Ukichelewa kuoa hadi miaka 40 utapata shida kumpata mwanamke utayendana naye

Jibu rahisi sana wanawake ni wengi kuliko wanaume kifupi tinaweza kuoa wanawake watatu na tusiwamalize.

Kama tuna pool kubwa hivyo ya wanawake unafikiri wanawake bora hawapo?
Ni kweli wanawake ni wengi kuliko wanaume lakini kupata mwanamke wa ndoto yako au unaendana nae ni ngumu sana kwa sababu.....

Sio kila mwanamke anaweza akawa tiyali kuvaa viatu vyako na sio kila mwanamke anaweza akakupenda jinsi ulivyoooo
 
Kuna imani flani imejengeka kwa vijana wenye umri kuanzia 25-35 kwamba mwanaume umri wowote anaweza kuoa hata akichelewa hamna shida ataoa it's true kuoa mwanaume lakini kupata mwanamke wa ndoto yake ni ngumu sana
Tafuta Hela acha ndoto za Alinacha.Kuna Mabinti wabichi tu age ya 22 to 25 wanajielewa na ni waaminifu tena sana.na Watu wenye age ya 40+ Wanaishi nao Kwa furaha na Mahaba Mazito kama maziwa yasiowekwa maji🥰🌷Kikubwa ni Hela ya kumtunza, ata hao 40+ Ladies awawezi ishi na mwanaume Kapuku asie na pesa. Kikubwa Pesa za kumtunza

Tupe connection mkuu.....si unajua connection ndo kila ktu Karne hii.
 
Ni kweli wanawake ni wengi kuliko wanaume lakini kupata mwanamke wa ndoto yako au unaendana nae ni ngumu sana kwa sababu......

Sio kila mwanamke anaweza akawa tiyali kuvaa viatu vyako na sio kila mwanamke anaweza akakupenda jinsi ulivyoooo
Si kila mwanamke ila wapo na wengi sana, vijana wengi wanakwama kwasababu wanatafuta mwanamke huku wakiongozwa na hisia nyingi za ngono na mvuto wasura tu matokeo yake wanafikiri wamepata mke wa ndoto zao za maisha kumbe wamepata wa ndoto zao za usiku.
 
Kuna imani flani imejengeka kwa vijana wenye umri kuanzia 25-35 kwamba mwanaume umri wowote anaweza kuoa hata akichelewa hamna shida ataoa it's true kuoa mwanaume lakini kupata mwanamke wa ndoto yake ni ngumu sana
Usichokijua ni kwamba mwanamke akishavunja ungo anauwezo wa kuishi na mwanaume wa rika lolote na wakaendana kifikra na matendo.

Key point.

Huwajui wanawake.
 
Hizi ndiyo sababu zinazosabisha watu wanaangukia pua kwenye kuoa.

Mtu anafanya jambo kwa kufuata mkumbo na hamasa kutoka kwa ndg na jamaa matokeo yake anapalamia mtu ambae hakua fungu lake kwa ndg zangu waislam wanaoa kwaajiri ya ngono tuu hukuna kingine Cha ziada
 
Tupe connection mkuu.....si unajua connection ndo kila ktu Karne hii

Rahisi sana, Kwanza jitambue wewe ni mtu wa aina gani katika yale makundi ya aina ya watu, Malezi yako, Hali ya Maisha yako, Elimu yako, Matajario yako, hisia zako zikoje, Mapendezi yako yakoje, Ukisha jitambua wewe mwenyewe utatafuta couple inayokufaa, haitaongozwa na hisia na sura tu unapomchagua

Wanawake wanapatikana wapi?

Ujirani, Kanisani, Msikitini
Taasisi za elimu, Kazini
Kwa wajomba, kwa babu na bibi, shangazi, kwa shemeji yako, kwa washikaji zako, washikaji wa washikaji zako, kwenye sherehe, kwenye sehemu za starehe every where sasa ikiona una kosa mke wa kariba yako maeneo yote hayo ujue kuna shida mahali.
 
Mitandaoni mbna hujataja mkuu..!!
 
Kuna imani flani imejengeka kwa vijana wenye umri kuanzia 25-35 kwamba mwanaume umri wowote anaweza kuoa hata akichelewa hamna shida ataoa it's true kuoa mwanaume lakini kupata mwanamke wa ndoto yake ni ngumu sana
Na ss tusioa kbs je..
 
Hizi tafiti zako umezitoa wapi...
Unaleta habari za kufikiria baada ya kupata story mbili tatu za mahusiano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…