Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😀 Mnafanya watu waliopo nje ya Dar na hawajakaa Dar wahisi ukiamka unakunywa chai Serena au Hyatt, wanazoziona katika movie. Kwako una furniture za ulaya, bafu kubwa lina jaccuzzi na sehemu ya steaming,ki shower amazing. Ukienda beach unakodi yatch, unakunywa beer saafi imported,sehemu nzuri
Kumbe UHALISIA bana asubuhi vitumbua au mihogo ya mia mia kwa mama Mwaju, chai ya rangi. Kuoga unatoka na kopo lako la sabuni maji katika ndoo, mavi unayamwagia maji system ya kuflash haipo au maji hayaendi katika system. Mtu anaweza hisi pisi kali unaimiliki kumbe ni mjasiriamwili unapiga,na wengine wanapiga ila una picha yake.
Huyu sio wewe, ila ndio 80% ya life hapa Dar.
Kuhusu night life ni kweli kuna tofauti, ila nimezurura mikoa kadhaa, naijua nightlife ya Mwanza,Arusha,Mbeya na sehemu kadhaa inategemea na mapendeleo yako na hadhi yako.
Hii mada ni aidha ya mtu ambae ni mdogo, au ana experience ndogo katika mambo ya starehe na kuzunguka nchi hii. Nimeenda mpaka vijijini iringa nakuta sehemu unakesha na watu wanakula monde, na ukitaka kuichapa unauliza wakulungwa😀
Jamaa alietoa mada sio mtu wa night life bana, au alienda sehemu muda mfupi. Akataka kwenda kula bata jumatatu au jumanne usiku.
Hata Dar ukiona mtu anakesha mpaka asubuhi katika starehe, mara nyingi ni fala, mwizi au anatumia fedha za kupewa (baba,mama e.t.). Mjanja akienda club saa tano au sita saa 9 au kumi anasepa niamini, waliobaki ni aidha kuna issue maalum ni wachache wengi ni mafala, waomba bia,machawachawa,wezi, malaya(wabovu). wale smart,visu wanakuwa walishachukuliwa 😀
Mitandaoni watu wana mikwara sana, hawaulizi kujua. Inaweza isifikie Dar kwa sababu ya population na infrastructure ila kila sehemu ina night life yake. Night life issue kubwa ni ku refresh tu vinywaji,chakula n.k
AiseeeeMkoa gani ulitafuta chakula kwa tochi? Au unaongelea aina ya chakula,ulikosa chips kavu? Kama ulikuwa Arusha ungeenda Granmelia ipo pale mkuu ina hadhi ya nyota tano kama Serena unapokunywa chai. Au kama ni masikini masikini ungeenda maeneo Shivers/Mrina ungepata nyama choma na mad* wa kununua.
Tabora ungeenda hata Tabora Belmonte ni nyota tatu haifikii Hyatt unapokula mchana ila ingefidia kidogo, wazungu weusi wenzako huwa wanalala pale pia, kama ni masikini masikini unataka wa kununu ukachakate ungeenda Oxygen Lounge/Club nadhani bado ipo nilipita muda kidogo.
Mwanza zipo sehemu kibao, Iringa zipo.....Mbeya pia nimeshacheki night life yao.
Issue ni hela hamna, au nyie ni madogo na night life mnaigiza mnataka mkute watu weengiii muanze ukenge ukenge 😀 sababu mmeshazoea kufuata mikumbo ya msafara wa mamba.
Halafu watu wa hivi na mitazamo hii hata hapa Dar ndio nyie tunawakimbia club kubwa tunaenda katika vi bar vya nje sababu brother brother nyiiingiii ni bia ya saba zote za mizinga,na kusimulia historia za zamani, ulegend wa kibwege oooh hapa Kino mi legend, babu yangu sijui hivi, wakati watu wanataka kula life kwa kidogo kilichopatikana.
Ukiwasha sigara, haujafika hata katikati anaitaka, unampa nzima anaiweka mfukoni anasubiri unayovuta. Mwishowe unambwatukia dogo kuwa na adabu, kwanza nani kakuita hapa....umeshapata bia na sigara. Ondoka
NB SIO LAZIMA UWE WEWE NDIO WATU KIBAO WALIVYO
Tatizo ni hiviUsingizi ni Afya, ni Muhimu sana Mtu kupumzika vizuri kwa masaa at least 7 au 8, usijisifie kutokulala na kujiona mjanja🫠
wengi wanaopumzika vizuri wana pesa au hali nzuri kiuchumi, sio Hohehahe
Dsm ina hali mbaya sana kimazingira, inanuka sana, inanuka vinyesi, shombo na jalala kila kona
Joto pia ni kali sana
Kutokana na kero hizo utawezaje kupata utulivu na kulala vizuri kwa wakati? Labda kama wewe ni Funza au Inzi
Sasa kumbe Dar wanalala Mchana ili usiku eapige kazi, sasa Mkoani watu hawalali mchana zaidi ya kupambana na kazi ma usiki wanalala.....kumbe mwalala mchana 🤣🤣🤣🤣Tatizo ni hivi
Huko mnakokaa kwenye vijiji vilivyochangamka hakuna maisha ya Night Shift
Sio kwamba watu hawalali, Dar kuna Viwanda na kazi zinafanywa kwa shift, yaani watu wanalala mchana na usiku wanaingia kazi, kwa hiyo mji unakuwa unajipanga kuwahudumia kama sehemu ya kula, usafiri na mengineyo
Huko kwenu kwenye vijiji vilivyochangamka, maisha ni mchan tu............
Kumbe Dar Kuna manamba wengi hivyo?Umetujumuisha kwenye orodha ya manamba wana Daslam huwa tunaamka saa 4 Asubuhi kwa ajili ya supu tunarudi kulala.
Biashara za kupanga chini ni matesoWale wa mikoani....
Picha zinaongea zenyewe
View attachment 3138671
View attachment 3138674
View attachment 3138676
View attachment 3138677
Pita hayo maeneo muda wa mchana ujionee uhalisia wake, picha zinadanganya sana aiseee, hayo maeneo ni machafu sana ata mpangilio wake uko ovyo tofauti na hizo pichaAisee ila jamii forum kuna matapeli wengi sana..mtu.wa.simiyu.akiona hayo mapicha anaweza kuuza ng'ombe zake aje huko kumbe ni wizi.mtu hakuna la maana watu.wanaishi.maisha ya taabu kama watumwa