Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Niaje waungwana,

Kama swali linavojieleza hapo juu, ukiambiwa uchague sehemu moja tu ya kujenga kwa ajili ya makazi kati ya Chanika, Kibaha, Vikindu na Bagamoyo ila kiwanja unapewa bure.

Ndugu muungwana hebu tuambie utachagua kujenga na kuishi wapi? Na kwanini?
Hivi hili nalo linahitaji debate kweli.

Kulinganisha kibaha na hao wengine wote kwa miaka ya sasa atafanya mtu ambae hatumii morogoro road, na morogoro road ndio barabara kuu ya nchi hii
 
Mimi bagamoyo na ukanda wake naona kama kumekaa kushoto hivi, yaani ni kama sehemu ya wachawi wachawi hivi! Kibaha nako kumekaa kimkoani mkoani hivi!
Chanika nayo imekaa kiswahili Swahili hivi, kwa ufupi mbagara ya baadae.

Walau Vikindu naweza kuweka boma langu!
Wengine wanapaponda vikindu wengine wanapasifia vikindu 😂😂
 
Soma alama za nyakati, katika mkoa wa Pwani, Kibaha ndio kuna muelekeo zaidi. Future iko huko, hakuna uswahili uswahili.
Wewe ishi kote, lakini miji yenye ngome za kiswahili swahili hapakufai kukimbilia kuweka makazi ya kudumu.
Kwanini uwakimbie waswahili wenzako mkuu, au unaogopa kibebeshwa kishipa? 😂😂😂
 
Back
Top Bottom