Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Kama ulivyosema kuwa kila mwamba ngoma ngozi huvilutia kwake. Wengi wapendekaeza tu eneo bia kutoa sababu za msingi.
Ila mkuu kuchagua mahali au eneo kunatokana na hitaji au lengo kuu. Mimi naamini katika michango ya watu hapa nadhani kuna iliyogusa lengo lako.
Yuko mmoja ambaye nadhani amechanganua kila maeneo bila upendeleo akielezea uzuri na ubaya wa kila eneo. Huyu amemaliza kila kitu. Kazi kwako.
Sasa katika malengo yako angalia wapi panafaa kutokana na ufafanuzi alioeleza.
Kila la heri. Ila karibu Vikindu, hutajuta.
Asante ndugu yangu
 
Kwani wasiokuwa Waswahili wanakaa wapi?
Humu JF Kila mtu mambo safi!
Sinza yote ni full squatter, Magomeni, Temeke Buguruni, Tabata yote haijapimwa..

Niambieni nyie mnakaa wapi kusikokuwa na uswahilli, hakuna misikiti, watoto hawalii!

Au mnajenga humu humu mitandaoni?

Shenzy typ!
 
Ok kumbe ni huko hamna shida cha msingi uhakika wa mbususu upo, hospital ipo sehemu za kulala wageni zipo na pia nikifanga kosa la jinai jela ipo. Vipi kuhusu mafuriko lakini?
Ukiangalia kwenye taarifa nzima ya habari chanika ndio mahali hapajaripoti mafuriko ukilinganisha na maeneo mengine yes kuna baadhi ya maeneo machache sana yalipata maji e.g jirani na Nermat hotel
 
Kama ni BAGAMOYO ni chaguo sahihi kwenu,basi msisite kufika katika kampuni yetu ya PMG and ASSOCIATE Co.ltd kupata fursa ya viwanja vilivyopimwa na kupangwa kwa matumizi mbalimbali.
Kwa maelezo zaidi piga simu 0674376678
 
1. Bagamoyo - kuanzia mapinga mpaka Kiromo, hapa kiromo ndio kuna special economic zone, na bandari- kwa sasa usivuke round about, labda kwa uwekezaji wa baadaye, bagamoyo mjini waachieni wazawa

2. Kibaha
 
Kwanini?

Sehemu zinazopimwa kwa futi hata siyo pa maana.

Eneo la mita 20 kwa mita 20 mnajikuta mpo watu wawili.

Kiwanja kimoja kinapimwa futi 50 kwa 40 maana yake ni mita 12 kwa 17 chenye mita za mraba 204 wakati cha mita 20 kwa mita 20 kina ukubwa mita za mraba 400.

Hali kama hiyo ipo eneo lote la Wilaya ya Temeke (Mbagala ikiwemo), Homboza, Mkuranga-Vikindu, Kisemvule, na mikoa ya Kusini.
O
Kinachokuja hapo ni uswazi na vijumba vichafu.

Waswahili hawana utamaduni wa kujenga vyoo bora kwa hiyo hata ukijenga chako kizuri bado mtaa utakuwa mchafu na wewe utakuwa mchafu tu.
Sio Kwa CHANIKA broo
 
CHANIKA mbona Bomba MBAYA
Chanika ni ndugu wa Mvuti, Homboza, Mabagala, Vikindu na Kisemvule uswahili mwingi ustarabu kidogo.

Huwezi kulinganisha na Goba, Madale, Mbopo, Bunju na Kibaha. Mimi ni muumini wa Dar es Salaam Kaskazini-Magharibi ila huko Kusini-Mashariki kuanzia Chanika hadi Mtwara aisee hapana!
 
Niaje waungwana,

Kama swali linavojieleza hapo juu, ukiambiwa uchague sehemu moja tu ya kujenga kwa ajili ya makazi kati ya Chanika, Kibaha, Vikindu na Bagamoyo ila kiwanja unapewa bure.

Ndugu muungwana hebu tuambie utachagua kujenga na kuishi wapi? Na kwanini?
Tunajadilije hoja ya kufikirika ambayo kiuhalisia haitakuja kutokea kuwepo?

Hata nikijitamanisha kuchagua ni nini kitaninufaisha na uchaguzi wangu huo?
 
Labda Bagamoyo mjini lakini siyo mjini Daslam

Nina jamaa yangu anaishi Bunju Shule leo kutwa amelalamika maumivu ya mgongo na miguu baada ya kukaa kwenye Eicher 2 hours sababu ya foleni za hiyo barabara,yaani bisha utakavyobisha Morogoro Road haina mpinzani bro.
Siyo kweli, bunju mpaka mwenge huwezi kutumia masaa mawili
 
Sikatai lakini kwa Chanika hizo ni bei za heka siyo bei za viwanja vya kibiashara.

Mf;Kariakoo kiwanja 30x25 ni 1bill+ wakati hiyo hiyo B ukienda nayo Kibaha unanunua kijiji,na mil 20 ya Chanika Kibaha au Bagamoyo utapata 40x40.
Hizo bei za chakx nilizo kutajia ni maeneo ya biashara, halafu usifananishe karikoo cha chakx
 
Back
Top Bottom