KERO Ukienda Polisi kuwataka watrack Simu iliyobiwa, bila Pesa hufanikiwi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kama mtu kajinyonga tu lazima ujaze mafuta magari Yao

Sembuse simu
 
Potezea tu wajanja wapate ulaji hao walioiba.

Mtu anatrack simu akijua kuna vitu vingi amepoteza au anatakua kuconfirm mwizi aliyemuibia tu.

Tangia nianze kutumia simu 2003 sijawahi kupoteza ,huwa zinaharibika au nauza na nikinunua nakaa nayo hata miaka 7 kwasababu nanunua ikiwa mpya kabisa.
 
kweli, ila kama Kazi yangu ingefanyika ningewalipa hiyo 100,000. ila hapo kuna kupoteza simu na laki moja pia itapotea polisi sio mtu wa kumuamini hata mara moja, wanakula uku na uku.
usiwape hao pesa kwa maana wanaweza kuifatilia simu yako wakaipata na wakamtingisha waliyomkuta nayo then wakampiga pesa na wewe simu yako wasikurudishie,tena ukiwapa evidence kama IMEI na vingine hata kama hauifatilii wao wanaifatilia unakuwa ulaji wao
 
kama uko Dar nenda pale Ilala sokoni jengo la NSSF nadhani ni ghorofa la 6 kuna wajamaa wanatrack simu,mnaingia mkataba kiofisi kabisa na wanakupa muda na kama haijapatikana kuna refund ya asilimia flani,wanaitwa wetrack
 
Wanaiweza na pia ni wajibu wao lakini madai ya rushwa kwenye jeshi la polisi limekuwa ni tatizo sugu hasa kwa wananchi wenye kipato kidogo na wasio na ushawishi kwenye jamii yetu.
Wanajilipa pensheni mapema. Pensheni zao siku hizi nasikia ni 12m
 
Na ukisha aapa pesa wana kufanya ATM 🏧 Leo wata kuambia ina soma mahali fulani, tupe pesa ya mafuta kesho wata kuambia ame hamia mnara mwingine. Shida sana hawa watu
 
Swala la ku track simu ni kuwapelekea ulaji wale jamaa watakutoa hela na unaweza usiipate, ni bahati sana ukutane na mwenye integrity na kazi yake.

Miaka ya nyuma kidogo nilijichanganya mitaa fulani ya sokoni kumbe vibaka wanataget ka simu kangu mara chap simu imechomolewa mfukoni.

Kuna mhuni nilikuwa nafahamiana nae pale sokoni nilifanya kumtafuta na kumueleza anisaidie niipate ile simu, ebana kesho yake nilipewa taarifa hao vibaka waliwajua na wamewakamata, kwenda nakuta wamewapiga ile mbaya wapo na simu wananiomba msamaha kweli kweli, kuiangalia vizuri haikuwa simu yangu kudadadeki nikamwambia mchizi wafundishe adabu afu mimi nakuachia hiyo simu utajua utafanyaje maana sio yangu, hiyo ni shukrani yangu kwako.
 
Tafuta hela, hakuna simu ya laki 2
 
Bora wewe umesema
Na nilitaka kuongezea ya kuwa polisi hawana huo mfumo wa kutrack simu, ni ukanjanja tu, ni wewe mwenyewe ufatilie kama iPhone Find My Phone, siku ukijua iko wapi ndio umlipe 5000 ya bodaboda akakukamatie
 
Wengi humu wanasema police hawana hyo software ya kutrack simu kujua ipo wp sasa ww ukitaka udhibitisho kuwa wanayo au hawana hyo program nenda kwenye Instagram account ya mheshimu waziri yoyote halafu utoe maneno ya kashfa baada ya siku moja tu utapata jibu kama unaweza kujulikana upo wapi
 
Ukiibiwa kama hawajakudhuru kausha, Polisi wana mambo mengi
 

mmetishwa sana mmekuwa waoga, sana,
Kama simu yako unajiandikisha na kitambulisho chako, halafu unaweka picha yako kwenye insta, kwanini wasikukamate kirahisi halafu mnadanganywa wanamfumo wa kutrack simu wakati hata wewe unaweza kufanya hivyo kwenye mifumo kibao imejaa mitandaoni

 
[emoji23][emoji23]
 
Na wakati mwingine unaweza kutoa hiyo hela ikaliwa na usisaidiwe
 
Inategemea sasa unatumia device gani kwenda istagram mzee, kama unatumia computer yenye linux na ina browser ya tor na una vpn ipo on na ukawa unatumia proxy server ni ngumu hawawez kujua ulipo, ndio mana watu wengine wanaendaga tu kuwatukana hao viongozi kwenye page zao. Sio kila mtu anaetumia instagram and the likes anatumia simu
 
naomba msaada wako, ndugu yangu kama unaweza nikutanisha na huyo jamaa na Maana huyu polisi niliepewa mpelelezi wangu naoana kila siku kiswahili longo longo kibao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…