Chadema wanapata msaada Ujerumani, Ukawa wanapata msaada Ujerumani, Ukawa wanalipwa laki saba sijui nne, na mengine meengi kutoka CCM tumeyasikia, sasa yanatufundisha nini? Watanzania hawajitambui kwa mawazo yao ni sawa, lakini sio kiihivi. Walitutangazia ugaidi kwa vyama vyote vya upinzani nchi hii, tunakumbuka ngangali na ngunguli na mapanga yao, tunakumbuka uislam wa CUF na ukristo wa Chadema, hivi hata kama watanzania ni wapumbavu wa kununuliwa T shet na kanga na shingi elfu tano ndio muwadharau hivi? Kazi hamfanyi kazi kuiba tu na kuficha nnje ya nchi kwa umasikini huu hata mkidanganya vipi nani hauoni unasikini? Nani haoni maisha magumu? Matibabu hakuna nani haoni? Elimu mbovu nani hajui? Hebu jaribuni kuangalia maisha ya Watanzania kwanza ndio muwe mnatuletea hizo kampeni zenu za kizushi kwa sasa maisha yametufunza kujua baya na zuri.