Ukiachana na dunia kulizunguka jua na kujizungusha kwenye muhimili wake nadhani kuna mzunguko mwingine ambao wanasayansi hawajaugundua

Ukiachana na dunia kulizunguka jua na kujizungusha kwenye muhimili wake nadhani kuna mzunguko mwingine ambao wanasayansi hawajaugundua

konda msafi

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
1,696
Reaction score
8,763
Dar es salaam haijawahi kuwa na majira ya baridi kwa muda mrefu hivi. Biharamulo nimeona clip kuna hadi barafu inadondoka kitu ambacho hakijawahi kushuhudiwa. Ulaya wanateseka na joto.

Nadhani haya hayatokei kwa bahati mbaya bali kuna universal system ambayo wanasayansi hawajaigundua kama walivyoigundua solar system inayoleta majira ya mwaka au dunia kujizungusha kwenye muhimili wake kunakosababisha kuwepo kwa usiku na mchana.

Nadhani miaka michache ijayo africa tutaanza kushuhudia majira ya baridi kama ilivyo ulaya na Marekani na huenda huko Marekani na Ulaya wakawa na majira kama tuliyo nayo huku Afrika.

Nadhani huu mfumo ambao ushaanza kuleta baridi hii Afrika upo kwenye stages za mwanzo kabisa, nikimaanisha kwamba stages za mwanzo kwenye huu mzunguko huenda ikawa miongo 2 au 3 depending how long the system is. Maybe this is just the tip of the iceberg.

If the system let's say takes 22 centuries to complete that means the world has never experienced such a system hence there is no such a discovery as it has been for a Solar system.

Kwa hiyo hii baridi ya muda mrefu tunayoiona Dar na barafu kudondoka huko Biharamulo ndio mwanzo wa majira ya huu mfumo ambao dunia haijawahi kuushuhudia. Tutegemee miaka ijayo Africa itakuwa na majira kama ya Ulaya na Ulaya itakuwa na majira kama ya Africa.
 
Attachments

  • 2883413_ee6280a4-1272-49ff-beec-897d7be2c46c.mp4
    5.8 MB
Unapoint mkuu, lakini kwanini hichi tunachokishuhudia isiwe ni athari za mabadiliko ya tabia nchi kutokana na kuvuruga mazingira kwa shughuli zetu? Tunazalisha carbon kwa wingi, tunakata miti sana bila kupanda mingine mingi zaidi, tunaharibu vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.

Unachokisema kina mantiki ila binafsi nafikiri ni athari za uharibifu wa mazingira unaopelekea mabadiliko ya tabia nchi.

Wataalam wanakuja kutupa taaluma na muongozo.
 
Unapoint mkuu, lakini kwanini hichi tunachokishuhudia isiwe ni athari za mabadiliko ya tabia nchi kutokana na kuvuruga mazingira kwa shughuli zetu?
Tunazalisha carbon kwa wingi, tunakata miti sana bila kupanda mingine mingi zaidi, tunaharibu vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla...
Na hizo nchi zilizoendelea wanaharibu mazingira mkuu au..
 
I may be wrong I may be right. This is just my speculation. Inaweza ikawa athari ya uharibifu wa mazingira au inaweza ikawa ndio "utungo" wa mfumo ambao dunia haijawahi kuushuhudia.
 
Mpaka sleo sijaonna tafiti ya kuniridhisha inayonishawishi kyamini eti dunia inazunguka kutoka sehemu moja kwenda sehemu ingine.

Na utandawazi huu wote bado siamini kwamba dunia inazunguka.

Aliyekuwa na ushahidi mzuri anaweza akanisaidia pengine...
 
I may be wrong I may be right. This is just my speculation. Inaweza ikawa athari ya uharibifu wa mazingira au inaweza ikawa ndio "utungo" wa mfumo ambao dunia haijawahi kuushuhudia.
Mkuu South unaenda tena lini wakakuKhumbu tena maana hujatosheka kuwa Khumbunized
 
Na hizo nchi zilizoendelea wanaharibu mazingira mkuu au..

Swali zuri, mimi sio mtafiti ila natumia akili ya kawaida tu hii hii ya kuvukia barabara.

Nnavyofaham madhara yanayotokana na shughuli zetu hayana mipaka. Tunatumia ozone layer moja, huko wana viwanda na ndio maana wakaweka mkataba wa Kyoto kuhakikisha tunapunguza uharibifu wa mazingira.

Umewahi kusikia China wanawaza kuanza kutafuta sehem nyingine za kuweka viwanda kwa sababu kule hewa imeharibiwa sana na inahatarisha maisha kwa wananchi?

Sasa hapo hatujaongelea hiyo athari huko juu angani.

Ndio maana nikasema, konda msafi , smary boy anachokisema kina mantiki.
 
I may be wrong I may be right. This is just my speculation. Inaweza ikawa athari ya uharibifu wa mazingira au inaweza ikawa ndio "utungo" wa mfumo ambao dunia haijawahi kuushuhudia.

Ni jambo linahitaji uchunguzi na utafiti zaidi.

Kwa heshima na taadhima, nimwalike kaka yangu akipata muda aje atoe maoni yake. Kiranga ukipata wasaa pitia huku mkuu, mchango wako muhimu sana.

Shukrani
 
Pengine kuna cycles zinatokea baada ya miaka mingi sana you never know mleta mada una mashiko
Kabisa mkuu. Huenda kuna cycle ya karne 23 au 24 kukamilika. Sasa hivi ndio inaelekea kukamilisha mzunguko wake kwa hiyo hizi ndio dalili za mwanzo kuanza kuingia kwenye cycle mpya.
 
Kabisa mkuu. Huenda kuna cycle ya karne 23 au 24 kukamilika. Sasa hivi ndio inaelekea kukamilisha mzunguko wake kwa hiyo hizi ndio dalili za mwanzo kuanza kuingia kwenye cycle mpya.
Hivi mkuu kuna ushahidi wowote wa kipekee unaoonesha dunia kuzungika kutoka sehemu moja kwenda nyingine ?
 
Hivi mkuu kuna ushahidi wowote wa kipekee unaoonesha dunia kuzungika kutoka sehemu moja kwenda nyingine ?
Mkuu ushahidi unataka uuonaje? Usiku na mchana huuoni? Majira ya masika na kiangazi huyaoni mkuu? Huo ndio ushahidi mkuu.
 
Kwa sisi ambao tuna idea kwa mbali sana kuhusu mysteries tunajua kuna ages mbalimbali ambazo kutakuwa na mabadiliko mbalimbali.Mfano sasa hivi tuko katika age inayotawala inaitwa Age of Pisces ambayo ilianza kutawala karne kadhaa nyuma.

Ikitoka Age of Pisces tunakuja Age of Aquarius ambayo itatawala karne kadhaa na kupokewa na age nyingine.Moja ya ages ambazo zimepita zamani sana ni Age of Leo.

Hizi ages zinaenda kama vile zile alama za zodiac zilivyo ambazo zinaenda kwa miezi miezi katika 1 solar year ambayo ni miezi 12.
 
Kwa sisi ambao tuna idea kwa mbali sana kuhusu mysteries tunajua kuna ages mbalimbali ambazo kutakuwa na mabadiliko mbalimbali.Mfano sasa hivi tuko katika age inayotawala inaitwa Age of Pisces ambayo ilianza kutawala karne kadhaa nyuma...
Mkuu unaweza kuelezea japo kwa ufupi hizi ages? Na mnazijuaje?
 
Back
Top Bottom