Ukienda ugenini Kuna vitoto vinapenda sana sifa

Fanya shambulizi la kimya kimya hakuna haja ya kushika fimbo.

Shika mkono vizuri kwenye msuli(hawezi kua na msuli) binya na dole gumba kwa nguvu kiasi utakutana na mfupa, kandamiza kama sekunde 10 hivi uone kama katarudia
Mi ndio niwe mzazi wake nikikustukia utakula za chembe
 
Kama wazazi wake wameshindwa acha ma anko tufundishe kulea....maana asiyefunzwa na ***** hufunzwa na ulimwengu..na ulimwengu wenyewe ndo sisi ma anko.

utakuta katoto kengine ukikiambia kiache kufanya upuuzi kinalia kama kimeguswa vile...sasa kama sio madeko ni nini..

au utakuta kitoto kimechukua simu ya mgeni kinairusha rusha akitaka kumpokonya...mama yake anasema muache tu achezee asije akalia..sasa malezi gani hayo..

Shida watoto sikuhizi wanalelewa kifala sana...miaka sisi tuko wadogo watoto wa hivvyo walikuwa sio wengi kama sasa hivi..
 
Wengine hukasirika mkimpigia mtoto wake🀚

Atakwambia unaujua uchungu wa labour πŸ€“πŸ˜Š
 
Mtu mzima kushindana na mtoto wa miaka minne ni tatizo, ni wazi malezi yako hayakua ya kitoto, ndio maana huoni furaha mtoto akicheka, akicheza, akideka, akiimba, akiiruka, sababu wewe vyote hivyo ulikosa.
 
Dah,nimecheka Sana. Hasa hapo kwenye kuirusha rusha simu alafu mama anasema anachezea tu hataharibu.

Yani huyo Ni anko wangu kabisa.
 
[emoji28][emoji28][emoji28]

Hujawai kuona mpo sebuleni mtoto hataki kupita hata karibu yakoo.. kuna mifinyo pia ya siri.. mtoto anashindwa kulia wala kucheka ila anakuwa hakusogelei hata akitumwa kwako unaona kanatingisha tu mageba
Ni kweli kabisa .
Wazazi wengi ni kizazi Cha nyoka. Ni watu waovu na wanawalea watoto wao katika matendo maovu.

Mimi mtoto wangu akifanya jambo jema nampongeza na kumwomyesha furaha. Akifanya jambo baya namwadhibu pale pale Kwa ukali na Kwa adhabu Kali sana,kama ni fimbo namchapa imwingie kisawasawa na kama ni kumfinya namfinya kisawasawa. Pawe Kuna wageni au hakuna akifanya jambo lisilofaa namwadhibu. Matokeo yake watoto wamekua wastaarabu Kwa kila mtu mpaka majirani . Akija Mgeni kama tulikua tumekaa sebuleni watoto watainuka wenyewe na kwenda nje au vyumbani mwao bila kuwaambia.

Kuwachekea watoto wakati wote hata kama wamefanya makosa ni kuwalea vibaya sana watoto na kuwafanya washindwe kujua jema na baya.
Watoto waliolelewa vibaya ndio wanaosumbua sana jamii hata wakiwa wakubwa Huko maofisini na hata mitaani. Wengi hawana maadili kabisa na kupenda kutokana tukana matusi ovyo .
 
Kuna huyu Dr. Mariposa anaonekana mtetezi Sana wa watoto watundu,itakuwa hajakutana na vitoto kama vingedere vinakufanyia utundu hadi vinakuharibia moood.
 
Mtu mzima kushindana na mtoto wa miaka minne ni tatizo, ni wazi malezi yako hayakua ya kitoto, ndio maana huoni furaha mtoto akicheka, akicheza, akideka, akiimba, akiiruka, sababu wewe vyote hivyo ulikosa.
Stupid..yaani furaha ya mtoto wako ndo imkere mgeni khaa.

Lazima mtoto awe na mipaka...kwani akicheza bila kumdandia mgeni hawezi kufurahi au mgeni kabla hajaja alikuwa anafanya nini ili apate furaha

angalia vizuri malezi yako...isije siku huyo mtoto akakudhalilisha mbele za watu...maana mbwa ukicheka naye utaingia naye hadi nyumba ya ibada
 
Dah,nimecheka Sana. Hasa hapo kwenye kuirusha rusha simu alafu mama anasema anachezea tu hataharibu.

Yani huyo Ni anko wangu kabisa.
Unatia konzi moja takatifu hatokaa akarudia...ili wazazi wake wajifunze kulea vizuri....wasije tuletea vibaka baadae.
 
Kuna watoto ni watundu na wakorofi pia ila kuwa hivyo tusiwalaumu sana bado ni watoto inabid tujitahid kuwaonya pale tunapoona wanafanya sio
Mtoa mada umeshindwa kumkataza mtoto wa kaka yako kufanya jambo fulani
Huko kwa kaka yako unakuwa mgeni kiasi hicho huyo kuwa kaka yako maana yake huyo mtoto ni wako pia
Nawe ni wale wale unachangia mtoto wako (wa kaka yako ) kupotea kama ulivyoona
 
Narudia tena umekosa malezi bora utotoni ndio maana furaha ya watoto wengine kwako unaiona ni shubiri kiasi cha kutolea mfano wa Mbwa kuingia msikitini,

Over come hiyo trauma yako otherwise jiepushe kucross kwa watoto wasiokua wako utanishukuru oneday.
 
Kuna huyu Dr. Mariposa anaonekana mtetezi Sana wa watoto watundu,itakuwa hajakutana na vitoto kama vingedere vinakufanyia utundu hadi vinakuharibia moood.
Natetea watoto kwa ujumla lakini pia kama kuna hatari ya kuharibika kwa mtoto tunafanya jitihada za kurekebisha pia, lakini hii habari yako ni normal kabisa ila ukiwa na stress za ajira lazima uwe na hasira
 
Hahahah kata bao tu, wewe si bamdogo wake. Bro hawezi bonga sababu wewe ni mshua pia.
Wanamuharibu dogo kumpa uhuru wa kupitiliza. 😁😁😁
Tatizo unaweza kujikuta unakuwa na mgogoro na shemeji. Alafu Mimi siyo mpigaji.

Hawachelewi kukuuliza "unaujua uchungu wa leba wewe?"
 
Kuna huyu Dr. Mariposa anaonekana mtetezi Sana wa watoto watundu,itakuwa hajakutana na vitoto kama vingedere vinakufanyia utundu hadi vinakuharibia moood.

Si umeona taarifa kama hiyo uliwahi kuileta? Sina shaka ni mtu wa karibu kabisa na huyo workmate wako akaona tu jamaa anamdekeza mtoto wake acha amkomeshe, ndio maana tukiona Mtu anachukia mtoto lazima tumuwekee alama ya hatari sababu hatujui chuki yake itaishia wapi,

Unapata wapi ujasiri wa kupanga hadi mbinu za kumkomesha mtoto mdogo eti ni mtundu je huyo mtu kufanya hayo atashindwa???

Tuwapende, Tuwatunze na kuwalinda Watoto wote.
 
Kuna wazazi miyeyusho Sana,hasa wamama.

Mwishowe unajikuta unaishi kinafiki "aaah mwache tu shemeji mtoto huyo skikua ataacha" Kumbe moyoni unasema dogo tungebaki wawili hapa ungekula makonzi balaa.
 
Kanaandaliwa kashoga kadogo dogo hapo. Ila na ww usipende kununua bidhaa feki fulana inatanukaje shingo alafu umenunua bei kweli kisa kwa vunja bei
 
Hahaha. Unabinya mifupa twas.
Asante sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mimi nilienda kwa jamaa yangu ana mapaka kama sita ndani na ni mapaka yasio na adabu kabisa yanakuja yanakupandia kama ww ndio kochi basi muda wa kula yakaja kwangu yakijua kabisa mm mgeni siwezi yanyima chakula yanasimama kwenye meza nikalikanyaga moja shingo kila likifurukuta halichomoki mwishoe likatoa mlio wa maumivu nikaliachia mpka naondoka hakuna paka alienizoea tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…