UKAWA wapokea mabilioni ya pesa kutoka Ujerumani kuvuruga mchakato wa Katiba


Jitekenyeni wenyewe kisha mucheke.
 
Hadithi hadithi = Hadithi njoo uongo kolea. Hapo umeona umeandika hadithi nzuri ya kupendeza? Nani alikufundisha hadithi hiyo Idd Ninga?
 
Jambo Leo ni gazeti longo longo. Ukawa wapate pesa na serikali iwaachie hivi hivi? Ni kuweweseka tu.
 
Kweli ccm bado wapo karne ya 20 kwenye propaganda, hiyo taasisi mnaweza mkawafanya serikali iwaombe msamaha serikali ya Ujerumani.
Massele alimtukana balozi wa Uingereza nadhani bado anaugulia na sidhani kama anaruhusiwa kukanyaga ardhi ya EU, sasa na hilo gazeti linakokwenda ndio kulekule.
 
Lumumba homa inawapanda.
Kikwete ajisalimisha na kuwaangukia UKAWA na bado
 

Mimi naona tuongeze idadi ya vyama, tupate mkwanja mrefu zaidi tujitegemee kwenye bajeti badala ya kuomba misaada ya wahisani.
 
Mkuu kwa hiyo wewe kwa akili zako ulizoletwa nazo duniani unawaamini UKAWA wako peke yao?

Na wewe mkuu unaamini kwamba yuko aliye peke yake? Tatizo ni mvuta kamba na mkuki kwa nguruwe!
 
Chadema si ndio washirika wa kile chama kinachoongoza ujerumani cha Christian Democracy Union.? Hawa wajerumani wanataka kuleta ukoloni kwa mgongo wa Chadema.
 

Kama yote hayo ni kweli, SWALI: je misaada hiyo ya wafadhili toka Nchi ya Ujerumani ni batili au ni halali? Naomba tu kujua hilo ili Nielekee Ubalozi wa Ujerumani kupata ufafanuzi kuhusu tuhuma hizi.
 


Ni jambo la ajabu kuona chama kilichopo madarakani kikilalamikia jambo ambalo likondani ya uwezo wao. Ni jambo la kustaajabisha kuona ccm inalalamika kuwa ukawa wanapewa fedha kutoka nje ya nchi bila kuchukua hatua ya kudhibitisha uingizwaji huo wa fedha. Ccm ina polisi, ina pccb, ina TISS n.k. kwanini walalamike badala ya kuchukua hatua?.
Wenyeakili wanajua hizi ni propaganda za kitoto.
 
Linamilikiwa na nani siyo issue, issue ni limeandika habari gani muhimu. Hii taarifa imenigusa sana nimeona nitangulize uzalendo mbele. Kumbe kelele zote za UKAWA kuna weupe wako nyuma yao, hili haliwezi kuvumilika kabisa

Are you sure? Do you have evidence beyond reasonable doubts! Ndio maana nimeuliza linamilikiwa na nani kwa kuwa ndiye anadictate nini kiandikwe na nini kiachwe!
 
Hili liko wazi kabisa wadhani wawle wajumbe wangekubali kirahisi kuachia zile posho mdebwedo huko kwao wanapokea posho kama kawa huku wengine wakishinda baa tuu kunywa viroba
 
Jambo leo ni gazeti la udaku wa siasa wala huwezi kuliamini hata kama ni ukweli.

Je,CCM nao wanapokea wapi pesa au wao ni kwa kupitia kumnyonya Mtanzania?

S.N. jilala;
C
CM haihitaji kuomba omba kwa bakuli huko ulaya. Tunatoa kibali tu cha kupunguza tembo wa mikumi, tunapunguza magogo ya mninga na mvule (Magogo) siyo mbao kwani hamjui size inayo takiwa kule China, tunaruhusu mameli ya kichina yanyonye gesi yetu waipeleke kwao kuipima kama ni ya viwango. Hii ni lazima itwaliwe nyingi sana kuona kiwango kama tayari kimefikia hivyo hii haiuzwi, Meli zikirudi zirudishe sembe kutoka Afganistan kwa ajili ya wale wabunge maalum waliotajwa na wakatishia kwenda mahakamani lakini mpaka leo hakimu wala msajili wa mahakama hajaweza kutunga sentenzi nzuri ya kuwasilisha mahakamani shtaka kubwa hivi. Oh! nimesahau hata vyanzo nyeti vya kula kodi za walala hoi ka vile BMK ambalo litatoa katiba viza halafu tuwalaumu UKAWA. Nimesahau njia nyingine nyingi ka kule BoT.
Upo hapo? Kwa nini tujiaibishe kwenda kuwa matonya huko ulaya?? Hao wasio na uwezo waende huko na tukijua tu zinaingia lini na njia gani, tunaziwekea vikwazo. Full stop.
Oyaaa! Chama kimeshika hatamu za uongozi banaaa. Mpaka mileleeeee
 

hetu;
Aksante sana kwa hoja yako mujarab kabisa. Malalamiko haya yangetolewa na Chadema dhidi ya CCM tungepoteza mda kidogo kuyachunguza. Lakini, ukiona ndama anatoka povu huku ananyonya akilia, jua ulimwachia maziwa mengi.
UKAWA waliwaachia posho nyingi mno, sasa hawaamini kuwa kweli UKAWA wamewaachia mlo ka huo kwa sababu ya uzalendo. Kuleni tu ila hiyo ni kibudu si halal
 

Wakati hao watu wa vyama vya upinzani walopokuwa wanadai katiba mpya hoja ya kufadhiliwa na nchi za nje zilijitokeza. Kwa wakati ule CCM na serikali yake walikataa kata kata kuwa hakukuwa na haja ya katiba mpya. Sasa hao wapinzani wameona katiba mpya waliyohitaji siyo itakayopatikana. Sasa wafadhili wale wale waliokuwa wakifadhili madai ya katiba mpya wanadaiwa kufadhili harakati za CCM kutengeneza katiba mpya. Je hapo kuna commonsense? Naona tunarudi kulekule enzi ya kuambiwa kila anayetofautiana na serikali anatumiwa na maadui wetu wa nje, wakati ule walikuwa maadui wa siasa yetu ya ujamaa. Ilikuwa wanafunzi wa chuo kikuu wakigoma wimbo unakuwa maadui wetu wa nje. Watu wakikosoa foleni ni maadui wa nje. Je mpaka leo Watanzania wanaamini hayo???
 
Hawa jamaa bei chee sana wakichukua nchi tutauzwa asubuhi mapemaaaa....
yyyaaaaani ww ni mmoja wa watu wa ajabu, uuzwe mara mbili tayari ulishauzwa kama unadhani uwongo nenda Loliondo kama haujakaribisha ktk Falme za Kiarabu, mpaka ndege za jeshi zinatua ktk nchi yao na kubeba wanyama, hulijui hilo au unajifanya hamnazo?
unakumbuka wale wakazi wa dodoma waliojenga nyumba zaidi ya miaka kumi halafu nyumba zao zikavunjwa naaaliyennunua eneo miaka kadhaa baadaye baada ya wao kuhamia, nenda kwenye maeneo yenye madini na gesi uone wazawa jinsi wanavyoonewa kisa mzungu au umesahau yale mambo ya gesi ya tumbo kuleeeeeeeee... malizia bac
 
Kama yote hayo ni kweli, SWALI: je misaada hiyo ya wafadhili toka Nchi ya Ujerumani ni batili au ni halali? Naomba tu kujua hilo ili Nielekee Ubalozi wa Ujerumani kupata ufafanuzi kuhusu tuhuma hizi.

Mkuu ukishaona neno, 'inasemekana', hizo ni tetesi na tuhuma ambapo mwishowe huwa uzushi. Serikali haijalala kihivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…