In other words, CCM ilishajua Kwamba yenyewe Ndio tatizo na ni kikwazo cha kupatikana kwa katiba mpya, ilichokuwa inatafuta (CCM) ni mlango wa kutokea.
Ndugu Mchambuzi,
Kama ulikuwa unadhani CCM ilikuwa inatafuta mlango wa kutokea; unadhani kwa sasa imetoka baada ya tamko la TCD?
Tatizo lako ninaloliona ni kuiweka CCM katika mantiki ya siasa za uanaharakati wakati CCM ni chama kinachobeba majukumu na mwelekeo wa sasa wa kitaifa kama chama tawala.
CCM siyo chama cha upinzani na kwa maana hiyo, haifanyi siasa za majaribio ndani ya political theories.
Wananchi nchini wanaishi na kufanya kazi ndani ya Sera za CCM zilizoainishwa kwenye Ilani yake ya Uchaguzi. CCM ni chama tawala, na kwa maana hiyo, hakina muda wa kufanya majaribio ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika maisha ya wananchi.
Maamuzi ya Serikali ya CCM hayawezi yakafanywa katika msingi wa mchezo wa kamari. We can't afford to solve a real problem with an unrealistic solution.
Kama CCM iliyoaminiwa na kukabidhiwa madaraka na wananchi kwa mtazamo wako imekuwa ni tatizo, basi acha iendelee kuwa ni tatizo kwa sababu hata waharifu wanaweza wakasema serikali ni tatizo kwa sababu tu imeweza kuwaziba na kuwadhibiti kisheria ili wasifanye uharifu wao!.
Kama maamuzi ya CCM ya kuanzisha Mchakato wa Katiba mpya kupitia serikali yake na kuusimamia ipasavyo ni tatizo, basi acha iendelee kuwa ni tatizo, hasa ikichukuliwa kuwa, upendo, amani, umoja na mshikamano kama taifa uko mikononi mwa CCM kama chama tawala kupitia serikali yake.
Historia ya miaka zaidi ya 20 sasa inaweka Suala Hilo wazi yani - mikakati ya CCM kulinyima taifa katiba ya wananchi (rejea kazi ya tume ya nyalali pamoja na mapendekezo yake ambayo Kama jadi ya CCM, yalitupwa kwenye jalala Kama alivyojadili Nguruvi3.
Kwanza, Tatizo la watu kama wewe mnadhani kuwa mapendekezo/maoni/ushauri ni lazima vifuatwe. Nani alisema mapendekezo lazima yakubaliwe na kufuatwa?. Mapendekezo ni mapendekezo tu, yanaweza kufuatwa au kutupwa kapuni.
Pili, Kwa kuonyesha kuwa serikali ilikuwa inakubaliana na mapendekezo mbali mbali ya tume zilizoundwa, ndiyo maana katiba yetu ya mwaka 1977 imefanyiwa marekebisho mara 14.
Ni mawazo na fikra hizi hizi zinazopiga kelele kila siku na kusema Rasimu ya pili ya Katiba isifanyiwe marekebisho ndani ya Bunge Maalum kwa sababu ni maoni ya wananchi ''wengi''. Kwa maana kuwa wachache hawana nafasi ya kusikilizwa ndani ya Rasimu ya Katiba katika mitazamo tofauti ya jambo fulani ambalo wengi wametoa mapendekezo tofauti. Kwa lugha nyingine, Rasimu ya Katiba inahusu mawazo ya wengi pekee ambao mawazo yao yanafanana na siyo pia wachache wenye mawazo yanayofanana hata kama yana mantiki katika ujenzi wa Taifa.
Katika muktadha wa sasa, CCM ilikuwa Ikitafuta a way to share the blame and burden na ukawa ili chama kisionekane Kama Ndio kikwazo Wakati hivyo ndivyo historia itakavyokuja andika.
CCM inapimwa katika sanduku la kura na siyo katika mawazo na fikra za mtu mmoja au kikundi cha watu. Blame ya CCM inajulikana kwenye matokeo ya chaguzi mbali mbali na siyo kwenye fikra na mtazamo wa mtu mmoja.
CCM ndiyo iliyoanzisha Mchakato wa Katiba kupitia serikali yake na ndiyo CCM hiyo hiyo inayosimamia Mchakato wa Katiba kupitia Serikali yake. Hii dhana ya kusema CCM inatafuta a way to share blame ni fikra na mitazamo ya kitoto.
Kwa hiyo hicho kikundi kinachojiita UKAWA hawakufahamu kuwa CCM ilikuwa inatafuta a way to share blame? Are they stupid/foolish/ignorant?
Inakuwaje Leo Ndio CCM inakubali hata kutaja maneno haya Wakati Huko nyuma lugha na matamshi yenu na kina nape, kinana, Wassira, Sitta, lukuvi etc yalikuwa wazi na bayana Kwamba katiba inayotungwa ni I'm yenye kuangalia maslahi ya CCM kwanza? Iweje Leo muanze kutumia lugha na maneno ya wale mliowabeza kwa mfano kina jaji warioba, professor Lumumba n.k? Hawa na Wengine wengi walihimiza sana huu ya umuhimu wa maridhiano huku nyinyi kwenye uongozi wa chama mkukwepa maneno haya Kama ukoma.
CCM kila siku inasema, Maridhiano kuhusu Mchakato wa Katiba katika stage ya tatu ambayo ni Bunge Maalum yanapatikana ndani ya Bunge na siyo barabarani.
Rais Kikwete hakukutana na TCD ili kutafuta Maridhiano bali alikutana na TCD ili kutafuta maelewano(compromise) au mwafaka(consensus). Kilichotokea ni UKAWA kupata compromise na huku Serikali ikiondoka na consensus.
Nadhani unaelewa maana na tofauti ya maelewano (compromise) na mwafaka (consensus).
Baada ya UKAWA kugundua walichokubali ni maelewano (compromise), ndiyo maana kwa sasa wameanza kupiga kelele tena wakitaka eti Bunge lisitishwe mara moja. Waswahili wanasema, ''imetoka''. Mbaya kabisa kwa upande wao, kwa sasa wamejifunga kitanzi huku wakisema, Rais ajaye lazima auendeleze Mchakato wa Katiba kuanzia pale ulipoishia. Wanadai, hii lazima ifanyike kisheria. GOOD.
Ieleweke kuwa compromise huwa inazaa maamuzi legelege.
CCM Ndio iliyokwamisha mchakato wa katiba. Ukawa walichofanya ni kupigania Sheria ya mabadiliko ya katiba isimamiwe na isichakachuliwe na CCM na vikaragosi wao bungeni; ukawa ilichofanya ni kusimamia upande wa wananchi kwa Mujibu wa maoni waliyopendekeza wananchi, of which mmekuwa mkisema Kwamba ni batili na ya kutungwa na tune ya warioba; nikuulize - Kama maoni haya ni ya kutunga, kwanini mnaweweseka na ukawa, kwani msiendelee na katiba yenu huku mkizunguka nchi nzima kueleZea wananchi juu ya dhambi ya tume ya warioba kutungia wananchi maoni, na ukawa kuendeleza dhambi hiyo?
Hakuna hotuba au sehemu ya hotuba ambayo CCM imesema takwimu za tume ya Mzee Warioba niza kutunga. CCM inachokataa ni hoja za baadhi ya wajumbe wa Tume ya Mzee Warioba kuhusu mapendekezo ya Muundo wa Serikali tatu. Hoja za kusema tume imependekeza Muundo wa Serikali tatu kwa sababu wananchi ''wengi'' walipendekeza ndiyo msingi wa CCM kutokubali hoja hizo.
Ikumbukwe kuwa, mpaka tunapoandika hizi hoja, Mchakato wa Katiba kupitia Rasimu ya Pili ya Katiba unaendele Bungeni. Hii dhana ya kusema Mchakato wa Katiba umekwama ni kujifariji kihoja kwa kuukimbia ukweli.
Mchakato wa Katiba ni zoezi endelevu na kwa maana hiyo, utapisha Chaguzi Kuu kwa vile chaguzi Kuu siyo zoezi endelevu.
Kama kupisha chaguzi kuu ndiyo una tafsiri kukwama kwa Mchakato wa Katiba, basi endelea kutafsili hivyo hivyo wakati mchakato unaendelea.
Watanzania wengi walichoelewa ni Kwamba rais aliondoka na hoja Kwamba Hana mamlaka ya kulivunja bunge, hivyo ukawa Waende kulifanyia Hilo kazi. Au wewe ulielewa vipi?
Nope, TCD waliingia kwenye meza ya majadiliano bila kuwa na ajenda zinazoeleweka kama taasisi ya kisiasa. Kila mmoja alikuwa na ajenda zake wakati suala lilihusu pande mbili ambazo ni Serikali na TCD. Suala halikuhusu mmoja mmoja au kila chama. Kutokana na hilo, Rais Kikwete aliwaambia wakajipange tena kama TCD na warudi mezani na ajenda zinazoeleweka ambazo ziko katika kundi moja linalojengwa na TCD.
Na je, rais Hana mamlaka ya kufanya maamuzi Wakati wa dharura? Kinachoendelea bungeni hakitazaa katiba ya wananchi, na kuendelea kutafuna hela za walipa kodi Wakati CCM ikifahamu Hilo ni Jambo ambalo rais anaweza kulifanyia maamuzi Katika Hali ya dharura.
Rais anafanya kazi zake kisheria. Hata kama kungekuwa na sehemu katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inampa Rais uwezo wa kusitisha bunge wakati wa dharura, Dharura ipi iliyopo unayoisema mpaka Rais alisitishe bunge ambalo linafanya kazi zake kisheria?
Mchakato wa Katiba ni gharama. Kama kazi ya kutunga Katiba kupitia bunge ambalo lipo kisheria ni kutafuna hela za walipa kodi, basi acha hizo pesa zitafunwe kwa sababu demokrasia ndiyo imeamua hivyo kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83.
Isitoshe, Huko nyuma mliulizwa, je rais alihairisha BLK kupisha bunge la bajeti kwa Sheria Ipi? Hamkujibu.
Rais hakuahirisha Bunge Maalum la Katiba bali Bunge Maalum la Katiba lilimaliza muda wake wa awali ambao ulikuwa ni siku 70 kama ilivyokuwa kwenye Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyoainishwa kwa Kifungu cha 28 (3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2013 kwamba "
…… muda ambao Bunge Maalum litajadili Rasimu ya Katiba hautazidi siku sabini (70) kuanzia tarehe ambayo Bunge Maalum lilipoitishwa".
Baadaye Mwenyekiti wa Bunge Maalum aliliongeza siku 60 kwa kuomba ridhaa kwa Rais wa Tanzania ambaye alishauriana na Rais wa Zanzibar. Siku hizo zilianza kuhesabika tarehe 05/08/2014.
Mamlaka ya kuongeza muda yanapatikana katika kifungu cha 28 (4) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambacho kinazungumzia uwezekano wa kuongeza muda. Kinasema,
"Mwenyekiti wa Bunge Maalum baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti anaweza; kwa ridhaa ya Rais baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar kuongeza muda uliotolewa chini ya Kifungu Kidogo cha (3) kwa kipindi kitakachofaa kukamilisha shughuli za Bunge Maalum".
Awali mtazamo wa CCM ulikuwa Kwamba katiba ya wananchi haipatikani nje ya ukumbi wa bunge maalum la katiba, what changed?
Kauli hiyo haijabadilika ndiyo maana mpaka sasa Bunge Maalum la Katiba linaendelea na kazi yake ndani ya bunge.
Pia alisema Kwamba iwapo katiba mpya haitapatikana ndani ya kipindi hicho, katiba ya sasa/iliyopo (1977), itaendelea kutumika na Ndio hiyo hiyo itakayotumika kwenye uchaguzi mwakani. Hakusema Kwamba itafanyiwa marekebisho Kama vile tume huru ya uchaguzi, mgombea binafsi, na matokeo ya urais kupingwa Mahakamani.
Hoja yako hapa ni nini?. Kwani Marekebisho yatafanyika kwenye Katiba mpya au Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa kutumia Katiba mpya?
Hukuwahi kuwasikia Mawaziri kabla ya Mchakato wa Katiba mpya wakisema ili kukabiliana na Chaguzi Kuu (Serikali za Mitaa, Wabunge na Rais), serikali itafanyia marekebisho katiba ya 1977.
All that said and done, it's on the records Kwamba rais alishasema Kwamba serikali Tatu hazitatokea akiwa madarakani, na hili likachochea mgogoro uliopo sasa. Wenye Tabia ya kujisahau sahau ni Nani Hapa Katika ya CCM na ukawa?
Acha kumlisha Rais Kikwete maneno.
Rais Kikwete kila mara anasema hana tatizo na maamuzi ya Bunge Maalum kama watatunga Katiba yenye Muundo wa Serikali tatu lakini anachopenda wafanye hivyo huku wakiwa na informed decision kuhusu Muungano.
Inatakiwa tujiulize Kama taifa - je, kupitia mchakato wa katiba mpya tumethubutu, tumewezana tumesonga Mbele?
Kama tumeshindwa,ni kwa sababu gani?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Nimeishasema siyo mara moja na nitasema tena katika mantiki ya Mchakato wa Katiba mpya,
CCM ilithubutu kwa maana kuwa, kupitia Serikali yake ilianzisha Mchakato wa Katiba.
CCM iliweza kwa maana kuwa, hatua nne za Mchakato wa Katiba zinaendelea kama kawaida. Kwa sasa tuko kwenye hatua ya tatu ambayo ni Bunge Maalum.
Tunasonga mbele kwa maana kuwa kila changamoto inayojitokeza kwenye Mchakato wa Katiba, inapata majibu kwa haraka kutoka kwa wabunge, serikali na wananchi, na zoezi la linaendelea.