Ukifanyiwa hivi na mwanamke inamaanisha nini haswa?

Ukifanyiwa hivi na mwanamke inamaanisha nini haswa?

kama anakueleza akitongozwa anakupenda. na swala la kulewa nadhani ni company aliyonayo ndo tatizo. kwa ufupi huyo ukimbana ni anawezekana. try kuwa karibu nae na umpende atayaacha anayofanya.
 
pole ndugu tafuta mwingine haraka huyo cha wote
 
Mwambie hlo na ikiwezekana asitishe hyo mambo ukiwa nae.cjui kama umeshafanya hivyo??
 
Pole mkuu hapo unamegewa kimtindo ameishakuona ---- changamka mapema.
 
Ukiona manyoya ujue kashaliwa
 
Kuna wanawake wa namna hiyo kaka....We km anakuambia kila kitu muache akuambie....Ni bora akuambie kuliko yule anayeficha.....
We nenda nae tuu taratibu...Hiyo ubusy wa simu kweli kuna watu washakuwa wameathirika hawawezi kukaa bila kushika cm hata kuichezea tuu japo...Pia Je huo ubusy na cm ushaangalia msg anazochat ni za aina gani? Km ni mtu ambaye anapenda ku socialize muache au muambie.....Au pengine cm ni zamadili zinamuingizia hela mjini muache.....

Huo utakuwa ni upuuzi kumuacha mwanamke kisa anakuambia kila kitu....Hujui kupendwa....
Ukifichwa utasema mwanamke anakuficha, ukiambiwa unalalamika .....



Wakuu habari zenu.

Nimekuwa katika mapenzi na dada mmoja hivi sasa tunaelekea mwaka wa pili huu. Sijawahi kumkwaza kufikia hatua ya labda kuninunia week au siku kadhaa hivi. kifupi mimi ni muumini wa uaminifu katika mapenzi (though hii imenicost ktk relation zilizopita ila sitaki kuzungumzia hilo).

Ila yeye amekuwa akinikwaza sana hasa katika jambo zima la matumizi ya simu. Utakuta hatujaonana labda week lakini siku tutakapoonana hata kama ninashinda nae siku nzima yeye yupo busy muda wote na simu yake akichat watsapp na social networks nyingine. Sawa ninaweza kuonekana nina wivu ila hatambui kuwa ni muda mrefu hatujaonana anitengee muda wangu tuongee na kufurahi pamoja sasa yeye yuko busy tu anafesibuka.

Jambo jingine ni yeye kuwa muwazi kwangu kila afanyapo kosa lolote mfano akilewa tu lazima anipigie simu kuniomba msamaha kuwa mpenzi wangu nimelewa nakuomba unisamehee...hii inamaanisha nini wakuu? Ni kwamba ananipenda au ni geresha tu! Kingine kila mwanaume anayemtongoza lazima aniambie me hata huwa simfuatilii ila najua kutokana na yeye anavyoniambia...what does it mean??

Is she really love me...or should I take a leave in this relationship because of the way she is busy with her gadget? Wakuu naomba mawazo yenu without insultation.

Natanguliza shukrani
 
mkuu pole sana,mwambia unakerwa na tabia yake hiyo!
Nilikuwa na girl mwenyewe tabia ya kuwa busy na simu kama huyo wako,tuligombana sana lakini hakuacha,
mwisho wa siku nikagundua ananicheat na nikamwacha.
 
Hili la kuchat au kuwa busy mie pia linaniuzi sna, na hili kwa wanaume na wanaake kwa nini hatujaliani? Tena utakuta katikati ya mlo mtu anapokekea simu. Yaani hakuna respect kabisa hasa mkiwa wawili. Nile tabia ya kukaa na simu mezani. na simu. Wengi wetu linapokuja kuja swala la kuwa romantic inakuwa issue.

Yaani inaudhi kupitiliza. inakuwaje saa zote mchana kutwa uko na simu unachat na watu uwajuao mwenyewe.!!!inafika muda uko na mwenza wako( awe mume/mke ..awe boyfriend/ girl friend baado uko buzy kulikooo... haileti maana hata kidogo. Utakuta mtu na mwenza wako mahali fulani pa starehe lakini kila mtu haongei na mwenza wake yuko anafacebukika.. sasa si bora mngebakia nyumbani kwenu inakera hadi basi...tumekuwa watumwa wa simu na mitandao jamani. Badilikeni
 
Huyo demu yuko poa. Angalau ata yeye anajali anapokusea anaomba msamaha, kuna wengine ata kuomba msamaha shida. Jaribu kumueleza ukiwa na mimi punguza matumizi ya sim.
 
akitongozwa anakuambia je akinaniiiii huwa anakuambia? zinduka!
 
Back
Top Bottom