Ukienda ugenini Kuna vitoto vinapenda sana sifa

Ukienda ugenini Kuna vitoto vinapenda sana sifa

Usimpige bwana mpe kitu chakufanya muulize hata homework yake msaidie kanahitaji upendo kama kamekupenda Katoe hata out umpe juice na umpeleke akachezee na wenzake kwenye michezobumkanye akifanya kitu kiupole , mie nisingempiga ningempaka kazi anaakili sana so anataka uwe unanpa majukumu ukinywa kitu mwite anywe mpe achezee , na vitu Fulani, cheza naye mpiraa usikachukie Bhana
 
Nimekuja mkoani kumtembelea bradha. Kuna mzigo aliniagiza nimletee. Hapa kwa bro kuna mtoto wao wa kiume ana umri kama miaka minne au tano hivi. Asee, hiki kitoto ni kitundu sijapata ona. Mbaya zaidi, babaake na mama yake wanamlea kama yai, full kudeka-deka hovyo.
Watoto huwa hawatabiriki, kuna wapole na kuna watundu kupitiliza. Hiyo miaka 3 mpaka 5 ndiyo hapo utundu umekolea kabisa.

Nadhanai wewe bado hujapata mtoto (au ndiyo akina kataa ndoa?), subiri uone.
 
Fanya shambulizi la kimya kimya hakuna haja ya kushika fimbo.

Shika mkono vizuri kwenye msuli(hawezi kua na msuli) binya na dole gumba kwa nguvu kiasi utakutana na mfupa, kandamiza kama sekunde 10 hivi uone kama katarudia
Hapa Sana mkuu,Yaani nimecheka Kama mazuri vile😂
 
Usimpige bwana mpe kitu chakufanya muulize hata homework yake msaidie kanahitaji upendo kama kamekupenda Katoe hata out umpe juice na umpeleke akachezee na wenzake kwenye michezobumkanye akifanya kitu kiupole , mie nisingempiga ningempaka kazi anaakili sana so anataka uwe unanpa majukumu ukinywa kitu mwite anywe mpe achezee , na vitu Fulani, cheza naye mpiraa usikachukie Bhana
Kuna vitoto Ni vitundu kupitiliza sidhani Kama haya uliyoeleza yanaweza kusaidia kitu.
Suluhisho pekee Ni kukazaba vibao
 
Kwanza hapo mwenyeji wangu anatakiwa anishukuru Sana kwa kumfundishia mwanaye adabu.
Kunamtu alikuwa ananitisha sana ili nimkimbie , anasema eti yeye anakulaga watu masikio na anaweka chumvi kabisa anayala kama nyama Tena amesema anakata na kakisu kadogo ananionyesha kabisa analamba kwanza anasafisha ndio anachoma kwenye moto mkali anaweka chumvi anakula weh nilisepa sijawahi Kuja hapo sebuleni hata kumsalimia .
 
Ulikuwa na umri gani wakati huo?
 
Unaonekana ulikuwa mtundu Sana ndo maana jamaa alikuwa anakuchimbia mikwara ili umuogope😂
Eh sana nauliza maswali , umekuja kwetu kufanya Nini , kwako je umewaacha nani , unakaa siku ngapi, je umenileta zawadi gani??nishawahi mwambia unajua chai ya maziwa ??unajua mkate ?? Walahi hata akinywaa soda na mwangalia akiinywa
 
Nimekuja mkoani kumtembelea bradha. Kuna mzigo aliniagiza nimletee. Hapa kwa bro kuna mtoto wao wa kiume ana umri kama miaka minne au tano hivi. Asee, hiki kitoto ni kitundu sijapata ona. Mbaya zaidi, babaake na mama yake wanamlea kama yai, full kudeka-deka hovyo.

Sasa ni heri wangekuwa wanamlea hovyo, akawa anawasumbua wenyewe ingekuwa hakuna shida, ila akiwa na wenzake ni kakorofi, kanawapiga wenzake. Nimejilipua zangu fulana kutoka kwa vunja bei. Ameshaitanua shingo kwa kunivuta-vuta. Imekuwa kama nanyonyesha sasa. Mara aninyang'anye simu, mara aniparamie usoni kama mbwa, alafu ana vikucha vikali.

Basi naishia kujichekesha chekesha tu mbele ya mama yake. Maisha ya ugenini yana unafiki sana. Wazazi wake wala hawastuki, wanaona poa tu mtoto wao anavyo act kama kingedere. Mamaake ananiambia 'shemeji kama junia anakusumbua mchape.' Namchapaje mtoto wa watu ugenini? Kwa nini asimkataze kusumbua wageni na kukachapa kakiendelea kuleta ubishi.

Sasa mamaake akaenda dukani akaniacha na junia tunavutana-vutana. Happy ndiyo nikambadikilia, nikamwonyesha sura ya ukauzu na kumtoa shingoni maana ilikuwa kama ananidai kwa jinsi alivyokuwa ananikaba. Nikakashika mikono na kukaminya tu vidole vyake kama naminya karanga, huku namwambi acha utundu kwa wageni mtoto. Kakaanza kulia kanaelekea dukani kwa mamaake.

Maisha ya ugenini magumu sana. Nilipanga kukaa siku mbili, ila moja tu inatosha kwa kweli. Wazazi wengine hivi mnaleaje watoto kipuuzi kama hivi? Katoto ni ka-attention seeker. Mpo katika maongezi sebuleni, kenyewe kanapita-pita na kuvuta watu nguo, ili mradi tu kaonekane kapo live. Mkikapotezea, kataangusha hata glass!
Maisha ya ugenini Yana uunafiki hii kauli naafikiana na wewe mkuu maisha ya ugenini mtihani sana huna uhuru, Kuna siku nimeenda kwa mmoja ktk ndugu zangu ana watoto wawili , huyu wa mwisho mara ya mwisho kumuona alikuwa mdogo sana hivyo safari hii nilivyoenda nikakuta watoto watatu mkubwa namfahamu ila wapili nilishindwa kutokana kulikuwa na mwingine hivyo nikashindwa kutofautisha.

Sasa mwenyeji katoka nimebaki nao kmmoja katka Hawa ambao nimeshindwa kutofautisha nikamuuliza unaitwa nani kakasema mama ako (ni kakike) alinijibu jibu sikutegemea nikanyamaza nilitaka kumwambia ndugu yangu huyu mtoto unamleaje ila nikaanzia mbali nikamuuliza hapa wako ndo yupi akasema wangu ni huyu yule wa jirani(( wajirani ndo aliyenijubu hovyo) nikaacha. Kusema kweli maisha ya ugenini Yana unafiki
 
Halafu huyo mtoto wala sio mtukutu ila yupo excited kumuona Anko wake ndio maana anampandia pandia kwa furaha ila kwa kua watu mmejazwa roho mbaya na ukatili hata furaha ya watoto mnaigeuza chuki,

Hii gender ya Kiume ingeteketea tu [emoji849]
Inaonenana wanaume walikufanya jambo baya sana NYUMA uko lakini siku zijazo
 
Fanya shambulizi la kimya kimya hakuna haja ya kushika fimbo.

Shika mkono vizuri kwenye msuli(hawezi kua na msuli) binya na dole gumba kwa nguvu kiasi utakutana na mfupa, kandamiza kama sekunde 10 hivi uone kama katarudia
Shambulizi [emoji1787]
 
Haijulikani wazazi wengine wanaleaje watoto wao kimaadili wangali wadogo. Natoka ibadani kanisani natembea kwa miguu kuelekea nyumbani, napita mtaani njiani nakuta watoto wadogo wa chekechea wengi wanacheza pamoja michezo yao ya kitoto. Nawasalimia, watoto hamjambo? Kanaibuka katoto kamoja cha kike kanajibu salamu yangu, hatujajamba tukijamba tutakuambia. Kama mtu mzima nilighadhibika na kutaka kukaadhibu katoto hako ila mazingira hayakuruhusu kumpa kifinyo kwa kutoa jibu lile baya kama mzazi. Ingeleta taharuki mtaani kwa mtu mzima mpita njia kuadhibu mtoto wa mtu. Nichofanya ni kumkazia macho makali na kumkunjia uso kumuonesha sikufurahishwa na jibu lake, walipoona nimekaza uso watoto wote walikimbilia makwao na mimi nikaona isiwe taabu nikaachana nao na kuendelea na safari yangu. Kwa kweli kuna watoto wadogo hawana nidhamu kabisa, wazazi wao waliwazaa lakini hawawapi maadili mema kuheshimu watu wengine
KImsingi kwenye maisha ya makuzi ys watoto ukatili haukwepeki. Kuna visa viwili niliwafanyia watoto wa majirani ukatili.

Mi nina watoto 4, sasa kuna mtoto mmoja wa jirani na mama yake ni single mother. Yule mtoto analelewa kimayai na hajawahi pigwa maishani mwake. Siku moja namuona anamsukuma mwanangu wa kike then anataka mlalia juu. Nikamkataza kile kitendo anachofanya na nikamuita. Akaja kwangu akijua kuna amani. Nilichomfanya, hahaaaaaaa!!!! Ilikuwa suprise kwake na mama yake akaja na balozi jioni kwangu kwa maana alama za viganja vyangu zilibaki kwenye mashavu yake yaliyovimba tokana na vibao alivyokula.

Mwingine ni majuzi tu, mi napita na gari nimebeba mke na familia yangu kaninuita kibongeeee. Nilishamkatazaga siku moja kunitania kwani mimi ni mtu mzima na pia baba yake ni mnene na watoto wangu hawamtanii. Nilisimamisha gari, kakakimbia nikambembeleza na kumuita kwa upole na kwa urafiki. Nilichomfanya,hadi sasa ananiona kama kituo cha Polisi.
 
Back
Top Bottom