Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?


Kibaha kuna miradi mikuu minne hadi sasa.

1. Upanuzi wa Barabara ya Morogoro kuwa njia nne hadi Morogoro. Awamu ya kwanza ni Kibaha-Chalinze.

2. Ujenzi wa barabara ya kulipia kutoka Kibaha hadi Morogoro.

3. Ujenzi wa SGR ambao upo tayari na sasa bado kidogo treni inaanza kazi.

4. Kuna miradi mingine ya barabara za kuunganisha Kibaha na Bagamoyo, Masoko, Viwanda, na upimaji wa ardhi kiasi cha ekari 4000 kwa ajili ya kurasimisha makazi katika eneo la Halmashauri ya Mji Kibaha.

Kumbuka Wilaya ya Kibaha ina jumla ya halmashauri mbili; Halmashauri ya Mji Kibaha yenye kata 14 zikiwemo Kibaha, Kongowe, Maili Moja, Picha ya Ndege, Pangani, Mkuza n.k, na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha yenye kata 14 pia.

Kwenye hizi halmashauri kuna makampuni binafsi yanapima na kuuza viwanja na yote haya yanafanyika kwa kushirikiana na halmashauri.

Miradi yote hii inafahamika siyo tu na Halmashauri bali pia hata Serikali Kuu inatambua.

Sasa hoja kwamba kutakuja kubomolewa ni dhaifu sana.

Hiyo Vikindu ya Mkuranga. Mimi ninadhani ni muendelezo wa maisha ya Mbagala. Ninapajua vizuri na nimeenda hadi huko ndani. Hata hiyo Bagamoyo itapishana na Vikindu kidogo sana.
 
Wanaokwambia hivyo wauliza Kibaha ipi, wakikutajia Maili moja basi sawa, kinyume na hapo Kibaha ni kubwa sana na bado ni ile ile...
Kumbe Kibaha kumekucha baadhi ya sehem tu 😀😀😀
 
Asante.. nakuja haraka sana pacha wangu
 
Kwangu mimi nafikiri hapa umejibu na kufafanua vizuri sana.
 
Wanaokwambia hivyo wauliza Kibaha ipi, wakikutajia Maili moja basi sawa, kinyume na hapo Kibaha ni kubwa sana na bado ni ile ile...
Kata ya Maili Moja ipo Halmashauri ya Mji Kibaha na eneo kubwa limepimwa kwa ajili ya viwanda na miradi mikubwa ya serikali.

Hata kama kuna viwanja siyo affordable sana.

Uwekezaji kwenye ardhi ni mbinu, na ili uwekezaji huo uwe na faida unatakiwa upate faida ndani ya miaka isiyozidi mitano (5).

Sasa je, kwa vyovote iwavyo, mtu akinunua ardhi Kibaha sasa hivi baada ya miaka mitano hapati faida?

Faida ya kumiliki eneo Kibaha ni kubwa kuliko hasara.
 
Acha kuifananisha Bagamoyo na vitu vya ajabu.
 
Vikindu kumekucha wazeee acheni kukariri maisha
2021 nilinunua kiwanja Tshs laki 8.

Sasa hivi viwanja vinauzwa laki 6.

Halafu vinapimwa kwa futi.

Niliuza baada ya kuona nyumba za uswazi zinashamiri kunizunguka. Na msikiti ukajengwa jirani na kwangu.

Kama ni Mswahili, ni kweli pamekucha ila kwa mtu mpenda ustaarabu; hapana, hapamfai!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…