Kindeena
JF-Expert Member
- Sep 27, 2017
- 11,462
- 21,124
Naiona bomoabomoa kibaha Miaka 25 ijayo.
Sabb mji ule unatawaliwa na matamanio ya kuishi watu wengi.
Hapa nielewe wewe huwez kuitunishia pesa. Watawaondoa tu. Watasongizia factory zone na madudekibao.
Vikindu na Bagamoyo inategemea na City master plan.
Kibaha kuna miradi mikuu minne hadi sasa.
1. Upanuzi wa Barabara ya Morogoro kuwa njia nne hadi Morogoro. Awamu ya kwanza ni Kibaha-Chalinze.
2. Ujenzi wa barabara ya kulipia kutoka Kibaha hadi Morogoro.
3. Ujenzi wa SGR ambao upo tayari na sasa bado kidogo treni inaanza kazi.
4. Kuna miradi mingine ya barabara za kuunganisha Kibaha na Bagamoyo, Masoko, Viwanda, na upimaji wa ardhi kiasi cha ekari 4000 kwa ajili ya kurasimisha makazi katika eneo la Halmashauri ya Mji Kibaha.
Kumbuka Wilaya ya Kibaha ina jumla ya halmashauri mbili; Halmashauri ya Mji Kibaha yenye kata 14 zikiwemo Kibaha, Kongowe, Maili Moja, Picha ya Ndege, Pangani, Mkuza n.k, na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha yenye kata 14 pia.
Kwenye hizi halmashauri kuna makampuni binafsi yanapima na kuuza viwanja na yote haya yanafanyika kwa kushirikiana na halmashauri.
Miradi yote hii inafahamika siyo tu na Halmashauri bali pia hata Serikali Kuu inatambua.
Sasa hoja kwamba kutakuja kubomolewa ni dhaifu sana.
Hiyo Vikindu ya Mkuranga. Mimi ninadhani ni muendelezo wa maisha ya Mbagala. Ninapajua vizuri na nimeenda hadi huko ndani. Hata hiyo Bagamoyo itapishana na Vikindu kidogo sana.