Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Kibaha! Hali ya hewa ni nzuri!
Ni sehemu nzuri, napapendea kitu kimoja kuna mchanganyiko wa makabila mbali mbali!
Hakuna uswahili uswahili!
Nafikiri hapo point kubwa ni hali ya hewa. Swala la mchanganyiko wa makabila nafikiri hata Chanika lipo au vipi mkuu?
 
Unagongwa na vigagula wewe, Tabata maeneo yake mengi tu yamepimwa. Tuna nyumba ipo kwenye mipango miji from 1980s. Hio Tabata unayosemea squatter ni ile ya nyuma ya Mawenzi kunaitwa Upogoroni kushuka hadi mwananchi pamoja na maeneo yanyopakana na bonde la mchicha.
Kijana anataka kuwachungulia wenye mji wao machoni 😂😂😂
 
Kuna watu wanadai Chanika usafiri mpaka uwe mtu wa kuamka mapema yani kuanzia saa 11 hadi saa 1 ya asubuhi. Ukifika kituoni kinyume na hapo basi utarajie kuchelewa zaidi ndani ya basi kwa sababu ya foleni.
CHANIKA foleni Iko upande Gani SHEKHE mbona tunapanda daladala muda wote ma bus yapo
 
CHANIKA foleni Iko upande Gani SHEKHE mbona tunapanda daladala muda wote ma bus yapo
Mkuu kama nlivyokwambia hapo juu kuwa nasikia tu kutoka kwa watu. Mimi sio mwenyeji wa huko na wala sina ndugu maeneo hayo, hivyo badala ya kuniuliza nilitarajia ungenipa maelezo ya kutosha ili kunithibitishia kuwa yale nilioyasikia hayana ukweli wowote.

Asante sana 🙏
 
Nitachagua Chanika, ni mojawapo ya maeneo yanayokua sana kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu na makazi, itafika kipindi Chanika ataweza kuipiku Gongo la Mboto na kuwa na huduma zote muhimu

Kwa sasa wamefika mbali sana na uwepo wa barabara ya lami mpaka huko ni jambo ambalo limesababisha kuwa sehemu potential sana, maana maendeleo ni watu
 
Niaje waungwana,

Kama swali linavojieleza hapo juu, ukiambiwa uchague sehemu moja tu ya kujenga kwa ajili ya makazi kati ya Chanika, Kibaha, Vikindu na Bagamoyo ila kiwanja unapewa bure.

Ndugu muungwana hebu tuambie utachagua kujenga na kuishi wapi? Na kwanini?
Hapo kama ni fursa ya kuchagua japo viwanja viwili basi nitachagua kwanza kibaha alafu cha pili kitakuwa cha bagamoyo.

Huko chanika na vikindu yake kuna wafaa waswahili kama kina kingwendu nk.
 
Back
Top Bottom