Hivi Jambo Leo linamilikiwa na nani? Maana ni kama vuvuzela la CCM cum Government!
Mkuu, wakishawafadhili, mtawalipa nini?
Linamilikiwa na nani siyo issue, issue ni limeandika habari gani muhimu. Hii taarifa imenigusa sana nimeona nitangulize uzalendo mbele. Kumbe kelele zote za UKAWA kuna weupe wako nyuma yao, hili haliwezi kuvumilika kabisa
Mkuu Thatha, hakika nchi hii inatafunwa na wengi. Hivi unajua mzee mamvi alienda nchi gani vile? Maana na yeye ni sehemu ya wafadhili wa ukawa
Wamechoka kumchokonoa Kagame?
Serikali haijawahi kuomba msaada Ujerumani. Ni wahuni tu wale
Wanaoutafuna nchi hii ni CCM
Madai hao yametolewa na Kundi la Tanzania Kwanza
- Wamesema mabilioni hayo yanatoka katika taasisi mojawapo nchini Ujerumani na zinapitia akaunti iiyoko Uholanzi kuingia nchini.
- Inasemekana pesa hizo zinaingia kweneye akaunti za Katibu mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Harouna Lipumba na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe.
Source: Jambo Leo
hapana shaka mfadhili mojawapo atakuwa CDUunawajua GTZ wanafanya nini hapa Tanzania? fikiria wakati mwingine. narudi kwenye mada ni vyema wangetaja hayo mashirika wanayofaadhili UKAWA, pia tuwe wa kweli wote tunajua walioharibu/aliyeharibu mchakato huu ni akina nani? na endapo ccm ingeheshimu maoni ya wananchi kupitia tume mchakato ungeenda salama. ila naona bado mnaleta propoganda za magazeti. kwa hapa tulipofikia maridhiano yamechelewa, ni maamuzi ya wananchi ndio yaliyobakia, wacha waendelee kula posho kwa kitu kisichofikia lengo lake.
Unajua Pasco unaweza kumuona kama zuzu lakini ana upeo mkubwa sana.Kuna comment yake moja kwenye uzi ulioanzishwa na Mawazo kuhusu Faraja Kotta alisema watawala watafanya kila njia haswa kwa mali zao za wizi kufanya ukombozi usifanyike japo wapo wachache.
Uliotoa habari ushaanza kujifunza umbea sio bure.
unawajua GTZ wanafanya nini hapa Tanzania? fikiria wakati mwingine. narudi kwenye mada ni vyema wangetaja hayo mashirika wanayofaadhili UKAWA, pia tuwe wa kweli wote tunajua walioharibu/aliyeharibu mchakato huu ni akina nani? na endapo ccm ingeheshimu maoni ya wananchi kupitia tume mchakato ungeenda salama. ila naona bado mnaleta propoganda za magazeti. kwa hapa tulipofikia maridhiano yamechelewa, ni maamuzi ya wananchi ndio yaliyobakia, wacha waendelee kula posho kwa kitu kisichofikia lengo lake.
Kwani Tanzania ndiyo iliyosema ujinga huo? Ujinga usemwe na CCM na mawakala wake wewe unaisingizia Tanzania? Kwa taarifa yako chama chenu sio nchi bali ni kundi la watu wanaoiangamiza nchi.Tusubiri tuone , kama ni uongo Ujerumani si wataitaka Tanzania iombe msamaha, ikikaa kimya manake ni kweli
tusubiri tuone , kama ni uongo ujerumani si wataitaka tanzania iombe msamaha, ikikaa kimya manake ni kweli
Unataka kutuambiaje sasa, UKAWA waachiwe wafanye watakavyo na wazungu wao?