Mkuu,
Haya mazungumzo mazuri na muhimu sana. Ni muhimu kwenda na data, but you are definitely on to something here.
Definitely kuna mizunguko mingi zaidi ya uliyotaja ambayo wanasayansi wameigundua na imeandikwa, kwa hivyo tujielimishe kwanza kuhusu hiyo iliyogunduliwa na iliyoandikwa kabla ya kuongelea sana ambayo haijagunduliwa, ambayo nayo inawezekana ipo.
Kuna mizunguko kama ya solar system kuzunguka kitovu cha galaxy hujaitaja, ingawa sifikirii kwamba hii inaweza kuwa na impact kwenye hali ya hewa.
Sijaona ukitaja mambo kama ice ages. Kama hujazisoma hizi, anza kusoma zaidi hapa
Ice age - Wikipedia
Kuna mambo mengine hata si mizunguko per se, ila mambo kama sunspots, yani, maeneo ya jua ambayo yanakuwa na joto la chini na kusababisha imbalance katika nishati ya jua tunayoipokea, na hivyo kuweza kusababisha baridi sehemu ambazo hatujazoea.
Kama hujasoma zaidi kuhusu sunspots ona
hapa .
Kwa hivyo kuna mambo mengi ya kujifunza.
Ila, kuna mjadala mkubwa kuhusu climate change na jinsi gani inasababishwa na shughuli za watu kama vile kukata miti, kuongeza hewa za Carbon kwenye hewa yetu, na mambo mengine mengi kama hayo. Kuna watu wanasema mabadiliko haya ya hali ya hewa kwa kiasi kikubwa yanatokana na shughuli za watu, na watu wanaweza kubadili muelekeo huu kwa kubadili maisha yao, kuacha kukata miti na kupanda miti zaidi, kuacha kutumia vibaya nishati na kupunguza utoaji wa Carbon kuipeleka kwenye hewa yetu. Na kuna wanaosema kuwa mabadiliko haya yanatokana na mabadiliko ya asili zaidi kama hizo ice ages na sunspots, mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu kuyabadilisha.
Kwa sasa, ushahidi mwingi wa kisayansi, pamoja na wanasayansi wengi wasomi, wanakubali kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanasababishwa na maisha ya watu, si mambo ya kiasili, na tuna muda mchache sana wa kuzuia na kusahihisha mabaya haya yanatotokana na matumizi mabaya ya nishati. Wanasayansi wasomi wa mambo haya wanaokubali hivi ni wengi kuliko wanaokubali kwamba haya ni matokeo ya mizunguko na mambo ya kiasili tu.
Labda kwa sasa niseme hivi kama sehemu ya kuanzia tu, halafu, tuweze kupata chachu zaidi ya kuendeleza mjadala kuanzia hapa.
Shukurani
The Monk kwa heshima kubwa ya mualiko hapa.