Ukiacha Dar es Salaam, mikoa iliyobaki ujanja wao ni mchana tu, ikifika saa tatu usiku kila mtu yupo kwake

Kama ni kweli supu ya pweza, biashara ya malaya, bias, chapati na maharage, supu ya kongoro
Chapati za wapemba saa moja usiku ndio anawasha moto,huko kijijini kwetu ndio wanafunga milango walale
 


Aiseeee
Wewe wa mikoani unatufasiria mji wetu sisi tuliozaliwa, kuuishi na pia kutoka na kuzunguka dunia sio mikoani namaanisha miji mingine duniani, ikiwepo ya US, Europe, Asia na miji mikubwa hata hapa Africa
Halafu unalinganisha Dar na vijiji vilivyochangamka
 
Tatizo ni hivi
Huko mnakokaa kwenye vijiji vilivyochangamka hakuna maisha ya Night Shift
Sio kwamba watu hawalali, Dar kuna Viwanda na kazi zinafanywa kwa shift, yaani watu wanalala mchana na usiku wanaingia kazi, kwa hiyo mji unakuwa unajipanga kuwahudumia kama sehemu ya kula, usafiri na mengineyo
Huko kwenu kwenye vijiji vilivyochangamka, maisha ni mchan tu............
 
Sasa kumbe Dar wanalala Mchana ili usiku eapige kazi, sasa Mkoani watu hawalali mchana zaidi ya kupambana na kazi ma usiki wanalala.....kumbe mwalala mchana 🤣🤣🤣🤣

Hapo tofauti ni Wakati tu wa kufanya kazi
 
Dar unatoka kuamka mwenzio ndo anaingia kulala yani hakuna kupoa
 
Aisee ila jamii forum kuna matapeli wengi sana..mtu.wa.simiyu.akiona hayo mapicha anaweza kuuza ng'ombe zake aje huko kumbe ni wizi.mtu hakuna la maana watu.wanaishi.maisha ya taabu kama watumwa
Pita hayo maeneo muda wa mchana ujionee uhalisia wake, picha zinadanganya sana aiseee, hayo maeneo ni machafu sana ata mpangilio wake uko ovyo tofauti na hizo picha
 
kumbe ujanja ni kukesha usiku kucha .ndio maana mungu aliumba usiku na mchana .je wewe unayekesha usiku kucha unawazidi kitu gani wanaopata muda wa kupumzika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…