Unique Flower
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 12,838
- 25,282
Watoto huwa hawatabiriki, kuna wapole na kuna watundu kupitiliza. Hiyo miaka 3 mpaka 5 ndiyo hapo utundu umekolea kabisa.Nimekuja mkoani kumtembelea bradha. Kuna mzigo aliniagiza nimletee. Hapa kwa bro kuna mtoto wao wa kiume ana umri kama miaka minne au tano hivi. Asee, hiki kitoto ni kitundu sijapata ona. Mbaya zaidi, babaake na mama yake wanamlea kama yai, full kudeka-deka hovyo.
Hapa Sana mkuu,Yaani nimecheka Kama mazuri vile😂Fanya shambulizi la kimya kimya hakuna haja ya kushika fimbo.
Shika mkono vizuri kwenye msuli(hawezi kua na msuli) binya na dole gumba kwa nguvu kiasi utakutana na mfupa, kandamiza kama sekunde 10 hivi uone kama katarudia
Kuna vitoto Ni vitundu kupitiliza sidhani Kama haya uliyoeleza yanaweza kusaidia kitu.Usimpige bwana mpe kitu chakufanya muulize hata homework yake msaidie kanahitaji upendo kama kamekupenda Katoe hata out umpe juice na umpeleke akachezee na wenzake kwenye michezobumkanye akifanya kitu kiupole , mie nisingempiga ningempaka kazi anaakili sana so anataka uwe unanpa majukumu ukinywa kitu mwite anywe mpe achezee , na vitu Fulani, cheza naye mpiraa usikachukie Bhana
Wala kukazaba toka kwao kachukue room huyu ni mtoto wa watuKuna vitoto Ni vitundu kupitiliza sidhani Kama haya uliyoeleza yanaweza kusaidia kitu.
Suluhisho pekee Ni kukazaba vibao
Kwanza hapo mwenyeji wangu anatakiwa anishukuru Sana kwa kumfundishia mwanaye adabu.Wala kukazaba toka kwao kachukue room huyu ni mtoto wa watu
ulemavu ,sio sindano hiyo m-binyo TU huoLooh! Ukatili gani huo?
Akimtia ulemavu mtoto!?
Nyie wanaume mnashida gani lakini? Mbona mnakua makatili kila sehemu!
Kunamtu alikuwa ananitisha sana ili nimkimbie , anasema eti yeye anakulaga watu masikio na anaweka chumvi kabisa anayala kama nyama Tena amesema anakata na kakisu kadogo ananionyesha kabisa analamba kwanza anasafisha ndio anachoma kwenye moto mkali anaweka chumvi anakula weh nilisepa sijawahi Kuja hapo sebuleni hata kumsalimia .Kwanza hapo mwenyeji wangu anatakiwa anishukuru Sana kwa kumfundishia mwanaye adabu.
[emoji1][emoji3][emoji1][emoji3][emoji3][emoji3] daaaa aiseWatotot dawa yao makwenzi ya kwenye mifupa ya bega.. harudii tenaaa.. ikimuingia kisawa sawa anakaa na wewe mbali kama ukoma
Ulikuwa na umri gani wakati huo?Kunamtu alikuwa ananitisha sana ili nimkimbie , anasema eti yeye anakulaga watu masikio na anaweka chumvi kabisa anayala kama nyama Tena amesema anakata na kakisu kadogo ananionyesha kabisa analamba kwanza anasafisha ndio anachoma kwenye moto mkali anaweka chumvi anakula weh nilisepa sijawahi Kuja hapo sebuleni hata kumsalimia .
4 years oldUlikuwa na umri gani wakati huo?
4 years old
Eh sana nauliza maswali , umekuja kwetu kufanya Nini , kwako je umewaacha nani , unakaa siku ngapi, je umenileta zawadi gani??nishawahi mwambia unajua chai ya maziwa ??unajua mkate ?? Walahi hata akinywaa soda na mwangalia akiinywaUnaonekana ulikuwa mtundu Sana ndo maana jamaa alikuwa anakuchimbia mikwara ili umuogope😂
Duh! Ulitisha Sana jamani4 years old
Eh sana nauliza maswali , umekuja kwetu kufanya Nini , kwako je umewaacha nani , unakaa siku ngapi, je umenileta zawadi gani??nishawahi mwambia unajua chai ya maziwa ??unajua mkate ?? Walahi hata akinywaa soda na mwangalia akiinywa
Acha tu mama na baba walinishindwaa wakiona ni mgeni wa heshima wananifungia chumbani nakaa Huko hadi aende halafu natolewa nilikuwa keroo mara ingine naliaDuh! Ulitisha Sana jamani
Maisha ya ugenini Yana uunafiki hii kauli naafikiana na wewe mkuu maisha ya ugenini mtihani sana huna uhuru, Kuna siku nimeenda kwa mmoja ktk ndugu zangu ana watoto wawili , huyu wa mwisho mara ya mwisho kumuona alikuwa mdogo sana hivyo safari hii nilivyoenda nikakuta watoto watatu mkubwa namfahamu ila wapili nilishindwa kutokana kulikuwa na mwingine hivyo nikashindwa kutofautisha.Nimekuja mkoani kumtembelea bradha. Kuna mzigo aliniagiza nimletee. Hapa kwa bro kuna mtoto wao wa kiume ana umri kama miaka minne au tano hivi. Asee, hiki kitoto ni kitundu sijapata ona. Mbaya zaidi, babaake na mama yake wanamlea kama yai, full kudeka-deka hovyo.
Sasa ni heri wangekuwa wanamlea hovyo, akawa anawasumbua wenyewe ingekuwa hakuna shida, ila akiwa na wenzake ni kakorofi, kanawapiga wenzake. Nimejilipua zangu fulana kutoka kwa vunja bei. Ameshaitanua shingo kwa kunivuta-vuta. Imekuwa kama nanyonyesha sasa. Mara aninyang'anye simu, mara aniparamie usoni kama mbwa, alafu ana vikucha vikali.
Basi naishia kujichekesha chekesha tu mbele ya mama yake. Maisha ya ugenini yana unafiki sana. Wazazi wake wala hawastuki, wanaona poa tu mtoto wao anavyo act kama kingedere. Mamaake ananiambia 'shemeji kama junia anakusumbua mchape.' Namchapaje mtoto wa watu ugenini? Kwa nini asimkataze kusumbua wageni na kukachapa kakiendelea kuleta ubishi.
Sasa mamaake akaenda dukani akaniacha na junia tunavutana-vutana. Happy ndiyo nikambadikilia, nikamwonyesha sura ya ukauzu na kumtoa shingoni maana ilikuwa kama ananidai kwa jinsi alivyokuwa ananikaba. Nikakashika mikono na kukaminya tu vidole vyake kama naminya karanga, huku namwambi acha utundu kwa wageni mtoto. Kakaanza kulia kanaelekea dukani kwa mamaake.
Maisha ya ugenini magumu sana. Nilipanga kukaa siku mbili, ila moja tu inatosha kwa kweli. Wazazi wengine hivi mnaleaje watoto kipuuzi kama hivi? Katoto ni ka-attention seeker. Mpo katika maongezi sebuleni, kenyewe kanapita-pita na kuvuta watu nguo, ili mradi tu kaonekane kapo live. Mkikapotezea, kataangusha hata glass!
Inaonenana wanaume walikufanya jambo baya sana NYUMA uko lakini siku zijazoHalafu huyo mtoto wala sio mtukutu ila yupo excited kumuona Anko wake ndio maana anampandia pandia kwa furaha ila kwa kua watu mmejazwa roho mbaya na ukatili hata furaha ya watoto mnaigeuza chuki,
Hii gender ya Kiume ingeteketea tu [emoji849]
[emoji1787]
Shambulizi [emoji1787]Fanya shambulizi la kimya kimya hakuna haja ya kushika fimbo.
Shika mkono vizuri kwenye msuli(hawezi kua na msuli) binya na dole gumba kwa nguvu kiasi utakutana na mfupa, kandamiza kama sekunde 10 hivi uone kama katarudia
KImsingi kwenye maisha ya makuzi ys watoto ukatili haukwepeki. Kuna visa viwili niliwafanyia watoto wa majirani ukatili.Haijulikani wazazi wengine wanaleaje watoto wao kimaadili wangali wadogo. Natoka ibadani kanisani natembea kwa miguu kuelekea nyumbani, napita mtaani njiani nakuta watoto wadogo wa chekechea wengi wanacheza pamoja michezo yao ya kitoto. Nawasalimia, watoto hamjambo? Kanaibuka katoto kamoja cha kike kanajibu salamu yangu, hatujajamba tukijamba tutakuambia. Kama mtu mzima nilighadhibika na kutaka kukaadhibu katoto hako ila mazingira hayakuruhusu kumpa kifinyo kwa kutoa jibu lile baya kama mzazi. Ingeleta taharuki mtaani kwa mtu mzima mpita njia kuadhibu mtoto wa mtu. Nichofanya ni kumkazia macho makali na kumkunjia uso kumuonesha sikufurahishwa na jibu lake, walipoona nimekaza uso watoto wote walikimbilia makwao na mimi nikaona isiwe taabu nikaachana nao na kuendelea na safari yangu. Kwa kweli kuna watoto wadogo hawana nidhamu kabisa, wazazi wao waliwazaa lakini hawawapi maadili mema kuheshimu watu wengine