Simshauri mtu kuwekeza kwenye media. Wajanja wachache walipiga hela enzi hizo.
Media haitokuwa biashara tena miaka ijayo sababu ya social network, najua kuna watu watalipinga hili ila ukweli ndio huo. Tena radio ndio hazina muda mrefu zitaanza kufa kifo cha mende.
Zamani tulikua tunapiga simu redioni kuomba kupigiwa wimbo wa diamond lakini leo hii nikitaka kusikiliza diamond its just a single click kwenye simu yangu napata list ya nyimbo za chibu la machibu dangote. Sasa nipige simu redioni kutafuta nini?
Zamani ilikua ikishafika saa mbili kamili usiku, karibu kila nyumba utakuta wame tune ITV wanasikiliza taarifa ya habari za siku nzima(hapa namaana kwamba, hata kama tukio lilitokea saa kumi na mbili asubuhi, itakulazimu usubiri mpaka saa mbili usiku kusikiliza nini kimetokea, tofauti na sosha network taarifa itakufikia kiganjani tena kinagaubaga kuliko hata ile ya kwenye TV.
Hitimisho ni kwamba watu wanaendelea kusikiliza redio na kuangalia TV kama mazoea tu au tuseme imekua ni kama utamaduni tu. Ni sawa na kumkuta mtu kasimama meza ya magazeti anasoma vichwa vya habari wakati mkononi ameshikilia smartphone, tupo katika transition kizazi kijacho itakua ni upuuzi kusikiza redio,kusoma magazeti na kuangalia tv.
Mwisho kabisa, hivi huwa hamjiulizi kwa nini TV na Radio stations zinafungua page sosha network?? Mf itv kuwa na page Facebook