InvisibleTarget
JF-Expert Member
- Dec 20, 2014
- 1,138
- 2,176
...nakubali mkuu. Wengi wanajidanganya na mapenzi ya kukutana mnakula raha bythen jioni au kesho yake kila mmoja anarudi kwake au kwa wazazi wake ,wanakaa hivyo kwa mwaka au miaka miwili mwisho wa siku wanajiona wanatosha kuishi pamoja bila kujua 99% ya vipimo vyao kuwa watawezana wameifanya pindi wakikutana kwenye raha tu...Mbungi inaanza wanapolala pamoja ,kuamka pamoja,kula pamoja, kuwa ndani ya ratiba flani automatically otherwise utoe taarifa n.k hapo ndipo wanapokuja kujua true color ya kila mmoja na issue inakuja kwenye kujibadili ili uendane na mwenzio alivyo na kwa hili bila hekima ya mwanamke hawatoboi.!Ndoa inaundwa na watu wawili na lazma muwe mmejuana inside out.
Hakikisha mwanamke wako anayajua madhaifu yako na wewe unayajua yake kisha ndio mfanye maamuzi sasa ya kuoana. Ikiwa hutayajua madhaifu ya mwenza wako basi ujue ndoa yenu ikimaliza miezi 6 bila mgogoro Mungu anawapigania.
Shida nayoiona wengi huwa tunagubikwa na fantasies na kusahau kuwa ndoa ni uhalisia. Ndoa sio maigizo hivyo kila mtu lazma awe real na mwenzake.