Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Kibaha! Hali ya hewa ni nzuri!
Ni sehemu nzuri, napapendea kitu kimoja kuna mchanganyiko wa makabila mbali mbali!
Hakuna uswahili uswahili!
Nafikiri hapo point kubwa ni hali ya hewa. Swala la mchanganyiko wa makabila nafikiri hata Chanika lipo au vipi mkuu?
 
Kijana anataka kuwachungulia wenye mji wao machoni πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hio ni Trend tu ila kukaa 90kms from City centre ni Ujinga wa aina yake.
Du klm 90 from City centre, hapo si unakuwa unaishi msata huko, yani sio Dar wala Kibaha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kuna watu wanadai Chanika usafiri mpaka uwe mtu wa kuamka mapema yani kuanzia saa 11 hadi saa 1 ya asubuhi. Ukifika kituoni kinyume na hapo basi utarajie kuchelewa zaidi ndani ya basi kwa sababu ya foleni.
CHANIKA foleni Iko upande Gani SHEKHE mbona tunapanda daladala muda wote ma bus yapo
 
CHANIKA foleni Iko upande Gani SHEKHE mbona tunapanda daladala muda wote ma bus yapo
Mkuu kama nlivyokwambia hapo juu kuwa nasikia tu kutoka kwa watu. Mimi sio mwenyeji wa huko na wala sina ndugu maeneo hayo, hivyo badala ya kuniuliza nilitarajia ungenipa maelezo ya kutosha ili kunithibitishia kuwa yale nilioyasikia hayana ukweli wowote.

Asante sana πŸ™
 
Nitachagua Chanika, ni mojawapo ya maeneo yanayokua sana kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu na makazi, itafika kipindi Chanika ataweza kuipiku Gongo la Mboto na kuwa na huduma zote muhimu

Kwa sasa wamefika mbali sana na uwepo wa barabara ya lami mpaka huko ni jambo ambalo limesababisha kuwa sehemu potential sana, maana maendeleo ni watu
 
Hapo kama ni fursa ya kuchagua japo viwanja viwili basi nitachagua kwanza kibaha alafu cha pili kitakuwa cha bagamoyo.

Huko chanika na vikindu yake kuna wafaa waswahili kama kina kingwendu nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…