenye uchaguzi mwakani. Hakusema Kwamba itafanyiwa marekebisho Kama vile tume huru ya uchaguzi, mgombea binafsi, na matokeo ya urais kupingwa Mahakamani.

All that said and done, it's on the records Kwamba rais alishasema Kwamba serikali Tatu hazitatokea akiwa madarakani, na hili likachochea mgogoro uliopo sasa. Wenye Tabia ya kujisahau sahau ni Nani Hapa Katika ya CCM na ukawa?

Hii ilikuja baada ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuanza kupiga kelele kuhusu Mchakato wa Katiba na hasa kuhusiana na muda kuingiliana na vipaumbele vingine ambapo Prof. Lipumba alinukuliwa na Gazeti la Mwananchi katika habari hii,
Hizi hazikuwa Kelele Bali hoja za msingi ambazo kwa mtu yet ore mwenye akili timamu aliona Ukweli upo wapi. Isitoshe, ni kumtusi rais Kikwete Unaposema Kwamba Kikwete reacted kutokana na Kelele badala ya hoja.

Kilichosema na Mwenyekiti wa Jukwaa la Demokrasia (TCD), Mh. John Cheyo kimantiki ndiyo hicho hicho kilichosemwa na Prof. Lipumba.

Mh. John Cheyo amekaririwa akisema,

Kwa mtu mwenye upeo mpana ataelewa kuwa kinachofanyika kwenye makubaliano ni kile kile kilichosemwa huko nyuma na Serikali.

This is just spinning politics. Let it remain as commentary.

Serikali inaongozwa kwa mujibu wa katiba na katika kuongoza, serikali inaangalia kwanza vipaumbele vyake kisheria katika kufikia malengo ya Kitaifa.
Ni kweli Kabisa, serikali inaongozwa kwa Mujibu wa katiba. MwanaDiwani,

Kuna tofauti kubwa baina ya:
1. A desire for a constitutional gvnt and a fair administration that governs according to and within the law.

2.a desire for the laws themselves to be fair, equitable and just.

Serikali ya CCM had consistently breached two, hasa the later/second.

A constitutional government doesn't simply mean that the government follows the letter of the constitution and the law. Prerequisite of a constitutional government is that the constitution and the laws themselves are JUST, FAIR and EQUITABLE, hence LEGITIMATE. If the latter wasn't a necessary condition, then apartheid gvnt in South Africa would have been one of the best constitutional governments in the world. During apartheid, law was observed scrupulously, by both rulers and the ruled. However, in that context is would have been silly if not ridiculous to suggest to Mandela and the ANC in general Kwamba they should strictly observe, follow and respect the law. If freedom fighters within the ANC were to do so, they would never be able to prosecute their struggle for their right to self determination, which was denied by the constitutional and legal order of the time. That's where we stand as TANGANYIKA!!!!!

Ieleweke kuwa, Rais Kikwete ana nguvu kisheria kuongeza muda wa Bunge Maalum lakini kusogeza mbele vipaumbele vya kisiasa kama Uchaguzi Mkuu vingeiondolea serikali yake uhalali wa kisiasa, hasa ikichukuliwa kuwa Taifa letu kwa sasa lina Katiba ya 1977 na linaendeshwa kwa Katiba hiyo.

CCM iliona kuongeza muda kwa Bunge Maalum na kusogeza mbele Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi wa Rais na Wabunge ni kuwapa wapinzani mpini wa kisiasa hasa ikichukuliwa kuwa kuna vyama vya siasa huwa vinatafuta umaarufu kwa njia ya Maandamano. Kusogeza mbele Uchaguzi Mkuu ni kuvipa vyama hiyo ajenda ya kuingia mitaani kutafuta umaarufu kwa njia ya maandamano.
Mna jichanganya sana. Rais Kikwete anabanwa na Sheria au itikadi ya chama kufanya uamuzi Mgumu?

CCM na Serikali yake wameliona hilo, na kwa maana hiyo, mlango wa kutafuta umaarufu kwa baadhi ya vyama vya upinzani imeufunga wakati huo huo kupitia serikali yake.

Kwahiyo maridhiano baina ya JK na ukawa yalilenga kuua umaarufu wa ukawa? Mbona ni Kama kutwanga uji kwenye kinu? Nini kilicho maarufu zaidi kwa wananchi baina ya harakati za kutafuta katiba Yao na ukawa?

Isitoshe, lugha yako Wakati wote imekuwa ni ya kutafuta umaarufu kichama zaidi kuliko kutetea maslahi ya watanzania; hapo chini hili lipo wazi Kama tutakavyoona.

Ieleweke kuwa, mchakato wa Katiba unaendelea mpaka tarehe 4/10/2014, Katiba mpya itatungwa na kupendekezwa kwa wananchi. Muda muafaka ukifika, wananchi wataipigia kura kuikubali au kuikataa kama sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyosema.
Ni maneno haya pia professor Mwandosya ameyasema bungeni Leo asuBuhi akichangia mjadala Kwamba katiba mpya itapatikana sana na sio 2016 or 2017. Are you guys serious really?

Serikali endelevu kwa siasa za Tanzania ni ile inayosikiliza sauti ya chama kilichoiunda na kutoa maamuzi katika msingi wa Sera na Ilani ya chama hicho.
Kama nilivyojadili hapo juu, upo kutetea zaidi umaarufu wa chama kuliko maslahi ya wananchi bila ya kujali itikadi zao. Tangia lini serikali ikadumu kwa kusikiliza zaidi sauti ya chama tawala kuliko wananchi?

CCM na Serikali yake vinaongoza, Vyama vya upinzani vinafuata kwa nyuma.
Unfortunately not any more. Kwa miaka karibia minne sasa, bungeni na kwenye majukwaa ya siasa, CCM inatumia muda mwingi zaidi kujadili chadema (now ukawa) kuliko kujadili matatizo ya wananchi na njia ya kuyatatua.

CCM ilithubutu, ikaweza na sasa inasonga mbele.
Inatakiwa tujiulize Kama taifa - je, kupitia mchakato wa katiba mpya tumethubutu, tumewezana tumesonga Mbele?

Kama tumeshindwa,ni kwa sababu gani?

Je tunajikwamuaje?

MengFONT]
[/QUOTE]

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Tunaendelea na sehemu ya III

JK ATAFUTA MALNGO WA KUTOKEA

AMEKWEPA LAWAMA LEO, LEGACY YAKE HAIKWEPEKI.

Tumemalizia bandiko hapo juu kwa kusema Legacy ya JK ni kushindwa kuliongoza taifa kuandika katiba.
Ni legacy iliyovunja heshima yetu kama 'viongozi' wa ukanda na Afrika''

Baada ya kubaini lawama zinamwendea kwa kulivuruga bunge, kuwadhalilisha tume JK alitafuta mkakati.
Mkakati wa kuvunja bunge kiaina bila kuonekana kalivunja.

Mbinu ziligonga mwamba na hakuwa na jingine isipokuwa kutimiza ahadi yake''S3 hadi atakapoondoka mwakani''

Kauli hii maana yake ni kumwachia mrithi wake suala la katiba.
Huo si uongozi, JK hakuchaguliwa kuacha viporo, alichaguliwa kufanya kazi.
Kitendo cha kusema hadi aondoke ni udhaifu wa hali ya juu kama tujuavyo.

MAHALI PA KUTOKEA

JK alibaini UKAWA hawarudi licha ya mbinu zote, katiba ini ya CCM, haina uhalali wa kisiasa na haitakubalika mbele ya wananchi.

Lawama za kuvuruga bunge zikamwelemea kila bunge la CCM lilipokaa.
Upinzani ukazuka ndani ya chama chake, na viongozi kama mwansheria wa

JK akatafuta njia rahisi ambayo ni kuwatumia wapinzani kujiondoa na kusoha mikono.

Kabla ya hapo, JK alimtuma mwanasheria mkuu aeleze ugumu wa kisheria kwa Rais kuvunja bunge.
Tunajua bunge hilo liliahirishwa kupisha bunge la bajeti chini ya mwanasheria huyo huyo, hatukuona ugumu mwingine wa kuahirisha kupisha majadiliano.

Werma alipewa kazi kubwa mbili
1. Kwanza kuwatisha UKAWA, bunge halivunjwi ili warudi, ikashindikana
2. Kutengeneza mazingira ya JK kumaliza mchakato akiwa ameosha mikonoingawa inanuka ubaya

JK akawakwepa UKAWA na kutumia TCD mabayo anajua ina mamluki wake.
Tulieleza hapa jamvini bila probability kuwa atakayesoma tamko la pamoja ni kiongozi wa upinzani ili kuwatupia mzigo,limetokea

Kwa bahati mbaya UKAWA kama kawaida yao hawakuona hatari ya jambo hilo.

Nao wakakubali kuwa pamoja na akina Mrema, Cheyo, na vibaraka wengine.
Hao wakawavuruga kwani walipokwenda kwa JK, wao walikuwa CCM na CCM original wakiwa kimya.

TAMKO
Tamako la kuahirisha mchakato limeacha maswali mengi

Kitendo cha bunge hilo kumaliza kazi Oktoba 4 kilimaanisha kuwapa muda wa kuendelea kuwalaghai wazanzibar kwa siku za usoni.

Mfano, kamati namba 5 eti imependekeza baraza la usalama la taifa iwe na Rais wa JMT na makamu wawili kutoka ZNZ na Rais wa ZNZ ili kuteua wakuu wa vyombo vya usalama.

Hapa kamati inatoa pipi kwakuwaweleza wznz madai yao ya kuwa na IGP na CDF yatafanikiwa na yamefikiriwa.
Kamati namba tano inafahamu uwezo wa wznz na hilo kwao linaweza kuwa mafanikio makubwa.

Kadri siku zinavyoendelea CCM itatumia nafasi hiyo kuwaonyesha wznz kuwa yapo mazuri yaliyoandaliwa kwa ajili yao ili siku za baadaye wabadilike. Ndivyo walivyoweza kumbadilisha Hamada wa CUF aliyeandamana kudai S3 na sasa ni S2 damu.

Hili ni kosa la UKAWA, kilichopaswa kufanywa ni kuahirisha mchakato kabisa na si kukubali CCM waendele kufuja pesa za wala hoi kwa kutengeneza mazingira ya siku za baadaye. UKAWA wajilaumu kwa kosa hili.

Lakini pia mchakao umeahirishwa, kwa maneno mengine utaendelea.
Hatujui utaendelea kuanzia wapi, pale UKAWA walipotka au hapo CCM walipoishia.

JK ASHINDWA KUKIRI MCHAKATO UMEFIA MIKONONI

JK anasema mchakato umeahirishwa hadi uchaguzi uatakpomalizika.
Hili lina maana Rais atakuwa mwingine.Haiwezekani Rais mwingine aendelee alipoachia JK.

Hivyo kusema JK ameahirisha mchakato haina maana, alichokataa kusema, ameshindwa na kufunga mchakato na hio ndio ukweli.

JK AMTUPA SITTA CHINI YA BUS

Kama ilivyokawaida ya JK kucheza beki na fowadi, safari hii amemtumia sana Sitta katika kuhakikisha anafanikiwa na mchakato.

Sitta kwa kutokuwa na kumb kumbu za kilichomkuata siku za nyuma naye kaingia kichwa kichwa

JK aliwahi kumtosa Sitta kwa kile kinachoitwa kuvua gamba.
Mwisho wa siku magamba yakamrudi na kumuondoa katika kiti cha Uspika. Safari hii ametumika tena na sasa kuachwa na aibu.

Sitta ametumia mbinu zote akidhani atafanikiwa kama ilivyokuwa wakati wa kufungua bunge.
Imefika mahali anawatumia viongozi wa dini, kuita wafugaji n.k. ili kuungwa mkono

Wakati akaitenda hayo, JK alikuwa na mwanasheria mkuu wakipanga namna ya kutoka salama.
Sitta akajikuta anakuwa kituko, na kituko kikubwa alichokifanya ni kuwatumia viongozi wa dini.

Tulionya katika mabandiko, kitendo cha kuwapa nguvu viongozi wa dini ni cha hatari na sitta analipeleka taifa pabaya.
Rejea kurasa chache nyuma ushahidi upo na wala si probability.

Ushahidi wetu umeanza kuonekana baada ya viongozi wa dini sasa kuwa na nguvu za kuita waumini wao kupanga mikakati.

Tunajua suala la kadhi lilivyo hadi sasa. Hii ni baada ya viongozi hao kupewa nguvu na Sitta na sasa wanazitumia kikamilifu wakijua nchi inawasikiliza.

Huu ndio mchezo mchafu anaotuachia Sitta. Yote tunayoeleza tuliyadili siku za nyuma kila kimoja na bandiko lake.

Itaendelea...
 
Sehemu ya IV

SITTA AMALIZA SAFARI YA KISIASA

KATUMIWA NA JK MARA MBILI, ZOTE AKIMTUPA CHINI YA BUS

BEGI LA HESHIMA SASA LINABEBWA NA CHEKECHEA

Wakati Sitta akiendelea na vituko Dodoma, tuliwahi kuandika nyuzi kwa kirefu sana tukimwelezea yeye ni nani na anasifa gani.

Hilo tulilifanya kabla ya uchaguzi wake, na wala hatukusubiri probability.

Leo amebaki akijadili mada za highschool pale Dodoma uso ukiwa umesajiwijika na kujawa na soni kama si aibu.

Kazi ya kutumbukiza mambo ya dini sasa inamgeukia, na viongozi aliowapa madaraka ya kuzungumza wanageukana na kuanza mijadala hatarishi ya kidini.

Upande mmoja ukitaka mahakama ya kadhi mwingine ukipinga.
Hisia zote zinazotokana na mijadala hiyo, mbegu inayochipua imepandwa na Sitta.

Sitta amefikia mwisho wa hatma yake kisiasa. Hataweza kuliongoza taifa hili tena.

Kushindwa kwa bunge ni dalili ya kutokuwa na uwezo wa kuleta taifa pamoja, maridhiano au makubaliano.

Ubabe alioutumia wakati wa kufungua bunge kwa kumwita JK awadhalilishe wazee sasa unamgharimu.

JK keshaosha mikono kwa kumtumia Memosa Cheyo. Suala zima la katiba kuvurugika sasa lipo mabegani mwa Samwel Sitta.

Licha ya uzito wake, Sitta anabeba uzito mwingine wa kutumbukiza mambo ya kidini kwa kuwapa viongozi wa dini nguvu za kisiasa.

Kwa ufupi ni kuwa kama JK alipanga kumtosa basi amefanikiwa.Sitta ametupiwa kamba na 'kujinyonga' kisiasa.

Mahasimu wake sasa wana la kusema, CCM yake imemtupa nje, na wananchi hawataki kusikia tena jina hilo katika mambo ya kitaifa.

Uwezekano wa Sitta kuwa hata mbunge sasa ni kama sifuri. Anachokitegemea ni uelewa finyu wa watu wa Urambo.

Nje ya Urambo Sitta amebeba zigo la ufujaji wa pesa, ubabe usio na maana na kushindwa kuiongoza taifa.

Sitta lazima ajilaumu mwenye, kamba na kitanzi cha kisiasa amefunga na kutumbukiza shingoni.

Wakati Sitta akidhani ni kamba ya mgomba, JK alikuwa anacheza karata zake vema, mwisho wa siku Sitta kakamilisha safari yake kisiasa. Huu ndio mwanzo wa mwisho wa Sitta

WABUNGE WA CCM NAO WATUPWA CHINI YA BUSA

Baada ya kufungwa matambara ya vinywani wabunge wa CCM wana la kujibu mbele ya wananchi.S

Swali muhimu la kuwauliza ni uhalali wa kuchezea fedha za walipa kodi kwa mieizi miwili

Na swali lingine litahojii misimamo yao kama ni ya chama au ilikuwa ya wananchi.

Wabunge waliosema jambo, wana nafasi nzuri ya kutetea misimamo yao kuliko 'bubu' wa Nape.

Kwa hili la katiba , wabunge wengi watakwenda na maji.

Itaendelea sehemua ya IV
 
Mfano, kamati namba 5 eti imependekeza baraza la usalama la taifa iwe na Rais wa JMT na makamu wawili kutoka ZNZ na Rais wa ZNZ ili kuteua wakuu wa vyombo vya usalama.

Hapa kamati inatoa pipi kwakuwaweleza wznz madai yao ya kuwa na IGP na CDF yatafanikiwa na yamefikiriwa.
Kamati namba tano inafahamu uwezo wa wznz na hilo kwao linaweza kuwa mafanikio makubwa.

Kadri siku zinavyoendelea CCM itatumia nafasi hiyo kuwaonyesha wznz kuwa yapo mazuri yaliyoandaliwa kwa ajili yao ili siku za baadaye wabadilike. Ndivyo walivyoweza kumbadilisha Hamada wa CUF aliyeandamana kudai S3 na sasa ni S2 damu.

...
Kwa sababu kutakuwa na serikali mbili, waziri wa fedha wa Jamhuri ya muungano bado anashughulikia mambo fulani ambayo yataathiri Tanzania bara bila kuathiri Zanzibar, kama vile bajeti za wizara na Taasisi nyingine ambazo mambo yake ni ya Tanzania bara tu.

Ili ku-balance, makamu wa Rais wa Zanzibar ataingizwa kwenye baraza la usalama. Kutokana na katiba ya Zanzibar ya 2010, serikali yao ni ya mseto, hivyo taasisi ya makamu wa Rais inajumuisha vyama viwili vikuu vyenye wabunge wengi na huwezi kumfanya Balozi Seif pekee au Maalim pekee awe mjumbe (kwa mfano tu).

Draft ya warioba ili-balance kwa kuwapa marais wawili wa Tanganyika na Zanzibar ujumbe na wajumbe wengine ni wa Federal government. Ukiondoa Federal government, Waziri wa Fedha unam-balance na makamu wa Zanzibar.

Ungeelezea hivyo ingekuwa ni jambo bora kuliko kupotosha. Na pia ungeipongeza kamati namba 5 kwa kukubali uwepo wa baraza la usalama kama lilivyopendekezwa na Tume ya mabadiliko ya katiba. Kwa sababu halikuwepo hilo kabla, na sidhani kama wananchi walipendekeza hilo, bali ni wataalam na wamesikilizwa.

Kuhusu kuahirishwa kwa Bunge la katiba ili kupisha general elections, I told you before ...
Katiba hii ni ya 2018, na ni UKAWA waliotaka sheria za uchaguzi zibadilishwe na Bunge la Jamhuri, halafu baadae waendelee na mambo ya katiba.

Ni jambo zuri kwa sababu tutaona legitimacy, ya kutunga katiba ita- shift wapi. baada ya uchaguzi, unless kama mnaogopa hilo.
 
In other words, CCM ilishajua Kwamba yenyewe Ndio tatizo na ni kikwazo cha kupatikana kwa katiba mpya, ilichokuwa inatafuta (CCM) ni mlango wa kutokea.
Ndugu Mchambuzi,

Kama ulikuwa unadhani CCM ilikuwa inatafuta mlango wa kutokea; unadhani kwa sasa imetoka baada ya tamko la TCD?

Tatizo lako ninaloliona ni kuiweka CCM katika mantiki ya siasa za uanaharakati wakati CCM ni chama kinachobeba majukumu na mwelekeo wa sasa wa kitaifa kama chama tawala.

CCM siyo chama cha upinzani na kwa maana hiyo, haifanyi siasa za majaribio ndani ya political theories.

Wananchi nchini wanaishi na kufanya kazi ndani ya Sera za CCM zilizoainishwa kwenye Ilani yake ya Uchaguzi. CCM ni chama tawala, na kwa maana hiyo, hakina muda wa kufanya majaribio ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika maisha ya wananchi.

Maamuzi ya Serikali ya CCM hayawezi yakafanywa katika msingi wa mchezo wa kamari. We can't afford to solve a real problem with an unrealistic solution.

Kama CCM iliyoaminiwa na kukabidhiwa madaraka na wananchi kwa mtazamo wako imekuwa ni tatizo, basi acha iendelee kuwa ni tatizo kwa sababu hata waharifu wanaweza wakasema serikali ni tatizo kwa sababu tu imeweza kuwaziba na kuwadhibiti kisheria ili wasifanye uharifu wao!.

Kama maamuzi ya CCM ya kuanzisha Mchakato wa Katiba mpya kupitia serikali yake na kuusimamia ipasavyo ni tatizo, basi acha iendelee kuwa ni tatizo, hasa ikichukuliwa kuwa, upendo, amani, umoja na mshikamano kama taifa uko mikononi mwa CCM kama chama tawala kupitia serikali yake.

Historia ya miaka zaidi ya 20 sasa inaweka Suala Hilo wazi yani - mikakati ya CCM kulinyima taifa katiba ya wananchi (rejea kazi ya tume ya nyalali pamoja na mapendekezo yake ambayo Kama jadi ya CCM, yalitupwa kwenye jalala Kama alivyojadili Nguruvi3.
Kwanza, Tatizo la watu kama wewe mnadhani kuwa mapendekezo/maoni/ushauri ni lazima vifuatwe. Nani alisema mapendekezo lazima yakubaliwe na kufuatwa?. Mapendekezo ni mapendekezo tu, yanaweza kufuatwa au kutupwa kapuni.

Pili, Kwa kuonyesha kuwa serikali ilikuwa inakubaliana na mapendekezo mbali mbali ya tume zilizoundwa, ndiyo maana katiba yetu ya mwaka 1977 imefanyiwa marekebisho mara 14.

Ni mawazo na fikra hizi hizi zinazopiga kelele kila siku na kusema Rasimu ya pili ya Katiba isifanyiwe marekebisho ndani ya Bunge Maalum kwa sababu ni maoni ya wananchi ''wengi''. Kwa maana kuwa wachache hawana nafasi ya kusikilizwa ndani ya Rasimu ya Katiba katika mitazamo tofauti ya jambo fulani ambalo wengi wametoa mapendekezo tofauti. Kwa lugha nyingine, Rasimu ya Katiba inahusu mawazo ya wengi pekee ambao mawazo yao yanafanana na siyo pia wachache wenye mawazo yanayofanana hata kama yana mantiki katika ujenzi wa Taifa.

Katika muktadha wa sasa, CCM ilikuwa Ikitafuta a way to share the blame and burden na ukawa ili chama kisionekane Kama Ndio kikwazo Wakati hivyo ndivyo historia itakavyokuja andika.
CCM inapimwa katika sanduku la kura na siyo katika mawazo na fikra za mtu mmoja au kikundi cha watu. Blame ya CCM inajulikana kwenye matokeo ya chaguzi mbali mbali na siyo kwenye fikra na mtazamo wa mtu mmoja.

CCM ndiyo iliyoanzisha Mchakato wa Katiba kupitia serikali yake na ndiyo CCM hiyo hiyo inayosimamia Mchakato wa Katiba kupitia Serikali yake. Hii dhana ya kusema CCM inatafuta a way to share blame ni fikra na mitazamo ya kitoto.

Kwa hiyo hicho kikundi kinachojiita UKAWA hawakufahamu kuwa CCM ilikuwa inatafuta a way to share blame? Are they stupid/foolish/ignorant?
Inakuwaje Leo Ndio CCM inakubali hata kutaja maneno haya Wakati Huko nyuma lugha na matamshi yenu na kina nape, kinana, Wassira, Sitta, lukuvi etc yalikuwa wazi na bayana Kwamba katiba inayotungwa ni I'm yenye kuangalia maslahi ya CCM kwanza? Iweje Leo muanze kutumia lugha na maneno ya wale mliowabeza kwa mfano kina jaji warioba, professor Lumumba n.k? Hawa na Wengine wengi walihimiza sana huu ya umuhimu wa maridhiano huku nyinyi kwenye uongozi wa chama mkukwepa maneno haya Kama ukoma.
CCM kila siku inasema, Maridhiano kuhusu Mchakato wa Katiba katika stage ya tatu ambayo ni Bunge Maalum yanapatikana ndani ya Bunge na siyo barabarani.

Rais Kikwete hakukutana na TCD ili kutafuta Maridhiano bali alikutana na TCD ili kutafuta maelewano(compromise) au mwafaka(consensus). Kilichotokea ni UKAWA kupata compromise na huku Serikali ikiondoka na consensus.

Nadhani unaelewa maana na tofauti ya maelewano (compromise) na mwafaka (consensus).

Baada ya UKAWA kugundua walichokubali ni maelewano (compromise), ndiyo maana kwa sasa wameanza kupiga kelele tena wakitaka eti Bunge lisitishwe mara moja. Waswahili wanasema, ''imetoka''. Mbaya kabisa kwa upande wao, kwa sasa wamejifunga kitanzi huku wakisema, Rais ajaye lazima auendeleze Mchakato wa Katiba kuanzia pale ulipoishia. Wanadai, hii lazima ifanyike kisheria. GOOD.

Ieleweke kuwa compromise huwa inazaa maamuzi legelege.
CCM Ndio iliyokwamisha mchakato wa katiba. Ukawa walichofanya ni kupigania Sheria ya mabadiliko ya katiba isimamiwe na isichakachuliwe na CCM na vikaragosi wao bungeni; ukawa ilichofanya ni kusimamia upande wa wananchi kwa Mujibu wa maoni waliyopendekeza wananchi, of which mmekuwa mkisema Kwamba ni batili na ya kutungwa na tune ya warioba; nikuulize - Kama maoni haya ni ya kutunga, kwanini mnaweweseka na ukawa, kwani msiendelee na katiba yenu huku mkizunguka nchi nzima kueleZea wananchi juu ya dhambi ya tume ya warioba kutungia wananchi maoni, na ukawa kuendeleza dhambi hiyo?
Hakuna hotuba au sehemu ya hotuba ambayo CCM imesema takwimu za tume ya Mzee Warioba niza kutunga. CCM inachokataa ni hoja za baadhi ya wajumbe wa Tume ya Mzee Warioba kuhusu mapendekezo ya Muundo wa Serikali tatu. Hoja za kusema tume imependekeza Muundo wa Serikali tatu kwa sababu wananchi ''wengi'' walipendekeza ndiyo msingi wa CCM kutokubali hoja hizo.

Ikumbukwe kuwa, mpaka tunapoandika hizi hoja, Mchakato wa Katiba kupitia Rasimu ya Pili ya Katiba unaendele Bungeni. Hii dhana ya kusema Mchakato wa Katiba umekwama ni kujifariji kihoja kwa kuukimbia ukweli.

Mchakato wa Katiba ni zoezi endelevu na kwa maana hiyo, utapisha Chaguzi Kuu kwa vile chaguzi Kuu siyo zoezi endelevu.

Kama kupisha chaguzi kuu ndiyo una tafsiri kukwama kwa Mchakato wa Katiba, basi endelea kutafsili hivyo hivyo wakati mchakato unaendelea.
Watanzania wengi walichoelewa ni Kwamba rais aliondoka na hoja Kwamba Hana mamlaka ya kulivunja bunge, hivyo ukawa Waende kulifanyia Hilo kazi. Au wewe ulielewa vipi?
Nope, TCD waliingia kwenye meza ya majadiliano bila kuwa na ajenda zinazoeleweka kama taasisi ya kisiasa. Kila mmoja alikuwa na ajenda zake wakati suala lilihusu pande mbili ambazo ni Serikali na TCD. Suala halikuhusu mmoja mmoja au kila chama. Kutokana na hilo, Rais Kikwete aliwaambia wakajipange tena kama TCD na warudi mezani na ajenda zinazoeleweka ambazo ziko katika kundi moja linalojengwa na TCD.
Na je, rais Hana mamlaka ya kufanya maamuzi Wakati wa dharura? Kinachoendelea bungeni hakitazaa katiba ya wananchi, na kuendelea kutafuna hela za walipa kodi Wakati CCM ikifahamu Hilo ni Jambo ambalo rais anaweza kulifanyia maamuzi Katika Hali ya dharura.
Rais anafanya kazi zake kisheria. Hata kama kungekuwa na sehemu katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inampa Rais uwezo wa kusitisha bunge wakati wa dharura, Dharura ipi iliyopo unayoisema mpaka Rais alisitishe bunge ambalo linafanya kazi zake kisheria?

Mchakato wa Katiba ni gharama. Kama kazi ya kutunga Katiba kupitia bunge ambalo lipo kisheria ni kutafuna hela za walipa kodi, basi acha hizo pesa zitafunwe kwa sababu demokrasia ndiyo imeamua hivyo kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83.
Isitoshe, Huko nyuma mliulizwa, je rais alihairisha BLK kupisha bunge la bajeti kwa Sheria Ipi? Hamkujibu.
Rais hakuahirisha Bunge Maalum la Katiba bali Bunge Maalum la Katiba lilimaliza muda wake wa awali ambao ulikuwa ni siku 70 kama ilivyokuwa kwenye Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyoainishwa kwa Kifungu cha 28 (3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2013 kwamba "…… muda ambao Bunge Maalum litajadili Rasimu ya Katiba hautazidi siku sabini (70) kuanzia tarehe ambayo Bunge Maalum lilipoitishwa".

Baadaye Mwenyekiti wa Bunge Maalum aliliongeza siku 60 kwa kuomba ridhaa kwa Rais wa Tanzania ambaye alishauriana na Rais wa Zanzibar. Siku hizo zilianza kuhesabika tarehe 05/08/2014.

Mamlaka ya kuongeza muda yanapatikana katika kifungu cha 28 (4) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambacho kinazungumzia uwezekano wa kuongeza muda. Kinasema, "Mwenyekiti wa Bunge Maalum baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti anaweza; kwa ridhaa ya Rais baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar kuongeza muda uliotolewa chini ya Kifungu Kidogo cha (3) kwa kipindi kitakachofaa kukamilisha shughuli za Bunge Maalum".
Awali mtazamo wa CCM ulikuwa Kwamba katiba ya wananchi haipatikani nje ya ukumbi wa bunge maalum la katiba, what changed?
Kauli hiyo haijabadilika ndiyo maana mpaka sasa Bunge Maalum la Katiba linaendelea na kazi yake ndani ya bunge.
Pia alisema Kwamba iwapo katiba mpya haitapatikana ndani ya kipindi hicho, katiba ya sasa/iliyopo (1977), itaendelea kutumika na Ndio hiyo hiyo itakayotumika kwenye uchaguzi mwakani. Hakusema Kwamba itafanyiwa marekebisho Kama vile tume huru ya uchaguzi, mgombea binafsi, na matokeo ya urais kupingwa Mahakamani.
Hoja yako hapa ni nini?. Kwani Marekebisho yatafanyika kwenye Katiba mpya au Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa kutumia Katiba mpya?

Hukuwahi kuwasikia Mawaziri kabla ya Mchakato wa Katiba mpya wakisema ili kukabiliana na Chaguzi Kuu (Serikali za Mitaa, Wabunge na Rais), serikali itafanyia marekebisho katiba ya 1977.

All that said and done, it's on the records Kwamba rais alishasema Kwamba serikali Tatu hazitatokea akiwa madarakani, na hili likachochea mgogoro uliopo sasa. Wenye Tabia ya kujisahau sahau ni Nani Hapa Katika ya CCM na ukawa?
Acha kumlisha Rais Kikwete maneno.
Rais Kikwete kila mara anasema hana tatizo na maamuzi ya Bunge Maalum kama watatunga Katiba yenye Muundo wa Serikali tatu lakini anachopenda wafanye hivyo huku wakiwa na informed decision kuhusu Muungano.
Inatakiwa tujiulize Kama taifa - je, kupitia mchakato wa katiba mpya tumethubutu, tumewezana tumesonga Mbele?

Kama tumeshindwa,ni kwa sababu gani?

Sent from my iPhone using JamiiForums
Nimeishasema siyo mara moja na nitasema tena katika mantiki ya Mchakato wa Katiba mpya,

CCM ilithubutu kwa maana kuwa, kupitia Serikali yake ilianzisha Mchakato wa Katiba.

CCM iliweza kwa maana kuwa, hatua nne za Mchakato wa Katiba zinaendelea kama kawaida. Kwa sasa tuko kwenye hatua ya tatu ambayo ni Bunge Maalum.

Tunasonga mbele kwa maana kuwa kila changamoto inayojitokeza kwenye Mchakato wa Katiba, inapata majibu kwa haraka kutoka kwa wabunge, serikali na wananchi, na zoezi la linaendelea.
 
MwanaDiwani;10576407]Ndugu Mchambuzi,Kama ulikuwa unadhani CCM ilikuwa inatafuta mlango wa kutokea; unadhani kwa sasa imetoka baada ya tamko la TCD?
Yes, ndiyo maana anayeongea ni Memosa na siyo Nape au Kinana. Ndiyo maana CCM inasema ilikuwa inatafuta consensus.
Tatizo lako ninaloliona ni kuiweka CCM katika mantiki ya siasa za uanaharakati wakati CCM ni chama kinachobeba majukumu na mwelekeo wa sasa wa kitaifa kama chama tawala.

CCM siyo chama cha upinzani na kwa maana hiyo, haifanyi siasa za majaribio ndani ya political theories.
Wananchi nchini wanaishi na kufanya kazi ndani ya Sera za CCM zilizoainishwa kwenye Ilani yake ya Uchaguzi.

CCM ni chama tawala, na kwa maana hiyo, hakina muda wa kufanya majaribio ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika maisha ya wananchi
Mchakato wa katiba ulianza kwa mswada kuchanwa na kuchomwa moto kule ZNZ. Tukio lilitokea mbele ya Sitta wakati anafanya majaribio kuhusu muungano.

Kauli ya Pinda kuwa wangelijua tatizo hili wangeanza na kura ya maoni, ni ushahidi wa majaribio

Kitendo cha Kikwete kusema muungano haujadili na baadaye kukubali mswada ni kielelezo kizuri cha majaribio.

Kitendo cha Kikwete kulazimisha aongee baada ya Warioba ni ishara ya kuvizia na majaribio.

Kitendo cha kikwete kulihusisha jeshi na tuhuma za mapinduzi, jambo ambalo halijawahi kufanywa na kiongozi yoyote wa taifa hili, ni kubahatisha, kukosa sera, kukosa maono na majaribio, na hili ni la hatari sana.

Kitendo cha CCM kuwafunga mdomo wabunge pale Dodoma ni majaribio, kutojiamini na kubahatisha.
CCM ingelikuwa na uhakika na inachokifanya, singewafunga wabunge wake mdomo bali kuwaachia waeleze uhakika!

Maamuzi ya Serikali ya CCM hayawezi yakafanywa katika msingi wa mchezo wa kamari.
We can't afford to solve a real problem with an unrealistic solution. Majibu ya kamari za JK yapo hapo juu
-Maamuzi realistic ya CCM ni yapi? Kuruhusu wezi wa umma wakae wakiandika katiba ya CCM ni realistic\
-Kuruhusu rasilimali za umma zibebwe tena kwa ndege za kijeshi ndani ya nchi yetu ni realistic
-Kuruhusu ufuajaji wa rasilimali za nchi kama CAG anavyoonyesha?
-Ni kuruhusu makasinga waje kubeba pesa kwa kuficha ukweli?
Kama CCM iliyoaminiwa na kukabidhiwa madaraka na wananchi kwa mtazamo wako imekuwa ni tatizo, basi acha iendelee kuwa ni tatizo kwa sababu hata waharifu wanaweza wakasema serikali ni tatizo kwa sababu tu imeweza kuwaziba na kuwadhibiti kisheria ili wasifanye uharifu wao!.
Wahalifu wapi unaoongelea? Mbona genge la wahaifu lipo CCM na halijachukuliwa hatua kama wezi wa kuku?Kuna mhalifu gani mkubwa kuliko Escrow, Meremeta, Richmond n.k. Au tunaelewa uhalifu kwa namna tofauti mkuu

Kama maamuzi ya CCM ya kuanzisha Mchakato wa Katiba mpya kupitia serikali yake na kuusimamia ipasavyo ni tatizo, basi acha iendelee kuwa ni tatizo, hasa ikichukuliwa kuwa, upendo, amani, umoja na mshikamano kama taifa uko mikononi mwa CCM kama chama tawala kupitia serikali yake
Kunazisha mchakato si uamuzi wa CCM na hata wao hawakujua hilo. Tueleze kikao gani kilipitisha hayo
Na kama ni uamuzi wa CCM leo iweje wakatae mchakato ule ule walioamua wao?
Nina shaka sana kama unazijua sera za CCM. Hakuna mahali katika sera zao au ilani ya uchaguzi CCM imeonyesha uwepo wa mchakato. Na kama unadhani ni hivyo, huo ndio ubabaishaji na kamari tunayozungumzia.
Huwezi kuendesha nchi kutoka mfukoni.
Kwanza, Tatizo la watu kama wewe mnadhani kuwa mapendekezo/maoni/ushauri ni lazima vifuatwe. Nani alisema mapendekezo lazima yakubaliwe na kufuatwa?. Mapendekezo ni mapendekezo tu, yanaweza kufuatwa au kutupwa kapuni.
Kama huwezi kufuata mapendekezo yako mwenyewe basi una tatizo. Unawezaje kupendekeza kitu usichokitaka au kukikubali? Mkuu, yaani unaamka asubuhi, unakwenda kitu cha basi, basi likiondoka unasema hukupendekeza liondoke. Uliamka asubuhi kwanini.
Pili, Kwa kuonyesha kuwa serikali ilikuwa inakubaliana na mapendekezo mbali mbali ya tume zilizoundwa, ndiyo maana katiba yetu ya mwaka 1977 imefanyiwa marekebisho mara 14.
Tume ya Amina Salum, Kisanga, Shamhuna, Warioba ya kwanza ziliundwa baada ya 1977. Mkuu hapo lumumba mumuchoma maktaba au!
Haya mambo yanatakiwa yawe kwenye damu mkuu, ukibabaisha hapa hatuoni aibu!

Ni mawazo na fikra hizi hizi zinazopiga kelele kila siku na kusema Rasimu ya pili ya Katiba isifanyiwe marekebisho ndani ya Bunge Maalum kwa sababu ni maoni ya wananchi ''wengi''. Kwa maana kuwa wachache hawana nafasi ya kusikilizwa ndani ya Rasimu ya Katiba katika mitazamo tofauti ya jambo fulani ambalo wengi wametoa mapendekezo tofauti. Kwa lugha nyingine, Rasimu ya Katiba inahusu mawazo ya wengi pekee ambao mawazo yao yanafanana na siyo pia wachache wenye mawazo yanayofanana hata kama yana mantiki katika ujenzi wa Taifa.
Wengi wapewe, wachache wasikilizwe-JK Kikwete the president of united republic of Tanzania

CCM inapimwa katika sanduku la kura na siyo katika mawazo na fikra za mtu mmoja au kikundi cha watu. Blame ya CCM inajulikana kwenye matokeo ya chaguzi mbali mbali na siyo kwenye fikra na mtazamo wa mtu mmoja.
Ni kweli, hasa pale wanapojiandikisha watu 70,000 na wakapiga kura watu 10,000. Mkuu Mag3 njoo hapa Mwanadiwani jibu la swali lako katika ule uzi

CCM ndiyo iliyoanzisha Mchakato wa Katiba kupitia serikali yake na ndiyo CCM hiyo hiyo inayosimamia Mchakato wa Katiba kupitia Serikali yake. Hii dhana ya kusema CCM inatafuta a way to share blame ni fikra na mitazamo ya kitoto
Well, tuambie ni kikao gani cha CCM kilifikia maamuzi hayo. Tuambie ni sera ipi ya CCM inasema hilo, tueleze ni Ilani gani ya uchaguzi ya CCM ilitaja hilo
Kwa hiyo hicho kikundi kinachojiita UKAWA hawakufahamu kuwa CCM ilikuwa inatafuta a way to share blame? Are they stupid/foolish/ignorant?
Njia imepatikana kupitia TCD na hakika tuliwaeleza UKAWA, wajilaumu.
Kkwete katokea mlango wa uani, CCM dirishani, Samwel Sitta yupo Dodoma, jengo bovu linamwangukia mzee wa watu. Mjini shule, sijui Smawel alikwenda shule ipi.
Katiba kushindwa, ni kushindwa uongozi wa Kikwete. TUmedharauliwa sana na majirani na bara hili.
Ahsante JK, hutasimamia tena jambo zito kama hili, baada ya kutokea mlango wa uani, chanja mbuga hadi mwakani utakapomaliza ngwe. Tutalipa mafao yao ingawa ni kwa uchungu sana.
CCM kila siku inasema, Maridhiano kuhusu Mchakato wa Katiba katika stage ya tatu ambayo ni Bunge Maalum yanapatikana ndani ya Bunge na siyo barabarani.
Nini kinawashinda hadi watafute consensus? Kinachoendelea Dodoma ni comedy chini ya stan up comedian Samwel Sitta. Wajanja wametoka mlango wa uani, sitta amebaki anatoa ze comedy. CCM kiboko, mlimmaliza Sitta uspika kiujanja kwa zamu ya akina mama , safari hii mumekatisha ndoto za Urais kwa kumsukumia zigo bovu. CCM kiboko, hapo ndipo nawapenda maana mkimwaga mtu, hamna mchezo. Mlianza na Mnasour Himid, Sitta mumemstahi hadi alipoingia kichwa kichwa, mkaondoa 'shingo' kama ISIS, ninyi kiboko
Rais Kikwete hakukutana na TCD ili kutafuta Maridhiano bali alikutana na TCD ili kutafuta maelewano(compromise) au mwafaka(consensus). Kilichotokea ni UKAWA kupata compromise na huku Serikali ikiondoka na consensus.
Umesesma maridhiano hayapatikani barabarani. Kikwete alikutana na TCD huko barabarani tena akitafuta consensus? Unataka kusema Rais na Mwenyekiti wako naye ni UKAWA.
Hakuna hotuba au sehemu ya hotuba ambayo CCM imesema takwimu za tume ya Mzee Warioba niza kutunga. CCM inachokataa ni hoja za baadhi ya wajumbe wa Tume ya Mzee Warioba kuhusu mapendekezo ya Muundo wa Serikali tatu. Hoja za kusema tume imependekeza Muundo wa Serikali tatu kwa sababu wananchi ''wengi'' walipendekeza ndiyo msingi wa CCM kutokubali hoja hizo.
OK, vipi kama wengi si hoja kwanini Rais aseme wengi wapewe wachache wasikilizwe. Na kwanini kuna kupiga kura kama wananchi wengi haina maana. Hizo kura ndani ya bunge zinaamua nini kama si wengi. Kwanini kamati zimeakilisha maoni yao kwa kutumia wengi na wachache. Kwanini CCM hawakukataa neno hilo, wewe unalikataa vichochoroni.
Ikumbukwe kuwa, mpaka tunapoandika hizi hoja, Mchakato wa Katiba kupitia Rasimu ya Pili ya Katiba unaendele Bungeni. Hii dhana ya kusema Mchakato wa Katiba umekwama ni kujifariji kihoja kwa kuukimbia ukweli.
Haya endeleeni maana Kenya nao walianza hivi hivi. Tunauhakika wa katiba mpya baada ya CCM kupitisha yao. Samwel hapa anawacheza shere, anajua mumshamtosa sasa anataka akamilishe milioni 150 arudi Urambo.
Ukiwa CCM akili tupu, mwaga mboga namwaga ugali.
Mchakato wa Katiba ni zoezi endelevu na kwa maana hiyo, utapisha Chaguzi Kuu kwa vile chaguzi Kuu siyo zoezi endelevu.
Katiba nayo imekuwa Mkukuta, Mkuza au Mkurabita. Hayo ndiyo mambo endelevu.
Kama ungekuwa endelevu siku 70 alizotoa JK zilikuwa na maana gani?
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi

Haya tulyaeleza kabla ya majadiliano ''barabarani' kama wasemavyo CCM. Matokeo yake sasa yanaonekana, rungu la kumaliza ukawa kapewa ''mpinzani'' John Cheyo

UKAWA KUKUTANA NA JK KWA JINA LA TCD

UKAWA WAGEUZIWA KIBAO NA KUSINGIZIWA

TCD ITAKUJA NA SULUHU GANI YA KISHERIA?

Habari zilizopamba magazeti ni kuhusu ''uungwana' wa Rais Kikwetekukutana na vyama vya siasa.
Habari zimegeuza ukweli ya kuwa aliyetaka kukutana na UKAWA kwa jina la TCD ni JK na si vinginevyo

Katika kuhakikisha janja inatumika, imesemwa rais anakutana na vyama vya kisiasa kupitia TCD kituo cha demokrasia.

TCD imetumika kukwepa fedheha ya JK aliyewaponda wapinzani na sasa 'anawapigia' magoti kiaina.

Kusema JK anakutana na UKAWA kungeleta dhalili na hivyo likatumika jina TCD

TCD ni jina kwasababu CCM ni mwanachama na yupo bungeni, mapalala na Chausta wapo bungeni, Mrema na TLP wapo bungeni, Hamadi Rashid na ADC wapo bungeni, Kuga Mziray na PPT wapo bungeni.

Ukweli ni kuwa JK anakutana na UKAWA kwa jina bandia, lakini huo ndio ukweli.

Kinachomsukuma JK ni baada ya kubaini nguvu ya umma inavyozidi kumbana na ukweli kuwa kuna uwezekano wa asilimia 80 kukosa muafaka katika bunge la CCM, kura za maoni au kuvurugika kabisa hata bila kuwa na pa kuanzia.

Ili kupeusha balaa hilo, propaganda zimeanza kutumika kwa kutumia viongozi wa dini.

Tayari viongozi wa kikristo kupitia taasisi zao na wale wa kiislama wametoa matamko ya kusifu uungwana wa kikwete.

Wasichojiuliza viongozi hao ni mambo haya
1. Nani alivuruga mchakato, na kwanini hawakumkemea JK alipokwenda kutibua Dodoma
2. JK alipoambiwa akutane na wapinzaini alikataa,uungwana unatoka wapi ambao ulikosekana mwezi mmoja uliopita
3. JK aliposhauriwa aahirishe bunge amekataa, leo uungwana upo wapi wakati bunge linaendelea?
5. Kwani tatizo ni kukutana au ni sababu za kisheria na kanuni?
6. Kwanini wapinzani hawakupongezwa walipotaka JK aingilie kati miezi 5 iliyopita baada ya sntofahamu

Viongozi wa dini wanatumika na nyakati hizi dini zinageuzwa kuwa miradi.

Hilo UKAWA walitambuePindi maridhiano yatakaposhindikana, na hakika yatashindikana hoja iwe juu ya UKAWA kutokuwa waungwana kama JK

Lakini pia UKAWA wajiulize. Hivi JK wanaenda kukutana naye ili iweje?

1. CCM wamepindisha sheria kwa maelekezo ya JK, sasa UKAWA wanategemea nini kuanzia hapo
2. Kifungu chenye utata ni cha kisheria na utata huo umetengenezwa na CCM, JK akiona. UKAWA wategemee nini?
3. JK keshawaambia S3 hadi aondoke, tume imepedekeza S3, CCM wanaendelea na S2 sasa UKAWA wategemee nini
4. Hivi kwanini UKAWA wadhani kuwa JK anadhamira njema katika hali ya kuachia akina Sitta wajiundie tume zao?
5. UKAWA watarudi bungeni kuanzia wapi, pale walipoondoka au hapo walipo sasa?

Ukiangalia hali ilivyo, hakuna shaka ni ulaghai tu unaoendelea.

UKAWA watapewa juisi, watarudi bungeni wakitegemea JK aliyemwaga Warioba na Salim utupu, anaweza kuwa muungwana kwao.

Laiti nginekuwa mmoja wa UKAWA nisingehudhuria mjadiliano hayo, na kama ingebidi ningeuliza maswali matatu tu na yakikosa majibu naondoka katika chumba cha mkutano na kuwaacha CCM na vibaraka wao waendelee kama wanavyotenda Dodoma.

Ningeuliza maswali haya
1. JK, je bado unaamini S3 ni hadi uondoke madarakani au umefuta kauli na kuomba wananchi radhi
2. JK, hivi uliunda tume ya kukusanya maoni kisheria, nini hatima ya maoni ya wananchi Vs maoni ya bunge
3. UKAWA warudi kujadili nini bungeni, Rasimu ya Warioba kama ilivyo au Rasimu ya Sitta kama anavyokusanya maoni

Maswali hayo yangekosa majibu, dakika 30 nigeondoka katika mkutano ili nisijeambiwa nimeshirika majadiliano na kukataa.

UKAWA wasipokuwa waangalifu,wapinzani walioletwa na CCM wanaweza kuja na mkakati mpya, kwamba sasa ni suala la vyama kupiga kura kuamua hatima. Ndipo UKAWA watajikuta katika wakati mgumu.

Duru tunasema majadiliano na JK hayana tija, ni afadhali utafutwe muafaka wa kisheria bunge likiwa limesitishwa kwa muda.

Tusemezane
 
Wanajamvi

Haya tulyaeleza kabla ya majadiliano ''barabarani' kama wasemavyo CCM. Matokeo yake sasa yanaonekana, rungu la kumaliza ukawa kapewa ''mpinzani'' John Cheyo

Mkuu Nguruvi3

Hivi JK alikutana na UKAWA kwa mwamvuli wa TCD au ni kinyume chake? Kwa mtazamo wangu sioni kama alikutana na UKAWA. Japo wana-UKAWA walihudhuria mkutano ule lakini walihudhuria kwa kofia TCD na si vinginevyo. Makubaliano yoyote yale yaliofikiwa mule ndani ni baina ya JK na TCD sio UKAWA....

Labda wangeweza kususia kikao kile waiache TCD ya kina Cheyo na Mrema ndio waonane na JK peke yao ingawa bado najiuliza kama hatua hiyo ingeleta athari zipi...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom