Tanzania Kwanza chukua hatua, kamata watu maana huu ni uhaini. Lakini mkilalama kwetu sisi wananchi ambao mmezika maoni yetu katika rasimu ya katiba mnataka tuwaeleweje? Tumewapa polisi, usalama wa taifa, magereza, jeshi halafu mnalalama utadhani nyie ndio wapinzani????? Kama mnafanya porojo tu bora mungeacha maana mnazidi kujifilisi kisiasa, mnaongeza agenda za kupondwa na wapinzani maana vituko vinazidi!!! Huku mnakusanya maoni ya wananchi ya katiba mpya, jambo lililokwisha fanyiwa kazi na Tume ya Jaji Warioba, Huku mnasema Kikwete hana mpango wa kukutana na Ukawa, huku CC ya CCM inasema imeridhishwa na mwenendo wa kinachoendelea katika BMK, huku mnamuagiza kinana aendelee kutafuta muafaka, huku mnasema hamuwahitaji UKAWA akidi inatosha, huku Kikwete anasema UKAWA ni muhimu waje tuongee, huku mnasema Chadema inakufa, huku mnasema sasa inavuruga mambo, nyie vipiiiiiiiii?