Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Kata ya Maili Moja ipo Halmashauri ya Mji Kibaha na eneo kubwa limepimwa kwa ajili ya viwanda na miradi mikubwa ya serikali.

Hata kama kuna viwanja siyo affordable sana.

Uwekezaji kwenye ardhi ni mbinu, na ili uwekezaji huo uwe na faida unatakiwa upate faida ndani ya miaka isiyozidi mitano (5).

Sasa je, kwa vyovote iwavyo, mtu akinunua ardhi Kibaha sasa hivi baada ya miaka mitano hapati faida?

Faida ya kumiliki eneo Kibaha ni kubwa kuliko hasara.
Asante ndugu kwa ufafanuzi huu
 
Vikindu poa sana.
Karibu mkuu, utakukubali tu.
Ingawa suala la kiwanja bure sidhani kama lipo miaka hii.
Niaje waungwana,

Kama swali linavojieleza hapo juu, ukiambiwa uchague sehemu moja tu ya kujenga kwa ajili ya makazi kati ya Chanika, Kibaha, Vikindu na Bagamoyo ila kiwanja unapewa bure.

Ndugu muungwana hebu tuambie utachagua kujenga na kuishi wapi? Na kwanini?
 
2021 nilinunua kiwanja Tshs laki 8.

Sasa hivi viwanja vinauzwa laki 6.

Halafu vinapimwa kwa futi.

Niliuza baada ya kuona nyumba za uswazi zinashamiri kunizunguka. Na msikiti ukajengwa jirani na kwangu.

Kama ni Mswahili, ni kweli pamekucha ila kwa mtu mpenda ustaarabu; hapana, hapamfai!
😂😂😂😂
 
Niaje waungwana,

Kama swali linavojieleza hapo juu, ukiambiwa uchague sehemu moja tu ya kujenga kwa ajili ya makazi kati ya Chanika, Kibaha, Vikindu na Bagamoyo ila kiwanja unapewa bure.

Ndugu muungwana hebu tuambie utachagua kujenga na kuishi wapi? Na kwanini?
Vya bure sio vizuri/salama 😅 Ila Kibaha ni pazuri zaidi
 
Back
Top Bottom